Thursday, April 23, 2015

Understanding Albinism: Baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu Watu wenye Albinism

Watu wenye Albinism wanakosa chembechembe  zinazotengeneza rangi  ya asili ya ngozi inayoitwa melanin.Chembechembe hizi hutengenezwa katika ngozi,macho na katika nywele. Watu wanaokosa rangi ya asili yaani Melanin ni rahisi zaidi kupata saratani ya ngozi kwa kuwa ngozi hiyo haina kinga dhidi ya mionzi ya jua. Pia kutokana na tatizo hilo watu wenye  Albinism wana uoni hafifu na wanapata shida wakati macho yao yanapokutana na mwanga mkali.

Tuesday, April 14, 2015

BAADA YA DIAMOND KUMKATAZA KWENDA A KUSINI KUJIFUNGULIA, HII NDIYO HOSPITALI ZARI ANAYO ENDEA KLINIKI HAPA BONGO...

CHEKI HAPA==>> http://goo.gl/VXpVhF
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemzuia mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenda kujifungulia nje ya Bongo pindi mambo yatakapokuwa tayari.
Habari zilizonyakwa na Ijumaa Wikienda kutoka kwenye chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zilieleza kwamba, tayari jamaa huyo amemuanzishia Zari kliniki Bongo.....CHEKI HAPA==>> http://bitly.com/1BdWcNS
“Yaani Diamond hataki kabisa Zari kwenda kujifungulia South Africa (Sauzi). Anataka kila kitu kifanyike hapahapa Bongo. Tayari amemuanzishia kliniki kwenye Hospitali ya AMI (ipo Masaki, Dar),” kilitonya chanzo hicho.....CHEKI HAPA==>> http://bitly.com/1Ir7UGT
Akizungumzia ishu hiyo, Diamond alisema kuwa anatamani kuwa karibu na mama kijacho wake huyo hivyo ni kweli anataka mwanadada huyo ajifungulie Bongo.....CHEKI HAPA==>> http://bitly.com/1C1bt2G
Diamond au Baba Kijacho alisema lengo la kufanya hivyo ni ili iwe shangwe kwa familia nzima tofauti na atakapojifungulia nje ambapo familia italazimika kusafiri kwenda kumuona Chibu Junior.
Kwa mujibu wa Diamond, Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akifukuzia huyo wa nne anatarajia kujifungua kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka huu.....CHEKI HAPA==>> http://bitly.com/1DGo1To

Monday, April 13, 2015

Dr. Slaa Amepokelewa Tayari Washington Kuanza Ziara Yake Kikazi

[Picture: Dr. Slaa , his wife Josephine and constitutional experts, Professors  J.M Curtis and Dickson Ramsey]
CHADEMA  Secretary General, Dr. Wilbrod Slaa has arrived safely into the United States, in the State of Indiana, where he was met by the State Governor Mike Pence at Indianapolis International Airport before proceeding to the State Capital, (Governors mansion) where they exchanged ideas and planned a follow up discussions in a couple of days to come. 
Dr. Slaa was accompanied by his wife Josephine, and his spokesperson, Liberatus Mwang'ombe. Among other things, both leaders discussed various issues of which constitutional challenges took the center stage. 
The Governor and other constitutional experts in discussion were particularly concerned with developments from Tanzania in which people's views might not be reflected in the proposed constitution. 
Long term peace and economic prosperity in any given country, depends on the kind of constitution they have. Tanzanians voices must be respected said Professor Curtis. A sentiment which was echoed by Dr. Slaa, who said that Chadema and its parters in UKAWA coalition will never accept a mutilated Constitution not meant for the people, but for the few corrupt rulers and their henchmen. 

Saturday, April 11, 2015

Mfahamu the Boss Lady hapa!


Childhood background: Born on the 23rd of September 1980. Zari grew up in a town called jinja in a country situated in east Africa known as Uganda, she attended her primary and later moved to Jinja girls high School where she thought to cultivate very positive personalities and passionate attitude towards achieving her dreams, on completion she moved to the city of kampala (The country capital city) where she performed karaoke in hang-outs during are vacation before she moved to London and acquired a diploma in cosmetology.
Music history: Zari started singing at early age in her primary days where she performed in musical concerts organized by her primary school staff, school’s end of the year functions and other community competitions representing her own school in shining colours. When she gained entrance into high school she joined the dance, drama and music groups which helped her score best actress for 2 consecutives years. After years of brilliant stage performances and school concerts, She took a break after moving from Uganda to London and continued with her studies but still with the compelling passion of music on her mind.
Zari with support from family fans and friends who love her style of music and believe in her career took a bold step in 2007 recording her 1st single called oliwange (meaning you’r mine) .The single album luckily made it to the Africa channel o awards in the category of best east African video of the year. The awards where held in South Africa, Johannesburg. Since then Zari has released more and more interesting tracks with satisfactory acholades from her fans in the recent times.
In 2009 she scored the Diva awards award of the year in the Diaspora category since then she has just continues making more music.
Compiled by: Zenobia


Zari (Zarinah Hassan) is a Ugandan musician.
Her heritage involves many countries, her grandfather on her moms’ side is Indian and her grandmother Ugandan, her grandfather on her dads’ side is Somalian and her grandmother a Burundian.


