Saturday, January 26, 2013


HAYA NDO MADHARA YA KUTUMIA SIMU IKIWA KWENYE CHARGE.



Siku chache zilizopita kuana mtu alikuwa anacharge simu yake nyumbani. Kila mara alipokuwa akipigiwa simu alikuwa anapokea wakati simu iko kwenye charge.Baada ya dakika kidogo simu ikapata short wakati anaongea na simu kilichomtokea ni kuungua mikono na pia kitanda na mto aliokuwa amelalia vyote viliungua. 
Kwa hali kama hii napenda kuwajulisha wadau wangu kuwa kuweni makini wakati unacharge simu na simu ikiita itoe kwenye charge yasije yakakutokea kama yaliyomtokea kijana huyo kwani vidole vyake vimearibika 

Sunday, January 20, 2013


KAMPUNI YA tiGO YAGOMA KUPUNGUZA GHALAMZA ZA SIMU, AIRTEL, VODACOM ZAKUBALI KUPUNGUZA.

WAKATI Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwasilisha rai ya kupunguza gharama za mwingiliano wa simu , Kampuni ya Tigo imekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa itahatarisha uwekezaji wake kwa punguzo la asilimia 69.

Msimamo huo wa Tigo, umekuja baada ya TCRA kukutana na wadau wa mawasiliano jana jijini Dar es salaam, ili kukusanya maoni kuhusu mapendekezo ya kupunguza gharama ya mtandao mmoja kwenda mwingine. 

Hatua hiyo inalenga katika kuwasaidia wananchi kumudu gharama za mawasiliano ya simu.

Naibu Mkurugenzi wa Utekelezaji wa Kanda wa TCRA, Victor Nkya, alisema punguzo hilo ni la kutoka asilimia 35 hadi asilimia 69 na kwamba litaanza kutumika Machi mosi mwaka huu na kukoma Desemba 31 mwaka 2017 .

Nkya alisema punguzo la gharama ya kupiga mtandao mmoja kwenda mwingine kwa mwaka 2013 litakuwa asilimia 34.92, mwaka 2014 asilimia 32.40, mwaka 2015 asilimia 30.18, mwaka 2016 asilimia 28.57 na mwaka 2017 ni asilimia 26.96.

“Lengo letu ni kupunguza gharama za mwingiliano wa simu, mfano mwananchi ambaye yupo Tigo anapiga kwenye mtandao wa Vodacom hizi gharama atazilipa mwenye kampuni ya Vodacom kuilipa kampuni ya Tigo badala ya kulipa mwananchi kama ilivyo sasa,” alisema.

Alisema maoni yanayotolewa na wadau yatachukuliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano na kuyafanyia kazi.

Ofisa Mdhibiti wa Kampuni ya Tigo, Levocatus Nkata, alisema punguzo hilo ni kubwa hivyo wawekezaji watashindwa kuendesha kampuni zao.

Alisema Kampuni ya Tigo inatoa huduma zake hadi vijijini na kwamba hatua hiyo itaifanya ishindwe kupeleka na kutoa huduma kwenye maeneo hayo.

Nkata alisema itachukua muda mrefu kurudisha gharama walizotumia kuendeshea kampuni yao kutokana bei ya kuendesha mitambo.

“Sisi hatukubaliani na hayo mapendekezo yaliyoletwa na TCRA, punguzo hilo kwa sisi wawekezaji ni kubwa sana, tunachoomba wasipunguze ibaki kama ilivyo na kwa mwaka 2017 tunaomba ipunguze kufikia asilimia 45 tu, “alisema Nkata.

Kampuni za Airtel, Vodacom , Benson na Dovetel zimekubali punguzo hilo lakini zimeiomba TCRA ipunguze asilimia chache.

Wednesday, January 16, 2013



NDEGE YA PRECISION AIR YATUA MUDA HUU UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA IKIWA NI SAFARI YAKE YA KWANZA , YAPOKELEWA KWA SHANGWE!! SHUHUDIA.


NDEGE YA PRECISION AIR IKIWA INAWASILI KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA MUDA HUU
MUELEKEZAJI AKIWA ANAELEKEZA WAPI NDEGE YA PRECISION AIR IPATE KUSIMAMA
VIONGOZI MBALIMBALI YA SERIKALI WAKIWA WANANGOJA MAPOKEZI YA NDEGE YA PRECISION AIR AMBAYO NDIYO INAANZA SAFARI ZAKE ZA KWANZA MKOANI MBEY

 

