Wednesday, October 30, 2013

DONT TRY THIS IF YOU ARE NOT PROFFESIONAL DIVER,SEE PHOTOS.


It looks like the definition of paradise, high in the sky, surrounded by luscious green branches, with the sun glowing softly and nothing but clear blue water down beneath.But clad in nothing but a pair of Speedos, faced with a 27-metre tumble from a crumbling cliff, many would think twice about that.

Not these men.


Paradise: Phi Phi Island in southern Thailand has hosted the final round of the sixth annual cliff diving championship series
Paradise: Phi Phi Island in southern Thailand has hosted the final round of the sixth annual cliff diving championship, where the men have just three seconds to perform


Eagerly bounding to the cliff-edge on Phi Phi Island in Thailand, 14 divers flung themselves, twisting and turning at break neck speed towards life-threatening rocks.
Their one shared objective: make it look good. 
Gathered for the sixth round of the sixth annual Red Bull cliff diving championship series today, they have all spent months preparing their moves.


Alain Kohl of Luxembourg
Artem Silchenko of Russia
Death-defying: Alain Kohl (left) of Luxembourg diving off the Viking Caves on the island. Artem Silchenko (right) is mid-twist as he falls towards the Andaman Sea

There is no hard-and-fast rule for the game - just the mantra, 'power and balance'.
 

But with just three seconds between leaving the podium and hitting the Andaman Sea, they don't have long to show off their best.
This year the series has taken the competitors all over the world.

Warriors: The sport was created as a challenge for Hawaiian warriors to demonstrate their loyalty to King Kahekili
Warriors: The sport was created as a challenge for Hawaiian warriors to demonstrate their loyalty to King Kahekili. Here Michal Navratil of the Czech Republic faces the clear water

Frightening: David Colturi of the USA dives from the 27-metre platform
Frightening: David Colturi of the USA dives from the 27-metre platform. There seem to be no qualms about the surrounding boats as the men tumble in nothing but Speedos

The season started in France's La Rochelle, followed by Copenhagen, and then Azores in Portugal. 
From there they went on to Italy, Boston, Pembrokeshire, before reaching the southern coast of Thailand for the final.
Unfortunately, the penultimate stop scheduled for Brazil earlier this month had to be cancelled due to bad weather.
Russia's Artem Silchenko won the day's competition - but it wasn't enough to take the overall title from Britain's Gary Hunt, who has held the top spot since 2010. 
The stand
Beautiful beach
Climb: The men face an 88-foot climb up wooden ladders balanced precariously on the cliff-side (left) before flinging themselves off a wooden podium (right)

Jonathan Paredes of Mexico
Alain Kohl of Luxembourg
Power and balance: Jonathan Paredes of Mexico (left) and Alain Kohl of Luxembourg (right) strike strong poses as the attempt to stay streamlined on their descent

Michal Navratil of the Czech Republic
Steven LoBue of the USA
Turn: Michal Navratil of the Czech Republic (left) and Steven LoBue of the USA (right) battle it out for the title with mind-blogging contortions

Worldwide: Before Thailand, the group competed in the beauty spots of France, Italy, Wales, Brazil
Worldwide: Before Thailand, the group competed in the beauty spots of France, Italy, Wales, Brazil, Copenhagen, Portugal, and Boston

Winning leap: Artem Silchenko of Russia prepares to launch an armstand dive from the 27-metre platform in the Andaman Sea
Winning leap: Artem Silchenko of Russia prepares to launch an armstand dive from the 27-metre platform in the Andaman Sea during the last competition day of the eighth and final stop of the 2013 Red Bull Cliff Diving World Series
Third place overall: Orlando Duque of Colombia takes the plunge.
Third place overall: Orlando Duque of Colombia takes the plunge. The main rule that divers must adhere to is 'power and balance' as they fall towards the water below
Going into today's final, former Olympic hopeful Hunt, 29, who has won a number of medals at the Great Britain National Diving championships, was already the tournament leader.
Silchenko stood in second place and 10-time world champion Orlando Duque, from Colombia, was in third.
Mexico's Jonathan Paredes holds fifth, ahead of David Colturi, from the US.
Professional rivals: The two potential series winners, Artem Silchenko (left) of Russia and Gary Hunt (right)
Professional rivals: The two potential series winners, Artem Silchenko (left) of Russia and Gary Hunt (right) of the UK pose for a portrait on the beach before competing
The final moments: Silchenko's land.
The final moments: Silchenko's land. The land is the most crucial part of the fall - to maintain the style they have worked tirelessly to hone, and to ensure they don't injure themselves

Relax: Finally Artem Silchenko of Russia can celebrate after his final dive during the last competition day
Relax: Finally Artem Silchenko of Russia can celebrate after his final dive during the last competition day of this year's season. He could not take the top spot but won the day's contest

Champion: Silchenko stands on the podium as the other divers spray him with champagne and fans wave flags, lauding his success
Champion: Silchenko stands on the podium as the other divers spray him with champagne and fans wave flags, lauding his success
Best seats: Crowds crammed onto boats to get the best view of divers
Best seats: Crowds crammed onto boats to get the best view of divers - such as winner Silchenko (pictured centre) - performing their finale


Proud: Local media in Thailand described the event - the first one to be hosted by Krabi - as a very proud moment
Proud: Local media in Thailand described the event - the first one to be hosted by Krabi - as a very proud moment for the nation. Crowds gathered to hail Silchenko, the winner

Runners up: Steven LoBue (right) of the US took second place for the day and third place went to Orlando Duque (left) of Colombia
Runners up: Steven LoBue (right) of the US took second place for the day and third place went to Orlando Duque (left) of Colombia
The sport started in the late 1700s as an initiation for Hawaiian warriors - as ordered by King Kahekili, who was obsessed by cliff diving.
He challenged his people to prove their loyalty by throwing themselves hundreds of feet into rocky water.
It is from that moment in time that the sport earned its mantra: 'mana and pona' - 'power and balance' in Hawaiian.
Now a global phenomenon, local Thai media has described the event - the first time it has been hosted by Krabi - as a very special moment for the nation.

