Friday, September 20, 2013


NIKO STUDIO ZA VOICE OF AMERICA ("VOA") JUMAMOSI WASHINGTON DC WAJIANDAE KWA SHOO KALI. By Ommy Dimpoz!


TANGAZAJI MASHUHULI SUNDAY SHOMARI  AKIMWEKA DIMPOZ KITI MOTO.
      POZ KWA POZI AKIJIBU MASWALI YENYE UTATA KUTOKA KWA SUNDAY SHOMARY
          LARY KING WA VOA NAYE ALIMWEKA DIMPOZ KITI MOTO
                                  BABU ALIKUWA ANAULIZA MASWALI YA KUFURAHISHA TU !

       PROMOTER/MANAGER WA DIMPOZ USA TOUR  BWANA "DMK" MWENYE TSHIRT NYEKUNDU AKIFURAHIA JAMBO PAMOJA NA SUNDAY SHOMARY NA DIMPOZ
POZ KWA POZ NDANI YA MITAA YA WASHINGTON DC AKIWA AMECHILL MBELE YA GARI LA PROMOTER/ USA TOUR MANAGER WAKE BWANA DMK


DIMPOZ NA DMK WAKIWA BUSY KWENYE TEXT WAKIPOKEA REQUEST NYINGI ZA TICKET ZA SHOW  CAMERA YA SWAHILI TV AMBAO NDIO WADHAMINI WA DIMPOZ USA TOUR ITAENDELEA KUKULETEA HABARI EXCLUSIVE ZA DIMPOZ AKIWA MITAANI USA. ENDELEA KUSIKILIZA SWAHILI RADIO ONLINE NA KUSOMA 
WWW.SWAHILITV.BLOGSPOT.COM KUWEZA KUJISHINDIA FREE TICKETS.

Angalia Picha za Matajiri 10 wa Marekani kwa mujibu wa Forbes – 2013


bill-gates-600x403
1. Bill Gates – Age: 57; net worth: $72billion
Kwa mara nyingine tena, Bill Gates amekamata nafasi ya kwanza kwa mwaka wa 20 mfululizo kama mtu tajiri zaidi nchini Marekani. Tazama orodha ya Forbes ya watu 10 matajiri zaidi nchini humo mwaka 2013.


2. Warren Buffet- Age: 83, net worth: $58.5 billion
warren-buffett-600x420

3.Larry Ellison – Age: 69; net worth: $41 billion
larry-ellison-600x426

4. Charles Koch – Age: 77; net worth: $36 billion
charles-koch-600x337
5. David Koch – Age: 73; net worth: $36 billion
david-koch-600x401
6.Christy Walton and family – Age: 58; net worth: $35.4 billion
christy-walton-600x380
7. Jim Walton – Age: 65; net worth: $33.8 billion
jim-walton-600x337
8. Alice Walton -Age: 63; net worth: $33.5 billion
alice-walton

9. S. Robson Walton – Age: 69; net worth: $33.3 billion

s-robson-walton-600x400
10.Michael Bloomberg – Age: 71; net worth: $31 billion
michael-bloomberg-600x401

wasanii na viingilio vyatajwa Miss TZ


Na Mwandishi Wetu
WAKATI zikiwa zimebaki siku tatu ili Redd’s Miss Tanzania ajulikane, viingilio kwa ajili ya shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi vimetangazwa.
 
Kiingilio cha juu katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa (Jumamosi) katika Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ni Sh 100,000 kwa viti maalumu, huku viti vya kawaida vikiwa Sh 50,000.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro, ambao ndio wadhamini wakuu wa Redd’s Miss Tanzania alisema, wanaamini viingilio hivyo ni vya kawaida kutokana na ubora wa shindano lenyewe.
 
Victoria alisema, burudani katika shindano hilo inatarajiwa kutolewa na msanii mahiri kutoka Uganda, Mike Ross atakayeshirikiana na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ pamoja na kundi la Mama Afrika katika kukonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza ukumbini hapo.
 
“Tunaamini kabisa wasanii hawa watakonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya urembo hapa nchini, hivyo napenda kutoa wito kwa mashabiki kujinunulia tiketi mapema ili kuepuka usumbufu,” alisema Victoria.
 
Naye Lady Jadee alisema, kwa kushirikiana na bendi yake ya Machozi wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki wote watakaohudhuria.
 