SHEREHE ZA MAPOKEZI YA NDEGE YA PRECISION AIR MKOANI MBEYA MUDA HUU,


 KIKUNDI CHA NGOMA KIKITUMBUIZA MUDA MCHACHE BAADA YA NDEGE KUWASILI 

 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKISHUHUDIA UJIO WA SAFARI ZA KWANZA ZA PRECISION AIR MKOANI MBEYA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE.
 KILA MWANDISHI ANAJITAJIDI KUPATA PICHA NZURI YA NDEGE 
WAFANYAKAZI WA PRECISION AIR WAKIWA WAMEPENDEZA MUDA HUU KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA
 UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA
 BURUDANI BADO INAENDELEA HAPA
 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKIWA WANATAZAMA KWA UMAKINI NGOMA YA ASILI IKITUMBUIZA
 HII NI MEZA KUU
 NAO WAKAZI WA SONGWE MKOANI MBEYA WAMEFIKA UWANJA WA NDEGE KUSHUHUDIA JINSI NDEGE YA SHIRIKA LA PRECISION AIR ILIPO TUA ENEO HILO.
 MKUU WA WILAYA WA MBEYA MHESHIMIWA NORMAN SIGALA, AKIONGEA MUDA BAADA YA NDEGE KUWASILI
MKURUGENZI MTENDAJI WA PRECISION AIR NDUGU SHIRIMA AKIONGEA NA WAGENI WAALIKWA PAMOJA NA WANANCHI WALIO JITOKEZA KATIKA KUPOKEA NDEGE HIYO AMBAYO INAANZA SAFARI ZAKE ZA KWANZA MKOANI MBEYA NA KUWASHUKURU  KWA MAPOKEZI HAYO.


NDEGE YA PRECISION AIR YATUA MUDA HUU UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA IKIWA NI SAFARI YAKE YA KWANZA , YAPOKELEWA KWA SHANGWE!! SHUHUDIA.


NDEGE YA PRECISION AIR IKIWA INAWASILI KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA MUDA HUU
MUELEKEZAJI AKIWA ANAELEKEZA WAPI NDEGE YA PRECISION AIR IPATE KUSIMAMA
VIONGOZI MBALIMBALI YA SERIKALI WAKIWA WANANGOJA MAPOKEZI YA NDEGE YA PRECISION AIR AMBAYO NDIYO INAANZA SAFARI ZAKE ZA KWANZA MKOANI MBEY

 

SHEREHE ZA MAPOKEZI YA NDEGE YA PRECISION AIR MKOANI MBEYA MUDA HUU,


 KIKUNDI CHA NGOMA KIKITUMBUIZA MUDA MCHACHE BAADA YA NDEGE KUWASILI 

 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKISHUHUDIA UJIO WA SAFARI ZA KWANZA ZA PRECISION AIR MKOANI MBEYA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE.
 KILA MWANDISHI ANAJITAJIDI KUPATA PICHA NZURI YA NDEGE 
WAFANYAKAZI WA PRECISION AIR WAKIWA WAMEPENDEZA MUDA HUU KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA
 UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE MBEYA
 BURUDANI BADO INAENDELEA HAPA
 VIONGOZI WA SERIKALI PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI WAKIWA WANATAZAMA KWA UMAKINI NGOMA YA ASILI IKITUMBUIZA
 HII NI MEZA KUU
 NAO WAKAZI WA SONGWE MKOANI MBEYA WAMEFIKA UWANJA WA NDEGE KUSHUHUDIA JINSI NDEGE YA SHIRIKA LA PRECISION AIR ILIPO TUA ENEO HILO.
 MKUU WA WILAYA WA MBEYA MHESHIMIWA NORMAN SIGALA, AKIONGEA MUDA BAADA YA NDEGE KUWASILI
MKURUGENZI MTENDAJI WA PRECISION AIR NDUGU SHIRIMA AKIONGEA NA WAGENI WAALIKWA PAMOJA NA WANANCHI WALIO JITOKEZA KATIKA KUPOKEA NDEGE HIYO AMBAYO INAANZA SAFARI ZAKE ZA KWANZA MKOANI MBEYA NA KUWASHUKURU  KWA MAPOKEZI HAYO.

Monday, January 14, 2013

PICHA ZA MATUKIO YA WANAFUNZI IFM WALIPOVAMIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI NI BAADA YA KUKOSA ULINZI KWENYE HOSTELI, BAADA YA WENZAO WAKIUME WAWILI KUBAKWA NA MAJAMBAZI NA KULAZWA HOSPITALI. SAKATA LINAENDELEA KIGAMBONI MIDA HII CHINI YA USIMAMIZI WA KAMANDA KOVA.

Wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa  hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.

Ulinzi uliimarishwa nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.
Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo"
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.
Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
Mitaani Posta.
Hadi kieleweke!
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.
Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure!
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue!
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani.

