Thursday, February 6, 2014

MBUNGE WA CHADEMA NA DIWANI KORTINI KWA KUJERUHI MKOANI SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi.

 Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki (Chadema), Sylvester Kasulumbayi na Diwani wa Kata ya Buselesele, Crispian Kagoma na watu wengine 14 wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujeruhi katika vurugu zilizoibuka katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kasulumbayi na wenzake 15, ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kahama saa 8.00 mchana jana na kusomewa mashtaka sita kila mmoja.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Gadiel Mariki, Mwendesha Mashtaka Shukrani Madulu alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 4, mwaka huu.
Madulu aliiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa hao wakiongozwa na mbunge huyo walitenda kosa hilo la kuwashambulia kwa mapanga wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa kampeni za kuwania udiwani wa Kata ya Ubagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.
Alisema mashtaka matano ni kushambulia na kujeruhi kwa mapanga, na moja la kuharibu mali, ikidaiwa kuwa katika vurugu hizo washtakiwa waliishambulia gari la CCM la wilaya hiyo na kuliharibu.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yote na kuomba mahakama iwape dhamana ili waendelee na kampeni za kumnadi mgombea wao wa nafasi ya udiwani katika kata hiyo ya Ubagwe.
Maombi hayo yalipingwa na Mwendesha Mashtaka, akiiomba mahakama isitoe dhamana kwa kuwa hali za majeruhi watatu ni mbaya kwa kuwa tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa na Bugando mkoani Mwanza, baada ya matibabu yao kushindikana wilayani Kahama.
Kutokana na hali hiyo, Hakimu Mariki alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo kesi hiyo itasikilizwa.
Watuhumiwa wote walipelekwa mahabusu baada ya dhamana hiyo kuzuiliwa.
Waliojeruhiwa kwenye vurugu
Wafuasi watano wa CCM wilayani Kahama akiwamo ofisa mtendaji wa Kata ya Ubagwe walijeruhiwa kwa mapanga kwenye vurugu hizo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Andrew Emmanuel alisema Masunga, Kamaro na Peter walisafirishwa kwenda Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Chanzo cha vurugu
Vurugu hizo zilitokea juzi saa moja usiku katika Kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya wafuasi hao kumaliza kampeni zao za kumnadi mgombea wa CCM, Hamis Majogolo anayewania udiwani kwenye kata hiyo.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, wafuasi hao walikumbwa na mkasa huo wakati wakiwa kwenye gari la CCM ambalo pia lilikuwa na watuhumiwa watatu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema waliokuwa wakipelekwa Kituo Kidogo cha Polisi Bulungwa.
Ilidaiwa watuhumiwa hao nao walidaiwa kufanya fujo kwenye mkutano wa Kampeni wa Chama cha Tadea ambacho pia kina mgombea anayewania nafasi hiyo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa wanachama wa Chadema waliweka kizuizi kwa kutumia gari la Kasulumbayi kwenye barabara ya kuelekea kituo kidogo cha polisi.
Peter, ambaye ni dereva wa gari la CCM alisimulia kuwa walipofika kwenye kizuizi hicho walisimama, ndipo wafuasi wa Chadema waliposhuka kwenye gari la Mbunge huyo na kuanza kuwashambulia kwa mapanga wakitaka kuwaokoa wenzao watatu.
Watatu wakamatwa Njombe
Pia Jeshi la Polisi wilayani Njombe linawashikilia watu watatu wanaodaiwa kufanya fujo katika ofisi ya CCM ya tawi la Matalawe, Jumatatu iliyopita.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani alisema kuwa watu hao walikwenda kwa gari kwenye maeneo ya tawi hilo na kuanza kuchana picha za mgombea udiwani wa CCM, Menard Mlyuka.
Aliwataja watu waliokamatwa kuwa ni Award Karonga (40), Ally Mhagama (43) na Robert Mabu (24).
Mwananchi

ANGALIA PICHA MCH PETER MSIGWA AKIWA KIZIMBANI KWA KUJERUHI

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa sambamba na mtuhumiwa mwingine
akiwa ndani ya mahakama ya wilaya ya Iringa jana kabla ya kuahirishwa kwa kesi yakeya kujeruhi mtu
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa akizungumza na wakili anayemtetea
katika kesi yake ya kujeruhi mtu kwenye kampeni za siasa, Lwezaula Kaijage 
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mch Peter Msigwa sambamba na mtuhumiwa mwingine akiingizwa mahakama ya wilaya ya Iringa jana kujibu mashataka ya kujeruhi yanayomkabili

FAMILIA KUMI NA TANO HAZINA MAHALA PAKUISHI GEREZA PAWAGA

 Ofisi za Gereza Pawaga zilizo ezuliwa na upepo mkali ulio ambatana na mvua juzi jioni.
 Sehemu ya masalia ya bati na matandiko yalio haribiwa na mvua
 SACAP Deusdedit Kamugisha Afisa wa Magereza Mkoa wa Iringa pichani kulia akiongozana na Mkuu wa gereza Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala akikagua uharibifu ulio jitokeza katika nyumba za askari na majengo wanayo tarajia kuhamia kwamuda.

