Tuesday, February 4, 2014

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA.


IMG_9522Jaji Mkuu  wa  Tanzania  Mohamed  Chande Othman (kushoto)  mstari  wa kwanza akiwa katika maandamano ya siku ya sheria jana na  baadhi ya  majaji  kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads . IMG_9524 Bendi ya polisi ikiongoza maandamano ya siku ya sheria katika  viwanja  Mahakama Tanzania  vilivyoko Ocean Roads yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam IMG_9559Rais Jakaya Kikwete akipokelewa (kushoto) na  Jaji Mkuu  wa  Tanzania  Mohamed  Chande Othman (kulia) leo mara baada ya  kuwasili  kwenye   maadhimisho ya   siku  ya sheria   mara baada na  baadhi ya  majaji  kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads IMG_9586 Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba  leo  kwenye   maadhimisho ya   siku  ya sheria    kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads IMG_9641Jakaya Kikwete akipokelewa (katikati ) na  Jaji Mkuu  wa  Tanzania  Mohamed  Chande Othman (kulia) jana mara baada ya  kuwasili  kwenye   maadhimisho ya   siku  ya sheria   mara baada na  baadhi ya  majaji  kwenye   viwanja  Mahakama Tanzania vilivyoko Ocean Roads .
Picha Magreth Kinabo – MAELEZO

HAWA NDIO WATU 10 WENYE NGUVU TANZANIA,SOMA ZAIDI HAPA

KWA muda wa miezi miwili , magazeti ya Global Publishers Ltd yaliendesha zoezi la kuwashirikisha wasomaji wake juu ya mtu gani mwenye nguvu zaidi ya ushawishi katika jamii ya Watanzania.

Rais Jakaya Kikwete.
Jumla ya Watanzania 438,726 walipiga kura kupendekeza majina mbalimbali. Watu 10 waling’ara zaidi kwa kugawana jumla ya kura asilimia 97.4, huku wengine ambao hawakuweza kuchomoza wakiambulia mgawo wa asilimia 2.6.
Katika hao 10 waliong’ara zaidi, mtiririko kulingana na wingi wa kura unagawanywa kama ifuatavyo.
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete anashika nafasi ya kwanza. Kwa nafasi yake kama mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi na usalama, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM, ndiye aliyeongoza kwa kupata kura nyingi kwamba ana ushawishi mkubwa katika makundi yote. Watu 118,456 ambao ni sawa na asilimia 27 walimchagua.
Edward Ngoyai Lowassa
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa anashika nafasi ya pili kwa nguvu ya ushawishi katika Tanzania. Ingawa hayumo kwenye Baraza la Mawaziri, ameonesha anakubalika sana kijamii kwa kuchaguliwa na watu 83,358 ambao ni sawa na asilimia 19.
Zitto Zuberi Kabwe
Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini Chadema ndiye alifungua milango kwa vijana wengi kujiingiza katika siasa mwaka 2005. Umahiri wake katika kujenga hoja zinazotikisa nchi, zilimpatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya chama chake. Anachukuliwa kama kijana aliyewapa wenzake uwezo wa kujiamini. Pamoja na misukosuko ya kisiasa inayomkabili lakibi bado ameng’ara kwa kuchaguliwa na watu 65,809, sawa na aslimia 15.
Reginald Abraham Mengi
NI mfanyabiashara mkubwa mzawa, maarufu pengine kuliko wote Tanzania. Ndiye mtu anayemiliki vyombo vingi vya habari, vikiwemo televisheni, redio na magazeti. Ni mmoja wa matajiri wachache wenye utamaduni wa kuwasaidia wasiojiweza. Kutokana na mchango wake kijamii, naye ameng’ara. Watu 43,873 ambao ni sawa na asilimia 10 walimchagua.
Kadinali Polycarp Pengo
MUADHAMA Polycarp Kardinali Pengo ni kiongozi wa madhehebu ya Kikatoliki anayeheshimika katika jamii ya Kitanzania. Ni mtu makini na anayehubiri amani na upendo muda wote. Taswira yake kwenye jamii imemuwezesha kuchaguliwa na watu 35,098 (asilimia 8).
Dk. Willibroad Peter Slaa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Alijipatia umaarufu mkubwa wakati alipokuwa mbunge wa kuchaguliwa Jimbo la Karatu. Uwezo wake wa kujenga hoja na kuitetea, msimamo mkali dhidi ya rasilimali za taifa kulimfanya kupendwa na wengi.
Jambo hili lilimfanya kuwa mpinzani mkubwa wa CCM wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ingawa baadaye alishindwa na Rais Kikwete. Mvuto wake kwa wananchi, ulichangia pia kuongezeka kwa idadi ya wabunge wa chama chake, kutoka 11 mwaka 2005 hadi 48. Watu 26,324 (6%) wamempigia kura.
Said Salim Bakhressa
MFANYABIASHARA maarufu nchini na mmoja wa watu wanaotajwa kuwa na fedha nyingi zaidi Tanzania. Anamiliki viwanda vya kutengeneza unga, juisi, matunda, biskuti, soda na koni. Pia ndiye msambazaji mkubwa wa unga kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Bakhressa ambaye ni Mzanzibari, pia anamiliki timu ya mpira wa miguu ya Azam FC ambayo ni ya kwanza nchini kuwa na uwanja wake wa kisasa. Ndiye mmiliki wa kituo cha televisheni cha Azam TV, vilevile ana vyombo vya usafiri wa majini. Watu 21,936 (5%) wamemchagua.
 
John Pombe Magufuri
MMOJA wa mawaziri wenye historia nzuri ya uchapa kazi kiasi cha kusifiwa sana na wananchi. Tokea alipoibuliwa kwa mara ya kwanza na kuwa waziri wakati wa utawala wa Awamu ya Tatu, kasi yake imezidi kung’aa na kumfanya kuwa kipenzi cha wananchi. Katika orodha hii amechaguliwa na watu 17,549 (4%).
 
