Saturday, October 5, 2013

MSANII OMY DIMPOZ ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI



Omar Nyembo aka Ommy Dimpoz, jana alipata fursa ya kukutana na balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bi. Lebarata Mulamula kwenye ubalozi wake uliopo mjini Washington DC, Marekani.
IMG-20131003-WA001
Ommy Dimpoz akiwa na balozi Mulamula ambaye amekuwa balozi wa pili wa kike kuiwakilisha Tanzania nchini Marekani, baada ya Mwanaidi Maajar

IMG-20131003-WA000
Ommy Dimpoz, Balozi Mulamula na maafisa wengine katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

“Niliongea naye mambo mengi kuhusu muziki wa Bongo Flava na vijana tunavyotumia fursa na vipaji vyetu kujiajiri,” Ommy ameiambia Bongo5.
IMG-20131003-WA003
Ommy Dimpoz akiangalia picha za waliowahi kuwa mabalozi wa Tanzania nchini Marekani

IMG-20131003-WA002
Ommy akiwa na Bi. Mulamula ambaye kabla ya uteuzi huo, aliwahi kuwa Msaidizi Mwandamizi wa Rais katika masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Kwanza kuiongoza Sekretarieti ya Nchi za Maziwa Makuu kwa kipindi cha miaka minne kuanzia Januari, 2007 hadi Desemba, 2010
 
IMG-20131003-WA004


Ommy Dimpoz akisaini kitabu cha wageni kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
 
IMG-20131003-WA005

Ommy Dimpoz akiwa kwenye mazungumzo na Balozi Mulamula pamoja na maafisa wengine wa ubalozi huo

IMG-20131003-WA011
Ommy, Bi. Mulamula na Mkurugenzi wa MMK Media Group LLC , Dickson Mkama aka DMK

Wakati huo huo, Ommy aliyeenda nchini humo kwa ziara ya wiki tatu, amerekodi wimbo kwenye studio ya Xtrem Recs ya Houston, Texas ambapo producer ni Giggz kutoka Kenya.
IMG-20131003-WA008
Ommy akiwa kwenye studio za Xtrem Recs

IMG-20131003-WA009
Giggs ambaye Ommy amesema amefanya kazi na wasanii wakubwa kama Davido, Wizkid na Tuface

TAZAMA PICHA ZA KIJANA ALIYEPEWA ADHABU YA KUOSHA GARI LA ZIMA MOTO MBEYA,BAADA YA KUPIGA SIMU YA UONGO AKISEMA MOTO UNAWAKA.



Mmoja wa wakazi wa Rugelele kata Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya  DUKA MKWILA[20]ni miongoni mwa wananchi waliopiga simu za uongo katika kikosi cha zimamoto mkoa wa mbeya akiwa amepewa adahabu ya kuosha gari la zimomoto




Hata hivyo DUKA alikiri kutenda kosa na kuomba msamaha kwa jeshi hilo ambapo aliachiwa huru na kisha kurejea kwao huku akijutia kosa alilolifanya na kuahidi kutorudia tena.





JESHI la zimamoto na uokoaji limewataka wananchi kuacha matumizi mabaya ya miito ya simu ya dharula kwa Jeshi hilo ili kuepusha usumbufu kwa Jeshi pindi wanapopigiwa simu za dharula.

Wito huo umetolewa na Jeshi hilo baada ya kupata kero za mara kwa mara kutoka kwa wananchi wanaopiga simu kwenye Jeshi hilo wakihitaji huduma za gari hilo lakini wanapofika eneo waliloelekezwa wanakuta hakuna tukio lolote.
Wamekuwa wakipokea simu nyingi za uongo hivyo serikali kuingia gharama kubwa za mafuta ambayo yangetumika kwenye maafa pindi yanapotokea.

Mmoja wa wakazi wa Rugelele kata Rujewa wilaya ya MBARALI DUKA MKWILA[20]ni miongoni mwa wananchi waliopiga simu za uongo katika Jeshi hilo mara kadhaa na kuomba huduma nyingine badala ya ajali ya moto hali iliyofanya Jeshi hilo kumkamata na kumhoji.
DUKA amesema yeye namba hiyo alipewa na mtu mwigine aliyedai kuwa mwenye namba hiyo huwa anatoa pesa za FREE MASON pia dawa za kienyeji kwa matatizo mbalimbali.

Hata hivyo DUKA alikiri kutenda kosa na kuomba msamaha kwa jeshi hilo ambapo aliachiwa huru na kisha kurejea kwao huku akijutia kosa 
alilolifanya na kuahidi kutorudia tena

Na Mbeya yetu

Kenya - Bila usalama Somalia, hatutoki !