 Bustani ikiwa imeharibiwa na Mvua ilionyesha ikiwa na upepo mkari 
Baadhi ya Vyombo vya familia za Askari Magereza vikiwa nje baada ya Mvua kuharibu makazi yao.
Nyumba kumi na tano za Askari Magereza wa Gereza Pawaga wilaya ya Iringa zimeezuliwa na Upepo mkali ulio ambatana na mvua kubwa ya mawe ilionyesha juzi majira ya saa 9 alasiri mpaka saa kumi na moja jioni na kuanza tena saa mbili ya usiku mpaka saa tano usiku.
Akiongea na mwandishi wa habari Mkuu wa Gereza la Pawaga SP.Sosthenes Mwakapala alisema adha hiyo ya mvua imesababisha familia hizo kukosa mahala pa kuishi pamoja na thamani zilizo salia wakati walipokumbwa na mvua hiyo ingawa hakuna madhara kwa binadamu sambamba na hilo kumeezuliwa ofisi za tano za gereza zinazojumuisha Stoo, Bohari, Mapokezi, Utawara pia Bafu ya wafungwa.
 Madhara mengine yaliyo jitokeza ni kuharibiwa vibaya kwa heka tano za Bustani ya gereza yenye mazao mchanganyiko ikiwamo mashina ya Ndizi, Mipapai, Mihogo, Mahindi pamoja na Miwa mimea hiyo imevunjika kabisa haitegemewi  kupona tena.
Mkuu wagareza la Pawaga SP. Sosthenes Mwakapala alisema wao kama uongozi wagereza na viongozi wasaidizi wake wamechukua jukumu la kuhakikisha askari hao na familia zao wanapata mahali pakujihifadhi kwa muda wakati wakisubiri ufumbuzi toka ofisi ya Magereza mkoa wa Iringa. Kwakuwahamishia katika majengo ya Shule ya Msingi, Bwalo la gereza, Ghala la chakula  wakae kwa muda.na mjengwa blog

TAZAMA PICHA ZA MBUNGE WA CHADEMA IRINGA ALIPOACHIWA KWA DHAMANA LEO BAADA YA KESI YAKE


1_23b06.jpg
Mchg.Peter Msigwa (Mb) Iringa Mjini akitoka mahakamani baada ya kuachiwa kwa dhamana
2_86b21.jpg
Msigwa akiwa na wafuasi wake akiwa amebebwa juu juu
3_a5a5e.jpg
Msigwa akipitishwa mbele ya ofisi za Manspaa

4_93c0b.jpg
Msigwa akiwa amebebwa na kushangiliwa nje ya ofisi za Manispaa
5_d0fb7.jpg
Msafara wazuiliwa na Polisi 

6_32bb0.jpg
Msigwa amuliwa kushushwa chini na kutembea  
7_7d5a9.jpg
Msigwa apanda gali
8_fca33.jpg
Msigwa aanza msafara kuelekea ofisi za chama Mtaa wa Mshindo
Ni baada ya kuachiwa kwa dhamana Mbunge wa Iringa Mjini Mchg. Peter Msigwa dhidi ya kesi ya kuhusishwa na mapigano ya wafuasi wa CCM na CHADEMA Mkoani Iringa katika harakati za kampeni za ugombea udiwani kata ya Nduli na kupelekea Kiongozi wa usalama CCM Kamanda Kasmu Keita kujeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa.

BREAKING NEWSSSS::::::TAZAMA PICHA ZA POLISI WAKITUMIA MABOMU KUWATAWANYA WANAINCHI WA MOROGORO ENEO LA MELELA BAADA YA KUFUNGA BARABARA.


MABOMU ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.






Wakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali sehemu za siri na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha msongamano mkubwa wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.

Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.
Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.
Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo.

Wednesday, February 5, 2014

MWANAUME, WAOGOPE WANAWAKE WA NAMNA HII, WATAKUUMIZA NA KUKUHARIBIA MAISHA


 










Hii leo blog yako maarufu ya SKY BONGO inakuletea mada hii kali, ifuatilie hapa mwenyew
WAPO wanawake ambao hawastahili kutongozwa au hawafai mwanaume kua na urafii nao hasa ule wa kimapenzi.

Uwezo wa kuwatambua wanawake wa namna hiyo, ndiyo utakutofautisha mwanaume kamili na wanaume washamba wanaoparamia mapenzi.

Wanawake ambao hawafai wana sifa hizi.
1. Watafutaji
Wapo wanawake ambao wanasema kabisa kuwa hawahitaji wanaume lakini ukweli moyoni mwake anataka kuwa na mwanaume. Ukimpata mwanamke wa namna hii kwa kumazimisha utakipata cha moto maana yeye mapenzi kwake amekuwa kama toashi.

2.Bikira.
Mwanamke mwenye bikra kwa wanaume wanaotaka ngono kabla ya ndoa siyo rahisi kumpata na hata ukimpata hautafurahia mambo fulani wasababu hajui mambo mengi ya kumsisimua mwanaume.