Dk. Harrison George Mwakyembe
Makali yake yalidhihirika zaidi alipoongoza Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kuhusu uwepo wa ufisadi katika kampuni ya kufua umeme ya Richmond mwaka 2007-2008, kazi ambayo ilimalizika kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo, Edward Lowassa kuachia ngazi pamoja na Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, waliokuwa mawaziri wakati huo.
Kazi yake nzuri akiwa mbunge, baadaye kuwa naibu waziri wa Uchukuzi na hata baada ya kuwa waziri kamili, imemfanya achaguliwe na watu 8,775 (2%) kuwa mmoja wale 10 wenye ushawishi.
 
Issa Ponda     
Ni Katibu wa Jumuiya za Kiislam Tanzania. Amekuwa akiendesha harakati nyingi kudai haki za Waislam, hivyo kumfanya awe akilumbana na serikali mara kwa mara. Anachokifanya kinabeba maana kubwa kwa watu, ndiyo maana amechaguliwa kwa kura 6,142 (1.4%), hivyo kufunga orodha ya wale 10 wenye mvuto zaidi Tanzania kwa mwaka 2013-2014

VITA YA URAIS CCM YAWAPELEKA MWINYI, MKAPA DODOMA

h11 8958d
KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana mjini Dodoma Jumapili wiki hii, huku Baraza la Ushauri linaloundwa na marais wastaafu, likitarajiwa kuwasilisha taarifa ya hali ya chama hicho. (HM)
Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya CCM, zinasema Baraza la Ushauri, linaloundwa na marais wastaafu, linatarajia kutoa tamko zito kutokana na mwenendo unaoonyeshwa na makada wake.

Baraza hilo, linaundwa na wenyeviti na makamu wastaafu wa chama, likiongozwa na Mwenyekiti wake, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Katibu wake ni Pius Msekwa.
Wengine ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Amani Abeid Karume na Waziri Mkuu mstaafu, John Malicela.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya kuibuka malumbano yanayowahusisha makada wa chama hicho wanaotajwa kuwania mbio za urais mwaka 2015 kuanza harakati mapema.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka CCM, kiliiambia MTANZANIA kuwa kikao cha CCM, pamoja na mengine, kitatoa dira ya chama na kuweka mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"CCM itakutana Februari 9, mwaka huu kati ya mjini Dodoma au Dar es Salaam, lakini katika kikao hicho wajumbe wa Baraza la Ushauri la chama watakuwepo.
"Sijui watazungumza nini katika kikao hicho, huenda ikawa haya mambo yanayoendelea ndani ya chama hivi sasa, kwani tambua wajumbe wa baraza wanaweza kuomba kukutana na CC au NEC wakati wowote pale wanapoona inafaa," kilisema chanzo hicho.
Katika siku za hivi karibuni, makada wa CCM wameibuka na kuunga mkono hatua ya Katibu wa Uhamasishaji wa Chipukizi, Paul Makonda, ambaye alimtuhumu Waziri Mkuu wa zamani, EdwardLowassa, kuwa ameanza harakati za kuwania urais.
Baada ya kauli hiyo, Malecela naye aliibuka na kuutaka uongozi wa CCM kumchukulia hatua Lowassa.
Malecela alidai, Lowassa anakiyumbisha chama hicho kutokana na kampeni za kutaka kuwania urais wa 2015.
Alisema Sekretarieti ya CCM inapaswa kuwachukulia hatua kali makada wanaojipitisha maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kusaka urais, kabla ya chama hicho kupanga muda. Chanzo: mtanzania

TAZAMA PICHA::CHADEMA (M4C PAMOJA DAIMA) YATETEMESHA MWANZA, DR. SLAA ATOA TAMKO.


Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa wameinua mikono kuonesha ishara ya Kusurrender katika Mkutano wa hitimisho wa Chadema M4C Pamoja Daima ulifanyika katika Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza 
  Helkopta iliyokuwa imembeba Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbroad Slaa ikitua katika Uwanja wa Furahisha ili aweze kuhutubia katika Mkutano wa Kampeni wa Chadema M4C Pamoja Daima.
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akiingia Uwanjani ili aweze kuhutubia maelfu wa Wana Mwanza waliofika Kumsikiliza.



 
 Mbunge wa Musoma mjini, Vincent Nyerere akihutubia katika Mkutano wa hitimisho wa M4C Pamoja Daima lillofanyika katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.
 Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Highness Kiwia akitoa ya moyoni katika Mkutano wa Movement For Change Pamoja Daima.
 Mh. Higness Kiwia akimpokea Bwana Darius Ngoko ambaye ameamua kuhama chama cha Mapinduzi CCM na Kujiunga na Chadema katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima.
 Katika hali ya kushangaza jeneza ambalo lilikuwa limechorwa picha ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe.
 Bwana Kaswahili aliyevaa shati la blue kamanda kutoka chama cha Chadema ambae anajiandaa kugombea katika Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema akifuatilia kinachoendelea katika Mkutano huo.
 Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Bwana Laban Aggrey naye akifuatilia kwa umakini matukio kadha wa kadha katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima akiwa na baadhi Makamanda wa Chadema.
 Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasiana Maendeleo Chadema Bwana Wilfred Mganyizi Lwakatare akizungumza kwenye mkutano wa M4C Pamoja Daima katika viwanja vya Furahisha.
 Mdhamini wa Chadema Mzee Masinde akizungumza jambo katika Mkutano wa M4C Pamoja Daima katika viwanja vya Furahisha.
 Mbunge wa Nyamagana, Mh. Ezekia Wenje akiwa na Matibu wa Chadema Taifa Bwan Mudi mwenye kombati ya Green na Mbungue wa Jimbo la Ilemela Mh. Highness Kiwia.
 Umati wa watu wakiwa wamekaa wakisikiliza hotuba kutoka kwa Dr. Wilbroad Slaa kama inavyoonekana katika picha.
 Umati mkubwa wa wananchi waliofika kwenye uwanjaa wa Furahishaaa wakisikiliza hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi wa Chadema kwenye Kampeni ya M4C Pamoja Daimaa.
 Katibu wa Chadema Taifa, Dr. Wilbroad Slaa akihuthubia maelfu ya wananchi waliofurika katika uwanja wa Furahisha Mwanza kusikiliza hitimisho la Kampuni ya M4C Pamoja Daima.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimesema hakitalalamika tena kwa lolote au kukilamu Chama Cha Mapinduzi CCM maana wameshaongea sana na sasa watafanya utekelezaji wa Ilani ya Chama chao.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Chama hicho Dr. Wilbroad Slaa katika hitimisho la Kampeni za M4C Pamoja Daima lililofanyika katika uwanja wa Furahisha Mwanza.