“Nawaomba mashabiki wangu na wale urembo kujitokeza kwa wingi ili kufurahia burudani nzuri toka kwangu na bendi yangu ya Machozi, pia wasanii wenzangu waalikwa naamini watafanya vizuri siku hiyo,” alisema.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashimu Lundenga ambao ni waratibu wa Redd’s Miss Tanzania alisema, tiketi za shindano hilo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 
Alitaja maeneo ambayo yameteuliwa kuuza tiketi za Redd’s Miss Tanzania kwa mwaka huu ni duka la Shear Illusion lililopo Mlimani City, City Sports Lounge na Steers zilizopo Mtaa wa Samora, Faberk Fashion, Rose Garden Pub na ofisi za Redd’s Miss Tanzania ambazo zote zipo eneo la Mikocheni.
 
“Kwa mara nyingine tena napenda kuwashukuru wadhamini wetu wakuu  kinywaji cha Redd’s Original na wadhamini wenza ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa sana kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa zuri na lenye tija kubwa.”
 
Lundenga alifafanua kuwa, ili kuwapa fursa watu wengi zaidi tiketi itakayonunuliwa katika vituo vilivyopangwa kabla ya shindano itakuwa ni Sh 80,000 na kutakuwa na ofa kadhaa.
 
Taji la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred, aliyefanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
 
Shindano la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku wadhamini wenza wakiwa kinywaji cha Zanzi, hoteli ya Giragge, Star TV, gazeti la Nipashe, Uchumi Supermarket na Marie Stopes.

ANGALIA PICHA WEZI WA MTANDAO WAKAMATWA KATIKA OFISI ZA TIGO BUGURUNI


 

Mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na  kutaka kuja kurudisha line ambayo sio yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi za tigo buguruni rozana 
Huyu ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyu mwanamke kutumia kitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandao
Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani 
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi  na hawafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi
Watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baaada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa matapeli haya ya kimtandao 
Hiki ndicho kitambulisho alichokitaka kutumia huyu mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi lakini sura yake bahati mbaya kwa umakini wa mfanyakazi mmoja wa tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi  mara moja 
Aliyesimama hapo yeye aliibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa alirudisha namba na kuiba pesa 
Hiki pia ni kitambulisho  cha mteja huyo hapo juu  aliyeibiwa pesa kwenye acount yake ya NMB kiasi cha milioni moja kwa njia ya NMB Mobile baada ya mmoja wa hawa watuhumiwa  kuja kurudisha laini yake kwa kutumia kitambulisho hiki ambacho kimetengenezwa kwani si halisi na hatimaye kufanikiwa kuiba pesa kwa sim banking baadae 
Hapa mtuhumiiwa mmoja akiwa amejilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi waliowaweka chini ya ulinzi 
Hapa huyu binti akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe
Wakiwa ndani ya gari ya polisi kuelekea kituo cha polisi Buguruni
Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake 
Mmoja ya wafanyakazi mahiri wa tigo Bw Octavian Rweyendera ambaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya maafande wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa kimtandao 
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa. 
 
PICHA NA HABARI NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 20. 09. 2013.



WILAYA YA  ILEJE  -  AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA KUSABABISHA 
                                     KIFO NA MAJERUHI.

MNAMO TAREHE 19.09.2013  MAJIRA YA  SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDOLA WILAYA YA ILEJE  MKOA WA MBEYA. GARI STK 5485 AINA YA TOYOTA HILUX MALI YA  HALMASHAURI YA  WILAYA YA  ILEJE IDARA YA  UJENZI LIKITOKEA KIJIJI CHA ITALE KUELEKEA ITUMBA  LIKIENDESHWA NA  DEREVA VICENT S/O SCOT, MIAKA 35, MUHA, MKAZI WA ITUMBA  LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI  YENYE NAMBA T. 367 BTB AINA YA T-BETTER    AITWAE CHONDE S/O MWASIMIAKA 32, MNDALI,  MKAZI WA ITUMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI ANAPELEKWA HOSPITALI KWA MATIBABU PIA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE WAWILI MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA  AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA  RUFAA MBEYA.  CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 



WILAYA YA MBOZI  - AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA  SAA 17:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SELEWA BARABARA YA  MBEYA/TUNDUMA  WILAYA YA  MBOZI  MKOA WA MBEYA. GARI T. 598 BTK  AINA YA FUSO TIPPER LIKIENDESHWA NA  DEREVA JAPHET S/O MWASHIUYA, MIAKA 21, MNYIHA, MKAZI WA ILEMBA - VWAWA  LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA BAADA YA  GURUDUMU LA MBELE UPANDE WA KUSHOTO KUPASUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA  MATOKEO S/O STEVEN MWASHIUYA MIAKA 27, MNYIHA,MKULIMA   MKAZI WA ISANGU PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE WATANO AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA  SERIKALI WILAYA YA  MBOZI.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO, GARI LIPO ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIOA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA  ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE  MWENYEWE MARA MOJA.