3.Asiyeridhika.
Kuna wanawake hata ukienda raundi za kutosha huwa hawafiki kileleni hivyo kwa wanaume wa mwendo mmoja tarajia nyimbo na lawama ama masimango hata ungemfanyia jambo lolote zuri.

4.Mchoyo.
Kufika kwake kileleni ni muhimu kuliko kufika wewe. Hii hutokea zaidi kwa wanawake warembo na wazuri na wanafanya hivyo na kukataa kuendelea na mchezo ambapo wanaume wengi kwa kubabaika kuachwa na wazuri wao hao wanawatii kwa kinyongo.

Akitaka yeye hata kama umechoka siku hiyo lazima anakulazimisha lakini yeye hata kama wewe umetingwa atakuambia hataki na amechoka, pia huuliza maswali na kujijibu mwenyewe...mfano''kwani wewe bado.....mimi tayari''

5.Jamvi la wageni na mchunaji

HIKI NDIO KINADAIWA KUWA CHANZO CHA WANAFUNZI WA ST ANE MARIE KUFANYA VURUGU

VuruguWanafunzi_4bb68.jpg


WANAFUNZI wa shule ya msingi na sekondari ya St Anne Marie Academy ya Dar es Salaam, wamefanya vurugu zilizoambatana na uharibifu mkubwa wa mali ikiwamo kuvunja vioo vya magari, mabweni, madarasa na kompyuta, chanzo kikidaiwa kuwa ni hatua ya uongozi wa shule kuwapa walinzi mamlaka makubwa ya kuwaadhibu.Mamlaka hayo walidai yameendelea kujidhihirisha kwa muda mrefu ambapo usiku wa kuamkia jana, mwanafunzi Loshilaa Emmanuel wa kidato cha sita, alipigwa na mlinzi na kushonwa nyuzi kadhaa, jambo lililosababisha wanafunzi wa bweni kuamka na kufanya vurugu za kuharibu mali baada ya kumkosa mlinzi aliyedaiwa kumpiga mwenzao.Vurugu hizo zinadaiwa kufanywa katika kipindi cha saa moja, kati ya saa nane usiku na saa 10 alfajiri jana na tayari Polisi Mkoa wa Kinondoni inashikilia wanafunzi tisa wanaodaiwa kuwa vinara wa vurugu hizo.

Wanane kati yao ni wa kidato cha sita na mmoja ni wa kidato cha nne. Mali zilizoharibiwa ambazo gazeti hili pamoja na kuelezwa, lilizishuhudia shuleni hapo ni pamoja na kuvunjwa vioo vya magari 17 ya shule, madirisha, taa na milango ya mbao katika madarasa yote hasa ya sekondari na ofisi, kompyuta 40 kuharibiwa huku nyingine 16 mpya za mpakato zikiibwa.

Viongozi wa wanafunzi waliozungumza na gazeti hili shuleni hapo jana, kwa nyakati tofauti walilaani vurugu hizo na kudai kuwa, lawama hazipaswi kuishia kwa wanafunzi pekee hata kama wamefanya kosa kisheriam kwa kuwa tukio hilo linahusisha malalamiko ya muda mrefu ambayo hayajashughulikiwa yaliyojenga uhasama baina ya walinzi wa shule, uongozi wa walimu na wanafunzi.

Miongoni mwa malalamiko ni pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari, Mary Msangi kuwapa mamlaka walinzi wa shule hiyo yenye wanafunzi wa kutwa na bweni kuanzia chekechea hadi kidato cha sita, kupiga wanafunzi wa sekondari kipigo chochote wanapokosa kutii sheria za shule.

“Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya wanafunzi kuhusu hawa maafande (walinzi) wetu, usiku wanapokea hongo na kuruhusu wanafunzi watoke huku wengine wakiwazuia, wengine wanaingiza vitu mpaka vileo, lakini wengine wakitaka kutoka kunazuka ugomvi, ni kama wana njaa kali, sasa kuna adhabu wanatoa zilizopitiliza ikiwamo vipigo,” alisema kiranja mkuu wa kiume wa kidato cha sita, Innocent Mwombeki.

Kiranja mkuu wa kiume wa kidato cha kwanza hadi cha nne, Hassan Haruni alisema kuna matukio ya kupigwa wanafunzi hata kwa makosa ya kurekebishwa pekee bila adhabu na kueleza kuwa, kabla ya tukio la jana, wanafunzi zaidi ya wanne walishapigwa na walinzi.

“Mambo yanakuwa mabaya zaidi kwa kuwa baadhi ya walimu viongozi wanahusika, kwa mfano hivi karibuni Mkuu wa Shule (Msangi) alitangaza katika mkusanyiko wa shule, kwamba amewapa mamlaka askari wapige wanafunzi ila wamwachie roho,” alisema Emma Mhagama, kiranja mkuu wa kike wa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Mkuu wa Shule Kiongozi Mkuu wa Shule Kiongozi, Johanssan Rwebugisa aliliambia gazeti hili ofisini kwake kuwa, ni mapema kuthibitisha madai hayo kwa kuwa mengi yalishashughulikiwa ingawa alikiri kuwa tukio la mwanafunzi kupigwa na mlinzi usiku wa kuamkia jana haliwezi kuwafanya wanafunzi washambulie shule nzima na kuharibu mali kama walivyofanya.

