Sunday, December 23, 2012

Ajali ya basi kubwa la Abiria kabla ya Chalinze


Basi limedondoka Mboga nje kidogo ya Chalinze. Hakuna aliyefariki ila wapo majeruhi. Basi lilikuwa linatokea Pangani Tanga kwenda Dar es Salaam. 
 Na hizi ndio baadhi ya picha tulizo fanikiwa kupiga katika eneo la tukio.








Attached Thumbnails Attached ThumbnailsClick image for larger version. 

Name:	photo1.JPG 
Views:	0 
Size:	173.7 KB 
ID:	76385   Click image for larger version. 

Name:	photo.JPG 
Views:	0 
Size:	161.9 KB 
ID:	76386   Click image for larger version. 

Name:	photo3.JPG 
Views:	0 
Size:	159.1 KB 
ID:	76389  Click image for larger version. 

Name:	photo4.JPG 
Views:	0 
Size:	149.3 KB 
ID:	76390  

Saturday, December 22, 2012


Friday, December 21, 2012

Picha za Hukumu ya Lema Akirudishiwa Ubunge Na Mahakama Ya Rufaa


 Lema,Mbowe na nassari mahakamani
 Mawakili wakiwa kwenye viti vyao
 Hawa ndiyo waliokuwa wamefungua kesi dhidi ya lema
 Mahakamani,lissu,nassari,mwenyekiti mbowe na kilewo wakiteta na mke wa lema
 Lema akianza kutoa hotuba fupi baada ya kutoka mahakamani.kulia ni joshua nassari
 Vitalisi kimomogoro,wakili wa lema.huyu ndiye amekuwa na kesi hii tangu kuanza
 Tundu lisu,mtetezi wa lema.aliingia baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa.ameshangiliwa sana

 Askari wakisindikiza msafara wa wafuasi wa CHADEMA
 hapa lema akiwa na kilewo wakati wa maandamano ya kutoka mahakamani kuelekea makao makuu ya chadema


Hukumu imeangalia haswa swala la Locus Stand ya kama waliofungua kesi walikuwa na haki kisheria ya kufanya hivyo.imeangaliwa kwa kina na kuonekana kuwa kadiri ya pingamizi ya mawakili wa lema kimomogoro na Tundu Lissu,waliofungua shitaka dhidi ya lema hawakuwa na locus stand ya kufanya hivyo.kwa hiyo mengine yote yanakuwa null and void.hukumu haikuchukua hata nusu saa.so lema ni mbunge halali wa arusha mjini tangia leo

DEREVA BODABODA ACHINJWA KISHA KUNYANG'NYWA PIKIPIKI NA KUTUPWA VICHAKANI

MADEREVA WA PIKIPIKI WAKIPITA KATIKA BARABARA YA MKENDO KWENDA KUMSHUHUDIA MWENZAO HOSPITALI YA MKOA WA MARA

MWENZAO ACHINJWA

BODABODA WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA MKOA WA MARA

WANANCHI WAKISHUHUDIA MWILI WA BODABODA ANYEDAIWA NI MKAZI WA KIGERA KIARA ALIYECHINJWA NA KUNYANG'ANYWA PIKIPIKI


SEHEMU YA MGUU AMBAO PIA ULIKATWA NA MAPANGA


ASKARI POLISI WAKIWAPA NAFASI WANANCHI KUUTAMBUA MWILI HUO UKIWA NDANI YA GARI


DAKTARI AKIWA KAZINI KABLA YA KUPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI

MWILI WA DEREVA WA PIKIPIKI MAARUFU KAMA BODABODA ALIYECHINJWA NA KUNYANG"ANYWA PIKIPIKI ULIOKOTWA KATIKA MAENEO YA NYANKANGA NJE KUDOGO YA MJINI WA MUSOMA UKIPELEKWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA MKOA WA MARA.
         Nb;tunaomb radhi kwa baadhi ya picha ya tukio hili

Saturday, December 15, 2012

Askari polisi wanaohudumia kitengo cha dawati la Jinsia Wanawake na Watoto wametakiwa kuwa na kauli nzuri wanapokuwa wanawahudumia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wanapowafikia.