Saturday, October 26, 2013

MAJENEZA MAWILI YATUMIKA KWENYE MAZISHI YA NYAISANGAH




NI vigumu kutokea! Lakini safari hii imetokea, mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Abood TV, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ ambaye alifariki dunia Jumapili iliyopita mjini Morogoro, ulisafirishwa kwa majeneza mawili.
Usiku wa Jumatatu iliyopita kamera za Risasi Jumamosi, zilishuhudia jeneza lenye rangi nyeupe likiwa limetumika kuusafirisha mwili wa marehemu huyo kutoka Morogoro hadi Hospitali ya Taifa, Muhimbili jijini Dar.
Jumanne iliyopita, saa tatu asubuhi kamera zetu zilishuhudia jeneza lenye rangi ya kahawia (brown) likitumika kuusafirisha mwili huo kutoka Muhimbili hadi Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar ambako marehemu aliagwa.
Baadhi ya watu walipoulizwa na Risasi Jumamosi wana mawazo gani kuhusu mwili wa marehemu kusafirishwa na majeneza mawili walionekana kushangazwa na tukio hilo.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa siku hiyohiyo kwenda Bunda, mkoani Mara alikozaliwa kwa mazishi yaliyofanyika Alhamisi iliyopita.

Risasi Jumamosi lilimtafuta mjumbe mmoja wa kamati ya mazishi ya Anko J aliyeomba kusitiriwa jina lake na kumuuliza kulikoni majeneza mawili yatumike kusafirisha mwili mmoja ambapo alijibu:
“Lile lililotoka na mwili Morogoro lilionekana kukosa ubora halafu lilitengenezwa ‘chapchap’ ndiyo ikaamriwa linunuliwe jingine zuri zaidi.”
Risasi Jumamosi: Sasa lile jeupe lililotoka Morogoro limepelekwa wapi?
Mjumbe: Mh! lile tuliliacha muhimbili ,ndugu watajua cha kufanya.
Kwa Waislam, jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu ni la wazi na hurudishwa msikitini baada ya mwili kuzikwa kaburini.
Kama mwili utasafirishwa hutumika jeneza la sanduku lakini haliendi kuingia kaburini na huvunjwavunjwa punde mwili unapofika.
Kwa Wakristo, jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu hutengenezwa kama sanduku na huingizwa kaburini na marehemu akiwemo ndani.
Awali ilidaiwa kuwa, mwili wa marehemu ungesafirishwa kwa ndege kwenda tarime na gharama za usafirishaji zingesimamiwa na wizara ya habari vijana utamaduni na michezo, lakini juzi naibu waziri wa wizara hiyo, Amos makalla alikanusha wizara yake kutoa tamko hilo.
 
“Wizara haikutoa tamko hilo, wala hatukuwa kwenye kamati ya mazishi  ila tulituma mwakilishi,” alisema Waziri  makalla.


GPL

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA BODA BODA ADAI ALIPEWA MASHARTI NA SANGOMA WAKE.


 PICHA ZA MATUKIO SIKU AMBAYO MAUAJI YA BODA BODA
 KISU KINACHODAIWA KILITUMIKA KUMUUA BODA BODA
MAITI IKIWASILI HOSPITALI YA WILAYA SERENGETI


Oktoba 25,2013
MTU mmoja anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa boda boda mjini Mugumu Wilayani Serengeti Gwitembe Yagera(60)amekamatwa na kudai kuwa aliambiwa na Sangoma wake aue mtu yeyote ili apate utajiri.
 
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Fernandi Mtui alithibitisha kukamatwa kwa Mtuhumiwa huyo anayeshikiliwa na polisi wilayani Serengeti Elias Jonathan(23)mkazi wa kijiji cha Burunga kata ya Uwanja wa Ndege wilayani hapa,amekamatwa hivi karibuni eneo la Sirari na kuwa uchunguzi zaidi unaendelea .
 
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa mtuhumiwa huyo alisema kuwa alitekeleza mauaji hayo kutokana na masharti ya mganga wake ambaye anasakwa na jeshi la polisi,kuwa afanye mauaji pekee yake na kwa mtu yeyote ndipo na atapata  utajiri.
 
“Alisema aliamua kumkodi huyo boda boda kwa kuangalia umri wake kwa madai kuwa anakwenda Mosongo…kufika eneo la Nyisense Nyichoka akamchoma kisu na kusababisha mauaji yake na kukimbia akitelekeza kisu hapo na hakuchukua kitu chochote”kilisema chanzo cha uhakika kutoka ndani ya jeshi la polisi.
 
