Sunday, December 29, 2013

FILIKUNJOMBE: RAIS WETU KIKWETE AMEMALIZA MGOGORO WA MPAKA KATI YA MALAWI NA TANZANIA ENDELEENI NA SHUGHULI ZENU

Wananchi  wa Manda  wakiendelea na shughuli zao katika ziwa Nyasa
Mkazi  wa Manda  akichota maji  ziwa Nyasa
Mzee  wa matukio  daima  akizungumza na mmoja kati ya  wakazi wa Mwambao mwa  ziwa Nyasa ambae alikutwa akiendelea na shughuli zake katika eneo la Manda baada ya mbunge Deo Filikunjombe  kuwaondoa hofu ya  kutokea  vita kati ya Tanzania na Malawi
Mwalimu Dominic Haule  akiuliza bei ya  samaki kwa mvuvi  wa ziwa nyasa eneo la Manda ambapo samaki huyo alikuwa akiuzwa Tsh 5000
Katibu  wa mbunge Filikunjombe Bw  Stanley  Gowele kulia akimtazama  samaki aliyekuwa akiuzwa kwa  kiasi cha Tsh 5000 kutoka kwa mvuvi wa ziwa nyasa kulia kati ni Dominic Haule
Wananchi  wakiongelea  katika  ziwa Nyasa  eneo la Manda
Mkazi  wa Manda  akifua ngua kado ya ziwa Nyasa  eneo la Manda
 Samaki  waliovuliwa  ziwa  nyasa 
Mbunge  wa jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  wa tatu  kulia akiwa na mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Solomon Madaha wa tatu  kulia ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Bw Kolimba na  viongozi  wengine  wakitembelea ziwa  nyasa
Mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjome wa  pili kushoto akimwonyesha mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha  kushoto nchi  ya Malawi  inavyoonekana  ukiwa eneo la Manda mwambao  mwa ziwa Nyasa  baada ya  kutembelea  eneo hilo kuhamasisha  wananchi  kuendelea na shughuli zao na kuondoa hofu ya kutokea  vita ya mpaka kati ya nchi ya Malawi na  Tanzania
Na  Francis Godwi Blogu Ludewa
 
MBUNGE wa  jimbo la Ludewa  mkoani Njombe Deo Filikunjombe amepongeza  jitihada kubwa  zilizofanywa na serikali ya  chama  cha  mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dr Jakaya  Kikwete katika  kumaliza mgogoro  wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi na  kuwataka  wananchi   wanaoishi mwambao wa ziwa Nyasa  kuendelea na shughuli zao  bila hofu  yoyote.
 
Filikunjombe  alisema  kuwa serikali ya Rais  Kikwete ni  serikali  sikivu na  ndio  sababu  ya  kulishughulikia suala  hilo la mgogoro  wa mpaka kwa  wakati zaidi bila kutokea machafuko ya aina  yoyote .
 
Akizungumza kwa nyakati  tofauti na  wananchi wa kata ya Ilela na Manda wakati  wa ziara  yake ya  kusherekea pamoja na wapiga kura  wake  sikukuu ya Krismas na Mwaka  mpya juzi ,Filikunjombe  alisema  kuwa awali  baada ya  kuwepo kwa  taarifa ya Rais  wa Malawi Joyce Banda  kudai ziwa Nyasa  lote ni mali ya nchi yake  ya Malawi wananchi  wa Tanzania  wanaoishi jirani na ziwa  hilo  upande wa Tanzania  walianza kuigiwa a  hofu  kubwa .
 
Mbali ya kuingiwa na  hofu  hiyo ya kiusalama  ila  bado  walikuwa wakifanya shughuli  zao kwa hofu  kubwa na baadhi  yao kushindwa  kuwajibika  vema katika  shughuli za kimaendeleo kwa kuhofu vita kutokea .
 
