Sunday, October 26, 2014

MAKUBALIANO YA UKAWA YALIYOSAINIWA KWENYE MKUTANO WA UKAWA JANGWANI LEO.

Leo Wamesaini Makubaliano  kati ya vyama vinne vya kisiasa yaani CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD
Makubaliano ya UKAWA: Kuandaa muongozo wa kugombea nafasi zote
Makubaliano ya UKAWA: Kushirikiana kuelimisha Umma kuipigia kura ya Hapana Katiba inayopendekezwa.
Makubaliano ya UKAWA: Kujenga ushirikiano wa dhati katika mambo yote na hoja zote za kitaifa zenye maslahi ya Watanzania wote
Makubaliano ya UKAWA: Kuulinda Muungano bila kuwa na migongano ya maslahi
Makubaliano ya UKAWA: Kulinda na kuenzi Muungano bila kunyenyekea kikundi chochote wala itikadi yoyote.
Maalim Seif Sharrif Hamad: Katiba iliyopendekezwa haikubaliki wala haivumiliki, Wazanzibar na watanganyika walishaukaa mfumo wa serikali mbili imekuaje Sitta na Chenge waurudishe.
Maalim Seif Sharrif Hamad: Katiba iliyopendekezwa Wazanzibar walio wengi hatuutaki, unanuka.
Maalim Seif Sharrif Hamad: Rasimu imepitishwa kimakosa kwani haikupigiwa kura kwa Rasimu kwa ujumla wake.
Maalim Seif Sharrif Hamad: Zanzibar tumechakachuliwa sana katika kura za maoni.
Maalim Seif Sharrif Hamad: Theluthi mbili ya Zanzibar haikupatikana, wabunge na wawakilishi walikuwa 217, 219 wamepatikana vipi? theluthi mbili ni 146, waliosema Hapana ni 76 hivyo waliopiga ndiyo ni 143. Theruthi mbili imepatikana wapi?
Maalim Seif Sharrif Hamad: Tunamsubiri Kikwete na Shain watuletee kura ya maonim tupige kura ya Hapana.
James Mbatia: Baada ya kudhalilishwa viongozi wa dini wanyoshe mkono wao kwa Bunge la Katiba kwani walishaliasa.
James Mbatia: Katiba iliyopendekezwa ni janga la Taifa, haifai haifa kabisa.
James Mbatia: Serikali haiaminiki juu ya kura ya maoni, kumekuwa na kauli tofauti tofauti kutoka katika dola hiyo hiyo moja.
James Mbatia: Tumekuja na utulivu wa ndani ya mioyo, na nawaomba Viongozi wa mikoani watuamini na waangalia nani anakubalika aachiwe kugombea katika ngazi zote. 

Makubaliano ya UKAWA: Kuwa na kauli zinazolingana wanapozungumza na 
watanzania wote Makubaliano ya UKAWA: Kusimamisha wagomnbea wa pamoja 
kwenye ngazzi zote za uchaguzi kuanzia kwenye mitaa hadi Rais wa Tanzania


Maalim Seif Sharrif Hamad: Katiba ya Sitta na Cgenge mahala pake ni kutiwa
 kwenye debe la taka, kwani haikubaliki kabisa.



James Mbatia: Historia iliyoandikwa leo iwe njia ya kuikomboa Tanzania kwani
 wameamua kuweka maslahi ya Taifa mbele na siyo maslahi ya vyama vyetu.
James Mbatia: Viongozi wa dini walilikanya Bunge la Katiba kwa kuwa walijua 
kuwa wanaenda sehemu siyo sahihi, lakini kinyume chake wakadhalilishwa.

Dk.Slaa asisitiza mkutano lazima tutashiriki.