Kuhusu kukamatwa kwake  chanzo hicho kilisema baada ya kutenda unyama huo alitoroka hadi Sirari na ambako alihusika katika mauaji ya baiskeli na kukamatwa ,na baba yake alitoa ushirikiano baada ya kujua kuwa anatafutwa kwa mauaji na kunaswa na kuletwa Mugumu kuhusiana na tuhuma hizo.
 
Oktoba 4,mwaka huu majira ya saa 8 arasili mtuhumiwa huyo anadaiwa alimkodi Yagera kwa sharti kuwa wakifika kijijini Mosongo angemlipa fedha yake,lakini kabla ya kufika inadaiwa alimchoma kisu eneo la kushoto chini ya ubavu na kusababisha kifo chake.
 
Na baada ya kutenda unyama huo hakuchukua kitu na kutokea na maiti yake iligunduliwa na wapiti njia ambao walitumia simu ya marehemu kuwataarifu viongozi wa chama cha waendesha pikipiki wilayani hapo,na askari polisi. 
 
Habari tulizozipata wakati tunaandaa taarifa hizi zinadai kuwa mtuhumiwa huyo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti kuhusiana na tuhuma hizo,hata hivyo hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Friday, October 25, 2013

VITUO VYA DALADALA UBUNGO, MWENGE KUHAMISHWA


Thursday, October 24, 2013

MBUNGE WA CCM MWENYE MIAKA 60 AJIKUTA KWENYE KASHFA NZITO BAADA YA KUOLEWA NA KIJANA WA MIAKA 26....



MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.

Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge wanaoifahamu pamoja na majirani wanaoishi na mbunge huyo.
  
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya wanandoa hao na majirani wanaowazunguka, vililiambia gazeti hili kuwa ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na imebaki kuwa siri kabla ya wawili hao kukorogana.
  
Kabla ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa, mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwa mbunge huyo.
  
Inaelezwa kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
  
Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao waliamua kufunga ndoa katika Kanisa la TAG baada ya mbunge huyo kufanikiwa kumshawishi Mchungaji Rwakatare kwamba ndoa hiyo itakuwa siri, hasa kutokana na tofauti ya kiumri kati yao.
  
Hata hivyo ndoa hiyo kwa sasa imekumbwa na mgogoro mkubwa, huku mbunge huyo akidaiwa kuzuia kila kitu cha mumewe huyo, hasa vyeti vyake vya shule kama njia ya kumbana warudiane.
  
Siku ya harusi 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa harusi hiyo ya aina yake, mbunge na kijana huyo walikwenda kanisani wakiwa wawili bila mashahidi kama ilivyo kawaida, na ndoa hiyo ilifungwa katika ofisi ya kanisa na sio ndani ya kanisa.
  
Mashahidi wa ndoa hiyo waliitwa hapo hapo kanisani na walisimamia na kushuhudia utiaji saini wa cheti cha ndoa na kisha wanandoa hao kutawanyika kwenda kwenye fungate (Honey Moon). Hakukuwa na sherehe baada ya kufungwa ndoa.
  
Inadaiwa kuwa hakukuwa na ndugu yeyote wa maharusi hao aliyeshuhudia tukio hilo la kihistoria la wawili hao kuunganishwa na kuwa mwili mmoja.

Kauli ya Bwana harusi
Tanzania Daima Jumatano, lilifanikiwa kumpata Michael, ambaye katika mazungumzo yake alikiri kufunga ndoa na mbunge huyo Septemba Mosi mwaka 2011, lakini kwa sasa wametengana kutokana na sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.
  
“Mimi nadhani hili ni jambo binafsi, sio vizuri kulizungumza hadharani ila kweli nilifunga naye ndoa maana inaonekana mnajua mambo mengi kunihusu, na ni kweli kwa sasa tumeachana,” alisema kwa kifupi.
  
Alisema walikutana na mbunge huyo Bagamoyo wakati alipokuwa akifanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali ya wilaya hiyo kama muuguzi mkunga wakati mbunge huyo akiwa muuguzi mkuu wa wilaya katika hospitali hiyo.
  
Alipoulizwa sababu za kukubali kufunga ndoa na mama wa umri wa miaka 60 wakati ana miaka 26 na sababu za ndoa hiyo kuvunjika, Michael alisema ana historia ndefu katika maisha yake kwani alizaliwa yatima na amekua na kulelewa kwa ufadhili wa kituo  cha Safina Street Network.
  
“Katika mazingira niliyokulia, unaweza kujua kwanini nilikubali kuingia kwenye ndoa hiyo. Sina ndugu hata wa kunishauri. Hata hivyo, hayo tuyaache. Lakini ukweli ndio huo, lakini kwa sasa tumeachana, kila mtu ana maisha yake,” alisema Michael kwa masikitiko.
  
Michael ambaye kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Muhimbili, pia alikiri kuwa mbunge huyo anashikilia vyeti vyote vya shule ambavyo anavihitaji sana kwa ajili ya kusaka ajira baada ya kumaliza masomo yake Muhimbili.

Alitaja sababu ya kuvunja ndoa hiyo kuwa ni manyanyaso kwa vile ni mdogo na masikini kwani hakuwa na sauti na alibanwa kwa kila kitu kiasi cha kukosa kabisa amani katika maisha yake.
  
“Kimsingi ndoa yangu na mama imevunjika na ilivunjikia mikononi mwa Rwakatare wakati akijaribu kutusuluhisha, alinitaka nirudi kwa mama, hapana, siko tayari na hapa nataka vyeti vyangu tu basi,” alisema Michael. 