“Siwezi kuwa na maelezo mengi, ila hii inaonekana kuwa ni jambo la muda linalohitaji uchunguzi, hatutajua sababu hasa, kwa kuwa kama ni malalamiko kuna utaratibu wa kuyawasilisha na kushughulikiwa na hawajawahi kuyaleta kwangu, labda walipeleka kwa Mkuu wa Shule,” alisema Rwebugisa.

Akielezea kilichotokea, Rwebugisa alisema wanafunzi wa bweni, wengi wao wakiwa kidato cha sita, walifanya vurugu baada ya kupata taarifa kwamba mwanafunzi mwenzao aliyekuwa akijisomea, kapigwa na mlinzi.

Mwombeki alisema hana uhakika kama ni kidato cha sita pekee walihusika na vurugu, kwa kuwa saa nane usiku waliamshwa na wenzao kwenda kumsaidia aliyejeruhiwa na mlinzi baada ya kupishana kauli, na wakiwa zahanati ya shule, wanafunzi wa bweni wa vidato vya chini waliamka na kufanya vurugu wakati wao wakiwa zahanati na mwenzao.

“Inaelezwa Loshilaa alitaka kutoka nje, mlinzi akamzuia, wakaanza kubishana, ndipo mlinzi akachukua shoka, upande wa mpini akampiga nao, tuliposikia tuliamka ilikuwa saa nane usiku hivi, tukampeleka hospitali tukiwa wengi kiasi, tulikaa nje kumsubiri, wazazi wake walipofika wakamchukua na kumpeleka Kituo cha Afya cha Bochi, Kwa Musuguri, ndipo wengine wakaamka na kuanza kuvunja mali,” alieleza Mwombeki.

Kiranja wa kike wa Kidato cha Sita, Lidya Mkumbo alisema katika bweni la wasichana la kidato cha sita, walishuhudia wanafunzi wa kiume waliokuwa wamevaa kaptula bila mashati wakirusha mawe kwenye bweni lao na kuvunja taa ndipo mwalimu mlezi alipowaamuru waingie ndani na kuwafungia mlango kwa nje hadi saa moja asubuhi.

Mkumbo alisema awali walitoka baada ya kuelezwa kuwa mlinzi anapigwa huku baadhi ya wanafunzi wakidai kama ni mlinzi anapigwa ni bora aendelee kupigwa, kwa kuwa hakukuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu baina ya walinzi na wanafunzi.

Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana alitembelea shuleni hapo jana akifuatana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura na kuagiza chanzo kitafutwe na uchunguzi zaidi ufanywe, huku akielezea wasiwasi wake kuwa tukio hilo huenda likahusisha pia ushawishi wa walimu kutokana na uharibifu uliofanywa na wanafunzi.

“Siamini kama mwanafunzi mmoja kupigwa na mlinzi, adhabu inaweza kuwa ni uharibifu huu wa mali, ingeingia akilini kama tungesikia mlinzi kajeruhiwa baada ya kushambuliwa na wanafunzi kwa kumpiga mwenzao, ingawa nalo ni kosa kisheria, lakini kuna mantiki kuliko la kushambulia mali za shule namna hii, iko wapi nidhamu ya elimu?” Alihoji Rugimbana.

Alisema kama mwekezaji wa shule hiyo akiamua kufunga mradi huo na kufungua mwingine, hasara ni kwa Taifa, kutokana na mchango mkubwa wa sekta binafsi katika elimu, hivyo alisisitiza wanafunzi kuheshimu maadili na thamani kubwa ya ada wanayolipiwa na wazazi ama walezi wao kupata elimu hiyo.

Ada kwa sekondari katika shule hiyo inakaribia Sh milioni mbili kwa mwaka. Kamanda Wambura alisema polisi imeimarisha ulinzi eneo hilo hasa kutokana na kuwapo kwa wanafunzi watoto wa chekechea na shule ya msingi ambao vurugu kama hizo huwaathiri zaidi zikitokea na kwamba wanaendelea kuchunguza chanzo hasa cha tukio pamoja na thamani ya uharibifu wa mali.

Alitaja wanafunzi waliokamatwa kuwa ni Marko Mkemi, Mandela Soka, Fabran Fulena, Stanford Shomiki, Mwombeki Abdoni, Anyengise Frank, Amandus Kimano, Godfrey Ndimila wote wa kidato cha sita na Emmanuel Mtesha wa kidato cha nne. Msangi alipoulizwa kuhusu madai ya uongozi wa shule kuwapa mamlaka walinzi ya kupiga wanafunzi, alisema msemaji pekee wa shule kwa sasa ni Mkuu wa Shule Kiongozi ingawa alidai walinzi hao hawana mamlaka hayo.