WILAYA YA  MBEYA MJINI  - KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA  SAA 20:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA MAKUNGURU  JIJI NA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA GREGORY S/O JOHN, MIAKA 20, KYUSA, MKAZI WA MAKUNGURU  AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 2. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE KIBANDA CHAKE CHA BIASHARA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

WILAYA YA  CHUNYA  - KUPATIKANA NA BHANGI.


MNAMO TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA  SAA 14:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MTANILA WILAYA YA  CHUNYA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA STAFORD S/O SOMBAMIAKA 26, MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA MTANILA   AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 1. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO NDANI YA  NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.


Signed by:

                                                      [ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Rais Kikwete kutunukiwa Shahada ya Uzamivu leo



 

Jakaya-Mrisho-Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Septemba 20, 2013, anatunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph cha Canada kwa kutambua mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.          
Viongozi wa Chuo hicho wanasema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania na Afrika.

Rais Kikwete ambaye amewasili hapa usiku wa jana, Alhamisi, Septemba 19, 2013 akitokea Washington, D.C., Marekani ambako alikuwa kwa siku mbili akitokea Jimbo la California atakuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa shahada ya juu kabisa katika historia ya Chuo hicho.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
Chuo hicho ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na ubora wa shughuli zake za utafiti kimekuwa katika mstari wa mbele kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili dunia katika masuala ya kilimo, raslimali za maji, matatizo makubwa ya magonjwa ya mimea, matatizo ya ukuaji haraka wa miji duniani na changamoto za biashara za kimataifa.
Katika miaka ya karibuni kufuatia tishio kubwa kimataifa la ongezeko la bei za vyakula duniani na hasa katika nchi masikini, mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama duniani, kazi ya Chuo hicho imeongezeka sana.
Chuo hicho kimeichagua Tanzania kama nchi ya kufanya nayo kazi katika Afrika kukabiliana na changamoto hizo na kimemtambua Rais Kikwete kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo katika miaka yote ya uongozi wake na mipango yake ya kuboresha kilimo katika Tanzania kama ASDP, Kilimo Kwanza na SAGCOT ambayo yote inasifiwa sana kimataifa.
Chuo hicho kina mahusiano ya karibu na Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na UDOM – Dodoma. Kati ya mwaka jana na mwaka huu, Chuo hicho kimetiliana saini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mara nne kati ya Januari, mwaka jana, 2012 na Juni, mwaka huu, 2013, uongozi wa Chuo hicho ukiongozwa na Rais na Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Alastair Summerlee na Makamu wa Rais wa Utafiti Dkt. Kevin Hall umetembelea Tanzania na kukutana na viongozi wa Serikali pamoja na wale wa Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam na Sokoine cha Mzumbe, Morogoro.
            Mbali na ujumbe ambao unaongozana na Rais Kikwete, sherehe za kutunukiwa kwa Kiongozi Mkuu huyo wa Tanzania pia zitahudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Jumuia ya Watanzania wanaoishi Canada pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Wednesday, September 18, 2013

TAZAMA PICHA JINSI MAMBA ALIVYO ZUA BALAA BAADA YA KUINGIA CHINI YA KITANDA HOTELINI


Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8.



Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.





Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.





Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe alilala naye kwenye chumba hicho usiku mzima.



Mamba ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr Whittall.



Na huweza kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.



Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.







TAZAMA PICHA JINSI MAMBA ALIVYO ZUA BALAA BAADA YA KUINGIA CHINI YA KITANDA HOTELINI


Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8.



Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.





Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.





Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe alilala naye kwenye chumba hicho usiku mzima.



Mamba ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr Whittall.



Na huweza kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.



Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.







DUNIA INAISHA:::HUYU NDO MSANII WA NYIMBO ZA INJILI ALIYEJITANGAZA KUWA YEYE NI SHOGA


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Jijini Nairobi,Kenya,George Barasa maarufu kama Joji Baro amejiatangaza kuwa yeye ni shoga.Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akizungumza na mtandao mmoja wa nchini humo alisema kuwa alizaliwa Jijini Nairobi na baadaye kuhamia Bungoma miaka michache baadaye. 

 Aidha ameongeza kuwa pamoja ya kuwa ni shoga pia ameathirika na ugonjwa hatari wa Ukimwi pia ni mwanaharakati wa kutetea Haki za Mashoga na Wasagaji na wana zaidi ya wanachama 2,800,Ambao wote ni mashoga na wasagaji ambapo vijana idadi yao 15 na watu wazima ni 68.
Alisema kuwa aliamua kuhamia Mjini EMBAKASI BAADA YA FAMILIA yake kumtenga alipojuliakana anajihusisha na vitendo hivyo.