Mbunge ang’aka
Kwa upande wake, mbunge huyo alipoulizwa, kwanza alikuwa mbogo na kukataa katakata kuzungumza kwa madai kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo zito kwenye simu.
  
Mbunge huyo alikiri kuwapo kwa ndoa hiyo, lakini alipinga kwamba haijavunjika na kumhoji mwandishi wa habari hizi kama anajua taratibu za kuvunja ndoa.
  
“Michael kakuambia hiyo ndoa imevunjika? Wewe si unajua taratibu za ndoa kuvunjika? Kwanza nimeshasema sitaki kuzungumzia suala hili kwenye simu ukitaka tuonane kesho kwani kuna haraka gani? Jambo la haraka ni la mjamzito kutaka kujifungua, lakini kama ni suala hilo hakuna sababu ya uharaka,” alisema mbunge huyo.
  
Hata hivyo baada ya kubanwa, mbunge huyo alimtaka mwandishi wa habari hizo kukutana naye katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufafanuzi, lakini cha ajabu mwandishi alipofika katika ofisi hizo hizo, mama huyo alizima simu yake na  hakupatikana tena.

Mchungaji Rwakatare
Alipotakiwa kuzungumzia ndoa hiyo, Mchungaji Rwakatare kwanza aling’aka kwamba hajawahi kufungisha ndoa ya aina hiyo.
  
Lakini alipobanwa alikiri kuikumbuka ndoa hiyo na kwamba ilifungishwa na mchungaji wa kanisa lake, aliyemtaja kwa jina la  Mchungaji Mtetumo.
  
Alimtetea mchungaji wake kwamba alichokifanya ni kutimiza wajibu wake wa kichungaji wa kufungisha ndoa, hasa kama wanandoa wametimiza vigezo.
  
“Wajibu wa kanisa ni kufungisha ndoa, kama wanandoa wamekidhi vigezo vya kanisa. Sio kazi ya kanisa kuwachagulia wachumba kwa maana hakukuwa na sababu ya kuhoji umri wao, wala jambo lolote zaidi ya kufungisha ndoa hiyo,” alisema Mchungaji Rwakatare.

-Tanzania daima

HAYA NDIYO MAANDALIZI KUFURU KWAAJILI YA FIESTA ITAKAYOFANYIKA DAR!!! CHEKI PICHA JINSI STAGE ILIVYO


10

Hapa bado haijakamilika, ni stage ambayo kukamilika kwake inachukua siku kumi ikiwa inatengenezwa… ni stage ambayo itakua na winch ya kupandisha wasanii kuja kufanya show, kutakua na screen za kisasa zaidi kuonyesha kila kinachoonekana kwenye stage..

7Kama unavyoona kwa mbali, kwa mara ya kwanza Fiesta hii backstage yake imejengewa nyumba ya kisasa zaidi na ndefu kwenda juu, ndani yake kutakua na baa, screen kubwa, makochi ya  kisasa kwa ajili ya watakaokuwepo hapo.
6
8
9Hii ni stage nyingine
3
4
1Ukiangalia kwa makini hapa kuna stage mbili kubwa ambazo zimeunganishwa na barabara ambayo inamuwezesha msanii kutembea juu huku mashabiki wakiwa pembeni kulia na kushoto yani…
2Hivyo ni baadhi tu ya vitu nimeamua kukupa kwa sasa mtu wangu, ungana na mimi saa moja usiku kwenye AMPLIFAYA ya Clouds FM ujue mengine mengi kuhusu teknolojia itakayotumika jumamosi hii kwenye stage ya Fiesta Leaders club Dar es salaam.

Habari na Millardayo.com

Wednesday, October 23, 2013

MADUDU MUHIMBILI YAENDELEA KUFUMULIWA, HAYA NI MAPYA KABISA. SOMA HAPA


Na Mwandishi Wetu

HUDUMA za afya nchini Tanzania ni wasiwasi jumlisha majanga, wapo madaktari wasio waaminifu wanaocheza na maisha ya wagonjwa, miili ya Watanzania ikichokonolewa na kupasuliwa bila sababu.
Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha gazeti hili, kilipata malalamiko kwamba kwenye hospitali nyingi binafsi, wapo wanaopewa magonjwa ambayo hawana ili wapunwe pesa bure. OFM kilipofanyia kazi tatizo hilo, kilijiridhisha pasipo chembe ya shaka kwamba mchezo huo upo na umeenea kwa kiwango kikubwa, kwani hata mwandishi wetu aliyejifanya mgonjwa ili kubaini ‘uhuni’ huo, nusura apasuliwe tumbo.
Awali, mama wa Kitanzania, Mary-Stella Maulid alitoa malalamiko yake OFM: “Sikuwa na tatizo la appendix (appendicitis au kidole tumbo), pale … (anataja jina la hospitali moja binafsi Dar es Salaam), waliniambia nina appendix.
“Waliniambia natakiwa kufanyiwa oparesheni haraka. Nilimpigia simu mume wangu, akaja pale hospitali, akanipeleka Muhimbili (hospitali ya taifa), alisema haziamini hospitali binafsi kwa oparesheni.
“Pale Muhimbili nikapimwa tena lakini majibu yalipotoka yalionesha sikuwa na appendix, isipokuwa nilikuwa na matatizo katika mfuko wa uzazi, nikapelekwa kwa mtaalamu wa mambo ya uzazi (gynecologist) ambaye alinisaidia sana.  