President-Uhuru-Kenyatta3_9e43d.jpg
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa majeshi ya Kenya yataendelea kukaa Somalia hadi usalama utakapoimarishwa katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya miaka mingi.
Rais Kenyatta amesema kuwa nchi yake haitashurutishwa na magaidi walioteka jengo la maduka la Westgate kwa siku 4.
Rais Kenyatta alihutubia umati uliokusanyika kwa maombi ya pamoja ya dini mbali mbali, kwa ajili ya watu 67 waliouawa katika shambulio la Westgate.
Shambulio hilo ndio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Kneya tangu majeshi yake yaingie nchini Somalia mwaka wa 2011.
''Hawa wauaji waliokuja kutenda ukatili wao ulio na woga hapa nchini kwetu, walikuwa wanadai kuwa wanafanya hivyo kwasababu majeshi ya Kenya yapo nchini Somalia. Nataka niwaeleze bayana kuwa, majeshi yetu yatakaa huko hadi kuwepo amani katika nchi hiyo.''
Mmoja wa makasisi walioongoza maombi hayo, alisema,'' Baba tunakuomba utawale nchi hii. Na uwaoneshe maadui wote wa taifa hili kuwa wewe unaipenda nchi hii na jina lako litatukuzwa.''
Wapiganaji hao wa Al Shabaab wamesema kuwa walifanya shambulio hilo kulipiza kisasi kwa namna majeshi ya Kenya yaliingia na kuwapiga nchini Simalia.
Rais Kenyatta pia ametangaza kuwa serikali itaunda tume maalum kuchunguza upungufu mkubwa uliojitokeza kwa vyombo vya usalama kufuatia shambulio la Westgate.
''Tutaunda pia tume maalum kuangalia ni wapi tulikosea, ili tujirekebishe kuendelea mbele. Tuone ni wapi kumetokea upungufu na ni vipi tutarekebisha.''
Ushirikiano
Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya Raila Odinga, alikuwa miongoni mwa waliohudhuria maombi hayo. Bwana Odinga ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuisaidia Kenya kukabili ugaidi.
Aliongeza kuwa ni makosa kwa mataifa ya magharibi kutoa tahadhari kwa raia wao kutotembelea Kenya huku kwa upande mwingine zikishinikiza Kenya kufayia mabadiliko idara zake za usalama.
Bwana Odinga amesisitiza kuchukuliwa hatua za kuimarisha usalama nchini Kenya.
''Shambulio hili ni ishara kuwa tunaingia katika makabiliano makali zaidi. Ni lazima tubadilishe mbinu zetu za kukusanya intelijensia na uharaka wa kuchukua hatua. Ni lazima pia tuweke adhabu kali kwa maafisa wanaolinda mipaka yetu ambao wanakubali mlungula na kuruhusu maadui kuingia nchini na kutuumiza.''
Mwandishi wa BBC anasema kuwa wakenya walivyojitokeza kwa wingi, walitaka kuonesha ishara ya utangamano wa dini mbali mbali licha ya tofauti za imani.
Wiki moja baada ya shambulio la Westgate kumalizika, watu 39 wameripotiwa kutoweka.

Wednesday, October 2, 2013

FALLY IPUPA ATOA MSAADA WA AMBULANCE 'MERCEDES-BENZ' MJI WA GOMA, KUPITIA FALLY IPUPA FAUNDATION'WASANII WA TZ TUIGE MIFANO HIYO.



Mwanamuziki huyu amekuwa akijitahidi kutoa misaada mbalimbali nchini kwake pamoja ya kwamba amehamishia makazi yake Paris, Ufaransa.
Miezi ya hivi karibuni alitoa pia misaada mbalimbali kwenye kituo cha watoto yatima cha Matumayini cha nchini humo na kupiga nao picha kwa lengo la kuwafariji.MSANII wa muziki wa dansi wa nchini Kongo,Fally Ipupa ametoa msaada wa gari la wagonjwa(ambulance)katika Mji wa Goma,Kongo kupitia mfuko wake wa Fally Ipupa Faundation(FIF).
Mwanamuziki huyo amekuwa akijitahidi kutoa misaada mbalimbali nchini kwake pamoja ya kwamba amehamishia makazi yake Paris,Ufaransa.

-

Tuesday, October 1, 2013

TAZAMA VIDEO YA HAWA JAMAA WAMEWEKA REKODI KWA KULALIA MISUMARI



Hii ni record ya hatari sana iliyowekwa na hawa vijana kutoka nchini India. Walifanikisha kuingizwa katika Record za Dunia Hii Baada ya kufanikisha zoezi Moja lakulalia Misumari mirefu kwa Muda kadhaa, Pamoja na maumivum makali waliyoyapata lakini walifanikisha adhma yao ya kuingizwa katika REecord ya Dunia zinazotambulika kama GuinnessWorldRecords

Bofya hapa kuona Watu hawa!

HUZUNI::MUME AMUUA KIKATILI MKEWE KWA KUTUMIA KISU HUKO MANZESE BAADA YA KUMTUHUMU KUWA ANAMSALITI....!!