Slaa amesema kuwa wameshaongea kero mbalimbali za wanainchi wa Tanzania lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika hicho wao kuanzia sasa wao kama Chadema hawatalalamika zaidi ya kuchukua maamuzi ya utekelezaji tu.

Kampeni hizo ambazo imefanyika kwa siku 14 kwa kutembelea Majimbo yote ya upigaji kura ambazo zilikua zimegawanyika katika makundi mawili kwa kutumia helkopta tatu ambazo zilikuwa zinaongozwa na Dr. Wilbroad Slaa, Freeman Mbowe na Tundu Lissu.

PICHA NA HABARI NI KWA HISANI YA  MATUKIOMEDIA BLOG

KIGOGO WA ZAMANI BOT ALIVYOTUPIWA VYOMBO NJE!


Mkurugenzi wa zamani wa Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Elisa Issangya, akiwa ameduwaa baada ya vyombo vyake kutolewa nje ya nyumba na Kampuni ya  Udalali ya Mwafrika jana. Picha na silivan Kiwale 
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa zamani wa Fedha wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Elisa Issangya amejikuta akitupiwa vyombo vyake nje na Kampuni ya Udalali ya Mwafrika kwa kile kilichoelezwa kutakiwa kuondoka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.
Nyumba hiyo iliyoko Mtaa wa Ruhinde Block 2 Plot 294 eneo la Ada Estate wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, inaelezwa kuwa inamilikiwa na BoT.
Akizungumza nyumbani kwake baada ya kutupiwa nje vifaa vyake, Issangya alisema: “Nimeshtukizwa na maofisa wa Kampuni ya Udalali ya Mwafrika kuingia ndani kwangu na kuniomba nishirikiane nao kutoa vitu vyangu nje.

“Maofisa hao wa Kampuni ya Mwafrika walifika nyumbani kwangu asubuhi na kunionyesha barua kutoka BoT ya kunitaka kuvitoa vyombo vyangu nje, sikukubaliana nao, nikaamua kwenda polisi kutoa taarifa,” alisema.
Alisema wakiwa polisi na ofisa mmoja wa kampuni hiyo aliyemtaja kwa jina moja la Gama ambaye alikuwa akimweleza kuwa, watamuelewesha suala hilo baada ya kuondoa vyombo hivyo , lakini waliporejea nyumbani kwake, walikuta vyombo vyote vimetupwa nje.
Issangya alisema kitendo cha kutupiwa vifaa nje ni udhalilishaji kwani walitakiwa kwenda nyumbani kwake wakiwa na barua ya mahakama ya kuwaruhusu kufanya hivyo.
“Nimeshangaa hatua hiyo wakati mpaka sasa kesi yangu ya kudai haki zangu ipo mahakamani, wangesubiri mpaka hukumu ikitolewa ndipo waje na uamuzi huu,” alilalamika Issangya aliyeteuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha wa BoT mwaka 2000 kabla ya kusimamishwa 2008.
Alipoulzwa sababu za kufanya hivyo wakati suala la mlalamikaji bado liko katika vyombo vya sheria na uamuzi wa shauri haujafikiwa, Ofisa wa Kampuni hiyo ya Udalali, Joseph Gama alisema kuwa wanatekeleza maagizo ya tajiri wao na si vinginevyo.
“Sisi tunafanya kazi kwa amri ya tajiri wetu, hatuwezi kufanya mambo kinyume na maelekezo, tumeelekezwa na huu ni utekelezaji wake,” alisema.
 MWANANCHI

KUCHELEWESHWA KESI KUNACHANGIA MLUNDIKANO WA MAHABUSI: JAJI MKUU TANZANIA

JAJI_efd0f.jpg

Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman
Tanzania Jumatatu imeadhimisha siku ya sheria nchini humo huku changamoto kubwa ikiwa ni utoaji haki kwa wakati kutokana na matatizo yaliyopo kwenye mfumo wa mahakama nchini humo.
Kucheleweshwa kwa kesi bila sababu za msingi kunaochangia mlundikano wa mahabusu magerezani umekuwa chanzo cha malalamiko kutoka kwa wananchi na wadau mbali mbali wa sheria nchini Tanzania hali inayochangia vyombo hivyo vya kutoa haki kulalamikiwa.
Rais Jakaya Kikwete aliyeshiriki maadhimisho hayo ya siku ya sheria nchini humo pia alisisitiza suala hilo la utoaji haki kwa wakati huku akitumia fursa hiyo kusisitiza kwamba serikali itaendelea kuziwezesha mahakama nchini kwa kuziongezea bajeti, kupanua wigo wa ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya na kuboresha majengo ya mahakama zilizopo pamoja na kuongeza rasilimali watu katika kuhakikisha vyombo hivyo vya kutoa haki vinatimiza wajibu wao kwa ukamilifu.

kwa upande wake Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman amesema pamoja na changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya mahakama nchini, zikiwemo upungufu wa mahakimu na vitendea kazi, mahakama itaendelea kuboresha utaoji wa huduma baada ya kuanzisha mpango maalum ambapo kesi zote za jinai na madai zinatakiwa kumalizika katika kipindi cha miaka miwili kuanzia sasa
Kauli mbiu ya siku ya sheria nchini Tanzania ni utendaji wa haki kwa wakati umuhimu wa kuwashirikisha wadau.
CHANZO:VOA

