Sunday, June 12, 2016

B​ARCLAYS CUSTOMERS TO OPEN A BANK ACCOUNT IN 20 MINUTES.

Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (second left) and banks Head of Operations, Msungu Mwilingo (second right), displaying placard to official launch the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar and banks Head of IT, Dakshit Pandya. 
Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (second left) addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Ag. Head of Marketing and Corporate Affairs, Joe Bendera, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.
Barclays Bank Tanzania (BBT) Ag. Head of Marketing and Corporate Relations, Joe Bendera (centre), addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Head of Customers Network, Emmanuel Katuba, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya. 
Barclays Bank Tanzania (BBT) Head of Customers Network, Emmanuel Katuba (centre) addresses a media conference in Dar es Salaam at the weekend during the official launching ceremony of the Barclays 20 minutes account opening service in Dar es Salaam at the weekend. Looking on from left are, BBT Head of Change, Aleem Thawar, Ag. Head of Marketing and Corporate Affairs, Joe Bendera, Head of Operations, Msungu Mwilingo and banks Head of IT, Dakshit Pandya.

Saturday, June 11, 2016

MASAUNI ALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI MWANZA, ATOA RAMBIRAMBI KWA WAKE WA WALIOUAWA MSIKITINI.


 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi (wa tatu kushoto) pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia mapango ya utemini, jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya kupambana na majambazi baada ya majambazi hao kufanya mauaji katika msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani jijini humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini huo.
 wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa.
 Mzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akitoka kukagua nyumba za makazi ya askari Polisi zilizopo katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, nyumba hizo zimetengewa fedha kwa ajili ya kumaliza ujenzi katika mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa pole askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na majambazi wakati wa mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika mapango ya utemini, jijini Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi ya Mabatini, jijini humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na askari polisi katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, ambao walipambana na majambazi na kufanikiwa kuwakamata wakati wa operesheni hiyo. Majambazi hayo yalijificha katika mapango ya Utemini jijini humo na ndipo yakavamiwa na polisi mara baada ya kuvamia msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani jijini humo na kufanya mauaji. Masauni aliwapongeza askari hao kwa kupambana na majambazi hayo na kuwasisitiza kuwa kazi bado inaendelea wazidi kupambana mchana usiku ili wananchi waweze kuishi kwa amani. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kimpa taarifa ya hali ya usalama mkoani humo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa tatu kulia) wakati kiongozi huyo wa Wizara alipofanya ziara mkoani humo. Katika ziara yake, Masauni alitembelea mapango ya Utemini mkoani humo ambapo mapambano kati ya polisi na majambazi yalifanyika, pia alienda kuuona msikiti wa Rahman uliovamiwa na majambazi, pia alizungumza na wafiwa na baadaye akamaliza ziara yake kwa kuzungumza na askari polisi ambapo aliwapa pongezi kwa kazi nzuri ya kupambana na majambazi hao. 
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

BODI MPYA YA NHIF YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kwenye vitabu ambavyo ni muongozo wa kazi kwa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael John.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda, akitoa shukrani zake baada ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athuman akizungumza machache wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga akitoa hotuba yake wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga kwa pamoja wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi alipokuwa akitoa hotuba yake, katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), uliofanyika leo Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.

Wajumbe wapya wa Bodi Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi.


 




















Friday, June 10, 2016

Rais Magufuli mgeni rasmi siku ya Kimataifa ya Albino



Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu Wenye Ualbino Nchini (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina.
“Maadhimisho haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba.
Temba aliendelea kuainisha kwamba siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF.
Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu.
Na Lilian Lundo, MAELEZO (P.T

Obama amuidhinisha Clinton kuwania urais Marekani



Obama
Obama ataanza kufanya kampeni na Clinton
Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu nchini Marekani.
Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang’anyiro cha kumchagua mgombea wa chama hicho.
Akizungumza kwenye video ambayo imepakiwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani.
Clinton: Siwezi kushindwa na Bernie Sanders
“Niko pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni na Hillary,” amesema Obama.
Obama
Obama alikutana na Sanders ikulu ya White House
Wawili hao sasa wanatarajiwa kuanza kufanya kampeni pamoja.
Bw Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi Clinton, kumshinda mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu.
Hata hivyo hakujiondoa kinyang’anyironi. Alisema ataendelea kufanya kampeni yake na kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.BBC