SHUKA CHINI KWA PICHA NA MAELEZO ZAIDI


WANAFUNZI WA TARIME HIGH SCHOOL

WAUMINI WA KANISA LA ANGLICAN NAO HAWAKUWA NYUMA

POLISI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO YA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME

WATOTO WANAFUNZI WA SHULE NAO WALISHIRIKI

KAIMU KAMANDA ZACHARIA AKIFAFANUA JAMBO


ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA TARIME DK.MWITA AKILI AKISOMA HOTUBA KATIKA UFUNGUZI WA OFISI YA DAWATI LA JINSIA NA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

KAIMU KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA TARIME RORYA SEBASTIAN ZACHARIA KUSHOTO KATIKA MAAZIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NA UZINDUZI WA OFISI YA DAWATI KITUO CHA POLISI WILAYANI TARIME

Askari polisi wanaohudumia kitengo cha dawati la Jinsia Wanawake na Watoto wametakiwa kuwa na kauli nzuri wanapokuwa wanawahudumia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wanapowafikia.

Kauli hiyo ilitolewa na Askofu wa Kanisa la Anglicana Dayosisi ya 
 Tarime Dk.Mwita Akili alipokuwa akifunga siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijnsia sambamba na ufunguzi wa Ofisi ya dawati la Jinsia katika kituo kikuu cha Polisi Wilayani Tarime

Alisema wahanga wa Ukatili hawana budi kuzungumza nao kwa unyenyekevu ili waweze kuelezea kwa umakini yale yaliyowasibu na si vyema kuzungumza nao kwa kuwafokea na kuendelea kuonekana wanyonge.

Askofu Mwita alisema kuanzishwa kwa dawati la Jinsia na ufunguzi  wa Ofisi hiyo kuwe ni chachu ya kuwasaidia Wanawake hasa wale wanaokutana na vitendo vya ukatili pale wanapowafikia kutaka msaada kutoka kwao.

“Watakaowafikia katika ofisi hii ni sawa na mama zenu,dada ama ndugu kwenu hivyo wasaidieni kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuwa na moyo wa huruma ili wapate faraja na msifanye kinyume na hivyo.

“Mtu anaye kutana na suala la ukatili anahitaji msaada na kuwa naye kwa ukaribu naamini askari Polisi watakao kuwa katika dawati hili tayari wanayo mafunzo namna ya kuwahudumia wahanga wa Ukatili nawaombea kwa Mungu awape wepesi katikakutekeleza majukumu yenu ya kazi”,alesema askofu Mwita.    
Askofu Mwita alitumia nafasi hiyo kuihasa jamii kuachana na masula ya Ukatili hasa kwa Wanawake kwani wanapofanyiwa vitendo vya ukatili shughuli mbalimbali za kiuchumi zinakuwa hazifanyiki na hivyo jamii kuendelea kuwa masikini.

Alisema upo ukatili ambao hauzungumziwi sana katika jamii katika suala zima la kumnyima elimu Mwanamke na kudai kuwa hakuna ukatili mbaya kama huo kwani unakwamisha maendeleo.

“Mwanamke lazima apewe elimu pamoja na kumpa nafasi ya kumiliki mali ili aweze kufanya mambo ya faida katika jamii n asiwe Mwanamke wa kuomba kila kitu kwa Mwanaume ikiwa hata kama anataka kununua mafuta ya kupikia ama mboga,”alisema

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Tarime Rorya Sebastian Zacharia alisema kutokana na askari wanaoshughulika na dawati kupata mafunzo ya namna ya kufanya majukumu yao anaamini watafanya kwa uadilifu mkubwa.

Alisema Jeshi la Polisi limeingia moja kwa moja katika mapambano ya ukatili wa Kijinsia na kudai kuwa jamii inapaswa kushirikiana na Jeshi hilo ili kuweza kutokomeza matukio ya ukatili katika jamii.
 
Posted By Josephat Ogunya Musoma ndo Home !!