Wosia wa Mandela watangazwa




Johannesburg. Wosia wa aliyekuwa Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela umesomwa huku mgawanyo wa mali zake ukielekezwa katika maeneo tofauti.
Katika wosia huo uliosomwa rasmi jana, Mandela aliacha mali zenye thamani ya Dola za Marekani 4.1 milioni, sawa na Sh5.6 bilioni ambazo zimepangwa kugawiwa kwa taasisi mbalimbali, familia na wafanyakazi wake.
Katika wosia huo ulioandikwa na Mandela mwenyewe mwaka 2004 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2008, mkewe, Graca Machel anapata karibu nusu ya mali zake zote alizoziacha.
Mali hizo zinajumuisha nyumba kubwa alizokuwa akimiliki moja ikiwa Johanesburg, nyingine Qunu na ya tatu Mthatha. Mali nyingine ni sehemu ya mrabaha aliyokusanya baada ya kuuza machapisho mbalimbali ikiwamo kitabu chake maarufu cha “Long Walk to Freedom” ambacho kinatajwa kuuzwa kwa wingi duniani.
Pia sehemu za mali hizo zimetokana na kazi mbalimbali alizozifanya wakati akiwa rais na baada ya kuachia madaraka na kujihusisha na wakfu wake wa Mandela Foundation. Wakfu huo ndiyo uliofanikisha kuratibu shughuli mbalimbali za kijamii ambazo alizitekeleza baada ya kustaafu.
Kutangazwa kwa mali hizo kumemaliza minong’ono ya muda mrefu iliyokuwa ikihusisha sehemu kubwa ya familia yake ambayo imewahi kuingia kwenye malumbano juu ya nani anayepaswa kumiliki mali hizo.
Akisoma wosia ulioachwa na Mandela mbele ya waandishi wa habari, Naibu Jaji Mkuu Dikgang Moseneke alisema wanafamilia ya Mandela wamekubaliana na yote yaliyoandikwa na hakuna pingamizi lolote lililotijokeza.
Hata hivyo, kuna nafasi ya kuweka pingamizi juu ya wosia huo katika kipindi cha siku 90 kuanzia sasa vinginevyo, baada ya hapo utaanza kutekelezwa mara moja.
Wosia huo uliokuwa na kurasa 40 umeorodhesha watu na taasisi zinazostahili kuwa sehemu ya mgawanyo huo wa mali na kutaja kiwango stahili kinachopaswa kutolewa.
Chama cha ANC ambacho Mandela na marafiki zake walikiasisi kwa ajili ya kukabiliana na siasa za kibaguzi wakati wa utawala wa makaburu ni miongoni mwa taasisi ambazo zitapitiwa na mgawo huo.
Kamati Kuu ya ANC inatazamia kutumia fedha hizo kwa ajili ya kusambaza sera na misingi ya chama inayohusu maridhiano.
Wengine waliotajwa kwenye urithi huo ni pamoja na aliyekuwa msaidizi wake katika siku zake za mwisho, Zelda la Grange, Chuo Kikuu cha Wits, Shule ya Sekondari ya Qunu na Shule ya Sekondari ya Orlando iliyoko Soweto.

Monday, February 3, 2014

Lowassa ameanza safari, ni ndefu kiasi gani?