 KWELI huu ni unyama wa wanaume hata kama si wote! Wanawake wawili wakazi wa maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, wamepoteza maisha kufuatia madai ya kuuawa na waume zao. Inauma sana na Uwazi ndilo lenye mkasa mzima!
Matukio yote mawili yametokea jijini Dar es Salaam na kuacha vilio kwa ndugu na jamaa wakiwa hawaamini kilichowakumba wapendwa wao. 

WALIOTENDWA
Wanawake waliojulikana kwa majina ya Mwanahamisi na mwenzake Waisiko Robert Mtundi ndiyo waliodaiwa kuuawa na waume zao, kisa kikubwa kikidaiwa ni hofu ya wanaume hao kusalitiwa katika mapenzi.

WANAODAIWA KUTENDA
Juma Shaban, mkazi wa Manzese Kwamfuga Mbwa na Samuel Gesire Mlimi, mwenye makazi yake Msongola, maeneo yote hayo yapo Dar ndiyo wanaodaiwa kutekeleza ukatili huo wenye kutoa machozi mpaka basi.

MWANAHAMISI ALIVYOUAWA
Ilikuwa saa tatu usiku, Septemba 21, mwaka huu, kila familia ya eneo la Kwamfuga Mbwa ilikuwa ndani kwa chakula cha usiku au maandalizi ya kulala, ndipo waliposikia zogo kutoka ndani ya chumba cha kwa wanandoa hao.

ZOGO NA MANENO
Kwa mujibu wa majirani hao waliozungumza na gazeti hili baada ya tukio, zogo hilo liliambatana na maneno ya shutuma kutoka kwa Juma kwamba mkewe huyo si mwaminifu ndani ya uhusiano wao.
Majirani walisema shutuma za Juma ziliambatana na kelele za Mwanahamisi kuomba msaada akisema ‘nauawa jamani! Nauawa mwenzenu!’
Wakasema baada ya kama saa moja ya mzozo ulipita ukimya, ndipo kila jirani alitoka nje na kuulizana nini kinaendelea ndani ya chumba cha Mwanahamisi na mumewe!
Baada ya dakika kumi, tulimwona Juma akitoka chumbani kwake huku akiwa anabofyabofya simu yake ya mkononi na kutokomea kusikojulikana,” alisema jirani mmoja huku macho yakiwa yamevimba kwa sababu ya kumlilia Mwanahamisi ambaye wakati huo alikuwa chini ameshakata roho.
Akaendelea: “Baada ya Juma kuondoka tulipatwa na wasiwasi, tukaenda kumwangalia Mwanahamisi chumbani na kumkuta hajitambui, amelala kifudifudi, ana majeraha sehemu mbalimbali za mwili huku akiwa ametapakaa damu. Alikuwa akipumua kwa mbali.
“Alikuwa hawezi kuongea vizuri, mimi nilimsikia akisema hana uhai tena, tumwombee mtoto wake. Ndani ya chumba tuliona viroba vya pombe kali na kisu kikiwa kimelowa damu, nahisi ndicho alichotumia Juma kufanyia ukatili wake.
“Tuliamua kumwahisha hospitali Mwanahamisi lakini kutokana na hali yake tuliona ni vizuri kuwasiliana na polisi ambao walifika baada ya muda.
“Lakini siku yake Mwanahamisi ilitimia kwani wakati polisi wakijiandaa kumchukua kumkimbiza hospitali aliaga dunia.”

KUMBE NI MWEZI MMOJA BAADA YA KUHAMIA
Wengine waliozungumza na gazeti hili siku ya tukio huku wakitoa machozi, walisema Juma ambaye alitoroka baada ya ukatili huo, alihamia kwenye nyumba hiyo mwezi mmoja nyuma lakini walipata umaarufu mtaani hapo kutokana na tabia yao ya kupigana mara kwa mara.

MJUMBE WA MTAA NAYE ANENA
Akizungumza na gazeti hili katika eneo la tukio, Mjumbe wa Nyumba Kumi, Techla Tesha aliwalaumu majirani na wapangaji wa nyumba hiyo kwa kushindwa kumpelekea taarifa mapema huku wakijua mtuhumiwa alikuwa na tabia ya kumpiga mkewe mara kwa mara.

WAISIKO ALIVYOUAWA
Awali ya yote, inadaiwa Waisiko ni mke mkubwa, mke mdogo jina lake halikupatikana mara moja.
Siku ya tukio, saa tatu usiku inadaiwa Samuel alikwenda nyumbani kwa Waisiko ambapo si mbali sana na nyumbani kwa mke mdogo na kuangusha timbwili zito.
“Samuel aliingia ndani na kuanza kumpiga mkewe mkubwa huku akionya majirani kuwa asiwepo mtu wa kwenda kuamua ugomvi wao.
“Sisi kama majirani tuliogopa kwa sababu Samuel alikuwa akitishia kuwa atakayeingia atamchoma kisu.
“Licha ya vitisho hivyo, tulisimama nje ya chumba chao huku vitisho vikiongezeka lakini namna ya kutoa msaada tulishindwa. Hatukujua chanzo cha ugomvi wao.
“Kauli za mwanamke kila wakati ziliashiria alichokuwa akitendwa kwa wakati huo, mfano kuna wakati tulimsikia akisema anavunjwa mgongo, akasema anang’olewa kucha. Pia kuna muda alilalamikia kuvunjwa mkono. Jamani, marehemu aliteswa sana kabla ya kufariki dunia,” alisema shuhuda mmoja.