She grew up in Uganda doing karaokes and performances but now lives in South Africa where she runs cosmetics shop and a tertiary college in Pretoria while pursuing a career in music.


She won a Channel O Music Video Award nomination for best East African artiste in 2008.


Ten Things You Never Knew About The Bosslady
Zarinah Hassan known by her stage name as Zari is a Ugandan Musician based in South Africa where she lives with her husband Ivan and their three lovely sons Pinto, Didy and Quincy. She is an entrepreneur in South Africa where she owns a tertiary college and cosmetics shop. With her Zari All White Champagne Party slated for 21st April, we thought this would be the best time to bring you ten facts you never knew about Uganda’s top showbiz star.

Gwajima bado yuko ngangarii!

Atakiwa kupeleka polisi nyaraka zake, Vimo vielelezo vingine vya mali za kanisa.


Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.


Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, jana alihojiwa kwa mara ya pili na Jeshi la Polisi kwa takribani saa tano huku akitakiwa kupeleka vielelezo 10 ikiwamo nyaraka ya helikopta anayomiliki.
 
Askofu Gwajima aliwasili katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano hayo saa 1:14 asubuhi akiongozana na Msaidizi wake, Mchungaji Gwandu Mwangasa na Mwanasheria wake, John Mallya.
 
Licha ya juzi kuelezwa kuwa afya ya kiongozi huyo imeimarika, lakini jana Askofu Gwajima alisaidiwa kupanda ngazi na wasaidizi wake huku Mallya akiwa upande wa kushoto na Mchungaji Mwangasa upande wa kulia.
 
Ilipofika saa 6:40, Askofu Gwajima na wasaidizi wake walitoka ndani ya chumba cha mahojiano huku akijikongoja.
 
MWANASHERIA WAKE
Akielezea kilichojiri katika mahojiano hayo, Mwanasheria wake Mallya alisema kuwa Jeshi la Polisi lilimhoji Askofu Gwajima muda mrefu mambo ambayo hayaendani na kosa analotuhumiwa kulitenda.
 
VIELELEZO VYA KUPELEKA
Alieleza kuwa Jeshi la Polisi lilimtaka Askofu Gwajima kuwasilisha vielelezo 10 kituoni hapo Aprili 16, mwaka huu.
 
Alivitaja vitu hivyo kuwa ni hati ya usajili wa kanisa lake, nyaraka za idadi ya makanisa anayomiliki pamoja na  kuwasilisha muundo wa uongozi wa kanisa lake.
 
Viingine ni idadi ya nyumba na mali ambazo kanisa linamiliki, nyaraka ya umiliki wa helikopta anayomiliki na muundo wa Bodi ya Wadhamini wa Kanisa pamoja na majina yao.
 
Kwa mujibu wa Mallya, vingine ni returns (makusanyo) ya kanisa, kumpeleka mtu anayepiga picha za video) katika kanisa lake, waraka ulioandaliwa na Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo pamoja na namba ya usajili ya kanisa analomiliki.
 
Hata hivyo, Mallya alisema kuwa Polisi walimhoji Askofu Gwajima masuala ya familia yake na wazazi wake badala ya tuhuma anazotuhumiwa za kumtukana na kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
 
“Ninawashangaa polisi, wamemhoji mteja wangu masuala yanayohusu familia yake na wazazi wake kuliko tuhuma anazotuhumiwa,” alisema Mallya.
 
Mallya alieleza kuwa kutokana na hali hiyo, wamepanga kwenda mahakamani kufungua kesi kupinga kitendo hicho.
 
Katika hatua nyingine, Mallya alieleza kuwa Askofu Gwajima anatarajia kwenda nje ya nchi kutibiwa, lakini hakufafanua zaidi ni nchi gani wala hospitali gani.
 
KAULI YA GWAJIMA
Mara baada ya kutoka katika mahojiano, Askofu Gwajima alieleza kuwa mahojiano kati yake na Jeshi la Polisi yalikwenda vizuri.
 
WAFUASI WAFURIKA POLISI
Wakati Askofu Gwajima akihojiwa ndani, nje ya kituo cha polisi wafuasi wake walifurika wakitaka kufahamu hatma ya kiongozi wao.
 
Kutokana na hali hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi, Kamanda Simon Sirro, aliwasihi kutawanyika.
 
