Wednesday, February 12, 2014

UNALIJUA KABILA LA WACHAGA?SOMA HISTORIA YAO HAPA




Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro. Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.
Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga mkoani Kilimanjaro ni 200,000.
Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogo madogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia Mashariki Tarakea, Rombo hadi magharibi ya Kilimanjaro Siha, Machame. Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Marangu,Wa-Kilema, Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame. Makundi mengine madogo ya wachagga ni Wakirua-Vunjo, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga, inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro. Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kimarangu, Ki-Old Moshi,Kikibosho, Kimachame, Kikirua na Kisiha. Lugha hizi zinakaribia kufanana kulingana na jinsi makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Ki-Old Moshi kinafanana na Kikirua, ambacho nacho kinafanana kidogo na Kimarangu. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho. Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru Arusha na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Ki-meru. Kwa sababu hii Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Historia ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Kikristo walijenga makanisa na shule. Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamishinari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi. Wakati wakazi wa mikoa mingine walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1,2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro vimezidi sana idadi ya shule katika miko mingine yote.
Ni vema pia kusema kwamba shule hizi kuvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi wachagga tu.
Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe,viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.
Ndizi za Wachagga
Ingawa wachaga wa leo wanakula vyakula mbali mbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi. Kuna ndizi za aina mbalimbali na hutumika kwa matumiza tofauti. Mfano ndizi kisukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda. Ndizi mshare kukatwa zikiwa mbichi na kupikwa chakula mbalimbali pamoja na nyama ya ngombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko,kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi-ngombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi-mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Darisalamu utaona ndizi- mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku-vumbi au kiti-moto.
Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa "mchagga halisi, hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yao; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani hasa wa Machame walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba huko huko Kilimanjaro, majirani na watani wa wachagga yaani Wapare walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
Majina ya Kichagga
Majina ya kiukoo ya Kichagga pia huashiria wanatoka sehemu gani ya Uchaga, japo si lazima kuwa hivyo: mfano familia maarufu za Kichagga nchini Tanzania ni kama ukoo wa akina Mushi,Kimaro, Swai, Massawe, Lema, Urassa, Nkya, Ndosi, Meena hutoka Machame. Akina Temu, Mlaki, Mlay, Lyimo, Moshiro, Mselle, Kileo, Kimambo, Tesha wanatoka Old Moshi na Vunjo. Kavishe,Mariki, Tarimo, Laswai, Mallya, Mrema, Mkenda, Massawe, Lyaruu, Makyao, Mowo, Lamtey, Tairo, Mramba, Kauki wanatoka Rombo. Sawe, Usiri, Shayo, Kiwelu, Makundi, Urasa, Mtui, Moshi, Meela, Minja, Njau wanatoka Marangu na Kilema. Rite, Makule, Minja, Mashayo, Chao, Shao, Makawia, Ndesano, Kimario, Tilla, Mariale, Tarimo, Mafole, Kituo, Mrosso, Lyakundia, Kessy, Mmbando, Matemba, Ndenshau, Morio, Akaro, Matowo, Towo, Mkony, Temba na kadhalika hutoka Kibosho.Ukoo wa akina Teri wako Mamba Kiria na wachache Sango, Old Moshi na wengine walihamia Maji ya Chai, Mkoa wa Arusha.
Wachagga wengi hupenda kurudi nyumbani kipindi cha Krismasi, ikiwa ni kuwatembelea wazazi wao, rafiki, au ndugu. Ingawa wengi hudhani kwamba Wachagga wameathiriwa sana na dini ya Ukristo kwa kuwa wengi wao ni Wakristo na hiki huwa ni kipindi cha likizo kwao, inaaminika pia kuwa kurudi kwao Uchagani wakati wa Krismasi ni pamoja na kutembelea ndugu zao na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka baada ya kazi nyingi za kutafuta pesa kwa mwaka mzima.