NI MATESO YA USIKU KUCHA!!
Shuhuda huyo aliongeza: “Mateso ya mwanamke huyo huenda yalikuwa ya usiku kucha kwani nakumbuka mpaka alfajiri ndipo tukasikia sauti ya mwisho ya Waisiko akisema Samuel umeshaniua,  nimalizie kabisa basi. Baada ya hapo hatukusikia tena sauti wala vurugu.

SERIKALI YA MTAA YAZUNGUMZA
Makamu Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msongola, Juma Chacha alipohojiwa kuhusiana na mauaji hayo, alisema ana taarifa lakini mtuhumiwa alikimbia baada ya kutenda unyama huo na anatafutwa na polisi.

UWAZI LABAINI KISA
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa mapenzi kwani ilidaiwa kuwa Samuel alikuwa akimhisi mkewe huyo kutoka nje ya ndoa.
Chanzo chetu kilisema siku ya tukio, Samuel aliwachukua baadhi ya marafiki zake na kwenda nao baa ambako aliwaambia kuwa anahisi mkewe huyo ana jambo kwani akimuuliza kitu anamjibu jeuri.
Mtoa habari wetu alisema Samuel akiwaambia marafiki hao kwamba siku hiyo akirudi nyumbani, mwanamke huyo atamtambua.

POLISI WALIVYOIKUTA MAITI
Polisi walipofika na kuichunguza maiti waliikuta imevunjwa mkono wa kushoto na kung’olewa kucha za miguu huku uti wa mgongo nao ukiwa umevunjika.
Habari zinasema mara baada ya mtuhumiwa kufanya mauaji hayo, alikwenda kwa mkewe mdogo na kumtaka akamuone mke mwenzie, alipokwenda yeye nyuma akatoroka.
Polisi Mkoa wa Ilala tayari wamemfungulia jalada mtuhumiwa huyo lenye namba STK/RB/10058/2013 MAUAJI.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, ACP Marietha Minangi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo.

MBUNGE LEMA, AFUTIWA MASHITAKA YAKE YA UCHOCHEZI CHUO CHA UHASIBU ARUSHA



Godbless-Lema-ArushaNA FULLSHANGWE
Mahakama ya hakimu mkazi imefuta kesi iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la Arusha Goodbless Lema na kudai kuwa upande wa mashitaka hakuwa na nia ya kuendeleza kesi hiyo.
Aidha kesi hiyo iliyokuwa inamkabili mbunge huyo ilikuwa ni ya uchochezi  katika chuo cha uhasibu Arusha ambapo vurugu hizo
zilisababisha chuo hicho kufungwa.
Pia kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo  mbele ya Hakimu Devotha Msofe wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ili kuweza kuitolea
ufafanuzi zaidi.

Hataivyio mara baada ya hakimu huyo pamoja na Jopo la mawakili kuingia mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi Njiro, aliiomba mahakama kesi hiyo ifutwe chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kama ilivyorekebisha 2002.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa upande wa mashitaka uliona hauna haja wala tija ya kuendelea na kesi hiyo lakini pia ni vema kama kipengele
cha sheria kikaangaliwa zaidi.
Pia mara baada ya ombi hilo mahakama iliridhia na kudai kuwa kuanzia sasa Mbunge huyo yupo huru kwa mujibu wa kifungu cha sheria.
 “kwa mujibu wa kifungu cha sheria kuanzia sasa Lema upo huru”aliongeza hivyo. Awali Akisoma maelezo ya awali Julai 10 mwaka huu mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Elianenyi alidai Aprili 24 mwaka huu, Lema akiwa eneo la Freedom Square la IAA alifanya kosa la uchochezi wa kutenda kosa kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu.
Akifafanua shtaka hilo, Elianenyi, alidai kuwa Lema aliwaeleza wanafunzi wa chuo hicho ambao walikuwa wamekusanyika kufuatia kuuawa
kwa mwenzao na watu wasiojulikana kuwa;
Upande wa mashtaka tayari ulikuwa umewaleta mashahidi watano ambao ni Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Giles Mroto, Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi, Inspekta wa Polisi Bernard Nyambalya, Jane Chibuga na Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha, John Joseph Nanyaro.