Jeshi la Polisi Mkoani Mara linawashikilia watu tisa wanaodaiwa kujihusisha na ujambazi katika Ziwa Victoria kwa kuwanyang'anya Wavuvi mali zao zikiwemo boti, njini,pesa pamoja na vifaa vingine wanavyovitumia wakati wa uvuvi na kisha kuwatosa majini.

shuka chini kwa picha na maelezo zaidi
George Marato wa ITV akimuhoji kamanda Mwakyoma
nnjini zilizokamatwa na Jeshi la Polisi pamoja na majambazi
mkuu wa upepelezi afande Mahamud huku kushoto kwake akiwepo mkuu wa kituo mjini Musoma afande Hupa wakifatilia kwa karibu maelezo ya Kamanda Mwakyoma
Mpiga picha wa itv maxmilian Dominick akitafuta picha nzuri kwa ajili ya habari
Na Shomari Binda
        Musoma,

Jeshi la Polisi Mkoani Mara linawashikilia watu tisa wanaodaiwa kujihusisha na ujambazi katika Ziwa Victoria kwa kuwanyang'anya Wavuvi mali zao zikiwemo boti, njini,pesa pamoja na vifaa vingine wanavyovitumia wakati wa uvuvi na kisha kuwatosa majini.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake,Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Absalom Mwakyoma alisema kukamatwa kwa majambazi hayo kunatokana na ushirikiano ambao wameupata kutoka kwa Raia wema kutokana na kuchoshwa na vitendo ambavyo imekuwa vikitendeka kwa wavuvi.

Katika tukio lingine Kamanda Mwakyoma alisema Mahabusu mmoja Wilayani Serengeti anayetuhumiwa kwa wizi wa baiskeli Nichoilaus Magesa alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na askari Polisi baada ya kutaka kutoroka akiwa njiani kurejeshwa gerezani  na kulazwa katika Hospitali ya DDH Wilaya Bunda

Kamanda Mwakyoma alisema Mnamo Novemba 21 Mwaka huu majira ya saa za usiku katika Kisiwa cha Rukuba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara Wavuvi watatu Nyantora Nyihande (42),Mwita Nyamsya (35) na Nyaganga Tibe wa kambi ya uvuvi Elikana katika kisiwa hicho wakiwa katika shughuli zao za uvuvi walivamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi na kuwavua nguo na kuwanyang'anya njini pamoja na boti.

Alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo,Jeshi la Polisi liliamua kuendesha Operesheni isiyokoma katika ziwa Victoria na kufanikiwa kuwakamata majambazi hayo ambapo wengine wamekili kuhusika na vitendo hivyo ambavyo vikekuwa vikitokea mara kwa mara katika ziwa hilo.

"Hawa tumefanikiwa kuwakamata lakini sio kwa juhudi za Polisi pekee pia Raia wema wametusaidia sana katika operesheni hii ambayo imezaa matunda kwa kufanikiwa kuwatia nguvuni wanyang'anyi hawa ambao wamekwa wakiwakosesha amani wavuvi wanapokuwa katika shughuli zao za uvuvi.

"Nipende kuwahakikishia Waandishi wa Habari ya kwamba operesheni hii haitakoma itaendelea kufanyika kwa wakati wote ili kuhakikisha vitendo vya uhalifu ndani ya ziwa Victoria vinakomeshwa kwa kuwatia nguvuni wale wote wanaohusika na vitendo hivi.

Alisema katika operesheni hiyo wamefanikiwa kukamata njini nne za boti ambazo walinyang'anywa wavuvi walipoikuwa katika shughuli zao za uvuvi na kuwaomba Wananchi ambao walichuliwa mashine zao na wana vielelezo waende katika kituo kikuu cha Polisi Mjini Musoma ili waweze kizitambua.

Kamanda Mwakyoma aliwataja majamabazi hayo amabayo yanashikiliwa na Jeshi la Polisi kabla ya kufikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika kuwa ni Musa Ismail Matara mkazi wa Nyakato Mjini Msoma,Osunga Kiti,Otieno Zacharia,Guya Odudo Ayadu na Zuberi Christopher wakazi wa Rorya.

Wengine waliokamatwa kuhusiana na matukio ya unyang'anyia katika ziwa Victoria ni pamoja na Charles Nyaseri,Javen Baraka,Pamela Nyaumo na Nyambarya Matara ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika matukio hayo.

Aidha Kamanda Mwakyoma amewaomba Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwatia nguvuni wale wote wanaodaiwa kujihusisha katika vitendo vya uhalifu kwa kusema kazi hiyo haiwezi kufanywa na Polisi pkee yao bali kila mmoja analo jukumu la kuhakikisha hali ya usalama katika jamii inakuwepo.