“Gwajima yupo katika mikono salama, nendeni mkafanye kazi za kuzalisha mali sasa, mkirundikana wote hapa nani atafanya kazi?” Kamanda Sirro aliwaeleza wafuasi hao.
 
Kamanda Sirro aliwaeleza kuwa Jeshi la Polisi limeshamrejeshea Askofu Gwajima hati yake ya kusafiria, hivyo anaweza kwenda kutibiwa kokote.
 
“Askofu Gwajima yupo ndani anahojiwa akimaliza ataruhusiwa,” alisisitiza.
 
Hata hivyo, mmoja wa wafuasi hao alimjibu Kamanda Sirro: “Akiondoka nasi tutaondoka.” 
 
Naye Kamanda Sirro alijibu: “Makubwa.” Jibu lililowaacha wafuasi hao watapao zaidi ya 100 kuendelea kumsubiri nje.
 
Machi 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, lilimwamuru Askofu Gwajima kujisalimisha polisi kwa tuhuma za kumkashifu Kardinali Pengo.
 
 Machi 27, mwaka huu, Askofu Gwajima alijisalimisha kituoni hapo  lakini wakati akihojiwa alizimia akiwa chumba cha mahojiano kisha kukimbizwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu. 
 
 Jumanne ya wiki iliyopita, Askofu Gwajima aliondolewa TMJ na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay na kuachiwa bila masharti, lakini alielekezwa kuripoti Alhamisi iliyopita katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE

Friday, April 10, 2015

Mahita alikosoa Jeshi la Polisi, Mangu amfungukia


“Askari lazima atishe. Popote anapokuwapo wahalifu wajue kuwa kuna mtu hatari dhidi yao. Kama mhalifu atatiwa woga na uwepo wa polisi, uhalifu utapungua tu na hivyo kubakiwa na kazi ndogo ya kuwakamata wachache wanaoendelea na vitendo hivyo.” Omari Mahita
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu, Omary Mahita amesema askari polisi kwa sasa wamepoteza hadhi, hawaogopwi na wahalifu na ndiyo sababu kubwa ya kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu kila kukicha.
Mahita aliyestaafu mwaka 2006, alisema mbali na kuongezeka kwa uhalifu, inafikia hatua wahalifu wanawaingilia polisi kwa kuvamia vituo vya polisi na kupora silaha ilhali zamani hakukuwa na matukio hayo.
Hata hivyo, IGP, Ernest Mangu amejibu kauli hiyo akisema: “Siwezi kutumia mbinu za Mahita kwa sababu alichokuwa anakabiliana nacho, kwa sasa hakipo.”
Kauli ya Mahita
Kauli ya Mahita imekuja miezi minane baada ya askari 10 kuuawa na bunduki zaidi ya 20 kuporwa katika matukio mbalimbali ya uvamizi wa polisi na vituo vya polisi.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mkurugenzi wa zamani wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Dk Mohamed Mhita, Oysterbay Dar es Salaam juzi, Mahita alisema: “Ili kupunguza vitendo vya kihalifu vinavyozidi kuongezeka kila kukicha, ni lazima askari warudishe hadhi yao ya kuogopwa na wahalifu popote walipo.
“Askari lazima atishe. Popote anapokuwapo wahalifu wajue kuwa kuna mtu hatari dhidi yao. Kama mhalifu atatiwa woga na uwepo wa polisi, uhalifu utapungua tu na hivyo kubakiwa na kazi ndogo ya kuwakamata wachache wanaoendelea na vitendo hivyo.”
Mahita alikosoa kitendo cha askari polisi kuwa wapole na kueleza kuwa hilo ni suala lisilotakiwa kabisa kufanywa ndani ya jeshi hilo na polisi... “Unambembelezaje mhalifu? Hawa ni watu wanaostahili kubanwa kwa kila namna ili kukomesha vitendo vyao katika jamii. Mhalifu yeyote akiachiwa, madhara yake ni makubwa katika jamii.”
Licha ya suala hilo, IGP huyo mstaafu alieleza umuhimu wa doria katika kudhibiti uhalifu wa kila siku ambao hupunguza amani miongoni mwa jamii na kuwafanya wananchi washindwe kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na ratiba waliyojiwekea.
 Alitolea mfano wa vikundi vya uhalifu vilivyojitokea hivi karibuni kama ‘Panya Road’, ‘Mbwamwitu’ na ‘Libya’ kwamba vimekuwapo kutokana na kupungua kwa doria inayotakiwa ifanywe na jeshi hilo nchi nzima na hasa maeneo ya mijini.
“Enzi zangu doria ilipewa kipaumbele. Magari na pikipiki yalikuwa yanazunguka kote katika jiji hili na kwingineko mikoani karibu kila siku na walikuwa wanaogopeka… kwa sasa yapo lakini sidhani kama wanafanya kazi kama ilivyokuwa enzi zile,” alisema Mahita.
“Wahalifu walikuwa wanajua kuwa polisi wapo kazini muda wote. Lakini sasa hivi mambo hayo hayapewi uzito unaotakiwa ndiyo maana unaona kikundi kama Panya Road kinatingisha mji mkubwa kama huu (Dar es Salaam).
“Inawezekana vipi kikundi kama hicho kikatingisha amani ya jiji hili lenye viongozi wote wa jeshi?” alihoji Mahita.
Mahita alikuwa maarufu kwa jina la ‘Ngunguri’ kutokana na kauli yake alipokuwa akikabiliana na maandamano ya wafuasi wa CUF kwamba kama viongozi wake wako ngangari basi polisi iko ngunguri kukabiliana nao.
Akizungumzia uhalifu katika vituo vya polisi, Mahita alisema polisi imekosa kuungwa mkono hivyo kupunguza ufanisi wake katika kutekeleza majukumu yake.
“Hata jamii ipo mbali pia… Raia ndiyo wanavamia na kuua askari. Watu hawa wanaishi katika jamii hiihii. Hivyo ni vyema ikajirudi na kuona kuwa hii ni taasisi muhimu kwa maisha na mali ya kila mwananchi.”
Akizungumzia vifo vya askari hao, Mahita alisema kuwa jamii imewasahau na kuwatenga kwani hakuna anayeshtuka pindi wanapoteza maisha hata kama mauti hayo huwakuta wakiwa kazini.
IGP Mangu
Akizungumzia hoja hizo, Mangu alisema mabadiliko ya jamii na maendeleo ya kiuchumi yamebadili mbinu za uhalifu.
“Mbinu za kiuhalifu zimebadilika kiasi cha kulilazimu jeshi pia kubadilika ili kuendana na mbinu hizo mpya. Haiwezekani jeshi likabaki kama ilivyokuwa miaka 20 iliyopita.
“Jamii ya wakati wa Mahita ni tofauti na ya sasa. Hata askari hawawezi kuendelea kuwa wale waliokuwapo. Mazingira na kila kitu vimebadilika. Enzi hizo kulikuwa na uhalifu wa ulipuaji wa mabomu na utakumbuka ilishatokea huko Arusha na Zanzibar matukio ambayo hayapo kwa sasa,” alisema Mangu. Alisema ni vigumu kulinganisha vipindi tofauti vya viongozi na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kutowatendea haki kwani wanakuwa wanaongoza katika mazingira tofauti kwa kila kitu.
“Kubadilika kwa mbinu na aina za uhalifu kunamlazimu kiongozi husika kuitikia mabadiliko hayo pia. Mimi siwezi kutumia mbinu za Mahita kwa sababu alichokuwa anakabiliana nacho hakipo sasa hivi. 
Hapakuwa na mauaji ya albino wakati wake, hili peke yake linaonyesha jamii iliyopo ni tofauti na iliyokuwapo,” alisema.
“Hata mimi nikistaafu baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba atakayekuja atapata changamoto tofauti na hizi ninazokutana nazo au walizokutana nazo watangulizi wangu,” alisema.
“Rais Kikwete alikemea  mauaji ya polisi kila yanapofanywa... hivi ndivyo tunavyotakiwa kufanya,” alisema Mangu.
Copied from Paparazi Blog.

Mgomo Wa Madereva: Serikali Yakubali Kufuta Agizo la Kuwataka Madereva Kwenda kusoma ili Kumaliza Mgomo..


Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)


Kuhusu suala la Madereva kusoma, Serikali na Madereva wamekubaliana kukutana mwezi huu tarehe 18 kuzungumza njia mbadala ya kutumika.


Miongoni mwa malalamiko ya madereva ilikuwa ni kukerwa na tochi za barabarani, hivyo jeshi la Polisi wamekubali kuziondoa.


Pia serikali imeagiza Madereva wote wapewe mikataba ya ajira za uhakika na waajiri wao na Trafiki wameagizwa kulifatilia hilo.




------------------------------
Minister of Labour and Employment, Hon. Gaudencia Kabaka has successfully completed the strike of drivers after announcing cancellation command was ordering drivers of buses and trucks to read again in the National Institute of Transportation (NIT) 

Regarding the drivers to read, Government and drivers have agreed to meet this month on 18 speak alternatives used. 


Among the complaints of drivers was offended by the torch of the road, so Police have agreed to remove them. 


Also the government has ordered all drivers receive guaranteed employment contracts with their employers and Traffic kulifatilia commanded it.


TUPE MAONI YAKO TUNAOMBA  HAPA CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE!!!.