lowassa bda0d
Ile 'safari ya Lowassa' imeibua mambo na mjadala mzito ndani na nje ya CCM. Jambo la kujiuliza, je, safari hiyo ina urefu na vikwazo kiasi gani?
"Nimefarijika sana leo kuwaona hapa marafiki zangu wengi. Ninapowatazama hadi machozi yananitoka na kwa uwezo wa Mungu tutashinda kwani nyote mnajua nia na ndoto yangu...WanaCCM msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu zetu... Wingi wenu huu unanipa faraja katika safari yetu na kwa kumtegemea Mungu tutashinda." ni kauli ya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Lowassa alitangaza hivi karibuni kuanza rasmi kwa safari hiyo aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo anasema itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, majisafi na maendeleo ya uhakika.
Alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Usharika ya Monduli Mjini mkoani Arusha.
Bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, Lowassa anawataka waliohudhuria ibada hiyo waungane na kaulimbiu yake, 'Tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na tutashinda pamoja'.
Hafla hiyo ya kimkakati, ilihudhuriwa na baadhi ya wabunge, wengi wakiwa wa CCM, wenyeviti wa mikoa kadhaa wa chama hicho, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM, viongozi wa jumuiya za chama na wengineo.
Licha ya kutoweka bayana aina ya safari anayoanza, Lowassa ni miongoni mwa wanaCCM wanaotajwa kuwa wanaowania urais, kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Dalili hizi za Lowassa kuutaka urais na kutafuta kabla ya kipenga kupulizwa, zimeishtua CCM na kumtahadharisha kuwa atapoteza sifa ya kupitishwa ifikapo 2015.
Safari tangu 1995
Tamaa ya Lowassa kuutaka urais haikuanza leo wala jana, ni ya tangu 1995 alipojitokeza kwa mara ya kwanza. Mwaka huo alikuwa miongoni mwa wagombea 17 wa CCM walioomba kuteuliwa kuipeperusha bendera ya chama hicho.
Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na vikao vitatu vya CCM –Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Kikao cha kwanza kilikua ni Kamati Kuu ambacho Mwenyekiti wake alikuwa Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Ali Hassan Mwinyi lakini Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa bado na ushawishi na nguvu kubwa ndani ya chama hicho.
Nyerere bila kumung'unya maneno, alisema wazi akiwataja wazi Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela kuwa hawakuwa wanafaa kugombea.
Nyerere alisema Malecela alikuwa na madhambi mengi na kwamba alikuwa ameyabainisha katika kitabu chake cha 'Uongozi na hatima ya Tanzania' ambacho pia alielezea udhaifu wa Horace Kolimba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.Kuhusu Lowasa, habari zilizokaririwa kutoka kwenye kikao hicho, zilisema Nyerere alihoji utajiri wake;
"Huyu kijana wa miaka 42 tu amepata wapi utajiri wote huu? Licha ya kutetewa na wapambe wake, Lowassa hakufanikiwa kupenya kwenye hasira za Nyerere.
Baada ya mchujo kufanyika kwa wagombea hao 17, jina la Benjamin Mkapa likaibuka kidedea na kuchukua nafasi hiyo.
Aluta continua
Licha ya Nyerere kumwengua katika kinyang'amyiro cha urais mwaka 1995, Lowasa hakukata tamaa.
Baada ya Mkapa kupitishwa na hatimaye kuwa rais, Lowassa alijiunga na Rais Jakaya Kikwete aliyeleta upinzani mkali.
Kundi hilo ndilo lililomwezesha Rais Kikwete kupitishwa na CCM kugombea urais mwaka 2005 huku Lowassa akiteuliwa kuwa waziri mkuu.
Hata hivyo, 'la kuvunda halina ubani', mwaka 2008, Serikali iliingia kashfa ya uzalishaji wa umeme tata wa kampuni ya Richmond.
Sakata hilo lilipofikishwa bungeni, iliundwa Kamati iliyokuwa chini Waziri wa wa sasa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ambayo hatimaye ripoti yake ilitosha kabisa kumwengua Lowassa katika nafasi ya hiyo na hivyo Baraza la Mawaziri kuvunjika.
Hilo lilikuwa pigo la pili la Lowassa kisiasa. Bado hakukata tamaa. Licha ya kutoweka wazi, Lowassa sasa anaonyesha kila dalili za kuutaka urais ifikapo 2015.
Katika jitihada hizo yeye na wapambe wake, wamefanya mambo mengi ikiwa pamoja na kuweka mtandao mpana wa wafuasi na kuhakikisha kundi lake linaingiza wajumbe wengi kwenye Halmashauri Kuu ya CCM na mkutano mkuu pia.
Mbinu nyingine wanazotumia kujiweka karibu na makundi mbalimbali ya kijamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali, kuchangisha fedha makanisani na misikitini, kutumia vyombo vya habari, mitandao ya jamii na baadhi ya wabunge kumsafishia njia. Sasa ameanza kujiweka karibu vijana na hasa waendesha bodaboda.Akizungumzia suala hilo, Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Gaudence Mpangala anasema mwendendo wa Lowassa hautoi sura nzuri kwa ndoto yake ya urais.
"Mimi ukiniuliza, nitakwambia, Lowassa hafai kuwa rais... kwanza alishapewa tamko na Mwalimu Nyerere mwaka 1995 akihojiwa kuhusu utajiri wake ameupata wapi na hakujibu. Sasa amekumbwa na kashfa ile ya Richmond, hadi akajiuzulu," anasema na kuongeza:
"Watanzania tuwe makini, uongozi siyo lelemama, tutaivuruga nchi yetu."
Profesa Mpangala amekikosoa Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kuwadhibiti watu kama Lowassa.
"Hayo ni mambo ya chama... kama kweli ameshaanza kujinasibu, basi amekosea utaratibu wa chama, lakini hakichukui hatua. Hawa ndiyo walisema watajivua gamba, wameshindwa. Wanasema tu taratibu zimekiukwa lakini hawachukui hatua. Na Lowassa kwa kuwa ana utajiri na ushawishi mkubwa anaweza kupitishwa na kushinda," alisema.
Hata hivyo, kwa upande mwingine, Mhadhiri wa Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (Duce), Dk Kitila Mkumbo amemtia moyo Lowassa akisema anachokifanya ndiyo utaratibu wa demokrasia.
"Sioni kama Lowassa anatofauti na wana CCM wengine. Mengi yamesemwa juu yake lakini huwezi kuyashika mkononi. Ameshafafanua hadharani kuwa kashfa ya Richmond ilisababishwa na mfumo uliokuwapo, hivyo alijiuzulu kwa niaba ya CCM," anasema Dk Mkumbo na kuongeza:
"Nashangaa watu wanapozuiwa kujinadi kugombea urais mapema, huo ni ushamba. Mfumo wa vyama vingi wa kiliberali tofauti na chama kimoja ambao ungesubiri kutangazwa, unajiuza mwenyewe."
Akizungumzia zuio la Mwalimu Nyerere kwa Lowassa mwaka 1995, Dk Mkumbo anasema yalikuwa ni maoni yake binafsi.
"Mambo mangapi yalisemwa na Mwalimu Nyerere na hatuyafuati? Ni kweli aliandika katika kitabu chake cha 'Uongozi na Hatima ya Tanzania' lakini Lowassa hayumo. Ni kweli alisema na tunamheshimu lakini hatulazimiki kuyafuata," anasema Dk Mkumbo.

CHANZO MWANANCHI

TAARIFA YA CCM KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA EDWARD LOWASA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI --30/01/2014

Ndugu zangu waandishi wa habari, awali ya yote naomba niwasalimie na niwapongeze kwa kufika -mwaka mpya 2014, pia naomba niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mmekuwa mkiifanya hasa kuhakikisha watanzania wanapata habari kwa kila jambo linaloendelea kila kona ya taifa letu la Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari nimewaita hapa ili kuzungumza nanyi na mnisaidie kufikisha ujumbe kwa watanzania hasa kuhusu jambo hili ambalo limekuwa gumzo kwa watanzania wengi la mbio za urais 2015 kwa baadhi ya watu ndani ya chama changu cha mapinduzi (CCM), kilichonisukuma zaidi na kupata hamu ya kuongea nanyi ni baada ya kumsikia -na kumuona kijana wetu ndani ya chama cha mapinduzi bwana Paul Makonda akiwa na ujasiri wa kukemea vitendo mambo haya yanayofanywa na baadhio ya viongozi bila uwoga wowote naomba tuchukue fursa hii kumpongeza sana kijana huyu.

Nadiriki kusema nampongeza kijana huyu hasa kwa kauli zake nzito na za kijasiri kwa maslahi ya chama changu cha CCM ili chama kiendelee kupendwa na kuchaguliwa na watanzania.

Pia itakuwa si busara kama sitawapongeza vijana wangu katibu mkuu wa chama ndugu ABDULRAHMAN KINANA na NAPE NNAUYE kwa juhudi zao za dhati za kujenga chama na kuendelea kuwaeleza wananchi juu ya misingi bora ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwakemea viongozi wasiofaa bila kujali cheo na umaarufu wao ndani ya chama na serikali, nawaomba waendelee -na juhudi zao hizo nami naziunga mkono juhudi zao na kama kuna watru wanaowabeza naomba wasijali kwani kukemea viongozi wasiofaa ndani ya chama na serikali ni msingi wa chama chochote kilichounda serikali.

Aidha nawaomba watanzania wenzangu wazalendo wasikubali kukatishwa tama na kikundi cha watu wachache wasio na mapenzi mema na taifa letu ambalo limekuwa mfano wa kuigwa kwa amani, upendo, utulivu na mshikamano urithi tulioachiwa na baba yetu wa taifa mwalimu julias kambarage nyerere ndani na nje ya mipaka ya bara letu la afrika.

