Thursday, February 21, 2013
WAFUASI WA SHEKHE PONDA WAZUA KIZUNGUMKUTI PALE SHEKHE PONDA ALIPOKUWA AKIRUDISHWA RUMANDE TAZAMA PICHA.
Basi la
jeshi la magereza lililowabeba mahabusu wanaokabiliwa na kesi ya
uchochezi ambayo inamuhusisha Shekhe Ponda Issa Ponda likiwa linatoka
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Kuwarudisha Rumande mahabusu Hao huku
wafuasi wake wakizomea askari wa kutuliza ghasia muda mfupi uliopita
Baadhi
ya Askari wa Kutuliza Ghasia FFU wakiwa kwenye gari tayari kwa kupambana
na lolote litakalojitokeza wakati Shekhe Ponda akirudishwa Mahabusu
muda mfupi uliopita
Wafuasi
wa Shekhe Ponda wakiwa Nje ya Mahakama ya Kisutu na Maktaba ya Taifa
wakizomea askari wa Kutuliza Ghasi wakati wakisindikiza basi lililobeba
mahabusu akiwemo Shekhe Ponda Issa Ponda Muda mfupi uliopita kwenye
Barabara ya Bibi Titi Mbele ya Maktaba Kuu ya Taifa
Wafuasi
wa Ponda wakiwa na mabango mbele ya Maktaba Kuu ya Taifa pembeni kidogo
ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu muda mfupi uliopita huku wakiwazomea
askari wa kutuliza ghasia
Gari la
maji ya kuwasha likiwa linaishia huku likiwa kwenye msafara wa basi
linalowarudisha mahabusu rumande huku Shekhe Ponda akiwa Mmoja wao
Askari wa Kutuliza Ghasia wakiwa Kazini Muda mfupi uliopita
Askari wa Kutuliza ghasia wakiwa kazini
Gari la magereza likiwa linaongoza msafara wa kurudisha mahabusu rumande.
Wafuasi wa Shekhe Ponda wakiwa wamekaa nje ya Mahakama ya Kisutu na Mbele ya Maktaba Kuu
Wafuasi wa Shekhe Ponda wakisubiri Shekhe Ponda kutoka Mahakamani
Monday, February 18, 2013
PADRI WA KANISA KATOLIKI APIGWA RISASI WAKATI AKIENDA KANISANI ZANZIBAR.
Picha tofauti za Padri wa Kanisa
Katoliki, Padri Evarist Mushi zikimuonesha enzi za uhai wake, Padri
Mushi ambaye ameuawa leo asubuhi kwa kupigwa risasi wakati akiingia
Kanisani kwa ajili ya Ibada ya Jumapili katika eneo la Mtoni Mjini
Magharibi Zanzibar.
Eeneo la tukio la mauaji ya Padri Evarist Mushi.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa na
Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud
walipotembelea eneo la tukio leo.
Gari la Padri Evarist Mushi likiwa limetapakaa damu baada ya kupigwa risasi
Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel
Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar leo kufuatia
mauaji ya Padri wa Kanisa katoliki, Padri evarist Mushi. (Picha na Adrew
Chale, Zanzibar)
Sunday, February 17, 2013
KAMA UNA ROHO NDOGO HUWEZI KUTAZAMA HIZI PICHA.LAKINI HIVI NDIVYO UHAI WA MWANAMKE HUYU ULIVOKATISHWA KINYAMA.
KAMA UNA ROHO NDOGO HUWEZI KUTAZAMA HIZI PICHA.LAKINI HIVI NDIVYO UHAI WA MWANAMKE HUYU ULIVOKATISHWA KINYAMA.
Wiki
iliyopita tuliongea katika leo tena juu ya kisa cha Marehemu Nasra
pichani.Mama huyu alikuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara lakini Dar es
salaam alifika kufanya matibabu katika hospital ya Muimbili.Kwa miaka
takribani 23 alikuwa mke wa bwana Elia Makumbati na kujaaliwa kupata
watoto wanne mkubwa kabisa yupo chuo kikuu cha UDOM.Kwa miaka yote
wamekuwa na misuko suko sana kwenye ndoa mama akiwa anapigwa sana hata
kuchanwa na viwembe.
Mwezi
wa pili walitofautiana baada ya bwana kuoa mke mwingine.Wakiwa
wametofautiana na Nasra kuendelea na maisha siku hiyo bwana akamfata
akamkuta barabarani anatoka kazini.Akiwa na rafiki yake wanatembea
akamfungia breki mguuni akamwambia anataka kuongea nae.Nasra akakataa
akamwambia kama kuna maongezi hawezi kuongea nae kama vipi amfate
nyumbani huku anaendelea kutembea.Bwana yule akamfata kwa nyuma
akamgonga na gari na baada ya Nasra kuanguka akanasa chini hivyo
kuendelea kumburuza umali wa kama mita 150 hivi.Alipofika kwenye tuta
akanasuka bwana ndio kushuka kwenye gari kukimbia.
Kiukweli
aliumia sana sana ngozi yote ya mgongoni,mbavuni,makalio,ikavuka na
kubaki kwenye lami.Sikio lake la kushoto lote likaliwa na lami,mbavu 7
zilivunjika pamoja na mguu.Akapelekwa hospitali na baadae kulazwa
Bugando Mwanza lakini ikawa anahitajika kuhamishiwa hospital ya
Muhimbili kwa matibabu zaidi.Akiwa muhimbili alikuwa na hali mbaya sana
baadae ikathibitika kuwa ameumia ndani kwa ndani kwani alibadilika sana
akavimba na kuwa mweusi.Kwamuda wote wa miezi takribani sita alikuwa
katika maumivu makali na bahati mbaya hakuweza kupambana tena kupigania
maisha yake.
Nasra pichani kulia mwenye kilemba chekundu akiwa na ndugu zake wakati akiwa mzima.
Usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 10
Nasra akaaga dunia.Ilikuwa ni huzuni sana jinsi alivyoteseka na namna
mazingira ya kifo chake kilivyotokea.Tulikuwa na matumaini kuwa angeweza
kupona maana dakika za mwisho alikuwa anaongea japo kwa shida.
Tunaomba mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nasra mahala pema peponi,Amina.
Hii ni picha ya muwewe Elia Makumbati
ambae mpaka sasa anatafutwa na jeshi la polisi kwa kitendo cha kinyama
alichokifanya.Jeshi la polisi mkoani Mara wanafanya juhudi za kila namna
kumkamata lakini amekuwa akikimbia mara aonekane Kenya,Botswana na
kwengineko lakini bado hajakamatwa.Kwa utakae muona usisite kutoa ripoti
zake.Mpaka askari wa upelelezi wa kimataifa interpol ina taarifa zake.
Subscribe to:
Posts (Atom)