POLISI YASEMA INATAMBUA MKUTANO WA LEO NI WA CUF NA SII UKAWA KAMA WATAKUWEPO VYAMA VINGINE MABOMU KAMA KAWA:-

Kamanda wa Polisi wa kanda ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova
Wakati Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, likitoa kibali cha kufanyika kwa mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) leo kwenye viwanja vya Jangwani, limesema halitambui Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwamo kwenye mhadhara huo.
Limesema kibali hicho kikitumika kinyume, yatakayotokea uwanjani hapo watajua wenyewe.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Umoja huo ulisema utafanya mkutano leo ambapo pamoja na mambo mengine, utasaini makubaliano ya ushirikiano wa vyama wa kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.
Vyama vinavyounda Umoja huo ni CUF, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), chama cha NCCR-Mageuzi na chama cha NLD.
Kamanda wa Polisi wa kanda ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova, akizungumza na NIPASHE Jumapili jana kuhusiana na taarifa za mkutano huo, alisema kuwa jeshi lake limeuruhusu mkutano wa CUF kwa mujibu wa barua yao waliyoipokea Alhamisi.
Alisisitiza kuwa walioomba kufanya mkutano wa leo ni CUF na siyo Ukawa.
“Baada ya kupokea barua hiyo, jana tulikutana na viongozi wa CUF ambao tuliwauliza kuhusiana na hilo lakini walitueleza kuwa, mkutano huo ni wa chama chao,” alisema na kuongeza:
“Tumeruhusu mkutano wa CUF ambao ndiyo tutaweka ulinzi, siyo taasisi nyingine, tutasubiri yatakayojiri kama ni hatua tutachukua, Ukawa hatuutambui kwenye mkutano huu na hawajatuandikia barua,” alisema.
Aliongeza kuwa, endapo yataingizwa mambo mengine nje ya makubaliano na CUF, wataangalia makosa yatakayotendeka.
Alipoulizwa kama viongozi wa vyama wengine watajitokeza kwenye mkutano huo itakuwaje, Kamanda Kova alijibu kwa kifupi kuwa watajua hapo itakapokea.
Akijibu hoja hizo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, alisema jeshi la polisi halina wasomi na kama wapo hawana kumbukumbu.
“2007 tulisaini maadili ya vyama vya siasa, katika maadili hayo moja ni vyama vya siasa vinaweza kuamua kushirikiana katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na mikutano. Hili lilisainiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa niaba ya serikali, msajili wa vyama vya siasa na mkuu wa jeshi hilo nchini,” alisema.
Alisema ndani ya hati hiyo inaeleza ili washirikiane mmoja wao (chama), ataandika barua kwa niaba ya wengine wanapotaka kushirikiana.
“Hichi ndicho kilichofanyika, mmoja wetu amepeleka taarifa polisi ndani ya muda unaotakiwa kwa niaba yetu wote, lakini kwa mujibu wa katiba, tunapotaka kushirikiana ni ruksa,” alisema.
Alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo na wawe na amani.
Katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam, wananchi walikuwa wakihamasishwa kujitokeza kusikiliza mkutano huo kwa kutumia waendesha bodaboda waolikuwa wanapita kwenye mitaa nyakati za usiku.
Uhamasishaji huo ni pamoja na kuwaambia wananchi kuwa kutakuwa na mabasi ya bure yatakayowachukua kutoka maeneo yao hadi kwenye viwanja hivyo.
Hali hiyo ya uhamasishaji ilijitokeza katika maeneo ya Tabata - Segerea ambapo bodaboda hizo zilionekana kupita katika baadhi ya mitaa.

SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

SASA JAMANI DEMOKRASIA MI NAONA KAMA POLISI WANATUMIKA KUIMINYA : TOA
Bahati Nzumbi's photo.

Friday, October 24, 2014

TIMES FM YAJIPANGA KUWAPELEKA DAVIDO NA UONGOZI WA CLOUDS FM JELA KWA KUKAIDI AMRI YA MAHAKAMA

Kituo cha redio cha Times FM na kampuni ya Times Promotions, wamewasilisha mashtaka mahakamani ya kutaka viongozi wa juu wa Clouds FM pamoja na msanii wa Nigeria, Davido wapelekwe jela kwa kukaidi amri ya mahakama.
Kampuni hiyo kupitia wakili wake Peter Kibatala imewasilisha mashtaka hayo katika mahakama ya 


hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumatatu hii.
Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa Davido na Clouds FM walikaidi amri ya mahakama iliyotolewa kumtaka Davido asitumbuize kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika October 18 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Times FM walikuwa wameshaingia mkataba na Davido atumbuize November 1 kwenye tamasha lao ambalo linadaiwa kuahirishwa kutokana na kilichotokea.