Mmiliki wa Shule hiyo, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, alisema ameshtushwa na tukio hilo lakini hawezi kueleza chochote kwa kuwa hajui chanzo na kuwa leo, kutakuwa na mkutano wa dharura wa Bodi ya Shule, kuzungumzia suala hilo na hatua za kuchukua.

FALME ZA KIARABU WAONYESHA SILAHA ZAO MPYA ZA KIVITA ZA KISASA(MILLITARY WEAPON ROCKET LAUNCHER)




Hili ni jambo la kushangaza kabisa katika kukua kwa technologia Duniani kwa baadhi ya watu. Katika hili Majeshi ya Dunia yana zidi kujiimarisha katika Maswala ya ulinzi kwa kutengenezaa Sila zenye uwezo wa kufika masafa marefu, katika kuthibitiha hili Falme za kiarabu zimejiimarisha zaidi kwa kutengeneza silaha Zenye uwezo mkubwa ili kujilinda na mahasimu wao. . na hii ni silaha aina ya HEAVY ROCKET LAUNCHER, Gari hili limebeba mabom zaidi ya 240 na yote yanapigwa kwa dakika 2

Utafiti: Ngono ya mdomo ni hatari

Namna mdomo unavyoharibika kutokana na ngono kufanywa kwa kutumia mdomo.
Leo ni siku ya Saratani Duniani. Wakati tunaadhimisha siku hii hapa nchini idadi ya vijana ambao ni tegemeo la taifa inazidi kupungua kutokana kuangamia kwa saratani ikiwemo ya koo.Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Dunani (WHO) nchini umeonyesha asilimia 20 ya saratani ya koo husababishwa na ngono ya mdomo maarufu kama ‘Oral Sex”.Utafiti huo unaonyesha saratani ya koo licha ya kuambukizwa na njia mbalimbali ikiwemo ulaji wa vyakula vyenye pilipili,pombe kali, vitu vyenye uchachu pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.Utafiti unaonyesha watu wengi hasa vijana wanamejiingiza kwenye vitendo hivi vya kufanya ngono wakitumia midomo hasa  ndimi, hivyo kuhatarisha uhai wao.Katika utafiti  huo wa hivi karibuni, ulibaini wanaume 747  na wanawake wakiwa 472 hugundulika kila mwaka kuwa na saratani hiyo huku wanaopoteza maisha kila mwaka ni wanaume 444 wakifuatiwa na wanawake 270 kutokana na ugonjwa huo.
Utafiti unabainisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 45 wanatumia staili ya kuwanyonya wenza wao sehemu za siri lengo likiwa ni  kuwavutia wapenzi wao katika  kushiriki ngono.
Vijana  wenye umri huo ndio wahanga wakubwa kwa sasa kutokana na ugonjwa huo kuonekana kuwaathiri kwa kasi, huku wengi wakiwa hawajui athari zake. Baadhi hujisifia kwamba ni wajuzi, kumbe wanajitafutia kifo kwa kufanya vitendo hivyo.
Utafiti unaonyesha kwa watu wazima walio wengi hawana muda wa kufanya hayo wanayofanya vijana, hivyo kujikuta angalau wanakuwa salama na kupatwa na saratani ya koo kwa njia hiyo inayoonekana kama ni chafu pia.
Daktari  Bingwa wa Magonjwa ya Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa anasema saratani ya  koo ni  ya pili katika mtiririko wa saratani zinazowapata wanaume  nchini, ikiongozwa na ile ya  ngozi (Karposi’s Sarcoma) ambayo huambukizwa kwa njia ya kujamiana. Kuna saratani aina zaidi ya 24 zinazoisumbua Tanzania.
Anasema mbali na staili hiyo pia, kuna baadhi ya watu hupata saratani ya  koo kwa kurithi kutoka kwa wazazi wao na wengine kuwa na  umri mkubwa ambao huchangia kupata tatizo hilo, lakini siyo kwa asilimia kubwa kama ile ya ngono ya mgomo.
“Hali hii ya vijana wenye umri huo kuwanyonya wanawake inatokana na ujana, wengine wanaiga kwenye mitandao, lakini mambo haya hayakuwepo zamani tofauti na sasa, utakuta wanaume ili aweze  kumvutia mwanamke anamfanyia hivyo sehemu za siri, lakini zamani staili hii haikuwepo kabisa,” anasema  Dk Kahesa na kuongeza.
“Kuna njia nyingi tu za kumvutia mwanamke lakini siyo hii bila kujua madhara yaliyopo, vijana wengi nchini wanaona njia rahisi ya kupendwa na mwanamke ni hiyo wakati kuna njia nyingi za kufanya. Nje ya hiyo wanawake wengine huwa na magonjwa mbalimbali, kwa jumla hakuna usalama wowote kwa wanaume kufanya kitendo hicho,”anaongeza
Sababu nyingine zaidi
Anasema staili ya maisha nayo imechangia kuongezeka kwa ugonjwa huo, vijana wengi kwa sasa hutumia muda mwingi  kuangalia video za ngono na staili zinazofanywa na wenzetu wa nje na hivyo kuongezeka kwa matumizi ya ngono ya mdomo.
Dk Kahesa anasema asilimia 12 ya wagonjwa wote wa saratani  nchini wanasumbuliwa na saratani ya koo, hivyo kuna kila sababu kwa vijana kubadilisha tabia na kuepuka kuiga mitindo ya wenzetu wazungu ambayo mara nyingi inapotosha mila na tamaduni za Kiafrika.
Anasema  katika mtiririko wa saratani zinazoongoza nchini saratani ya koo  inashika nafasi ya tano, wagonjwa wengi wanaopatwa na ugonjwa huo ni watu wenye umri mkubwa wa miaka 60 na kuendelea  hiyo inaonyesha kuwa wengi wao walianza  ngono ya mdomo muda mrefu wakati wakiwa  bado wadogo.
“Asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatikana na kansa ya koo nchini, inawapata  watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea  kutokana na wengi wao kuanza mapema vitendo vya ngono kwa njia ya mdomo wakati  bado wadogo au wengine kurithi kutoka kwa wazazi wao,” anasema Dk Kahesa.
Aina ya kansa ya koo
Tafiti zinaonyesha kuna aina mbili za saratani ya koo; aina ya kwanza ni “Oesophagus Carcinoma na Squamous cell carcinoma, zote  hutofautiana wakati zinapimwa kwenye darubini lakini matibabu yake yanafanana.
Aina hizo ndizo zilizopo nchini na huanza mapema  kuharibu seli ambazo zipo katika  utandu uliopo katika ukuta wa koo kabla ya kuenea katika  maeneo mengine ya koo.
Visababishi vya kansa ya koo:
Moja kati ya vitu vinavyosababisha kansa ya koo ni mwenendo wa maisha yetu kwa kula vyakula vyenye  asidi, vyakula  vichachu, vyakula vyenye pilipili, pombe kali na  vyakula vigumu ambavyo hukwaruza koo na hivyo kusababisha saratani.