Mkenya aliyedaiwa kumteka Dk Ulimbokwa atozwa faini Tsh 1,000/-


fain_269e9.jpg

Mkenya Joshua Mulundi aliachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh1,000 kwa kupatikana na hatia ya kuidanganya polisi kuwa alihusika kumteka na kumjeruhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini hiyo. Mulundi alilipiwa faini hiyo na Mwandishi wa Habari wa Redio Times, Chipangula Nandule.
Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka kusoma maelezo ya awali na mshtakiwa huyo kukiri alitoa taarifa ya uongo kwa polisi kuhusu tukio hilo.
Kabla ya hukumu hiyo, Mulundi aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa hilo lilikuwa kosa lake la kwanza. Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na kupelekwa Dar es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi kufika.
Alisema kutokana na kutekwa huko alichanginyikiwa hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa aliyemteka alikuwa na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.
"Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho hivyo, nilikwenda Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye eneo la Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na kuungama kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande," alisema Mulundi na kuongeza:
"Siwalaumu Serikali, upande wa mashtaka wala polisi kwa kitendo cha kuniweka gerezani kwa muda mrefu, najilaumu mimi mwenyewe."
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Kweka aliiambia Mahakama kuwa hana kumbukumbu za uhalifu za mshtakiwa lakini aliomba apewe adhabu kali kutokana na mazingira ya tukio hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Katema alisema alifikia uamuzi huo kwa kuzingatia maombi ya mshtakiwa ya kupunguziwa adhabu.

LEO ULAYA MOTO, ARSENAL, CHELSEA, BARCA, DORTMUND, NAPOLI, AC MILAN…!!!


zzzzzchampions_league_wallpaper_2012_13-1203186_1d0c2.jpg

RAHA NI ARSENAL v NAPOLI, STEAU v CHELSEA, PORTO v ATLETICO, CELTIC v BARCA!
MECHI za Pili za Makundi E hadi H zipo Dimbani leo huku Chelsea wakiwa Ugenini wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kutandikwa katika Mechi yao ya kwanza, Arsenal wapo Emirates na mtanange mkali sana na Napoli huku Vigogo Barcelona, bila ya Supastaa Lionel Messi, wakiwa Ugenini Uwanja wa Celtic Park ambako Msimu uliopita walinyukwa.
PATA TAARIFA ZAIDI:
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumanne 1 Oktoba 2013
[Saa 1 Usiku]
Football Club Zenit v FK Austria Wien
[Zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku]
FC Basel 1893 v FC Schalke 04
FC Steaua BucureÅŸti v Chelsea FC
Borussia Dortmund v Olympique de Marseille
Arsenal FC v SSC Napoli
FC Porto Club v Atlético de Madrid
AFC Ajax v AC Milan
Celtic FC v FC Barcelona