Utawala wa jadi ya Wachagga
Watawala wa kichagga waliitwa "Mangi". Hawa walihodhi mashamba, ngombe na waliheshimiwa kama viongozi wa kikabila. Walikuwa na nguvu za kisiasa na utajiri. Baadhi ya ma-mangi mashuhuri katika historia ni kama Mangi Rindi aliyeingia mikataba na wakoloni (wajerumani), Mangi Sina wa kibosho - anajulikana kwa uhodari wake wa vita katika kupigana na wamachame na kupora ngombe na mazao yao na Mangi Marealle wa Marangu na Vunjo. Wakoloni walipokuja Kilimanjaro waliingia mikataba na viongozi hawa wa kikabila ili kuweza kuweka misingi yao ya kikoloni. Pia ndugu na watoto wa ma-Mangi walikuwa wa kwanza kupata elimu ya kikoloni, kwa hiyo waliweza kushirikishwa katika serikali za kwanza. Hawa pia wanaaminika walikuwa ni kama mabepari wa kwanza wa ki-jadi, maana walifanyiwa kazi na watu wengine wakati wao ma-mangi wamekaa kuhesabu mali zao. Usemi maarufu wa "u-Mangi-meza" nadharia
inawezekana kuwa umetokana na watawala hawa wa kichagga.
Ardhi
Ingawa ardhi ni msingi wa maendeleo kwa watu wote, kwa wachagga, ardhi ni mali sana kwa sababu kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na ndizi hukaa shambani kwa muda wa miaka mingi. Mojawapo ya urithi wapewayo watoto ni "kihamba". Hii ni sehemu ya ardhi ambayo mtoto anategemewa atajenga na kuanzisha familia yake. Bahati mbaya watoto wa kike walikuwa hawapewi kipaumbele katika ugawanaji wa vihamba. Uhaba wa ardhi uchagani ulipelekea wachagga wengi kuhamia mikoa mingine. Hivi leo utakuta wachagga wakiishi Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya nk wakiwa wamepanda migomba yao na kuendesha biashara za maduka ya vyakula. Ukienda kwenye mikoa hii utakuta wamejenga jamii zao na vyama vyao vya kusaidiana wakati wa sherehe au matatizo. Aidha hata pombe ya mbege utaweza kuikuta katika makusanyio ya wachaga mikoani mbali mbali.
Maoni juu ya Wachagga
Ingawa wanaume wa kichagga hupendelea kufanya kazi mbali na kwao, wake zao hukaa nyumbani (Moshi) na hufuga ngombe na kazi za shambani. ila kwa sasa kutokana na ugonjwa wa ukimwi tabia hii imepungua miongon mwao. Wanawake wa kichagga (hasa kutoka Rombo) hujulikana kama wafanyakazi hodari. Huchangia sana katika mapato ya nyumbani na chakula. Ingawa kipato cha wachaga ni kikubwa kulinganisha na cha makabila mengine, takwimu zinaonyesha watoto wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuongoza kwa utapiamlo. Sababu kubwa ya watoto kuwa na utapiamlo kunatokana na wazazi kujali zaidi kazi kuliko muda wa kuwahudumia watoto. Wengi wa wototo ni wale ambao wazazi wao ni watu wapombe na kipato chao kinaishia kilabuni. Utaona kwamba uchagani kuna vilabu vingi vya pombe na vinaongezeka kwa sababu imekuwa nibiashara kubwa. Karibu kila kaya kumi natano kuna kila cha pombe na kiwango cha chini kabisa cha pombe inayouzwa kwa siku katika vilabu hivyo si chini ya dede sita au lita mia moja. Pombe ni sababu moja ya watoto kuwa na utapiamlo Hii inawezekana kuwa matunda ya wazazi kutowalisha watoto wao chakula cha kutosha au chakula bora. Kuna sehemu nyingine za Uchaggani kama Old Moshi na Kibosho ambapo watoto wadogo hupewa pombe ya mbege asubuhi mchana na jioni. Sababu nyingi ni kazi; mama wa kichagga anaweza kushinda shambani kutwa na hawana desturi ya kubeba watoto mgongoni kwenda nao shambani hivyo wanakuwa nyumbani ama wenyewe au na mayaya. Mfano ulio dhahiri ni nyakati za asubuhi na mapema kwenye vyombo vya usafiri karibu robo tatu ya abiria ni wanawake wakienda katika shuguli za kibiashara na kilimo na vivyo hivyo nyakati za jioni wakirudi majumbani. Hao ni nje ya wale wanaotumia usafiri wa miguu ambao ni wengi zaidi. Pia baadhi ya wamama wa kichaga wanawajali waume zao zaidi kwani nyama nzuri ni ya baba. Kuepuka gharama baba ataandaliwa chakula kizuri tofauti na chakulawalichoandaliwa watoto japo ni chakula kilekile.pia wachaga wamekua na desturi ya kuwaenzi wazee wao walio tangulia mbele za haki kwa kuwatambikia kwa pombe na nyama za mbuzi pale tu wanapo rudi nyumbani ifikapo mwezi desemba. hili limekua ni swala la kawaida sana na halipingiki. wengi wao huwa wanarudi na magari ndio sababu utaona ya kwambwa kila ifikapo mwezi desemba kila mwaka foleni za magari zimekua zikiongezeka kutokana na wachaga kurudi nyumbani msimu wa sikukuu. wengi wao wamekua wakitoka sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi,Dj sek blog