Anasema  asilimia 90 ya wagonjwa wanaopokelewa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean road wanakuwa na  historia ya kutumia vikali kama pombe kali, kuvuta sigara kwa kupindukia, kula pilipili kwa wingi na kutumia vitu vyenye uchachu.
Dalili za saratani ya koo
Moja kati ya dalili za  mgonjwa wa saratani ni chakula kukwama kwenye koo, siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate.
Ugonjwa huo unachukua muda mrefu kugundua na kuona  viashiria kwani mwanzo  mgonjwa huanza kupata shida kumeza chakula na kwamba wagonjwa wengi wanaofika katika Taasisi hiyo ya Saratani wanakuwa tayari wamechelewa  kwani wanakuwa katika hatua ya mwisho.
“Unaweza usionyeshe dalili lakini kadri  siku zinavyokwenda  ndiyo kunakuwa na dalili zinajitokeza pia katika kipindi hicho mtu anakuwa na maumivu wakati wa kumeza chakula, maumivu katika kifua na mgongo  na hata kupungua uzito pamoja na kikohozi kikavu kinachoweza kudumu mwezi mmoja,” anasema.
Njia ya kuzuia saratani ya koo.
Kwanza mtu mwenye ugonjwa huo anapaswa kuhawi hospitali ili aanze matibabu mapema kutokana na ukweli kwamba mgonjwa anayewahi kupata matibabu ana uwezekano wa kupona kuliko yule ambaye amechelewa kugundulika na kuanza matibabu.
Kama  saratani hiyo itakuwa imeshambulia viungo  vyote vilivyopo jirani na koo na hadi kufika katika tezi  au kiungo kingine cha mwili, mgonjwa anaweza kutibiwa  kwa njia ya upasuaji, kutumia mionzi na hata kifaa maalumu ambacho ni kemikali.
Tafiti zilizofanywa nchini
Wataalamu mbalimbali nchi wamefanya tafiti zinazohusiana na ugonjwa huo na kusema kuwa kati ya mwaka 1983 hadi 1992 kulikuwa na kati ya watu 546 waliopimwa,  wanaume 430 na wanawake 116 waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Utafiti huo ulishirikisha watu  wenye  umri wa miaka 21 hadi 90, ulibaini kuwa wagonjwa wengi walikuwa wenye umri wa miaka 50-59 tofauti na hali iliyopo sasa ugonjwa wa kansa ya koo unawaathiri vijana wenye umri wa miaka 40.
Dk Kahesa anasema katika kipindi cha miaka saba iliyopita takwimu za taasisi yake imeongezeka kutoka kutoka wagonjwa 167 hadi kufikia wagojwa 277. Hali inaonekana huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa watu wanaonekana kuendeleza tabia hatarishi zikiwemo hizo za kutumia midomo.
Magonjwa mengine sehemu za siri
Miongoni mwa magojwa ambayo yanaweza kumpata mtu ambaye ananyonya au kulambana sehemu hizo ni pamoja na gonjwa wa  gonoreha, ambapo ugonjwa huu huanzia katika koo na mwanzoni huhisi kama ni ukavu wa kifua au maradhi ya kawaida ya kifua, ila baadaye hushuka na kuelekea katika viungo vya uzazi.
Ugonjwa mwingine ni kaswende ambao huambukizwa kirahisi zaidi kupitia mdomo na hasa pale inapotekoa mdomo unapokutana na kiungo chenye athari hizo.
Vile vile ugonjwa wa chlamydia ni moja wapo kati ya magonjwa ya zinaa ambao huambukizwa kwa bakteria  na kwamba ugonjwa huu pia  huambukizwa kupitia mdomo, ingawa waathirika wanaweza wasijijue maana huwa hauna dalili kwa muda mrefu.
Hepatitis A: Hiki ni  ni kirusi kinachopatikana  katika kinyesi cha binadamu, kirusi hiki huwaingia wale wanaopenda kunyonya na kulambana sehemu za haja kubwa. Ni kwamba kwa ugonjwa huu mtu anaweza akaharibika macho hadi kupofuka.
Hepatitis B: Ugonjwa huu huambukizwa kama virusi vya Ukimwi kwa sababu virusi vyake hukaa katika majimaji yanayotoka katika sehemu za siri na damu. Mtu akiwa na ugonjwa huu, mwili wake unakuwa na vipele vingi na hata majipu ambayo huwa magumu kupona na wapo wanaokufa.
Vile vile ugonjwa wa Hepatitis C:  ni ugonjwa ambao hupatikana pindi damu inapotoka maana vijidudu vyake vinakaa katika damu. Ugonjwa huu humfanya mtu kuvimba viungo na hata kukatika.
Hata hivyo kupitia staili hii yaupeana raha kwa kunyonyana sehemu za siri, kuna uwezekano wa kupata maambukiz ya virusi vya Ukimwi kwa uchache lakini  kwa nchi zilizoendelea wamebuni aina ya kondom ambazo huvaliwa katika mdomo  wa binadamu na hivyo kupunguza hatari ya kupata madhara hayo.
JE NGUVU ZA KIUME ZINACHANGIA?
Dk Kahesa anasema  hakuna utafiti wa moja kwa moja unao onyesha kuwa baadhi ya wanaume wanaofanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na upungufu wa nguvu za kiume.
“Utafiti wa mtu mmoja hautoshi kuonyesha kuwa baadhi ya wanaume wanafanya ngono kwa njia ya mdomo wanakuwa na ukosefu wa nguvu za kiume, hivyo kinachotakiwa ni kufanya utafiti wa kina ili kubaini kama tatizo hilo lipo licha ya kuwepo kwa kesi nyingi zinazodaiwa kuwa baadhi ya wanaume hawana nguvu za kiume na wapenzi wao huwafichia siri kwa kufanya nao mapenzi kwa njia yam domo”anasema.
NINI KIFANYIKE:
Wataalamu wa masuala ya ndoa na saikolojia wanasema kuna njia nyingi za kuandaana wakati wa tendo la ndoa tofauti na kunyonyanyana sehemu za siri.
Wataalamu hao wanasema sio sahihi kwa mwanaume au mwanamke kunyonyana sehemu za ndoa mwenzake  na kwamba staili hizo  ni staili za wanzetu wa nje lakini kitu kinachosababisha kukua kwa kasi kwa staili hiyo ya kunyonyonyana sehemu za siri au kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo ni kutokana na kasi ya  utandawazi.
Wadadisi wa mambo wanadai kuwa baadhi ya watu huiga staili hizo kutoka katika mitandao bila kujali kuwa kuna zina  madhara makubwa, hivyo ni jukumu la kila mtu kulinda afya yake na ya mwenza wake.
Sio kila kitu kinachowekwa katika mitandao ya kijamii  kina  manufaa la hashaa!  vitu vingine vinachangia kuhatarisha maisha.
MWANANCHI

