Wednesday, June 5, 2013

AJALI MBAYA YATOKEA TENA KIWIRA WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA NA KUUWA WAWILI.

Ona baadhi ya picha zinazohusu hiyo ajali!

HAPA NDIPO ENEO LINALOTAMBULIKA KAMA UWANJA WA NDEGE AMBAPO KILA MARA AJALI HUTOKEA KWA MAGARI KUFELI BREKI NA KUSHINDWA KUKATA KONA HIVYO KUPITILIZA BONDENI

MABAKI YA GALI AINA YA SCANIA T669ACU MALI YA KAMPUNI YA LAKE OIL ILIYOKUWA IKITOKEA DSM KUELEKEA KYELA

HAPA NDIPO WALIPOKUTWA TINGO  ALIYENUSURIKA KIFO AMBAPO DEREVA WAKE NA MWANAE WALIFARIKI PAPO HAPO

ENEO AMBALO GARI HILO LILISHINDWA KUKUNJA KONA KISHA KUTUMBUKIA KORONGONI

NASIBU RAMADHANI AMBAYE NI TINGO WA GALI HILO

MAJERUHI NASIBU RAMADHANI AKIPATA HUDUMA KATIKA HOSPITALI YA TUKUYU KABLA YA KUKIMBIZWA KWENDA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA


MABAKI YA GALI

POLISI WAKIWA ENEO LA TUKIO

PICHA NA ALLY KINGO-RUNGWE

LIVE TAZAMA PICHA TOKA MOROGORO AMBAKO ALBERT MANGWEA ATAZIKWA BAADA YA KUAGWA VIWANJA VYA LEADERS CLUB

  picha kabla msiba hujawasili Morogoro kwao Mangwea!


 Wageni waliofika msibani Morogoro kwa marehemu Mangwea. 
 Masufuliya ya chakula kwa watu waliokuwepo msibani morogoro.
 Wakipanga jambo kutokana na eneo la nyumbani kwao marehemu Mangwea kuwa padogo.
Baadhi ya bdg na jamaa wa marehemu wakiwa wanaugulia maumivu ya kutokwa na ndg yao mpendwa Ngwea!

LIVE TOKA LEADERS: WATU WAANZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU NGWEA .... TAZAMA PICHA

Dah this is it ndugu yetu mpendendwa ndo ametangulia mbele za haki na sasa ule muda wa kutoa heshima za mwisho ndo umewadia. Mungu awape nguvu wale wote waliofikwa na msiba huu.

Sasa ni mda wa kuanza kutoa heshima ya mwisho kwa ndugu yetu Albert Mangweha hapa Leaders Club

Zoezi la kumuaga mwanamuziki wa kizazi kipya, Albert Keneth Mangwea ndio unaoendelea kwa sasa katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Baada ya zoezi hili waombolezaji wataanza msafara wa kuelekea Kihonda Morogoro ambako ndipo mwanamuziki huyo aliyethibitika kuwa kipenzi cha wengi atakapopumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Umati mkubwa wa watu wanaonekana wakimiminika katika viwanja hivyo kumuaga.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amen

Gari lenye Mwili wa Marehemu Albert Mangwea
usalama wa kutosha
Umati wa watu waliohudhuria
Vijana wakiimba kwa huzuni kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea


Mwili wa marhemu Albert Mangwea ukiwa kwenye jeneza tayari kwa watu kutoa heshima za mwisho

Umati wa watu wakiwa wamepanga mstari tayari kwa kwenda kuaga huku kikosi cha msalaba mwekundu na polisi kikiwa stand by just incase anything happens. Sasa naskia watu badala ya kwenda na kuaga wao wako busy wanapiga picha kha hizi teknolojia aiseee tutajutaaaa 
Baadhi ya ma super star wa bongo wakiwa kwenye mstari tayari kwa kuaga.

KAMA ULIKUA HUJUI DIAMOND ANA UTAJIRI WA ZAIDI YA BILIONI 1 ZA BONGO, SOMA HAYA MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU DIAMOND.