TAZAMA PICHA ASKARI MAGEREZA NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA PRISONS AKAMATWA AKIUZA TIKETI FEKI UWANJA WA SOKOINE MBEYA




Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Tukuyu Stars na Prisons vya Mbeya John Joseph amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya akiuza tiketi bandia kwenye mchezo wa Mbeya City na Mtibwa Sugar.

John Joseph ambaye kwasasa ni askari wa jeshi la Magereza mkoani humo,alikamatwa na tiketi tano bandia akiziuza nje ya uwanja wa Sokoine.

Akiongea hapo jana usiku kwenye  kipindi cha SPORTS BAR cha Clouds TV kinachoruka kila ya Jumatatu, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya ndugu Ahmed Msangi alithibitisha kukamatwa kwa askali huyo na kusema uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani.

 Hapa John Joseph akiwa ameshikiliwa na polisi.
 Tiketi halali.....imeiva....
Hii ilikuwa tiketi feki......imepauka.CHANZO SHAFFIH DAUDA

Ripoti:Wasiojua kusoma na kuandika waongezeka

wasiojua 56c71
 
Moja kati ya sababu inayochangia wanafunzi wa shule za msingi kumaliza shule bila kujua kusoma na kuandika inatokana na kukosa mwongozo kuanzia ngazi ya familia kushindwa kuwanunulia vitabu vya kujisomea.
Ni kwamba familia nyingi hazina utamaduni wa kusoma vitabu, hali ambayo inasababisha pia kutowashawishi hata watoto wao kusoma vitabu.
Idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika
Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) inasema watu wasiojua kusoma na kuandika Duniani wamefikia 774 milioni .
Ripoti hiyo inaeleza wazi kuwa idadi kubwa ya watu hao wasiojua kusoma na kuandika wengi wao wanaishi katika bara ya Afrika na Asia, na kwamba takwimu hizo zinaonyesha kiwango hicho kimeongezeka wa asilimia nane kuanzia mwaka 1990.
Kwa upande wa Tanzania hadi kufikia mwaka 2002 idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ilikuwa watu 6.2 milioni. Idadi hiyo ni kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ambao ni sawa na asilimia 31, lakini kwa sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu zaidi ya milioni 14.
Mtaalamu wa Masuala ya Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT) John Masanja, anasema zaidi ya watu 14milioni hawajua kusoma na kuandika hapa nchini na kwamba idadi hiyo inasababisha washindwe kujitambua na kujishughulisha, hivyo kusababisha umasikini .
Masanja anasema Serikali ina wajibu wa kuboresha mifumo yake ya utoaji wa elimu, kwani bila kufanya hivyo kuna uwezekano wa kurudi nyuma kimaendeleo na kiuchumi kutokana kuendelea kuwa na watu wasiojua kusoma wala kuandika. Kutokana na tatizo hilo, Mradi wa Vitabu vya Watoto nchini uitwao Children Books Project (CBP) umeanzisha progamu ya usomaji wa vitabu katika shule za msingi 196 zilizopo katika wilaya 14.
Lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kujenga utamaduni wa kusoma kwa watoto wa shule za msingi kwa kuwapatia mafunzo na vitabu bora vya kujisomea.