Hata  hivyo  alisema  kutokana na  serikali  ya  CCM kuwa  sikivu  zaidi baada ya kubaini  suala   hilo mara  moja jitihada za  kulifanyia kazi hilo  bila kumwaga  damu  ilianza kufanyika na  kuwa  kwa  sasa Rais Kikwete amemaliza mgogoro  huo na hakuna tatizo  tena.
 
” Ninawahakikishia  wananchi  wangu  wa Manda na Ilela  pamoja na kata  nyingine  zote kama Makonde, Lifuma na  zote ambazo zipo jirani na ziwa Nyasa na  wanategemea  maisha  yao kwa kuvua  samaki na dagaa katika  ziwa  hilo ….kuendelea na shughuli  zao  bila hofu  yoyote” alisema  mbunge Filikunjombe  huku akishangiliwa na  wananchi  hao
 
Alisema  kuwa  Rais  Kikwete  amekuwa akijituma  sana katika  kuwatumikia  watanzania ila  wapo  baadhi ya   watendaji  wa serikali ambao  ni mzigo  katika  serikali yake na  wamekuwa  wakishindwa  kuwatumikia wananchi vema.
 
Filikunjombe  alisema yeye kama mbunge  na mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Ludewa kamwe hatakubali  kuona  wananchi  wake  wanakosa  huduma za msingi kama  ilani ya CCM inavyosema kutokana na baadhi ya  viongozi  kushindwa  kutimiza majukumu  yao vema.
 
Alisema  kuwa  kwa kutumia fursa    za ziwa Nyasa  wananchi  wa maeneo ya mwambao mwa  ziwa hilo  wanaweza  kujikwamua kiuchumi kwa  kupatiwa  vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya uvuvi  badala ya  kuendelea  kuifanya kazi  hiyo kwa kutumia  vitendea kazi duni na kufanya  uvuvi  wao  kutokuwa na tija ya kimaendeleo.
 
Akizungumza kwa niaba ya wananchi  wenzake John Haule  alisema  kuwa  awali  walikuwa na  hofu kubwa ya  kuendelea  kufanya  shughuli za maendeleo  kutokana na hofu ya kutokea vita  ya mpaka kati ya Malawi na Tanzania na kuwa  hata  wakati  mwingine   wakiona ndege zikipita angani   walikuwa  wakiogopa kuwa  yawezekana ni ndege za  vita kutoka Malawi na  zinataka  kuwaangamiza.
 
“Tunakupongeza kwanza  wewe mwenyewe  mbunge wetu Deo Filikunjombe kwa  kutuwakilisha  vema kwa Rais Kikwete na  bungeni  pia tunataka  kuwaeleza viongozi wa CCM sisi wana Ludewa  tumechoka  kuendelea kuwa na mbunge wa  kipindi  kimoja kimoja    sisi kwa  sasa hatuhitaji mbunge mwingine zaidi yako  na kama watafanya wao  watakavyo tupo tayari  kuhama na  wewe papote”
 
Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya ya  Ludewa Juma Madaha  mbali ya kuungana na mbunge Filikunjombe  kuwahakikishia usalama  wananchi hao bado  alisema  kuwa  ni  vema  wananchi hao kutumia  mvua  zilizopo kwa  kulima mazao yanayohimili ukame kama mihogo ambayo  imekuwa ikistawi zaidi katika maeneo hayo .
 
Kwani alisema  kuwa wataalam wa  hari ya  hewa  wanadai kuwa hali  ya mvua kwa mwaka  huu  si nzuri  sana pia   upo uwezekano  wa mwakani Taifa  kutokuwa na neema  kutokana na wataalam  hao   katika uzoefu  wao  kuonyesha  miaka  yote  inayo malizika na namba 4  kuwa na tatizo la neema.

Wednesday, November 27, 2013

MABOMU, RISASI VYARINDIMA KIVULE "ILALA" POLISI WAKIPAMBANA NA WAENDESHA BODABODA ZAIDI YA 100....SOMA HAPA


 
Waendesha bodaboda 13 wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuendesha mauaji dhidi ya watu wanaodaiwa kuwa ni wezi wa pikipiki katika mtaa wa Kivule Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. 