TAZAMA PICHA::ZA MWANAMKE WA MIAKA 64 AVUNJA REKODI KWA KUOGELEA KUTOKA CUBA MPAKA FLORIDA


Mwogeleaji mwenye umri wa miaka 64 kutoka Marekani, Diana Nyad ameweka rekodi mpya ya dunia katika kuogelea baada ya kufanikiwa kuogelea kutoka Havanna Cuba mpaka huko Florida Marekani.Ikiwa hii ni mara ya 35 mfululizo kufanya jaribio kama hili na kwa jumla ya hesabu, ameweza kukaa ndani ya bahari kwa masaa 52,  dakika 54, na sekunde 18.6, na aliweza kutoka mwenyewe mpaka beach kabla ya kuishiwa nguvu kabisa.
clip_image003

Safari ya mwanamama huyu imekuwa na umbali wa jumla ya maili 110 sawa na kilometa 180.
Safari zote ambazo mwanamama huyu amekuwa akijaribu kuvuka bahari amekuwa akipata changamoto kama vile kushambuliwa na samaki wakali wa baharini na mambo mengi ya kufanana na hayo lakini hakukata tamaa kujaribu tena na tena na safari hii amefanikiwa bila kutumia vifaa vya kujikinga.
Mwanamama huyu amesema kuwa amejifunza kuwa katika safari kufuatilia kutimiza ndoto zako, usikate tamaa hata siku moja, na hakuna swala la kizuizi cha umri katika kufuatilia ndoto zako.