Mratibu wa Mafunzo na Ufuatiliaji kutoka CBP, Marcus Mbigili anasema tathmini ya watoto wa shule za msingi inaonyesha kuwa watoto wengi hawana uwezo wa kutosha wa kusoma.
Anasema Mradi wa Vitabu vya Watoto ulianzishwa mwaka 1991 kutokana na hali mbaya iliyokuwepo ya ukosefu wa vitabu vya kujisomea hasa vitabu vya watoto.
Mbigili anasema katika awamu ya kwanza ya mradi huo, kazi kubwa ilikuwa kushirikiana na wachapishaji kuchapa vitabu vya watoto huku awamu ya pili ilikuwa na malengo ya kushirikiana na wachapishaji kuchapa vitabu, kushirikiana na walimu, kuboresha ujuzi wa kusoma na kuimarisha wadau wa tasnia ya vitabu.
Mratibu huyo anafafanua kuwa katika awamu ya pili, pamoja na kuwepo idadi kubwa ya vitabu vya watoto, bado kulikuwa na matatizo ya kusoma miongoni mwa wanafunzi katika shule mbalimbali hapa nchini.
"Kutokana na matatizo haya, mradi wa CBP ulizindua programu ya usomaji wa vitabu kwa baadhi ya shule za msingi kwa lengo la kumfanya mtoto asome kwa maana ya kupata maarifa, ufahamu na burudani"anasema Mbigili.
"Programu hii ilianza kwa majaribio katika shule sita za Mkoa wa Dar es Salaam na sita kwa Mkoa wa Pwani na kazi kubwa ilikuwa ni kutoa mafunzo kwa walimu wa shule hizo mbinu za kufundishia, uanzishwaji wa maktaba, uandaaji wa vitabu na zana za kufundishia,"anaongeza.
Shule zilizopo katika mradi huo wa CBP
Mpaka sasa jumla ya shule 196 kutoka wilaya 14 za hapa nchini zimeunganishwa katika mradi wa huo na kwamba wilaya hizo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Mkuranga, Bagamoyo, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Morogoro Mjini na Morogoro Vijijini, Kilosa, Kisarawe, Rufiji, Mvomero na Kongwa mkoani Dodoma. Chanzo: mwananchi

FUKWE ZA TANZANIA UCHOCHORO WA DAWA ZA KULEVYA

Baada ya kikosi kazi cha Jeshi la Polisi cha Kudhibiti Uharamia Baharini kukamata kilo 201 za dawa za kulevya aina heroini zilizokuwa zikiingizwa nchini kutoka Iran. Sasa imefahamika kuwa madawa ya kulevya yanapitishwa kwenye bahari ya hindi. Hii imethibotishwa  kwenye gazeti la MWANANCHI kutoa maelezo ya kina kuhusu madawa hayo.
 Polisi wa kikosi  kupambana na dawa za kulevya wakizifungua dawa hizo zilizokamatwa jana kwenye jahazi liitwalo Kunarak-Iran iliyokutwa katika bahari ya Hindi eneo la Tanzania ikiwa na Heroin kilo 201, pamoja na raia wa nane wa Iran na  wapakistan wanne.Picha na Michael Jamson
Gazeti la mwananchi linaeleza kuwa; wakati vita ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya ikiendelea nchini, wasafirishaji wa dawa hizo wameanza kutumia fukwe ndogondogo za bahari nchini kuziingiza kutoka Mashariki ya mbali, gazeti hili limebaini.
Januari 10, mwaka huu saa 6:30 usiku, mwandishi wetu alishuhudia mzigo unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya, ukishushwa kutoka kwenye boti, eneo la Salender Bridge, nyuma ya Kituo cha Polisi kilichopo eneo hilo.
Baada ya boti hiyo kutia nanga, walishuka watu zaidi ya 10; Wazungu wawili, Waafrika kadhaa na mmoja mwenye asili ya Asia na kuungana na wengine wanne ambao tayari walikuwa katika eneo hilo wakiwa ndani ya magari mawili.