1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1. d8fdca7eccf211e2a7ed22000a1f8f24_7
2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.
3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.
4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.
6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.
7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.
8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.
9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.
10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk..

Saturday, June 1, 2013

Shindano la QS Queens kufanyika Dar Live Jumamosi

Kutumika pia kama sehemu ya kuomboleza msiba wa Ngwea na kushirikisha wakali kibao kama vile Mb Dog, Madee, Diamond, Nay wa Mitego na wengineo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ONYESHO kubwa ambalo ni uzinduzi wa Shindano la QS Queens 'Utamu Extra' linalotarajiwa kufanyika leo Jumamosi ya Juni Mosi katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, pia limepangwa kuwa sehemu maalum ya kuenzi mchango wa msanii Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini.

Ngwea amepangwa kuletwa  kesho Jumapili kwa ajili ya maziko yake yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro, huku onyesho hilo la maombolezo likihudhuliwa na wakali kibao wa muziki hapa nchini lilioandaliwa kwa muda mrefu na kilele chake kuwa Jumamosi hii.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, jana mchana, Meneja Masoko wa Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment, Freddy Felix, alisema kuwa shindano hilo litafanyika pia katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata warembo 20 watakaoishi katika Jumba moja kwa ajili ya kupata kimwana huyo wa QS Queens.

Alisema kuwa wasanii wengi wamepangwa kupanda jukwaani kwa ajili ya kuomboleza msiba huo, akiwamo Ney wa Mitego, Wanaume Halisi, ikiongozwa na Juma Nature, MB Dog, Diamond, Inspector Haroun, Madee, H-Baba, Snura, Khadija Kopa, Solid Ground Family na wengineo, wakiwamo wasanii chipukizi, Amor na Shalviny.

“Wasichana wote wanaotaka kushiriki shindano hili ambao ni kama uzinduzi wake, watajiandikisha katika fomu maalum ukumbini hapo, ambapo baadaye watatafutwa wengine ambao wote wataishi kwa miezi miwili katika nyumba moja itakayotembelewa na watu mbalimbali.

“Huku mshindi akijishindia gari la kifahari, pia wanapokuwa katika jumba hilo kila siku mtu atalipwa kadri tutakavyokubaliana, huku tukiamini kuwa huu utakuwa ni mwanzo mzuri katika shindano hili,” alisema Felix.

Kwa mujibu wa Felix, shindano hili kabla ya kupatikana warembo hao litatembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara, kama vile Mwanza, Tanga, Morogoro, Mbeya, Iringa na kwingineko kwa ajili ya kutafuta msichana mmoja wa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha QS ilitangaza kuwa mabinti wanaotakiwa kushiriki katika shindano hilo ni wale wenye vipaji maalum na uwezo wowote wa kupambanua mambo, huku kigezo cha elimu kikiwekwa pembeni.

Shindano hilo pia litaonyeshwa katika vituo vya Channel Ten, DTV, Clouds, ambapo huko kote wadau na wapenzi wa mambo ya urembo na burudani watapata fursa ya kuwapigia kura washiriki kabla ya siku ya kilele chake kitakachofanyika baadaye mwaka huu.

CHADEMA: SERIKALI IANDAE UPINZANI KUINGIA IKULU.

MBOWE ASEMA UJENGWE MFUMO MPYA KUSAIDIA CCM KUKABIDHI MADARAKA BILA VURUGU.
SERIKALI imetakiwa kuandaa mfumo wa kikatiba utakaowezesha chama cha upinzani kuongoza iwapo kile kinachotawala kitaondolewa madarakani.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alipokuwa akihutubia mikutano ya kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata za Mpapa, wilayani Momba na Myovizi, Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya.
Alisema kutokana na vuguvugu la siasa za mabadiliko.
 zinazoendelea nchini, ni wakati mwafaka nchi ikawa na mfumo wa kikatiba na sheria kwa ajili ya kusimamia mabadiliko ya uongozi kufanyika kwa amani ili kuepusha nchi kuingia katika vurugu na mkanganyiko wa kisiasa.
Mbowe alisema ingawa hiyo inaweza kuonekana kuwa ni dhana mpya, kutokana na umuhimu wake kwa ajili ya mustakabali mwema wa Taifa, ni vyema Watanzania wakaanza kuitafakari.