OFM KAZINI
Oktoba 16, mwaka huu, OFM ilimtuma mwandishi wa kike kwenda katika hospitali iliyotajwa na Mary-Stella ili kujiridhisha, hali ilikuwa hivi;
Mwandishi akijifanya anaumwa sana, alikuwa akitembea kwa kuinama, akilalamikia maumivu ya tumbo.
Saa 4:45 asubuhi alifika hospitalini hapo, akapokelewa na muuguzi mwanamke mwenye umri wa makamo ambaye alimsaidia kumpeleka mapokezi ambako rekodi zake ziliandikwa kisha akapewa kadi yenye namba ya faili lake.
Baada ya hatua hiyo, mgonjwa-mwandishi alisaidiwa kupelekwa kwenye chumba cha daktari ambako baada ya kujieleza, daktari aliagiza akafanyiwe kipimo cha Ultrasound ambacho gharama yake ni shilingi 30,000 kwa bei ya hospitalini hapo.
Kabla ya kuingia chumba cha ultrasound, mwandishi-mgonjwa, alitakiwa kunywa maji kiasi kisichopungua lita moja, baada ya kutekeleza hilo, aliingizwa kwenye kipimo.

UTANI UKAANZA
Majibu ya ultrasound katika hospitali hiyo, yalionesha kwamba mwandishi wetu hana tatizo la appendix lakini daktari akasema: “Utakuwa na tatizo la appendix, ultrasound haioneshi lakini ngoja nikupime zaidi.”
Daktari huyo (jina linahifadhiwa) akaanza kufanya kazi ‘manyuali’, akimshika mwandishi-mgonjwa kwa mikono, akipapasa sehemu ya tumbo kwa chini kisha akaibuka na jibu: “Ni appendix kabisa, inabidi tukufanyie oparesheni.”
Aidha, daktari alimtaka mwandishi-mgonjwa atoe shilingi 600,000 ili afanyiwe oparesheni ya kuondoa kidole tumbo.
Hata hivyo, mwandishi-mgonjwa alisema hana fedha, kwa hiyo akaomba apewe muda na angerudi siku iliyofuata ambapo daktari akiwa na macho makavu, alimruhusu.

MWANDISHI MPAKA MUHIMBILI
Kwa mtindo uleule, mwandishi wetu akijifanya hawezi kutembea vizuri, alikwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, Oktoba 17, mwaka huu na kufanikiwa kuonana na daktari (jina kapuni).
Daktari huyo baada ya kumsikiliza mgonjwa, alimwambia arudi Oktoba 28, mwaka huu (yaani siku 11 baadaye) ndipo atafanyiwa ultrasound.
Katika cheti cha mwandishi wetu, daktari alimwambia kuwa siku hiyo arudi na maji lita moja, tishu (makaratasi) na afike hospitali saa 2.00 asubuhi.

MWANDISHI AKUNA KICHWA
Majibu ya daktari Muhimbili yalimfanya ajiulize: “Mtu unaumwa tumbo hata kutembea huwezi, unaambiwa urudi nyumbani mpaka Oktoba 28, yaani siku 11 baadaye, je, appendix ikipasuka nikifa?”
Mwandishi aliwaza na kuwazua kisha akaenda Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi) ambako alipokelewa na kupimwa ultrasound chapchapu kwa gharama ya shilingi 40,000.
Majibu ya Moi kama yanavyoonekana ukurasa wa kwanza, ilibainika hana appendix na daktari alishauri afanyiwe CT Scan ili kama kuna tatizo lingine tumboni lionekane.