Mara moja walianza kupakua mizigo iliyokuwa imefungwa kwenye maboksi na kupakia kwenye magari ambayo yalikuwa yameegeshwa mbali kidogo na ufukwe huo. Kazi hiyo ilichukua muda usiozidi nusu saa na baada ya mizigo kupakiwa, magari hayo moja likiwa ni Land Cruiser liliondoka na kuelekea upande wa Morroco na jingine aina ya Nissan liliondoka kwenda uelekeo wa Posta Mpya.
Wakati magari hayo yakiondoka kwa mwendokasi, boti iliyokuwa na mzigo huo nayo iling’oa nanga na kuelekea katikati ya Bahari ya Hindi.
Chanzo chetu kilisema mzigo ulioshushwa ni dawa za kulevya na kwamba boti hizo ndogo hufika eneo hilo hata mara mbili kwa wiki.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa dawa hizo huingizwa nchini kwa meli kubwa za mizigo, hasa zile zinazotoka Iran, Pakistan na Afganistan.
Ukamataji polisi
Mwandishi wetu aliwasiliana na polisi kuhusu njia hiyo ya kuingiza dawa za kulevya nchini na jeshi hilo kuahidi kutoa majibu baada ya kufanya ufuatiliaji. Kabla ya kutoa majibu juu ya ufuatiliaji huo, polisi ilikamata meli kutoka Iran ikiwa na kilo 201 za heroini katikati ya Bahari ya Hindi.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kama taarifa hizo zingeripotiwa katika vyombo vya habari, ingekuwa vigumu kwa jeshi hilo kufanikisha kukamatwa kwa wahusika.
Katika wiki moja iliyopita, kilo 846 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh38 bilioni zimekamatwa kwenye mipaka ya Tanzania iliyoko katika eneo la Bahari Kuu, kiwango ambacho ni kikubwa katika rekodi ya kukamatwa kwa dawa za hizo.
Dawa hizo zilikamatwa kati ya Februari 2 na 5 mwaka huu. Kilo 350 za heroini zilikamatwa Februari 5 na wadhibiti wa dawa za kulevya wa Australia na kilo 265 za heroini zilikamatwa na wadhibiti wa kimataifa wa Canada, zote zikiwa zinaelekea Tanzania.