Mbali ya waendesha bodaboda hao, pia pikipiki 17 zilikamatwa na polisi kwa tuhuma kama hizo jana.

Hata hivyo, kazi hiyo haikuwa rahisi kwani polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi pamoja na risasi za moto kukabiliana na waendesha pikipiki zaidi ya 100, hali iliyozua mtafaruku mkubwa kwa wakazi wa mtaa huo na viunga vya jirani.

Kabla ya  tukio hilo, madereva wa bodaboda walijikusanya kwa ajili ya kuendesha msako wa nyumba kwa nyumba baada ya kupata majina ya mtandao wa wezi wa pikipiki katika mtaa huo na maeneo ya jirani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Marietha Minangi, alisema kuwa hatua kali zimechukuliwa na jeshi hilo baada ya waendesha bodaboda hao kujichukulia sheria mkononi ya  kuwaua watu waliokuwa wakiwakamata.

Kamanda Minangi alisema msako huo utaendelea kwa kuwa waliojitokeza katika mauaji hayo ya kinyama walikuwa ni wengi.

“Nawasihi waendesha pikipiki kama wanahitaji biashara wafanye biashara, vinginevyo waache mara moja vitendo vya kihalifu kwa kuwa tunaendelea kuwasaka hadi kieleweke,” alisisitiza Kamanda Minangi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule, Joseph Gassaya, alisema kuwa mtaa wake ulivamiwa na vitendo vya uhalifu yakiwamo mauaji ya vijana wawili.Gassaya alifafanua kuwa vijana hao waliuawa na madereva wa bodaboda kutokana na kuwahisi kuwa ni wezi.

"Nikiwa kiongozi wa mtaa huo, nafahamu kuwa matukio ya mauaji yamekuwa yakitokea mara kwa mara ikiwamo waendesha bodaboda wanne kuuawa na kuporwa pikipiki zao na taarifa zinatolewa polisi," alisema.

“Pengine vijana hao wameamua kuchukua sheria mkononi baada ya kuona taarifa zao hazifanyiwi kazi ipasavyo, bila kujua kuwa jeshi hilo linachukua hatua baada ya kuthibitisha,” alisema.

Naye mmoja wa waendesha bodaboda hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha polisi kutumia nguvu kupita kiasi.

Alisema taarifa za kuporwa pikipiki na kunyongwa kwa wenzao wanne, alitoa taarifa katika kituo cha Polisi Stakishari, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kuwasaka wahalifu hao.

“Sielewi kama waendesha pikipiki waliokufa hawakuwa watu. Kwa nini hao wezi waonekane kuwa wana haki zaidi...Jeshi lipo kwa ajili ya raia wote si kwa baadhi ya watu,” alisema.

Alisema kabla ya kutekeleza zoezi hilo, waliweka mtego kwa mtu waliyemhisi kuwa ni mwizi na aliponaswa mmoja wao, aliwataja wenzake wote aliokuwa akishirikiana nao kuiba pikipiki.

Aliongeza kuwa Jeshi la Polisi halipendi kutoa ushirikiano kwa kuwa matukio ya mauaji yameripotiwa lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, jambo lililowaudhi na kuamua kujichukulia sheria mkononi ili kujihami.

CHANZO: NIPASHE
Commedy za nje ya Tz.

HUYU NDO MDADA MREMBO ANAYE ONGOZA KWA SWAGA BONGO.. MTAZAME HAPA.