Soma zaidi habari hiyo iliyoandikwa kwenye gazeti la Jana la Daily News 

TAZAMA PICHA 20:: WANAJESHI WA CHINA NA TANZANIA WAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA

Askari wa majini wa Tanzania na China, wakiwasubiri maelekezo mwanzoni mwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwenye komandi kuu ya wanamaji wa JWTZ, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Jumanne Oktoba 21, 2014
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa JWTZ, Meja Jenerali James Mwakibolwa, (Kulia) na Meja Jenerali Wu Xiao Yi wa jeshi la wanamaji la China, wakibadilishana hati za makubaliano ya mafunzo ya pamoja ya Surpassing 2014









































HUZUNI::KOMANDOO WA JESHI LA WANANCHI AMPIGA RAFIKI YAKE NA KUSABABISHA KIFO,KISA IKIWA NI MAPENZI


 Aron Kihundwa alipokuwa mahututi hospitali kabla ya kifo chake.Tukio hilo lilijiri wiki iliyopita na kumfanya Mchungaji Elaina Msuya wa Kanisa la KKKT aliyekuwa akiongoza misa ya kumuombea marehemu huyo, kuingilia kati na kusema mwili usiendelee kuagwa ili kuzuia watu kuzidi kuzimia.
 INAUMA sana! Baadhi ya ndugu waliokuwa wakiuaga mwili wa Aron Kihundwa (28) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar walijikuta wakidondoka na kuzimia kufuatia uchungu wa kumpoteza mpendwa wao huyo aliyedaiwa kuuawa na Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Octavian Mgowele.
Komandoo Octavian Mgowele mwenye cheo cha Luteni wa Kikosi cha 94 KJ Ngerengere,


 Morogoro, Oktoba 13, mwaka huu alidaiwa kumuua Aron kwa kumpiga kipigo kibaya.Tukio hilo lilidaiwa kutokea kwenye baa iitwayo Mbondela iliyopo Yombo - Buza maeneo ya Kipera, jijini Dar kwa madai kwamba alikuwa akimbughudhi mke wa komandoo huyo. Taarifa toka kwa mtu aliyekwepo kwenye baa hiyo zinasema siku hiyo mjeshi huyo alikaa meza moja na mkewe ambaye alitoka kufunga naye ndoa jana yake. Pia kwenye meza hiyo alikaa Aron huku wakiendelea kunywa bia ambapo mnunuaji mkuu alikuwa komandoo.

Marehemu Aron Kihundwa enzi za uhai wake.Ikadaiwa kuwa, kuna wakati komandoo alikwenda kaunta aliporudi alishangaa kumkuta mkewe amehama katika kiti alichomuacha. Chanzo hicho kikaendelea kusema komandoo huyo alimuuliza mkewe kisa cha kuhama kiti, naye akamjibu; si huyu rafiki yako ananisumbua.’

Wakati huo, marehemu alikuwa anauchapa usingizi kutokana na kulewa.
“Marehemu akiwa usingizini alishtukia komandoo akimwadhibu bila kujua sababu ni nini hadi akamjeruhi.

”Baada ya kumpiga sana hadi kumjeruhi tulimchukua marehemu na kumpeleka Kituo cha Polisi Chang’ombe (Dar) na kupewa PF3, tukamkimbiza Hospitali ya Temeke, ilipofika saa kumi usiku wa kuamkia kesho yake alifariki dunia.

“Aron ni rafiki yake sana komandoo, hata siku ya ndoa yake, yeye ndiye aliyempambia gari la harusi na ukumbi. Siku ya tukio ilikuwa ni sherehe ya kuvunja kamati.