Dawa nyingine ni kilo 201 za heroini zilizokamatwa ndani ya mpaka wa Tanzania na Kikosi cha Polisi cha Wanamaji na kilo 30 zilizokamatwa Zanzibar.
Kamishna Msaidizi wa Tume ya Kuratibu Dawa za Kulevya, Aida Tesha alisema, kiasi hicho kikubwa kilikamatwa na wadhibiti wa bahari wa kimataifa walioshirikiana na wadhibiti wa Tanzania.
“Huu msimu ni wa wasafirishaji wa dawa za kulevya kwa njia ya maji. Ni wakati ambao wasafirishaji huleta dawa kwa wingi kwa sababu ya hali ya hewa. Ieleweke kuwa zinazokamatwa ni asilimia 10, tu. Wapo wengi ambao wanapita bila kubainika,” alisema Tesha.
Tesha alisema wadhibiti wa kimataifa wanapokamata dawa huziharibu majini ili kuwapa hasara wauzaji hao kwani wanapowaacha au kuzikabidhi kwa nchi zilizo mipakani, zinaweza kuwafikia watumiaji. Mkuu wa Interpol, Tawi la Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Gustav Babile alisema hana taarifa za kina za kukamatwa kwa kiasi hicho cha dawa za kulevya isipokuwa wenzake wamemtumia taarifa hizo akiwa Algeria.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu alisema: “Nina taarifa za Kilo 201 za heroini, ambazo watuhumiwa wake 12 Raia wa Iran na Pakistan tayari wameshafikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yao”.
DCI Mngulu alisema polisi wanaendelea na doria kwenye maeneo ya bahari kwa kutumia mbinu zote ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua.
Kwa upande wake, Kamishna wa Kikosi cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema: “Ni kweli hicho ni kiasi kikubwa kukamatwa kwenye mipaka ya Tanzania na kinaonyesha kuwa watu hawa wanadharau mipaka yetu, pia kunaonyesha kuwa tunafanya misako mikali.”
Fukwe nyingine
Uchunguzi ulibaini kuwa fukwe nyingine ndogo za Dar es Salaam zinatumika kushusha dawa za kulevya bila kugundulika kwa urahisi na kukwepa nguvu nyingi za udhibiti ambazo zilikuwa zimewekwa katika viwanja vya ndege na mipaka ya barabara.
Miongoni mwa fukwe hizo ni Mbezi Jogoo, Dar es Salaam na eneo maarufu la Loliondo ya Kigamboni ambako pia kunadaiwa kuwa na vitendo vya kutisha vya ukahaba, biashara ya pombe haramu ya gongo na bangi.
Uchunguzi umebaini pia kuwa katika eneo la Loliondo, wavuvi hutumika kubeba dawa hizo kwa kutumia boti kutoka kwenye meli kubwa na kufikisha mizigo husika nchi kavu ambako hupokewa na watu maalumu na kuanza usambazaji.
Katika Pwani ya Bagamoyo, kiasi kikubwa cha dawa za kulevya hupitishwa na mara nyingi huwa zimefungashwa kama makopo ya samaki waliosindikwa.
Mkoani Mtwara, wasafirishaji hutumia fukwe ndogondogo kama za Mikindani kuingiza dawa hizo ambazo baadaye husafirishwa kupelekwa Msumbiji.
Katika Mkoa wa Lindi, maeneo ya Songo Mnara, Kilwa nayo yanatajwa kwamba yanatumika kuingiza dawa za kulevya kutoka Dar es Salaam na Zanzibar.
Uchunguzi wetu umebaini baadhi ya mbinu za kusambaza dawa hizo mitaani. Mizigo hufungwa kwenye khanga au matenga ili isitiliwe shaka na kisha kupelekwa mitaani kwa miguu na watu kati (middlemen) ambao hulipwa ujira kwa kazi hiyo.
Katika siku ambazo kuna wasiwasi au hofu ya kukamatwa, mizigo hufukiwa ardhini hadi hali inapotulia.
Kamanda wa Kikosi cha Wanamaji, ACP Mboje Kanga alisema kwa Tanzania ni kazi ngumu kusimamia fukwe na uharamia unaofanyika, kwani ina fukwe zenye urefu wa kilometa 1,424.
Ripoti ya 2013 ya Kitengo cha Uhalifu na Dawa za Kulevya cha Umoja wa Mataifa (UNODC), inataja Bahari Kuu kuwa njia kuu zinazotumika kusafirisha dawa za kulevya hadi Tanzania hasa Tanga na Zanzibar, kisha kusafirishwa kwa boti ndogo kwenda Dar es Salaam na baadaye nchi za Kusini mwa Afrika.
Kadhalika, taarifa ya 2011 ya kitengo cha dawa za kulevya iliyochapishwa katika Ripoti ya Kitengo cha Dawa za Kulevya cha Marekani inaeleza kuwa, heroini huingia Tanzania kupitia Bahari ya Hindi ikitokea Afghanistan, Iran na Pakistan kupitia Dubai.
 MWANANCHI

SUMAYE APOKELEWA NA MABANGO YANAYOMUHUSU LOWASSA AKIWA JIJINI MWANZA JIONEE


                IMEANDIKWA NA Shadrack Mgaya  
 Hapa ni baadhi ya washiriki kwenye kongamano lilofanyika katika ukumbi wa nyanza jijini mwanza washiriki walikuwa wanafunzi wa vyuo jijini mwanza
 Mh. Sumaye akizungumza katika kongamano hilo leo




 waandishi wa habari nao hawakuwa nyuma katika kongamano hiliwalikuwepo na walifuatilia kwa makini pia 




 Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa

 Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa















 Baadhi ya wageni waalikwa waliokuwepo katika kongamano hilo wakiwa wanafuatilia kwa makini kabisa

Bandari sasa kutoa huduma saa 24

Meli ikishusha mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Mamlaka ya Bandari Tanzania na wadau wake kuanzia sasa wataanza kufanya kazi saa 24

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wadau wake, kuanzia sasa wataanza kufanya kazi kila siku kwa mwaka mzima ili kuongeza ufanisi ikiwa ni utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
 
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shaaban Mwinjaka alisema hayo jana wakati wa utiaji saini makubaliano kati ya wizara hiyo, TPA na wadau mbalimbali.
 