NINI CHA KUJIFUNZA?
Hali ni mbaya nchini hususan kwenye Jiji la Dar es Salaam kwa sasa, ni wazi kwamba kama Mtanzania asipokuwa mwangalifu, anaweza kufanyiwa oparesheni bila sababu ili mradi  watu wapate pesa!
Uchunguzi wetu umebaini kuwa wetu wengi katika hospitali binafsi wanaingiwa na tamaa mbaya ya fedha, kiasi cha kucheza na maisha ya watu.
“Wengi wameshafanyiwa oparesheni wakati haikuhitajika wafanyiwe. Mtu anachanwa tumbo halafu anashonwa, anaambiwa amekatwa appendix wakati siyo kweli, kuna utapeli mwingi katika baadhi ya hospitali binafsi,” alisema Mary-Stella.
Wakati Watanzania wakitendewa hayo, hali halisi inaonesha kwamba serikali yao haijui chochote.
Uchunguzi zaidi unaonesha kuwa hospitali binafsi zimekosa udhibiti kiasi kwamba zinachaji bei kubwa utadhani huduma za afya ni anasa na siyo mahitaji ya  lazima kwa binadamu.
Imebainika kuwa katika baadhi ya hospitali binafsi, madaktari wake ambao mara nyingi ni waajiriwa wa muda (part-time), wamekuwa wakitumiwa na wamiliki wa hospitali hizo kuwakamua wagonjwa fedha nyingi katika vipimo na matibabu yasiyo ya lazima ili kuingiza fedha.
“Hali ni mbaya sana, imefikia madaktari wanamwandikia mgonjwa vipimo vingi bila sababu lengo likiwa ni kumfanya alipe fedha nyingi ili mradi wao wamechukua sehemu ya malipo hayo,” alisema Anania Bella wa Sinza Mori, Dar es Salaam.
Aidha, OFM imebaini kuwa hata pale daktari anapofahamu mgonjwa wake ana ugonjwa fulani mfano,  malaria, badala ya kupima kwanza damu ili ijulikane, atamwandikia lundo la vipimo kama widal test (typhoid), kipimo kikubwa cha damu  (full blood picture) na mkojo, ili mradi alipe pesa nyingi.
Muuguzi mmoja wa Muhimbili mwenye moyo wa uzalendo (jina tunalo) alisema: “Kinachosikitisha zaidi ni pale mgonjwa anapokuwa anaumwa tumbo, ataandikiwa vipimo vingi vikubwa vya gharama kubwa kama ultrasound ambayo hugharimu shilingi 20,000 mpaka 50,000, CT-Scan shilingi 300,000 na MRI (magnetic resonance imaging) shilingi 450,000.”
Aliongeza kuwa hali huwa mbaya zaidi pale mgonjwa huyo anapolipiwa na bima, kwani gharama hufanywa karibu mara mbili ya bei anayotozwa mgonjwa anayelipa taslimu sababu inayolipa ni serikali.
“Kwa huu mwendo na kama serikali haitafanyia kazi hili, huko mbeleni tunaweza kushuhudia NHIF (Mfuko wa Bima ya Taifa) ikifilisika.
“Tujiulize, kwa nini  kama mgonjwa anaumwa tumbo ili kumpunguzia gharama usimfanyie kwanza ultrasound, usipopata jibu ndipo umfanyie CT-Scan nayo isipoonesha majibu ndipo umfanyie MRI?” anahoji muuguzi huyo.
Taarifa za kusikitisha zaidi zimedai kwamba baadhi ya hospitali jijini zimekuwa zikiwalazimisha wagonjwa kufanyiwa oparesheni hasa za uzazi ambazo hutozwa hadi shilingi milioni mbili ili tu ziingize pesa, wakati wahusika wanaweza kujifungua kwa njia ya kawaida.

MAJANGA MENGINE
Gazeti hili linazo taarifa pia kwamba vifaa katika hospitali za serikali huharibika mara kwa mara kwa sababu ya hujuma ili wagonjwa waende hospitali binafsi.
Nesi aliyejitaja kwa jina la Subi wa hospitali moja binafsi inayomilikiwa na watu wenye asili ya Bara la Asia, alisema: “Huoni siku hizi watu maskini wanakuja hapa kupima? Muhimbili, Mwananyamala na hata Amana wanawaambia waje huku.
“Daktari ambaye anamleta mgonjwa kupima huku anapata kamisheni. Vilevile tambua kwamba madaktari haohao wa hizo hospitali ndiyo hufanya hapa na kwenye hospitali nyingine binafsi kwa part-time,” alisema Subi.

SERIKALI INASEMAJE?
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, (pichani) alipoulizwa kuhusu skendo hii alijibu: “Hayo mambo siwezi kujibu sasa, labda mpaka mniandikie maswali halafu niwasiliane na vitengo vinavyohusika.”
MWANDISHI: Mheshimiwa, kuna hili hata la bei, hizi hospitali binafsi mbona zinachaji bei kubwa utafikiri kutibiwa ni anasa?
DK. MWINYI: Hilo pia siwezi kujibu, kuna vitengo vinavyohusika.
MWANDISHI: Wewe ni waziri mwenye dhamana, je, huna mpango wa kuweka sheria ya udhibiti wa bei kwenye hospitali binafsi? Mbona Ewura wanadhibiti bei za mafuta japo ni soko huria?
DK. MWINYI: Niandikie maswali halafu niletee nitashughulikia.
MWANDISHI: Na hawa Watanzania si wataendelea kupasuliwa na kutibiwa magonjwa ambayo hawaumwi kwa sababu watu wanataka pesa?
DK. MWINYI: Haya mambo yapo katika vitengo, nitayajibu kwa pamoja baada ya kunipa maswali na kuwaita wahusika

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI, JOHN CASMIR MINJA AFUNGA KIKAO CHA BAJETI YA SHIRIKA LA UZALISHAJI LA MAGEREZA MKOANI, MOROGORO.



1
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba ya ufungaji wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kilichofanyika kwa muda wa siku mbili katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro. Kikao hicho  cha  Bajeti ya Shirika la Magereza kwa mwaka wa fedha 2013/2014 kilifunguliwa rasmi Oktoba 21, 2013 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb). 2Baadhi ya Wajumbe Washiriki wa Kikao cha Bajeti ya Shirika la Magereza kwa mwaka wa fedha 2013/2014 wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya ufungaji wa Kikao hicho katika Ukumbi wa Hoteli ya Edema, Mkoani Morogoro. imageKamishna Jenerali wa Magereza Nchini( wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza Mikoa yenye miradi ya Shirika la Uzalishaji la Magereza kwa waliosimama katika picha( wa pili kushoto) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile( wa tatu kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa( wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga( wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ndg. Janabi(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna wa Magereza, James Selestine. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

MAENDELEO YA MSIBA WA "BI MARTHA SHANI" WASHINGTON DMV



KWA WATANZANIA WOTE
Marehemu Martha Shani ( 1976- 2013 )
Marehemu Bi Martha akiwa na Mumewe Alex pamoja na Watoto wao Jose na Chris