Ndugu zangu waandishi wa habari naomba niwaambie kuwa msemaji wa UVCCM kijana wetu Paul Makonda namuunga mkono kwa -kitendo chake cha ujasiri cha kumkemea ndugu EDWARD NGOYAI LOWASSA bila uwoga kwa jinsi anavyokivuruga chama chetu kwa lengo la kutaka urais 2015 huku secretariet ya chama ikiwa imekaa kimya wakati inajua kuwa muda wa kuanza mbio hizi bado na kufanya hivi kwa sasa ni kukiuka misingi na katiba -ya chama. Hapa najiuliza kuwa ile misingi imara ya uongozi ndani ya chama chetu cha mapinduzi iko wapi? Mpaka tumuachie mototo ndio akemee haya? Je, hapa chama kiko wapi?

Ukweli ni kwamba wanachama wetu na vijana wamekuwa njia panda huku wakitamani kusikia tamko au karipio la chama juu ya suala hili la harakati za urais 2015 bila mafanikio.

Naomba niseme kuwa bila kuwa na karipio au tamko la chama, hawa wanaotumia pesa zao hadharani kwa lengo la kutafuta umaarufu na ushawishi kwa vijana ili kupata madaraka wanaharibu misingi yetu bora ya uongozi iliyowekwa na waasisi wetu ndani ya chama.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona juhudu za uongozi wa sasa wa chama ngazi ya juu ikiwa ni pamoja na sekretarieti inayoongozwa na katibu mkuu ABDULRAHMANI KINANA na katibu mwenezi NAPE NNAUYE za kutetea chama hiki zinatiwa mchanga.

Ninaomba juhudi hizi zisibezwe na watu wenye nia njema na chama. Ukweli ni kwamba vijana hawa wamekuwa na juhudi kubwa sana ya kujenga na kuimarisha chama chetu -kwa wananchi kila pembe ya taifa letu kwa kukemea na kueleza misingi ya uongozi bora. Swali: Je! Chama hakioni haya mpaka vijana ndio waone?

Kwa hili ni lazima tubadilike ili kujenga chama chetu na naishauri -secretariet ya chama lazima ichukue hatua mara moja, kijana huyu paul makonda asingesema haya yote kama hana uhakika wa ushahidi wa wa haya aliyoyasema na nampongeza sana.

Vijana na wanachama wengi wa CCM wamekuwa na hamu kwa muda mrefu ya kutaka kujua msimamo wa chama chao bila mafanikio na ndio sababu ya baadhi ya-wengine kupoteza mwelekeo.

Sisi tulikijenga chama hiki kwa taabu sana hapakuwa hata mtu mmoja aliyediriki kutumia fedha zake kutaka madaraka. Nidhamu, busara na uchungu wa rasilimali za taifa hili kwa maslahi ya wananchi ndio vilituongoza kufuata misingi na maadili ya uongozi ndani ya chama na serikali, ndio maana tunaumia sana kuona chama sasa kinataka kutekwa na wenye fedha kwa uchu wa madaraka, mpaka tunashangaa na kujiuliza hizi pesa wanatoa wapi? Na haya madaraka wanayotaka kwa kununua ni kwa maslahi ya nani? Huku watanzania wakiendelea kuwa maskini.

Mfano hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama ngazi ya juu wamejibishana kwenye vyombo vya habari,vitendo hivi havina tija kwa chama na wala havileti umoja na mshikamano ambao umedumu ndani chama kwa muda mrefu.

Mwisho Ninaomba sekretarieti ichukue hatua haraka kama alivyoomba kijana wetu makonda na kweli kuchelewa kuchukua hatua jambo hili kumejionyesha wazi kwamba utaleta kutokuelewana ndani ya chama kusiko kuwa na lazima.


JOHN SAMWELI MALECELA

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

TAZAMA PICHA ZA BIBI ANAYESADIKIKA KUWA NI MCHAWI AMEKUTWA CHUMBANI KWA MTU MJINI BUKOBA


 Bi. Kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70, ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa urahisi  amenusurika kifo baada ya polisi kumnusuru kwa kudaiwa kukutwa akiwa uchi chumbani kwa mtu  akifanya mambo yasiyoeleweka alfajiri ya leo  Ijumaa Januari 31,2014 
 Bi. Kizee akiwa kwenye gari la polisi baada ya kuokolewa na polisi kutoka kwa wananchi wenye asila kali mara tu ya kukutwa kwenye chumba. Mashuhuda wa mwanzo wanasema Bibi huyo amekutwa akitapatapa bila kujua la kufanya huku mwili wake ukiwa Uchi na nguo zake  zikiwa pembeni kitendo kinachopelekea kusadikiwa kwamba Bibi huyu ni  mchawi wakati wengine wakisema wasubili taarifa ya Polisi.



 
 Polisi wakiondoka eneo la tukio wakiwa na  Shuhuda mmoja aliyedai alikuwa miongoni mwa watu waliomkurupusha bibi huyo chumbani.
 Wakielekea kituo cha cha polisi cha Bukoba Mjini leo asubuhi.
 Bibi huyo akiwa kwenye ulinzi mkali baada ya kufikishwa kwenye kituo kikuu cha polisi mjini Bukoba