Mwanjika alisema lengo la mkataba huo ni kuhakikisha TPA kwa kushirikiana na wadau wote, wanafanya kazi kwa saa 24, siku saba za wiki kwa mwaka bila kupumzika.
 
Miongoni mwa wadau 15 waliotiliana saini ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Chama cha Wakala wa Forodha na Uondoshaji Shehena Tanzania (Taffa), Benki za NMB, CRDB na Chama cha Wenye Magari ya Mizigo (Tatoa).
 
Kabla ya mpango huo, bandari imekuwa ikifanya kazi kwa saa 24 kwenye maeneo muhimu, lakini wadau wamekuwa wakifanya kazi kwa muda wanaojipangia wenyewe hivyo kukwamisha baadhi ya kazi.
 
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Madeni Kipande alisema kila mdau atatakiwa kutekeleza wajibu wake kama mkakati wa kufikia malengo ya mpango huo.
“Hivyo mdau yeyote asipotekeleza yaliyo kwenye mkataba, atakuwa amekwamisha mkakati mzima,” alisema Kipande.
wa kuboresha shughuli za bandari zetu,” alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wadau hao, Mwenyekiti wa Taffa, Steven Ngatunga alisema wizara hiyo itatakiwa kuwachukulia hatua wadau wasitekeleza wajibu wao.
“ Mizigo inapocheleweshwa kutolewa bandarini kuna wanaofaidi na kuna wanaoumia, hii ina maana wenye mizigo wanatozwa faini lakini kuna wadau wanaosababisha hilo hawatozwi faini, sasa hivi yoyote atakayechelewesha mizigo apewe adhabu,” alisema.
Ngatunga ambaye alitishia kutosaini mkataba huo kutokana na mapungufu yaliyopo, baadaye alisaini baada ya Katibu Mkuu kumweleza kuwa kila wakati kutakuwa na mabadiliko yenye lengo la kuboresha mpango huo.
Aliipongeza Serikali kuwa kuanzisha mpango huo wenye lengo ya kuboresha ufanisi katika bandari hiyo.
“Napongeza kuanza kwa utekelezaji wa mpango huu licha ya kuchelewa kuanza kwa sababu nilishatoa ushauri miaka mingi iliyopita,” alisema.
Wadau wengi waliotia saini ni Mkemia wa Serikali, wizara ya Ujenzi, Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Uvuvi na Mifugo, Wakala wa Vipimo na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
Wengine ni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Kampuni ya Kupakia na Kupakua Makontena Bandarini (Ticts).
Chanzo;Mwananchi.

MAKAO MAKUU YA CHADEMA YANUSURIKA KUUNGUA MOTO TAZAMA PICHA


gari ya matangazo ya chadema ikiwa imeungua upande mmoja

Makao makuu ya chama cha demokrasia na maendelea Chadema yaliyopo jijini Dar es salaam yamenusurika kuteketea kwa moto baada ya watu wasiojulikana kufanya jaribio la kulipua makao hayo usiku wa kuamkia tarehe 11 Febuari mwaka huu.
  Waandishi walifika katika makao makuu ya chama hicho na kushuhudua askari wa upelelezi wakiendelea na hatua za awali za upelelzi huku katibu mkuu wa chama hicho Dkt Wilbrodi Slaa akilaani kitendo hicho na kutaja tukio Hilo ni mwendelezo w
a matukio ambayo yamekuwa yakikikumba chama hicho na kuitaka serikiali kuwa makini na vitendo hivyo kwani vinaweza kuchangia upotevu wa amani hapa nchini.