BADO TUNAHITAJI MSAADA WENU WA HALI NA MALI ILI KUWEZESHA KUSAFIRISHA MWILI WA MWENZETU MARTHA SHANI ALIYEFARIKI GHAFLA SIKU YA JUMAMOSI OCT 19, 2013. KUTOA NI MOYO NA CHOCHOTE UTAKACHOWEZA KITASAIDIA NA HATIMAE KUWEZESHA SAFARI HII NDEFU YA KUMPELEKA MAREHEMU KATIKA MAPUMZIKO KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE TANZANIA.
GHARAMA ZA MSIBA  KUSAFIRISHA MAREHEMU NA FAMILIA YAKE NI  $19,500
FEDHA ZILIZOPATIKANA HADI SASA  NI $4,300
ZILIZOBAKI $ 15,200

TAFADHALI TUMA RAMBI RAMBI ZAKO KUPITIA ACCOUNT IFUATAYO :-
# 446030759150 BANK OF AMERICA,MD
ROUTING # 052001633
MAJINA KWENYE ACCOUNT NI ALEX KASSUWI & FAITH ISINGO

CHEKI ZINAWEZWA ANDIKWA KWA ALEX KASSUWI AU FAITH ISINGO.

PIA UNAWEZA KUTOA RAMBIRAMBI ZAKO KWA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU AMBAKO NDIKO MSIBA UPO
ADDRESS NI 
482 ARWELL CT
FREDERICK, MD,21703

AU WAWEZA WASILIANA NA MMOJA YA WANAKAMATI HAPO CHINI NA KUMUELEKEZA UPO WAPI ILI AWEZE KUKUSANYA MCHANGO WAKO 

Tino Malinda -240-565-7133
Dickson Mkama - 301-661-6207
Mariam Mtunguja - 240-422-1852
Quizella Ntagazwa - 240-602-5011
MV Mtunguja- 240-593-0575
Victor Marwa - 240-515-6436

Julius Manase-240-393-8445
Faith Isingo - 240-705-1055

UKISOMA UJUMBE HUU TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZIO.
WAJIBU HUU NI WETU SOTE NA KWA PAMOJA TUNAWEZA
HAKUNA KIDOGO PALIPO NA NIA. NA HAKUNA KIKUBWA PALIPO NA UMOJA

Chanzo   changamotoyetu.blogspot.com

‘Elimu ya Tanzania iko mahututi’