“Hatujajua ni kwa nini komandoo aliamua kumpiga Aron kiasi kile, mambo ya kuambiwa na mwanamke siyo ya kuyafanyia kazi kama haukushuhudia ama hauna uthibitisho,” alisema shuhuda huyo.
Marehemu Aron alizikwa Oktoba 18, mwaka huu kijijini kwao Kyengia Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.HABARI NA GPL (GLOBAL PUBLISHERS)

Saturday, October 18, 2014

Wakili asema Pistorius 'amefilisika'

 Mahakama inayosikiliza kesi dhidi ya mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imeambiwa kuwa mwanariadha huyo amefilisika.
Hili lesemekana huku pande zote kwenye kesi zikitao akuli yao ya mwisho kabla ya mahakama kutoa hukumu dhidi ya mwanariadha huyo.
Pistorius alipatikana na hatia ya mauji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp bila ya kukusudia mwaka jana.
Jaji Thokozile Masipa anatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya Pistorius Jumanne.
Anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 lakini jaji anaweza kuamua kumpa kifungo cha nje au hata kumtoza faini.
Jaji ataanza kusoma hukumu Jumatatu na upande wa mashitaka unataka Pistorius apewe adhabu kubwa kuambatana na kosa lake.
Lakini mawakili wa Pistorius wameteta wakisema anapaswa kupewa adhabu ndogo kama vile huduma kwa jamii.
Wanadai kuwa mwanariadha huyo huenda akateswa akiwa jela, hoja ambayo imepingwa vikali na mkuu wa magereza.
Pistorius aliangua kilio wakli wake aliposema kuwa pesa zake zimekwisha baada ya kesi yake kufanya kwa mirzi saba.


"sio tu kwamba hana pesa bali anahisi hana tena matumaini,'' alisema wakili wa Pistorius.
Hii ni kesi yake ya kwanza. Nini kimtendekea mwanamume huyu? Nyota yake ilikuwa inaanza kung'ara,'' aliongeza bwana Roux.
Wakili alimuomba jaji kumuonea huruma Pistorius wakati atakapotoa hukumu.
Mnamo siku ya Ijumaa, kiongozi wa mashitaka alikosoa pendekezo la Pistorius kuikabidhi familia ya Reeva pesa. Hata hivyo familia ya Reeva ilikataa pesa hizo ikisema ni pesa za uovu.
Bwana Nel pia alisema ikiwa Pistorius atapewa adhabu ya kiungo cha nje na kuamrishwa kuihudumia jamii, itakuwa ni hujuma kwai adhabu hiyo itakuwa ndogo sana kulingana na kosa lake.chanzo BBC

Friday, October 17, 2014

SERIKALI YA TANZANIA YAPOKEA ZAIDI YA SH. BILIONI 10.

1a
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akitia saini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.

2a
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV waliosaini leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.


3a
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika (kushoto) akishukuru Serikali ya Finland kwa ushirikiano mzuri wanaoendelea kuipa Tanzania mpaka sasa na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika malengo yaliyokusudiwa. Kulia ni Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila.
4a
Balozi wa Finland nchini Bi. Sanikka Antila (kulia)PFM akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuipongeza kwa kusimamia fedha za umma na kuwa na uongozi unaosimamia utawala wa kidemokrasia, uchumi imara, ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo na hivyo kupunguza umasikini. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dae es salaam wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano wa Mpango wa Mageuzi ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM) Awamu ya IV. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Doroth Mwanyika.
Na Eleuteri Mangi -MAELEZO
Nchi nyingine wahisani ni pamoja na Canada, Ujerumani Ireland na Uingereza.

PICHA:;:MAJERUHI WA AJALI LORI LA MAFUTA LILILOLIPUKA MBAGALA WAENDELEA KUAPTIWA MATIBABU



Baadhi ya majeruhi wa ajali ya moto wakiwa wodini.
 MAJERUHI 9 kati ya 15 waliofikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuungua na moto uliosababishwa na kuungua kwa lori la mafuta huko Mbagala jijini Dar es Salaam Oktoba 15 mwaka huu, wanaendelea na matibabu huku hali zao zikiwa bado mbaya.