Alitola mifano wa Ghana ilivyopitia misukosuko kutoka utawala wa Jerry Rawlings kwenda chama cha upinzani cha Rais John Kufour.
Akiwanadi wagombea wa Chadema katika maeneo hayo, Mbowe alisema ni hatari kwa nchi kama Tanzania ambayo sasa inapitia kwenye wimbi kubwa la mabadiliko, kukosa mfumo huo wa kuhakikisha mabadiliko ya mpito kutoka utawala wa Serikali moja kwenda nyingine yanafanyika kwa amani na kulinda masilahi ya nchi bila vurugu.

“Ni muhimu sana kuwa na sheria itakayohakikisha 'transition' (kipindi cha mpito) kutoka Serikali ya chama fulani kwenda chama kingine au Serikali moja kwenda Serikali nyingine, kufanyika kwa amani na kwa kuhakikisha masilahi ya umma na nchi yanazingatiwa,” alisema na kuongeza:
“Lazima tuepuke hali kama hiyo. 
Wenzetu wale (Ghana) walijifunza, walipoingia madarakani wakaamua kutunga sheria ya kusimamia ‘transition period’ kutoka uongozi wa Serikali moja kwenda nyingine.”
“Watanzania wanaweza kujiuliza kwa nini Marekani inachukua siku 72 kwa Rais kuapishwa na kukabidhiwa rasmi mamlaka ya kuongoza nchi tangu achaguliwe? 
Ni kwa sababu kuna vitu vya muhimu sana vya kusimamiwa na kufanyiwa kazi kabla utawala mpya haujakabidhiwa Ikulu.”
Mbowe alisema hapa nchini upo mfano mzuri wa madhara ya kukosekana kwa sheria ya namna hiyo ya kusimamia kipindi hicho cha mpito.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alidai kwamba sehemu ya mabilioni ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) yalihamishwa kutokana na kukosekana kwa mfumo huo.
Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema wakati Marekani inachukua takriban siku 72 tangu uchaguzi na uongozi mpya kukabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi, Tanzania inachukua wastani wa saa 48 pekee, akisema hali hiyo ni hatari kwa nchi kwani, kuna masuala ya msingi ambayo yanahitaji muda wa kutosha katika kufanya makabidhiano kutoka Serikali moja kwenda nyingine.
“Ni wakati mwafaka kuanza kufikiria kuwa na mfumo huu wa kikatiba na kisheria. 
Huwezi kutumia saa 48 tangu uchaguzi kufanyika kumkabidhi Rais mpya madaraka. 
Kwanza kwa muda huo nani anasimamia kikamilifu rasilimali za umma, nini hatma ya watumishi wa umma. 
Kuna masuala ya majeshi, nyaraka za siri na kila kitu, vitu ni vingi. Wenzetu walio makini na nchi zao wanajua umuhimu wa masuala kama haya. 
Wanapata muda wa kufanya 'orientation' (uelewa wa mazingira), alisema Mbowe na kuongeza:

“Ndiyo maana hapa kuna wakati watumishi wa Serikali wakaamua tu kuikumbatia CCM hata kama nao wameichoka, kwa sababu wanakuwa hawajui hatma yao ni nini kwenye Serikali au uongozi mpya, baada ya uchaguzi. 
“Ghana katika kipindi hicho cha mpito kutoka Serikali moja hadi nyingine wameweka utaratibu wa mamlaka inayoongozwa na mtu ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa anasimamia rasilimali zote, nyaraka zote, zinakuwa zimeandikishwa, zinajulikana zikoje.”
Alisema lazima hatari hiyo izuiliwe kwa kuwa wakati Serikali mpya ilivyoingia Ghana, waliokuwepo madarakani walichoma moto nyaraka muhimu na kuharibu vitu, kitendo kilichosababisha Serikali iliyoingia madarakani kuhangaika kuanza upya.
Alisema kutokana na hali kama hiyo ni lazima wananchi waanze kudai mfumo huo kwani hivi sasa Katiba na sheria ziko kimya kitu kinachoweza kusababisha siku moja mtu akakabidhi ukuta wa Ikulu tu kukiwa hamna kitu ndani.