PICHA ZOTE NA BUKOBAWADAU BLOG

ZITTO KURUKA KAMA CHADEMA


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.
USHINDANI wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umefikia hatua mpya baada ya CCM kuibuka na mkakati wa kumtumia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kupambana na CHADEMA waziwazi.
Katika mkakati huo CCM imepanga kukodisha helikopta ya kumpeleka Zitto katika mikoa minne kwa gharama ya sh milioni 50 mara tu baada ya CHADEMA kuhitimisha Operesheni yao ya M4C Pamoja Daima.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vilivyo karibu na Zitto na CCM, yeye na chama hicho sasa wana adui mmoja – CHADEMA; na wameamua kujibu mapigo baada ya kuridhika kwamba kwa vyovyote Zitto amekwisha kupoteza uanachama wake katika CHADEMA.
Nia yao ni kumtumia Zitto kuleta mpasuko katika CHADEMA, na kufunika mjadala wa mgogoro wa CCM, kero za wananchi na mchakato wa Katiba mpya.
Zitto ambaye alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA – Naibu Katibu Mkuu Bara, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Baraza Kuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni – anatarajia kutumia helikopta yenye uwezo wa kubeba watu wanne, ambayo inadaiwa kukodishwa na wapinzani wa CHADEMA.
Kwa mujibu wa habari hizo, lengo la ziara ya Zitto ni kujibu mapigo ya CHADEMA, hasa katika maeneo ambayo baadhi ya makada na viongozi wa chama hicho wamepita na kuzungumzia hatima yake kisiasa, hasa walipojibu maswali ya wananchi kuhusu sakata lake kuvuliwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, na hatimaye Zitto kwenda mahakamani kuzuia chama kujadili uanachama wake.
Katika kesi ya msingi, Zitto aliyewahi kuwa maarufu akiwa kiongozi wa CHADEMA, anaomba arudishiwe nyadhifa zake zote, na apatiwe nakala za uamuzi wa Kamati Kuu (CC) ili aweze kukata rufaa Baraza Kuu.

Taarifa zinasema tayari chama kimempatia nyaraka hizo, lakini kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, Zitto amekwisha kujiondoa kwenye chama hicho kwa kupeleka shauri mahakamani.

Taarifa za Zitto kuanza ziara mikoani zilianza kusikika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mikoa iliyotajwa ni Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam, ingawa maandalizi yanaendelea na kuna uwezekano wa kubadili baadhi ya mikoa kulingana na mkakati wao.

Kwa hadhi yake ya sasa, CHADEMA imeshasema haitahusika na mikutano yake, na wanachama wake hawatajihusisha nayo. Uratibu wa mikutano yake unafanywa na viongozi waandamizi wa CCM.

Baadhi yao walizungumza na gazeti hili kwa kujitapa kwamba hii ndiyo njia ya kuimaliza CHADEMA, lakini hawakutaka kutajwa majina gazetini.

Iwapo Zitto atakubali ufadhili huo wa CCM na kuendelea na mikutano yake, ni wazi atakuwa amekamilisha ushahidi wa kinachodaiwa na chama chake kwamba amekuwa akikisaliti kwa masilahi ya CCM.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa CCM walipoombwa maelezo juu ya urafiki wao na Zitto kiasi cha kumkosanisha na chama kilichomlea kisiasa, CHADEMA, walisema kwamba urafiki uliopo si wa Zitto na CCM, bali Zitto na Rais Jakaya Kikwete.

Gazeti hili linafahamu kwamba wakati fulani mwaka juzi Zitto alipobanwa na wabunge wenzake kuhusu tabia zake za kuwasaliti kwa Rais Kikwete, alisisitiza kuwa Rais Kikwete ni rafiki yake binafsi, kwa hiyo wamwelewe.

Vilevile, wapo wanaohoji nia ya ziara hii wakati kwa muda mrefu amekuwa akikwepa kuambatana na viongozi wenzake katika ziara na operesheni nyingi za kichama.

Wanasema kwa kuwa operesheni ya sasa ya CHADEMA imepewa jina la M4C Pamoja Daima, kitendo cha CCM kuandaa ziara ya Zitto na kumkodishia helikopta, ni uthibitisho kuwa Zitto hayuko pamoja na CHADEMA tena.

Wameongeza pia kuwa kama hilo litafanyika, litakuwa limemwingiza Zitto katika orodha ya makada kadhaa wa upinzani waliotumikia CCM baada ya kufukuzwa au kunyimwa fursa za uongozi katika CHADEMA, kama Tambwe Hiza, Dk. Aman Walid Kabourou na Dk. Masumbuko Lamwai.

Alipotafutwa athibitishe kuhusu ziara hii na kama ni kweli inafadhiliwa na CCM, Zitto hakuweza kupatikana.

Mbowe kuwania tena uenyekiti

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema kuwa kamwe hatakiacha chama hicho katika uchanga wa harakati za kulikomboa taifa kama kiongozi wake wa juu.

Akihutubia katika mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima katika sehemu mbalimbali mkoani Morogoro jana, mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa, bado atagombea nafasi ya uenyekiti kwa lengo la kuendeleza harakati za ukombozi wa pili wa taifa hili.

Bila kutaja jina, Mbowe alionya kuwa wenye fikra za kuachiwa chama hicho kikiwa katikati ya ukombozi huo hawatapata nafasi, kwa sababu hawana nia thabiti ya kukiendeleza, bali wana nia ya kukibomoa kwa kutumiwa na wapinzani wa CHADEMA.

“Makamanda, kumbukeni kuwa chama hiki na sisi viongozi wake tumepita katika majaribu makubwa na hata kukoswakoswa kuuawa. Mimi nimekoswakoswa kuuawa kwa bomu huko Arusha, lakini pia kuna watu wamepoteza maisha, wamefungwa jela, wengine wamekuwa vilema, halafu watu wengine wanatusaliti kwa kupewa visenti ili wakivuruge chama na wanataka tuwape chama. Huu ni uendawazimu,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema CCM imekuwa ikifanya jitihada za kuihujumu CHADEMA kwa mbinu mbalimbali, zikiwemo za kupandikiza migogoro, jambo ambalo limeshindwa kufanikiwa kwani Mungu ameweka mkono wake ili kisisambaratike.

“Harakati hizi tunazofanya za kuwakomboa Watanzania mjue tunahatarisha maisha yetu, tumejaribiwa kushawishiwa ndani na nje ya Bunge ili tuwe kondoo, tumekataa. CCM wamekuja na mbinu za kupandikiza migogoro wameshindwa na sasa wanaomba nife wakifikiri nikifa na CHADEMA itakufa. Nawaambia CHADEMA haifi kwa kuwa tumezalisha makamanda wengi, watakiendeleza,” aliongeza Mbowe.

Akielezea kwa mara ya kwanza kwa undani zaidi kuhusu mauaji ya Arusha, mwenyekiti huyo alisema wana ushahidi wa kutosha kwamba polisi walihusika na mauaji hayo na kuongeza kuwa waliohusika ni polisi wa kutoka mkoani Morogoro.