mchome_e33b4.jpg

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome
Siku moja baada ya maudhui ya Ripoti ya Tume iliyoundwa kuchunguza matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana kuwekwa wazi, wadau wa elimu wamekiri na kusema kuwa mfumo wa elimu ya Tanzania upo katika hali mbaya.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, James Mbatia alisema matokeo ya tume hiyo yanaonyesha udhaifu wa hali ya juu katika sekta ya elimu jambo ambalo alishawahi kulisema katika hoja maalumu bungeni.
Mbatia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, alisema alishawahi kuishauri Serikali kuufumua mfumo wa elimu nchini na kuanza upya ili kunusuru taifa la kesho ambalo ndilo linaloathirika na rasilimali watu zisizo na ubora.
Matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana yalionyesha kuwa asilimia 60.6 ya wanafunzi Tanzania walipata alama sifuri na wanafunzi 23,520 sawa na asilimia tano ndiyo waliofaulu jambo ambalo lilisababisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuunda tume ya kuchunguza matokeo hayo.
Baadaye, mitihani hiyo ilisahihishwa upya na Pinda kukabidhiwa matokeo Juni, mwaka huu.
"Nilishasema katika hoja yangu bungeni Januari 31 na Februari 1, mwaka huu nikamwomba waziri anionyeshe mitaala ya elimu ya sasa, lakini hakuitoa," alisema Mbatia.
Mbatia alisema ili taifa hili liondokane na janga la elimu lililopo halina budi kukubali kuwa ni kweli Tanzania ipo katika janga la elimu na kuunda dira ya elimu itakayotuongoza katika safari ya elimu nchini.
Mbatia aliongeza kuwa elimu ya Tanzania ipo mahututi na kuwa kila mwaka wanafunzi wanaomaliza katika shule mbalimbali hawana sifa za kutosha za kuweza kushindana katika masoko ya kimataifa.
"Tumeshaanza kuona taifa linaangamia kwa sababu ya ubovu wa elimu, ni lazima tukiri hilo kwa sababu hata Rais alikiri na kuikubali hoja yangu Aprili 30 mwaka huu alipokuwa mkoani Mbeya" alisema Mbatia
Mbunge huyu ambaye awali aliteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa tume ya uchunguzi wa matokeo haya na kukataa kushiriki alisema, ili Serikali iondokane na janga hili haina budi kuunda Kamati ya Bunge ambayo itaisimamia Serikali na kutoa mawazo mapana kuhusu elimu.
Mbatia alishauri Bunge lisiegemee itikadi za vyama au porojo za kutaka sifa za kisiasa na badala yake suala la elimu lijadiliwe kwa maslahi ya taifa.
Mdau mwingine wa elimu, Dk Method Samwel, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUSE), alisema tatizo la elimu hapa nchini lielekezwe zaidi kwenye mfumo uliopo kuliko laumu taasisi au mtu mmoja mmoja.
Dk Samwel alisema tangu zamani mfumo wa elimu umekuwa ni wa kudorora na haya ni matokeo ya mfumo huo ambao haukuwa na misingi imara kwa muda mrefu.
Alitolea mfano wanaokwenda kusomea ualimu wengi ni wale waliofeli kwa kupata daraja la nne, jambo ambalo linasababisha wataalamu wa kada hiyo kuwa ni wale waliofeli pekee.
"Yapo mambo mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi katika sekta ya elimu Tanzania, suala la kudai kuwa Baraza la Mitihani na Taasisi kuwa ndizo taasisi zenye makosa, hazina ukweli," alisema.
Hata hivyo, Dk Samwel alisema, tume hiyo bado ina maswali mengi ya kujibu kulingana na walichokisema katika sehemu ya ripoti yao.
"Nashindwa kuelewa kwa sababu kila nikisoma majibu ya tume hiyo napata maswali mengi zaidi. Kwa mfano, walimu waliofanya mtihani wakafeli walipewa muda wa kujiandaa? " alihoji na kuongeza:
"Na kuhusu mitihani ya Tanzania kuonekana kuwa ni migumu zaidi, Je waliwapa mitihani ya Tanzania wanafunzi wa nchi nyingine au walitumia mbinu gani kupata matokeo hayo?"
Hata hivyo, Mkuu wa Kitivo cha Elimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo, alipinga ripoti ya tume hiyo na kusema kuwa wamepotosha taarifa kwani tatizo halikuwa katika mtihani bali ni wanafunzi wenyewe wamefeli.
Dk Mkumbo amesema tatizo si la walimu, wala baraza, wala mitihani yenyewe bali ukweli utabaki kuwa wanafunzi walifeli mtihani wa Kidato cha Nne kwa sababu ya mfumo mbovu wa elimu.
Mhadhiri huyo alihoji tena kuwa tume hiyo ilitumia njia gani kujua kuwa mtihani wa Sayansi ulihitaji saa sita kuufanya na ni kwa mbinu gani waliupima mtihani wa Tanzania na kujua kuwa ni mgumu kuliko mitihani mingine.
"Nilipata ripoti fulani iliyoonyesha kuwa mitihani ya Tanzania ni mizuri na haina matatizo, ripoti ilionyesha kuwa haina chembe ya mashaka na inatungwa kwa ustadi. Tusitafute sababu, tatizo si mitihani ni wanafunzi wenyewe wamefeli," alisema.
Pia, Dk Mkumbo alisema kuwa ni dharau kubwa kusema kuwa baadhi ya wasahihishaji hawakuwa na sifa kwani hilo ni tusi kubwa kwa walimu kwani wao ndiyo wamekuwa wakisahihisha kila siku.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini,(Tamongsco), Albert Katagira alisema si kweli kuwa mtihani ulikuwa mgumu bali tatizo lipo katika uandaaji wa wanafunzi.
"Mtihani ulikuwan sahihi kabisa, mbona wanafunzi wengine walifaulu. Ni wanafunzi wenyewe, ambao nao hatuwezi kuwalaumu moja kwa moja," alisema Katagira.
Alisema taifa bado lina tatizo katika mfumo wa elimu na kuweka mkazo katika masomo ya sayansi na hisabati ambayo yanaonekana kuwa magumu kwa wanafunzi wengi.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mafinga, Mustapha Mambea alisema, mtihani wa Fizikia na Kemia haikuwa migumu, lakini kuna mada kadhaa ambazo hawakufundishwa.
Profesa Mchome aongea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema kuwa wameshindwa kuiweka hadharani ripoti hiyo kwa kuwa bado inafanyiwa kazi serikalini.
Profesa Mchome, ambaye ndio aliongoza tume hiyo, alisema kuwa ripoti hiyo inatakiwa kupelekwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa.
Alidokeza, hata hivyo, tayari walikuwa wameanza kufanyia kazi baadhi ya vitu vinavyotakiwa kufanyiwa kazi haraka kwenye ripoti hiyo.
Katibu Mkuu wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, ambaye ameomba likizo ya muda mrefu ikitafsiriwa pengine ndio mwanzo wa utekelezaji wa ripoti hiyo.
Chanzo:Mwananchi

Monday, October 21, 2013

TAKE CARE !! UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI



Sasa wanatumia mitandao ya Internet ya Kuomba ajira
Kwa hisani ya mdau Henry Kapinga

Kuna UTAPELI mpya umeingia nchini Tanzania.
Watu ambao wanajifanya wana makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za kazi, nafasi hizo hutangazwa kupitia mitandao ya Internet ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo ambayo tunaiongelea hapa.

Matukio yenyewe yanakuwaje?
Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai  wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi hicho.

Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.

Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao matapeli.

KUWA MAKINI EWE MTANZANIA

Friday, October 18, 2013

KIJANA ANAYETEMBEA NCHI NZIMA KWA BAISKELI KUHAMASISHA AMANI AWASILI MKOANI IRINGA.



Mkuu  wa  mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma (kulia) akimpongeza kijana Japhet kutoka mkoa wa Mwanza  baada ya kupokelewa mjini Iringa, kushoro ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Gervas Ndaki.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki akimpongeza kijana huyo kwa uzalendo.





Kijana Japhet wakati akipokelewa mkoani Iringa.

Safari ya kijana Japhet ilianzia mkoani Mwanza na sasa amefunga mikoa nane  kwa kumalizia mkoa wa Morogoro na malengo yake ni  kutembea nchi nzima hadi ifikapomwaka 2015 awe amefikisha ujumbe wa amani nchi nzima.
(PICHA NA FRANCIS GODWIN, IRINGA)