“Mfumo huo utahakikisha 'smooth exit' yaani wanaoondoka au anayeondoka aondoke kwa amani. Kwa sasa hakuna 'mechanism' (mfumo) yoyote ile, hakuna utaratibu, hakuna sheria, Katiba iko kimya. Tunataka 'smooth exit', 'smooth entry' (Kutoka kwa amani, kuongia kwa amani).”
“Watumishi wa umma wawe na uhakika wa kuwepo kwa Serikali, bila hivyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko kwa sababu tu watawala waliokuwepo hawataki kuondoka.”
Mwenyekiti huyo yuko kwenye ziara ya kuwanadi wagombea udiwani wa chama hicho katika kata mbalimbali za Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Njombe na Iringa, katika uchaguzi mdogo unaohusisha kata 29 nchini ambao umepangwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Haya ndiyo mabishano ya kisiasa yanayoendelea facebook baina ya Ridhiwani,Kimeta,Bananga,Nchemba na Wananchi wengine

Katika post iliyovutia wengi facebook kwajana mida ya usiku ilikuwa nihii iliyokuwa namajibizano ya kisiasa baina ya Ridhiwan Kikwete, Mwingulu Nchemba,Ally Bananga,Kimeta Wa Mpui Na Watanzania Wengine





 
 

 

 
 

RATIBA YA MSIBA WA MAREHEMU NGWAIR

KAMATI INAYOSIMAMIA MSIBA NA MAZISHI YA MAREHEMU ALBERT MANGWEA IKIONGOZWA NA MSEMAJI WAKE MKUU, DIR. ADAM JUMA IMETOA TAARIFA YA MAZISHI YA NDUGU YETU …
Tofauti na ilivyofahamika awali, kuwa marehemu NGWAIR atafikishwa Jumamosi, taarifa hizo zimebadilika … Na hapa chini ni ratiba mpya ya mazishi hayo … Isome hapa :
KAMA KAMATI TUNAOMBA KUTOA TAARIFA KWAMBA MWILI WA NDUGU YETU ALBERT MANGWEA UTAFIKA SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 2/06/2013 SAA NANE MCHANA NA SIO SIKU YA JUMAMOSI KAMA ILIVYOTAARIFIWA HAPO AWALI .
SABABU ZA MWILI WA ALBERT MANGWEHA KUSHINDWA KUFIKA JUMAMOSI KAMA ILIVYOPANGWA NI KUTOKANA WATANZANIA WENZETU WAISHIO AFRIKA KUSINI KUOMBA NA WAO KUTOA HESHIMA ZAO ZA MWISHO .
KWA MAANA HIYO BASI TARATIBU ZOTE ZA KUAGA MWILI WA ALBERT MANGWEHA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM NA MAENEO YA JIRANI ZITAFANYIKA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 03/06/2013 KUANZIA SAA MBILI ASUBUI MPAKA SAA SITA MCHANA , AMBAPO BAADA YA HAPO SAFARI RASMI YA KUELEKEA MOROGORO KWA AJILI YA MAZISHI ITAANZA. TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU WOTE ULIOJITOKEZA ASANTE.

ANGALIA PICHA ZA MAANDALIZI YA MSIBA WA NGWEA YAANZA MBENZI JIJINI DAR.






 

 

 
 
 
 



MAOMBOLEZO ya msiba wa aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya, marehemu Albert Mangwea, yameanza  nyumbanmi kwa baba yake mdogo, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako jana jioni ndugu, jamaa na majirani walikutwa wakiwa katika matayarisho ya kuupokea mwili wa marehemu.