“Kwa mara ya kwanza niliseme hili, mauaji ya Arusha yaliyofanyika kwa kurusha bomu katika mkutano wa kampeni za CHADEMA, yalifanywa na polisi ambao walitoka mkoani Morogoro. Ndiyo maana tunaendelea kumwambia Rais Jakaya Kikwete aunde tume ya kimahakama ili kupata ukweli wa jambo hili,” alisema.

Kuhusu Katiba
Akizungumzia msimamo wa CHADEMA kuhusu muungano, Mbowe alisema chama hicho kinaunga mkono maoni yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, ya serikali tatu.

Alisema hata tafiti mbalimbali zilizofanyika, zikiwemo za wanasheria na wachumi zinaonyesha kuwa Muungano utaimalika zaidi chini ya muundo wa serikali tatu.

“Nawaonya Wana CCM wasijaribu kuingilia mjadala wa Bunge la Katiba na kama wanataka nchi ichimbike, basi walazimishe serikali mbili,” alisema Mbowe.

“Zipo tetesi za CCM kutaka kupitisha hoja zao kwa nguvu kutokana na idadi yao ndani ya wabunge zaidi ya 600, wakiwemo 356 wa Bunge la Tanzania Bara, 84 kutoka Zanzibar na 201 kutoka makundi mbalimbali watakaokwenda kwenye bunge hilo. Wasidanganyike kwamba wanaweza kutumia wingi wao kubadilisha maoni ya Watanzania kuhusu serikali tatu,” alisisitiza Mbowe.

Halima Mdee anguruma

Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambaye yuko katika msafara wa mwenyekiti huyo, alisema vijana wengi wanaochipukia katika siasa kupitia chama hicho, wamelelewa na Mbowe, ambao leo wamekuwa chachu ya mabadiliko nchini.

“Ukweli ni kwamba kamanda huyu wa anga (Mbowe), ndiye ametulea vijana wengi nikiwemo mimi, tena wengine hatukuwa na ujasiri tulionao sasa, asiwadanganye mtu, hasa sisi vijana kwamba tuliingia CHADEMA na umaarufu, hawapo hao, tumelelewa na huyo kamanda,” alisisitiza huku akipigiwa makofi.

 
CHANZO NI TANZANIA DAIMA

BAADA YA KUWACHWA NA KIGOGO WA SERIKALI YA BONGO SUPER STAR WEMA SEPETU SASA AAANZA KUONGELEA KIFO CHAKE SOMA HAPA !!


Kazi ipo! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Wema Isaac Sepetu.Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda kuangusha shoo pande hizo.
Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa mwaka 2014.
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya Bongo viwanja hivyo havitatosha.

“Mimi nakwambia kabisa, pale Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho, niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa wengi sana so Leaders hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya kilamalavidavi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna mwanasiasa mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya wanahabari na malumbano makubwa juu ya serikali tatu.
Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu maarufu kama mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’, mpiga ngoma wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed ‘MCD’, mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga.

CHANZO: Ijumaa WeekEnda.

HUYU NDIYE MWANAMKE WA KITANZANIA ANAYEJITAMBUA, NA MWENYE KUIJUA NDOA!



Mme na mke walikuwa wamekaa wanatazama TV mara mke akasema, “Ushakuwa usiku sasa, nimechoka ngoja nikalale”

Akanyanyuka na kwenda jikoni akawaandaa samaki wa chakula cha siku ya pili mchana, akapika chapati kwa ajili ya chai ya siku ya pili asubuhi kisha akachemsha chai kwa ajili ya watoto asubuhi.

Akaiandaa meza na kuweka kila kitu muhimu kama vile vijiko, vikombe, sahani, cocoa, majani ya chai nk kwa ajili ya chai ya asubuhi.

Kisha akaingia ndani na kuandaa nguo za kuvaa mmewe asubuhi na watoto wake waendao shuleni, akaja sebuleni na kuondoa makaratasi na kuweka vitu sawa baada ya watoto kuvichezea, Akachukua simu na kuzichaji akaweka kila kitu sehemu yake.

Akajinyoosha, Akaorodhesha mahitaji ya kuchukua sokoni siku ya pili yake akitoka kazini na kuweka vitu vyote karibu na mkoba wake. Akaingia bafuni akauosha uso wake na kujikausha, akapiga mswaki ….. Mme akamwita, “Nilifikiri umeenda kulala kumbe bado.” “Ndio nataka kulala sasa,” akajibu.

Akanyanyuka na kwenda kuhakikisha milango yote imefungwa na kuifunga. Akapita chumba cha watoto na kuweka neti vizuri na kuongea na mmoja aliyekuwa akimalizia kazi za shule.

Akawategea kengele ya saa ya kuwaamsha asubuhi wasichelewe kujianda na kuhakikisha taa zimezimwa na radio pia akarudi chumbani kwake na kuweka nguo zake vyema za kuvaa kesho yake. Kisha akasali na kumshukuru Mungu kwa kumaliza majukumu ya siku salama.

Mme yeye alisimama pale alipokuwa amekaa akitazama TV, akaizima TV na kujisemesha, “Naenda kulala sasa" bila kujua anamwambia nani muda ule.” Na akaenda kulala bila kufanya chochote wala kuwa na wazo la kufanya chochote

Umeona umuhimu wa mwanamke hapa...?? Share ujumbe huu kwa kuonyesha umuhimu wa wanawake sababu Wao ni chimbuko la furaha na mafanikio yetu……





LIKE, COMMENT "MUNGU AWABARIKI WANAWAKE WOTE KAMA HUYU" na share kama una wapenda kina mama ..

Saturday, February 1, 2014

SUPPORT FOR MISS TANZANIA 2013 HAPPINESS WATIMANYWA

Hey
guys. At Miss World, contestants usually need as much support as they
can get. I would therefore like to ask for your help in spreading the
word to your fellow fans, friends, family, acquaintances etc. about the
representative for Tanzania this year;
Happiness Watimanywa.
People around the world can help me make an even bigger impact through social media and I would like you to be informed of my journey from as early as now. 

Please follow:
@misstanzania2013 on Instagram
@misstz2013 on twitter
And Like Miss World-Tanzania on Facebook
Thanks for the support.
Happy