Aidha Dr Slaa amefafanua kauli yake aliyowahi kuitoa kwa rais Kikwete kuwa kama hata ingilia kati vitendo hivyo nchi haitatawalika kwani itafika kipindi vitendo kama hivyo havitavumilika miongoni mwa Watanzania na kuitaka serikali iingilie kati ili wale wote wanaoendelea kufanya vitendo hivyo wawezea kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

MWALIMU AJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KALENGA KUPITIA CHADEMA


Katibu wa Chadema  Wilaya ya Iringa Vijijini, Felix Nyondo (kulia) akipokea fomu kutoka kwa Mwalimu Vitus Lawa (kushoto). Fomu hizo ni kwa ajili ya kuwania kinyang'anyiro cha kuwa mgombea wa Chadema Jimbo la Kalenga, Iringa. Baadhi ya wadau waliomsindikiza Mwalimu Vitus Lawa kurejesha fomu za kuchaguliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Kalenga katika ofisi za chama hicho zilizoko kata ya Gangilonga, Iringa. Mwalimu Vitus Lawa akizungumza na waandishi (hawapo pichani) baada ya kurudisha fomu za kuwania kuchaguliwa Ubunge wa Jimbo la Kalenga katika ofisi za chama hicho zilizoko Kata ya Gangilonga, Iringa.

(Picha zote na Denis Mlowe

Tuesday, February 11, 2014

VIGOGO TBA WAHUKUMIWA MIAKA 9 JELA‏ KWA KURUHUSU JENGO REFU KUJENGWA KARIBU NA IKULU

 
Vigogo wa TBA, Makumba Kimweri (kulia) na Richard Maliyaga (kushoto) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar! (Picha na Maktaba).

VIGOGO wa Wakala wa Majengo (TBA), Makumba Kimweri na Richard Maliyaga walioruhusu ujenzi wa jengo linalochungulia Ikulu wamehukumiwa kwenda jela miaka 9 kila mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni 15 kila mmoja na Hakimu Sundi Fimbo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar!

MAMBO YA KUANGALIA UNAPOKUWA NA MARAFIKI WA KAZINI


Katika mazingira yoyote ya kazi, watu wana marafiki ambao huhisi kuwa zaidi ya mtu “unayefanya nae kazi tu” mahusiano haya ya kazini husaidia kazi kufanyika, lakini kuna mambo ambayo yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa unapokuwa na marafiki wa kazini;
  • Kama shule ya msingi, ofisini kuna watu wakorofi, waongo, wenye hasira kali, wanafiki, wambea, wavivu. Kwa bahati mbaya mambo ya namna hiyo hayaishi kiwepesi .
  •  
  • ama umejikuta ofisini umeangukia kundi la watu ambalo hujitenga na wafanyakazi wengine, wasengenyaji, wenye kufuatilia maisha ya watu jiondoe kwenye kundi hilo. Kama shule kuna mtu atakuja kuliondoa kundi hilo, hivyo angalia usijeondoka nalo. .
  •  
  • Jaribu kuwa rafiki wa kila mtu, hata kwa wale ambao hawako karibu na wewe. Huwezi amini jinsi watu wanavyowapenda watu ambao ni wacheshi na ni marafiki wa kila mtu, itasaidia wakati unauhitaji au tatizo watu wengine wakusaidie.
  •  
  • Kitu cha muhimu na ushauri unatakiwa kuwafahamu vizuri marafiki zako wa kazini wakoje. Kwa kila kitu kinachoendelea ofisini, siasa zake, siri, tumaini, ndoto usijeukaruhusu mtu asiye rafiki wa kweli kukugeuka au kukusaliti na kuharibu mwelekeo wa taaluma yako. Hatua ya kwanza fahamu hulka za rafiki wa kazini na tabia zao kabla ya kuanza kuwashirikisha na kuongea vitu vingi kuhusu wewe.
  •  
  • Kwa wafanyakazi wote, marafiki au sio marafiki , fanya utani kwa umakini wakati wote uonekane kikazi.
Nenda kwenye matukio ya kiofisi, fanya utani unaohusiana na kazi, kula na kufurahi