Kamera yetu ilifika katika hospitali hiyo na kuwakuta wagonjwa hao wakiwa wamelazwa katika wodi namba 23 iliyopo katika jengo la Sewahaji na Afisa Uhusiano msaidizi wa Muhimbili, Doris Ihenga alisema majeruhi sita waliokuja pamoja nao, wamefariki dunia.

Alisema majeruhi wawili kati ya tisa waliolazwa, hali zao ni mbaya zaidi ambao aliwataja majina yao kuwa ni Mathayo Danie (21) na Hamis Ally (35).

Wengine waliolazwa kwa kuunguzwa na moto huo wakati wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tenki la gari lililoanguka ni Abbas Mohamed (25), Hamis Kambi (25) Idd Said (30) Mathayo Daniel (21) Hamis Ally (35) Ibrahimu Hamis (26) Maganga Mgombele (38) na Shabaki Martin.


(Picha/Habari na Haruni Sanchawa/GPL)

TRAFIKI WA MAHABA SIRI NZITO ZAFICHUKA, DILI LA NIPE NIKUPE LAFICHUKA

Na Ojuku Abraham
BAADA ya kuvuja kwa picha katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita, iliyowaonesha askari wawili wa usalama barabarani wakiwa ‘kimahaba niue’ ndani ya sare za kazi na kusababisha kupoteza ajira zao kutokana na kukiuka maadili, siri zaidi nzito zimezidi kuvuja kuhusiana na ishu hiyo na Amani limemuibua afande wa kike baada ya kumsaka sana.
Kwa mujibu wa vyanzo makini kutoka wilayani Misenyi mkoani Kagera, askari wa kike aliyeonekana kwenye picha hiyo chafu, WP. 8898 Veronica Mdeme, inadaiwa kuwa alipata uhamisho kutoka polisi mkoani humo na kupelekwa katika wilaya mpya ya Misenyi mwaka 2011 ambako mwaka mmoja baadaye, ndipo akapigwa picha hiyo iliyoleta gumzo kubwa ndani na nje ya Bongo.

Ilidaiwa kwamba, picha hiyo ilipigwa katika barabara ya lami iendayo Mutukura, umbali wa Kilomita 50 kutoka Misenyi na kwamba askari hao walikuwa katika Kituo cha Polisi cha Kyaka.
Nguzo ya umeme inayoonekana nyuma yao, ni zile zinazopeleka umeme nchini Uganda kutoka Bwawa la Umeme la Mtera, Tanzania.

ILIKUWA PICHA YA KISHKAJI TU LAKINI…
Habari zilidai kuwa, askari hao Veronica, F.7788 Mpaji Mwasumbi na PC Fadhil Linga, walikuwa zamu moja na kwamba picha hiyo ilipigwa katika mazingira ya kishkaji tu lakini baadaye ikaja kuzua balaa kubwa.

Ilisemekana kwamba, Linga ndiye aliyewapiga picha wenzake ambao habari zisizothibitishwa zilisema kuwa walikuwa na uhusiano wa kijamii.

Madai yalizidi kutiririshwa kwamba baada ya kupigwa kwa picha hiyo, Linga alibaki na nakala katika kamera yake kwa muda wa miezi kadhaa kabla ya kugundua kuwa kumbe ilikuwa ni dili.

AWAGEUZIA KIBAO
Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyotarajiwa, Mpaji na Veronica hawakuamini masikio yao baada ya Linga kuwaambia kwamba alihitaji kupata ‘kitu kidogo’ kutoka kwao ili aweze kuendelea kuhifadhi siri ya picha hizo.

Ilisemekana kuwa afande huyo aliwaambia wawili hao kama ataivujisha picha hiyo kwenye mitandao ya kijamii, watapoteza kazi.

“Baada ya kuambiwa hivyo, jamaa walilegea kabisa. Mwanzoni walitia ngumu lakini walipoona jamaa amekomaa, hawakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana naye, hivyo akawa anapata kitu kidogo kila alipojisikia  na kuwa nipe nikupe na hakuna uhakika kama dada Vero alisalimika kwenye mambo mengine kwani naye alikuwa akitumia nguvu kubwa kuhakikisha mumewe hajui,” kilidai chanzo hicho.