Alipokuwa anasoma shule ya Mtakatifu Paulo Miluki High School ndipo alipoanza kujifunza vitendo hivyo vya ushoga na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki.

Machi 11, 2012 , Madaktari walimpima na kugundulika kuwa ni mwathirika wa VVU / UKIMWI na kwamba amedai kuwa kwenye muziki wa INJILI amekuwa akipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanamuziki mwenzake wa muziki huo.
Anasema amechoka kuhukumiwa na kuonewa huku akinyanyapaliwa na watu wengine baada ya kugundulika kuwa nafanya vitendo hivyo.

‘Mimi ni binadamu,Kama binadamu yeyote naumia sana ninavyonyanyapaliwa,’alisema Barasa.

Anasema kwenye masuala ya urembo hayuko nyuma ana mawigi 15 na zaidi ya pea za viatu virefu ‘High hills’30.
‘Napenda sana urembo na pia naandika kitabu cha maisha yangu kiitwacho "Dream Boy"ambacho kitaeleza historia nzima ya maisha yangu na jina la albanu yangua ya injili inaitwa "Bora Siku"alisema Barasa.

‘Namtumikia Mungu na natumaini Mungu anakubali utumishi wangu,’alimalizia Barasa

SIMULIZI ZA MTU MZIMA GURUMO::NILIFUMANIWA NA MKE WA MTU NA NILITUMIAGA SIGARA KUBWA (BANGI)




SIKU chache baada ya kustaafu muziki, mwanamuziki mkongwe nchini, Maalim Mohamed Gurumo ‘Mzee Gurumo’ amekiri kupitia maisha mabaya ujanani ikiwemo kufumaniwa na mke wa mtu pamoja na uvutaji wa ‘sigara kubwa’ Ijumaa linaanika.

Akizungumza katika mahojiano na Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Runinga ya East Africa chini ya Mtangazaji, Salama Jabiri mwanzoni mwa wiki hii, Gurumo alisema miongoni mwa mambo mabaya ambayo hawezi kuyasahau maishani mwake ni pamoja na hayo.


KUFUMANIWA:
Katika sakata hilo, Gurumo alisema kuwa ilikuwa ni mwaka 1961 ambapo alikuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye aligoma kumtaja, ndipo siku moja wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ‘wakiponda kirauli’ ghafla walisikia hodi na ndipo mwanamke huyo alipomwambia kuwa anayegonga mlango ni mumewe.
“Niliogopa sana, ikabidi nijibanze nyuma ya mlango, alipoingia tu nikatimua mbio kali sana, lakini hakujua kama ni mimi,” alisema Gurumo.
Kuhusu uvutaji wa bangi, Gurumo alikiri kuwahi kuonja kilevi hicho ujanani mwake ambapo alibainisha kuwa alishawishiwa na mwimbaji mwenzake maarufu sana kwa wakati huo.


Alisema siku ambayo alivuta sigara kubwa, alipofika nyumbani baada ya kutengewa chakula, alimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa akidhani ni mchuzi.
“Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu, nilivuta kutokana na ushawishi, baada ya kufika nyumbani, wakati wa chakula nilimega ugali na kuchovya kwenye maji ya kunawa, nikasema mbona mchuzi hauna ladha nzuri, lakini baadaye nilijutia sana,” alisema Gurumo na kuongeza:
“Nimepitia maisha ambayo si mazuri sana ujanani, lakini yote hayo ni mapito na imebaki kama historia tu kwangu, namuomba Mungu anisamehe kwa hayo,” alisema Gurumo.

Monday, September 9, 2013

Zaidi ya abiria 280 wanusurika kifo katika ajali ya ndege



BANGKOK (AP) — Ndege ya abiria ya Thai Airways ikiwa imebeba zaidi ya abiria 280 imepata ajali wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Bangkok na kujeruhi watu 14
Muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea wafanyakazi wa ndege hiyo walilazimika kuondoa nembo (logo) ya ndege hiyo upande wa mkia na ubavuni ikiwa ni hatua ya kulinda hadhi yake na kutojichafulia jina
Ndege hiyo Airbus A330-300 ilikuwa ikitokea Guangzhou, China na ilipata hitilafu kwenye matairi wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege jana usiku, na kwamba abiria wote waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.
CHANZO TABIANCHI BLOG