KUNDI E
Basle v Schalke
Basle, ambao walifika Nusu Fainali ya EUROPA LIGI Msimu uliopita, wameanza Kundi hili kwa kishindo kwa kuitwanga Chelsea 2-1 huko Stamford Bridge kwa Bao za Mohamed Salah na Marco Streller na huo ukawa ushindi wa kwanza kwa Klabu za Uswisi Nchini England katika Mechi 20.
Mara ya mwisho Basel kukutana na Klabu ya Germany ni kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL Msimu wa 2011/12 na kuchapwa 7-0 na Bayern Munich.
Basel ndio wanaongoza Ligi ya Uswisi lakini kwenye Mechi yao ya mwisho walitoka Sare 2-2 na Sion.
Schalke walishinda Mechi yao ya kwanza ya Kundi hili kwa kuichapa Steaua Bucharest 3-0 lakini kwenye Bundesliga wapo katikati kwenye Msimamo na Jumamosi iliyopita waliongoza 2-0 dhidi ya Hoffenheim na kulazimishwa Sare ya 3-3.
Kevin-Prince Boateng, Nyota wao walipoifunga Steaua Bucharest, Jumamosi alifunga Bao.
Steaua Bucharest v Chelsea
Chelsea wamejitayarisha kwa Mechi hii kwa Jumamosi kutoka Sare ya 1-1 na Tottenham huku Straika wao Fernando Torres akitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Hii ni Mechi ambayo hata Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekiri hawatakiwi kuipoteza kwa vile walichapwa 2-1 na FC Basel katika Mechi ya kwanza ya Kundi hili.
Msimu uliopita Steaua iliifunga Chelsea 1-0 kwenye Raundi ya Mtoano ya EUROPA LIGI lakini wakachapwa 3-1 kwenye Marudiano huko Stamford Bridge.
KUNDI F
Arsenal v Napoli
Arsenal waliuanza Msimu huu kwa kuchapwa 3-1 na Aston Villa kwenye Ligi Kuu England lakini tangu hapo wameshinda Mechi 9 mfululizo na sasa wanaongoza Ligi hiyo na ushindi huo ni pamoja na kuifunga Ugenini Marseille Bao 2-1 kwenye Mechi ya kwanza ya Kundi hili.
Wikiendi hii iliyopita, Arsenal waliifunga Swansea City Bao 2-1 kwenye Ligi huku Kiungo wao Aaron Ramsey akifunga Bao na hiyo ni Gemu 4 mfululizo anapachika Mabao.
Rafael Benitez, aliewahi kuwa Meneja wa Liverpool na Chelsea, ndie aiongoza Napoli ambayo kwenye Serie A huko Italy inafanya vyema sana wakiwa wametoka Sare Mechi moja tu kati ya 6 walizocheza na wako Nafasi ya Pili, Pointi 2 nyuma ya Vinara AS Roma.
Jana Napoli walitangaza Kikosi chao ambacho kimetua London kuikabili Arsenal na nacho ni:
Makipa: Rafael, Reina, Colombo.
Mabeki: Albiol, Britos, Cannavaro, Fernandez.
Viungo: Armero, Behrami, Dzemaili, Hamsik, Inler, Mesto, Radosevic, Zuniga.
Mafowadi: Callejon, Mertens, Higuain, Insigne, Pandev, Duvan.
Borussia Dortmund v Marseille
Borussia Dortmund, ambao walifika Fainali ya Mashindano haya Msimu uliopita, wameanza vyema Bundesliga na kuongoza kwa kushinda Mechi 6 kati ya 7 na Jumamosi waliishindilia Freiburg Bao 5-0.
Lakini kwenye UCL kwenye Kundi hili wameanza vibaya kwa kufungwa 2-1 Ugenini na Napoli katika Mechi ambayo Kipa wao Roman Weidenfeller alitolewa kwa Kadi Nyekundu, hivyo hachezi Mechi hii, na pia Kocha wao Jurgen Klopp, kutolewa nje na Refa.
KUNDI G
Zenit Saint Petersbug v Austria Vienna
Timu zote hizi zimefungwa Mechi zao za kwanza kwa Zenit kufungwa Ugenini 3-0 na Atletico Madrid na Vienna kuchapwa Nyumbani kwao 1-0 na FC Porto.
Lakini Zenit, wakicheza Nyumbani ni wakali na ambako ndio wanaongoza Ligi ya Urusi na Juzi kuwafunga Spartak Moscow 4-2 huku Alexander Kerzhakov akipiga Bao lake la 208 kwenye Ligi na kumfanya awe Mfungaji Bora katika Historia ya Ligi ya Urusi.
Austria Vienna wapo Nafasi ya 5 kwenye Ligi ya kwao na walifungwa 1-0 na Admira hivi Juzi.
FC Porto v Atletico Madrid
Atletico Madrid wako moto huko kwao kwenye La Liga kwa kukamatana Pointi sawa na Vinara Barcelona na Juzi waliichapa Real Madrid 1-0, kwa Bao la Mbrazil Diego Costa, huko Santiago Bernabeu na kuua Rekodi ya kutoifunga Real kwenye Ligi kwa Miaka 14.
Hata hivyo, Atletico watatinga Mechi hii bila Diego Costa ambae anamalizia Kifungo chake cha Mechi za Ulaya 4.
Porto nao wanaongoza Ligi yao wakiwa Pointi 2 mbelle ya Sporting Lisbon huku kila Timu ikiwa imecheza Mechi 6.
KUNDI H
Ajax v AC Milan
Ajax wapo Nyumbani na katika Mechi ya kwanza ya Kundi hili walichapwa 4-0 Ugenini na Barcelona.
Ajax wamejitayarisha kwa Mechi hii kwa kuidunda Go Ahead Eagles Bao 6-0 kwenye Mechi ya Ligi ya kwao na kuwafanya wawe Pointi 1 nyuma ya Vinara PSV Eindhoven.
Nao AC Milan, ambao wameshinda Mechi 2 tu za Serie A kati ya 6 na wapo Nafasi ya 9, wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na Majeruhi kadhaa lakini walishinda Mechi yao ya kwanza ya Kundi kwa kuichapa Celtic 2-0.
Celtic v Barcelona
Msimu uliopita kwenye Hatua ya Makundi ya UCL, Celtic waliichapa Barcelona 2-1 ndani ya Celtic Park na leo Barcelona wanatinga tena bila ya Supastaa wao Lionel Messi ambae ni Majeruhi baada kuumia Jumamosi iliyopita kwenye Mechi ya La Liga walipoichapa Almeria 2-0.
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano 2 Oktoba 2013
[Saa 1 Usiku]
PFC CSKA Moskva v FC Viktoria Plzeň
[Zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku]
FC Shakhtar Donetsk v Manchester United FC
Bayer 04 Leverkusen v Real Sociedad de Fútbol
Juventus v Galatasaray A.Åž.
Real Madrid CF FC København
Paris Saint-Germain v SL Benfica
RSC Anderlecht v Olympiacos FC
Manchester City FC v FC Bayern München