WAAMUA KUJILIPUA, WAMSHTAKI
Ilielezwa kwamba, baada ya ‘kutolewa upepo’ kwa muda mrefu na kuonekana kama wangekuwa ATM ya kudumu ya Linga, Mpaji na Veronica waliamua kujilipua na kwenda kumshtaki kwa kigogo wa juu wa jeshi la polisi mkoani humo ambaye anatajwa kuujua mchezo mzima ulivyokuwa.

Ilisemekana kwamba, kiongozi huyo alilichukulia jambo hilo kwa uzito wake na kuwakalisha wote watatu ili kuzungumza nao.Iliendelea kudaiwa kuwa katika kikao kati ya askari hao na bosi wao, wawili hao walikiri kupigwa picha hiyo na kuomba msamaha, lakini wakamlalamikia mwenzao ambaye naye alikiri kufanya kitendo hicho, kwa kuwageuza kuwa ATM.

Ilidaiwa kuwa mkubwa huyo alimuamuru Linga kuzifuta picha hizo na kuwataka kusameheana, kwani kitendo walichokifanya ni kibaya na kinachoweza kuhatarisha ajira zao. Linga alikubali ‘kuzi-diliti’ picha hizo!

WAGAWANYWA, LINGA ARUDIA
Ikazidi kudaiwa kuwa ili kuwafanya waishi kwa amani, waligawanywa katika vituo tofauti vya kazi mkoani humo huku mmoja wao, Mpaji akipelekwa Dar ambako alikwenda kusoma Chuo cha Polisi Kurasini.

“Wakiwa katika vituo hivyo tofauti, Linga alitulia kwa muda mchache tu kabla ya kuanza tena usumbufu wake, hasa kwa Veronica ambaye anadaiwa kuwa mke wa mtu. Ni katika usumbufu huo wa mara ya pili, akina Mpaji wakaamua kumjibu jeuri jamaa, hawakuwa na uoga tena kwa vile suala lao lilishafahamika kwa wakubwa,” kilisema chanzo chetu.

Inaelezwa kwamba majibu ya jeuri kutoka kwa Vero na Mpaji yalimuudhi Linga ambaye kwa lengo la kuwakomoa, aliamua kuzitupa picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambako nako zilizagaa kwa kasi ya moto wa kifuu na kuwafikia watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari vilivyoamua kuripoti.

“Picha hiyo ilipoonekana mtandaoni, moja kwa moja polisi walijua imewekwa na Linga kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine aliyefahamu kuhusu picha hiyo. Ndiyo maana wote watatu walifukuzwa kazi siku moja, hawakuwa na sababu ya kuhangaika kujua nani kaweka,” kilisema chanzo hicho.

PICHA YA MREMBO YAWA GUMZO
Baada ya kufukuzwa kazi kwa wahusika hao watatu, kumekuwa na picha za mrembo mkali ambaye amekuwa akifananishwa na Veronica huku kukiwa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kama kweli ni yeye (angalia picha ukurasa wa mbele).

Kwa mujibu wa maoni lukuki katika mitandaoni, kama kweli mrembo huyo ndiye huyo askari wa kike, basi jamaa aliyekuwa naye kimahaba, alistahili adhabu yoyote kuliko kukosa mahaba hayo.

“Ni kama walivyoimba wale watoto wa Yamoto Band, yaani nzi kufia kwenye kidonda siyo ufala bali kupenda. Huyu mtoto mashalaah,” ilisomeka sehemu ya maoni ya stori hiyo ambayo ndiyo habari ya mjini kwa sasa.

Juzi, Amani lilimtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe ili kumsikia nini kinaendelea baada ya askari hao kufukuzwa kazi lakini hakuwa hewani.

Naye msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Advera Senzo alipopigiwa simu na kuulizwa alisema walishafukuzwa kazi hakuna kingine lakini akaelekeza apigiwe simu Mwaibambe.