 Photo


Photo

Photo


Read more: http://kilelechahabaritz.blogspot.com/2013/11/huyu-ndo-mdada-mrembo-anaye-ongoza-kwa.html#ixzz2lpyjI3Xf

Monday, November 25, 2013

LADY JAYDEE AMPA MAKAVU LIVE MH.JANUARY MAKAMBA. SOMA HAPA



Lady Jaydee
Lady Jaydee kweli ni Anaconda na sio mtu wa kuchezea kwani ukiingia kichwa kichwa kwenye kumi na nane zake anakumeza na kukupaka live kama huna hoja ya msingi. Hayo yamempata Mbunge wa Bumbuli January Makamba. Angalia alichoandika Makamba hapo chini na jibu la Lady Jaydee ambaye ni mwanamuziki mwenye jina kubwa Afrika mashariki.
                                                      January Makamba

Sunday, November 24, 2013

CHEZEA UREMBOO KOPE BANDIA ZAMPOFUA MACHO MREMBO JIONEE




Khadija Omar, mkazi wa Kigogo amepata pigo kufuatia kupofuka macho.
AMA kweli hujafa hujaumbika, mrembo Khadija Omar, mkazi wa Kigogo, Dar amepata pigo kufuatia kupofuka macho alipokuwa akiwekwa nyusi bandia katika saluni moja iliyopo maeneo hayo, Risasi Jumamosi lina mkasa mzima.

Tukio hilo lilitokea Novemba 14, 2013 na kuvuta hisia za watu wengi waliosikia na kushuhudia mkasa huo.
Akizungumza na paparazi wetu juzi huku akimwaga machozi, Khadija alisema siku ya tukio saa 11 jioni alikwenda kwenye saluni hiyo iliyopo jirani na anapoishi kwa lengo la kubadili mwonekano wake wa macho kama akina dada wengine wanavyofanya.
“Mara tu baada ya kunibandika kope nilianza kuona giza, nikawaeleza akina dada waliniweka lakini wakanipuuza na kuniambia mimi ni mwoga.
“Muda mfupi mbele hali yangu ikawa mbaya zaidi, ikabidi wazibandue kope lakini juhudi zao ziligonga mwamba kwa sababu walitumia gundi kali, ikabidi nirudi nyumbani,”alisema Khadija.
Akaongeza: “Nikiwa njiani macho yaliniuma sana na kuzidi kupoteza uwezo wake wa kuona, ghafla nikaanguka chini. Akatokea msamaria mwema na kunipeleka nyumbani,” aliongeza.                                                                                  Khadija Omar, mkazi wa Kigogo.
Khadija alisema kesho yake alikimbizwa Hospitali ya Amana, Dar ambako alipatiwa dawa bila ya kutolewa kope hizo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
“Nilipofika nyumbani hali ilizidi kuwa mbaya nikalazimika kupelekwa  Hospitali ya Macho ya CCBRT (Msasani, Dar) ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hilo,” aliongeza Khadija kwa majonzi.
Alisema kule CCBRT alijikuta akiangua kilio baada ya madaktari kumwambia kope hizo haziwezi kutolewa mpaka zikatwe na mkasi.
Baada ya zoezi hilo kufanyika, Jumapili iliyopita Khadija aliweza kufungua macho kwa mara ya kwanza tangu alipotokewa na hali hiyo lakini bila kuona sawasawa.
Jumatatu iliyopita Khadija aliruhusiwa kurudi kwake lakini akiwa hana uwezo wa kuona na kutakiwa kurejea tena hospitalini hapo baada ya wiki tatu kwa uchunguzi zaidi.
Daktari mmoja wa CCBRT ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake gazetini alisema: “Khadija anaweza kuona kama zamani lakini itamchukua muda mrefu kutokana na madhara ya gundi ya ‘supa glu’ iliyotumika.
Taarifa zaidi zinasema, Jane na Koku wafanyakazi wa saluni waliomuweka kope hizo Khadija  walikamatwa na Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar na kufunguliwa jalada la uchunguzi namba MGN/RB/13021/2013

Saturday, November 23, 2013

TAZAMA PICHA ZAIDI YA 20 JINSI PQUARE WALIVYOFUNIKA LEADERS CLUB NI SHIDAAAAA



























                                          
PICHA ZOTE KWA HISANI YA GPL