Friday, January 4, 2013


MAITI YA MTU AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA IMEKUTWA IMEFUKIWA KWA MAWE NA UDONGO HUKO MAKOKO KATIKA MANISPAA YA MUSOMA

KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA ABSALOM MWAKYOMA AKIWA NA MWANA HABARI GEORGE MARATO
  
     
Maiti ya mtu mmoja ambaye hakuweza kufahamika imekutwa imefukiwa kandokando ya miamba ya milima kwa mawe na udongo katika mtaa wa Nyarigamba Kata ya Makoko Manispaa ya Musoma na kuendelea kuwa na hofu kwa Wananchi juu ya mauaji yanayoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali katika siku za hivi karibuni.

Katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara ilisema awali kulikuwepo na uvumi  uliohusisha mwili wa marehemu na mwanamke mmoja ambaye amepotea na hajulikani alipo toka tarehe 14.12.2012 katika mazingira ya utatanishi anayeishi katika mtaa wa Ziwani katika kata hiyo ya Makoko.

Taarifa hiyo ilisema baada ya Mwili huo kufanyiwa uchunguzi na madaktari katika hospitali ya Mkoa wa Mara imebainika kuwa mwili huo uliokuwa umefukiwa haujulikani ni wa nani huku ndugu wa Mwanamke aliyepotea wamethibitisha mwili huo sio wa ndugu yao.

"Natoa wito kwa Wananchi wa Musoma na vitongoji vyake pamoja na sehemu nyingine wafike katika Hospitali ya Mkoa wa Mara katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kujaribu kuutambua mwili huo ambao umehifadhiwa pale,"alisema Kamanda Mwakyoma.

Mmoja wa shuhuda wa tukio la kufukuliwa kwa mtu huyo Vedastus Masige aliyezungumza na bLOG HII alisema Jeshi la Polisi bado halijaweka nia ya dhati ya kukabiliana na matukio hayo licha kulipotiwa na vyombo vya Habari lakini wamekuwa wakipuuzia huku Wananchi wakiendelea kuangamia.

Alisema hawajasikia Jeshi la Polisi limefikia wapi katika kuchukua hatua juu ya kukabiliana na hali hiyo huku mauaji yakiendelea kutokea na kuwafanya Wananchi wakiishi kwa mashaka na wasiwasi kutokana na hali hiyo inavyoendelea kutokea.

''Tulishuhudia katika siku za nyuma Jeshi la Polisi likihamia Wilayani Serengeti likiongozwa na Kamanda wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania Chagonja kutokana na kifo cha Mtalii mmoja na waliohusika kukamatwa leo kwa nini wanashindwa kupambana na mauaji yanayokuwa yanatokea mara kwa mara Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla.

"Haiwezekani kwenye Nchi yetu tuishi kama wakimbizi matukio ya mauaji ya ajabu yamekuwa yakitokea rakini hatua za haraka zimekuwa hazichukuliwi hali ambayo inaendelea kutupa hofu na kuishi kwa mashaka tukiwa katika ardhi yetu inayodaiwa kuwa ni kisima cha Amani,''alisema Vedastus.


Taarifa za kupatikana kwa mwili huo zilitolewa na wavuvi wa dagaa waliokuwa wakianika kwenye jiwe maeneo ya Makoko nje kidogo ya Mji wa Musoma na kusikia harufu ambayo iliwashitua na kuanza kuulizana ni harufu ya kitu gani na inatokea wapi.

"Siku ya kwanza tulisikia harufu lakini tulichukulia ni kawaida lakini muda ulivyozidi kwenda tuliona ikiendelea kuongezeka na kuamua kufatilia kwa kushirikiana na baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi ambao tunaishi nao jirani na kubaini kuna kitu kimefukiwa pembeni ya mlima na kuamua kulitaarifu Jeshi la Polisi,"alisema mmoja wa wavuvi hao aliyekuwa katika eneo la tukio.

Thursday, January 3, 2013


Breaking Newzzz....BALOTELI NA KOCHA WAKE MANCINI WASHIKANA MASHATI NA KUTAKA KUPIGANA ANGALIA PICHA

Face off: Mario Balotelli and Roberto Mancini (right) squared off in training
Leo asubuhi kumetokea hali ya kutokuelewana kati ya kocha Roberto Mancini na mchezaji toto tundu Mario Balotelli kiasi cha kufikia kushikana mashati na kutaka kupigana kama isingekuwa kuamuriwa na wachezaji wengine. Chanzo cha ugomvi wa wawili hao kinasemekana ni rafu ya Balotelli aliyomchezea mchezaji Scot Sinclair katika mazoezi hayo ya kujiandaa na mechi ya FA Cup dhidi ya Watford.
Altercation
The manager and player grapple with each other
Push and pull: Mancini and Balotelli raged at each other
Anger: Mancini was furious after a mistimed tackle from Balotelli 

Led off: The striker was pulled away from Mancini by a coach
SOURCE-SHAFIIDAUDA