HUYU NDO BAUNSA WA DIAMOND ANAYE LIPWA LAKI 5 KWA WEEK.




MBOWE AMJIBU JK kwa kuwapotosha wananchi!!!!!!!


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuacha kutafuta huruma ya Watanzania juu ya suala la Katiba na badala yake atumie nafasi hiyo kuwataka wabunge wake kuheshimu maoni ya wananchi.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete juzi kwamba Katiba haiwezi kupatikana kwa ngumi imejaa upotoshaji kwa wananchi.

“Huku ni kuwadanganya wananchi, pale hakuna ngumi wala vurugu yoyote, kila ibara iliyopo katika rasimu itajadiliwa ili upatikane mwafaka. Huku ni kukosa ukomavu wa kisiasa. Ni vema Rais Kikwete akaacha kuhangaika na wapinzani, badala yake awe tayari kuheshimu mawazo ya wananchi waliyotoa wakati wa kutoa maoni ya Katiba” amesema Mbowe.

Mbowe alisema kuwa Rais Kikwete ni mwanasiasa na mtu anayejaribu kupotosha hoja, kwani CHADEMA waliposema watapambana, hawakumaanisha kupigana ngumi kama alivyosema kiongozi huyo.

“Katiba ni ya wananchi, si ya chama chochote cha siasa, ndiyo maana hatukubali kuona mawazo ya wananchi yakishindwa kuheshimiwa,” alisema.

Alisema kuwa CHADEMA itahakikisha inashindana kwa hoja katika Bunge la Katiba litakaloketi hivi karibuni na iwapo hilo litashindikana watarudi kwa wananchi ambao ndio wenye uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo.

“Wajumbe watakaoshiriki Bunge la Katiba ni 640 ambao hao si waamuzi wa mwisho na kama tutaona kuna suala lolote linaloenda kinyume, sisi tutakachokifanya ni kurudi kwa wananchi kuwaeleza juu ya kilichotokea na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho katika kura ya maoni,” alisema.

Tuesday, February 4, 2014

‘Sabuni za kurudisha ubikira balaa' Wanawake waonywa..

DAWA ZISIZOFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU ZIKICHOMWA MOTO
WANAWAKE wameshauriwa kuacha kutumia sabuni za kunawia sehemu za siri ambazo hudaiwa kurejesha ubikira kwani zina madhara makubwa ikiwemo kusababisha kansa ya shingo ya kizazi. Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi wakati wa uteketezaji dawa, vipodozi na vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.
Kazi hiyo ilifanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati. Alisema kumekuwa na sabuni mbalimbali ikiwamo Kaisiki ambapo wanaoziuza wanadai zimekuwa zikisababisha bikira iliyopotea kurudi kitu ambacho si kweli.
“Sabuni hizo zinapunguza tu majimaji yaliyo sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo husababisha wakati wa kufanya mapenzi mwanaume kupata ugumu kwenye muingiliano kwa vile mwili unakuwa umekataliwa kutoa maji na hivyo kuleta michubuko kitu ambacho ni hatari hasa wenye maambukizi ya magonjwa,” alisema.
Alisema michubuko inapotokea ni rahisi mwanamke kuambukizwa magonjwa ya zinaa hata virusi vya Ukimwi. Mtaalamu huyo alisema sabuni hizo zinatengeneza hali fulani ukeni lakini haiwezi kurejesha hali ya maumbile iliyopotea.
Alisema wanaotumia sabuni hizo wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa na hata kupata saratani ya shingo ya uzazi kwani kemikali zinazotumika katika kutengeneza sabuni hizo zina athari kubwa kiafya.
Alisema ni vyema wanawake wakatambua thamani yao na kuachana na matumizi ya sabuni hizo ambazo hazina manufaa yoyote na badala yake zimekuwa na madhara makubwa kwao.
Kwa upande wake, Fredrick Luyangi , Mkaguzi wa dawa kutoka TFDA alisema matumizi ya sabuni hizo huleta athari kubwa mwilini na wakati mwingine kutengeneza kansa taratibu bila mhusika kufahamu.
Alisema sabuni hizo husababisha kansa ya kizazi na kubainisha sabuni hizo licha ya kupigwa marufuku zimekuwa zikiuzwa kwenye maduka ya vipodozi.
Alisema mara nyingi kwenye operesheni zinazofanyika zimekuwa zikiondolewa sokoni lakini hata hivyo zimekuwa zikiingizwa kwa wingi hali inayofanya zoezi la kudhibiti kuwa gumu.
Alisema ni muhimu kwa wanawake kuacha matumizi ya sabuni hizo ambazo zina madhara makubwa sana kwao kwani zikikosa wanunuzi zitaondoka sokoni.CHANZO HABARI LEO