SOurce:sokainbongo.co

HUYU NDIO MSAIDIZI WA BARACK OBAMA KWENYE TEKNOLOJIA ALIYEKULIA TANZANI




WAKATI anaingia madarakani rasmi Januari 20, mwaka 2009 kuiongoza Marekani, nchi kubwa yenye nguvu za kiuchumi na kisiasa duniani, Barack Obama alikuwa na malengo mengi. Mojawapo ni kuzidi kuipaisha Marekani na kuwasuta waliodhani nchi hiyo haiwezi kuongozwa na mtu mweusi.
Itakumbukwa kwamba, Obama mwenye asili ya Kenya ambaye kwa sasa ni Rais wa 44 wa Marekani, ndiye mtu wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuwahi kuiongoza Marekani.
Hivyo, katika kuhakikisha anatimiza ndoto zake, alipanga safu imara ya wasaidizi, miongoni mwao aliibuka kijana mdogo aliyekuwa na umri wa miaka 35 tu, lakini aliyekuwa na kichwa adimu katika utundu wa kazi, hasa kwa upande wa teknolojia.
Huyu si mwingine bali ni Vivek Kundra aliyezaliwa huko New Delhi, India. Huyu alipewa jukumu la kuwa Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Serikali ya Marekani. Kundra, ingawa ana asili ya India, ni ‘Mswahili’ anayeijua vyema Tanzania, kwani amekulia Tanzania.
Historia yake inaonesha kuwa, akiwa na umri wa mwaka mmoja tu, yeye na wazazi wake, walihamia Afrika, katika nchi ya Tanzania. Baba yake alikuwa miongoni mwa maprofesa na walimu waliokuja nchini kufundisha katika shule kadhaa.
Kutokana na mpango huo, Kundra alijikuta akiishi na wazazi wake huko Korogwe, Tanga na pia mkoani Dodoma. Ni huko ndiko alikozama katika Kiswahili, akiifanya lugha yake ya kwanza huku Kihindi na Kiingereza zikiwa lugha za ziada kwake.
Aliishi Tanzania hadi alipofikisha umri wa miaka 11 ambapo wazazi wake walihamia Washington D.C, Marekani.
“Kwa hiyo ninaijua vizuri Tanzania na ninakifahamu vizuri Kiswahili,” anasema Kundra ambaye akiwa Marekani, alihitimu Shahada ya Kwanza katika Saikolojia aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Maryland Park.
Hakuishia hapo, alirudi tena darasani kusoma Teknolojia ya Habari katika Chuo Kikuu cha Maryland, lakini pia alisoma katika Taasisi ya Uongozi wa Siasa ya Sorensin ya Chuo Kikuu cha Virginia.
Kutokana na umahiri wake kitaaluma, Machi mwaka 2011 alitangazwa kuwa mmoja wa waliothibitisha vipaji vya uongozi duniani, akichaguliwa na jopo la wajuzi na wasomi kutoka Mkutano wa Uchumi Duniani (WEF).
Mwaka huo, katika mkutano uliofanyika Amman, Jordan, Kundra alikuwa mwenye furaha kukutana na kijana mwingine aliyepewa heshima kama yake, Susan Mashibe wa Tanzania ‘milionea mtoto’ ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya TanJet, kampuni ya kimataifa na ya kwanza ya aina yake nchini inayoshughulikia masuala ya kiufundi katika ndege binafsi, za biashara na hata za kidiplomasia.
Mwanadada huyu, pia anamiliki kampuni nyingine inayojulikana kama Kilimanjaro Aviation Logistic Center, ambayo inashughulikia taratibu za utuaji na urukaji wa ndege binafsi katika Bara la Afrika.
Aidha, ameanzisha Huduma ya Matengenezo na Ukarabati wa Ndege Kilimanjaro, kwa lengo la kutoa huduma za kisasa, yenye kiwango na salama katika usafiri wa anga wa jumla na ushirika katika eneo la Afrika. Lakini pia Susan ndiye Mwanamke wa Kwanza Afrika Mashariki mwenye Cheti cha Rubani cha FAA na Mhandisi Matengenezo wa Ndege.
Tangu kuanzishwa TanJet mwaka 2003, Mashibe ametunukiwa Tuzo mbalimbali ikiwemo ya Askofu Desmond Tutu ya mwaka 2009 na ile ya Mwanamke Mjasiriamali mwenye Mafanikio ya mwaka 2009.
Tukirudi kwa Kundra, mwaka mmoja kabla ya tuzo ya WEF, alituzwa na taasisi ya teknolojia ya SANS kwa kuwezesha kufichua wizi wa dola za Marekani milioni 300 (Sh bilioni 450) uliokuwa unafanywa kwa njia ya mtandao kwa takribani kila mwaka na baadhi ya watendaji serikalini.
Aidha, Kundra amewahi kutunukiwa Tuzo kemkem kutokana na umahiri wake katika miundombinu ya teknolojia na habari na mawasiliano, akiwa amegundua mifumo kadhaa ya kisasa. Ndiyo maana Chuo Kikuu cha Harvard hakikutaka kuuachia ujuzi wake, na hivyo kuamua kuingia naye mkataba wa kufundisha kwa mkataba chuoni hapo.
Nje ya kazi hiyo, Kundra pia ni Makamu Mwenyekiti wa kampuni kubwa ya masomo ya Salesforce ya Marekani. Majukumu mengine ya kitaaluma aliyokuwa nayo kabla ya kuitwa Ikulu ya Marekani kumsaidia Rais Obama ni kuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya Teknolojia huko Arlington, Virginia mwaka 2001 na miaka mitano baadaye, aliteuliwa na Gavana wa Virginia, Tim Kaine kuwa mkuu wa shughuli za kiteknolojia jimboni humo.
Ilipofika Machi 27, 2007, Meya wa Columbia, Adrian Fenty alimteua Kundra kuwa Ofisa Teknolojia Mkuu wa Columbia.
Je, anazungumziaje kuaminiwa kwake na Rais Obama? Anasema: “Ni heshima kubwa. Sikuwaza kuwa msaidizi wa Rais katika nchi muhimu kama Marekani. Kama unavyojua, nilizaliwa India, nikakulia Tanzania.
Ni mhamiaji tu hapa na ikumbukwe nilikuja Marekani mwaka 1985 nikiwa sijui hata Kiingereza, zaidi ya Kihindi na Kiswahili.
“Lakini bidii katika masomo na nyanja ya utawala, vitu nilivyorithi kutoka kwa wazazi wangu, ndivyo vilivyonifikisha hapa, kiasi cha kuaminika na jamii na hata Rais wa nchi.Namshukuru Mungu kwa kila jema linalotendeka juu yangu. Namshukuru Rais Obama kwa kuwapa nafasi vijana pia.”
Huyo ndiye Vivek Kundra, mtaalamu wa teknolojia ya habari na mawasiliano aliyekulia Tanzania, lakini sasa akifanya vitu vikubwa nchini Marekani.

Source: HabariLeo

Magazeti ya Mtanzania na Mwananchi yafungiwa



                                             TAMKO LA SERIKALI

Serikali imeyafungia  kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba,2013  kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala  za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.

Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia 27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.

Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17 Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013”  kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri  haukupaswa kuchapishwa Magazetini.

Aidha, katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI”  habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa  mkali mwenye hasira.Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la  ukweli.

Jeshi la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya kiislam  mbwa ni najisi hapaswi kuingia  katika maeneo ya ibada.
Gazeti la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti hili limeonywa mara nyingi  lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa  kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za  fani ya Habari.
Pamoja na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha, siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta  kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika  na wahanga waliomizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na  waliyovamiwa na kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama  wavione kuwa haviwasaidii.
Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba 332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani  nchini.
Imetolewa na


MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013

SERENGETI FIESTA MWANZ ILIFUNIKA YANI NI NOMA SANAAA



Anaitwa Neylee,msanii wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema sana kwenye anga ya muziki huo,akiimba kwa hisia mbele ya mashabiki wake usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea 2013.


sehemu ya mashabiki wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa ccm kirumba,ambapo tamasha la serengeti fiesta likirindima usiku huu.

 

Msanii wabongofleva akicheza na shabiki wake jukwaani usiku huu.
 

Mashabiki wakishangweka kwa raha zao huku jukwaala fiesta likiwaka moto vilivyo usiku huu.

Kundi la Wasanii mahiri wa kuimba na kucheza kutoka THT,wajiitao Makomanda wakitumbuiza usiku huu ndani ya uwanja wa CCM Kirumba,ambapo tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea.

Muigizaji wa filamu lakini pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,aitwaye kwa jina la kisanii Shilole akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa ccm kirumba usiku huu.

Anaitwa Christian Bella ambaye alikuwa akifanya vyema sana kwenye bendi ya muziki wa dansi ya Acudo,akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.
Mkali mwingine wa hip hop,ambaye amekuwa akifanya vyema sana kwenye anga hizo,Kalla Jeramiah akishusha mistari mikavu mbele ya mashabiki wake usiku huu.

Wako live kinoma usiku huu,huku mayowe na miluzi ikiwa imetawala kila kona ya uwanja

Pichani kati ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya simu za mikononi ya Zantel akiwa na marafiki zake wakilifuatilia tamasha la serengeti fiesta 2013 usiku huu ndani ya uwanja wa ccm kirumba,ambapo wakazi wa jiji la Mwanza wamejitokeza kwa wingi.

Kila kona ni ileee full maraha tuu,huku wakiburudika na vunywaji mbalimbali kutoka kampuni ya bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la serengeti fiesta wakishirikiana na PSI kupitia bidhaa yao ya Salama kondom.

Vijana machachari kabisa kutoka kinondoni wakitambulika kwa jina la KINOKO wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma za Michael Jackson mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza.

Mmoja wa sanii waliofanya vyema sana katika shindano la BSS,Walter Chilambo,akiimba usiku huu kwenye jukwaa la Serengeti fiesta.

Mashabiki wa fiesta kibao usiku huu ndani ya ccm kirumba.

Vuta rahaa hakuna maneeeee.....manenooooo

Mtangazaji wa Clouds Paul James na wadau wake wakifuatilia yanayojiri ndani ya tamasha la serengeti fiesta usiku huu ndani ya ccm kirumba.
PICHA NA TANZANIA ONE PAMOJA NA JIACHIE