MAREKANI YARUSHA NDEGE ZA B52 KOREA KUSINI-NI TISHIO KWA KOREA KASKAZINI:
Ndege aina ya B52 ikiwa hewani |
Kabla ya kuruka |
SEOUL-KOREA KUSINI,
Marekani
imerusha ndege zenye uwezo wa kuzuia mabomu ya Nyuklia na kubeba silaha
nzito katika kile ilichoelezea kama itikio kwa vitisho vya Korea ya
Kaskazini ambayo hivi karibuni imetishia kuishambulia.
"Tunaonesha
uwezo kuwa tumepanua uwezo ambo ni muhimu dhidi ya tishio la Korea
Kaskazini" Alisema msemaji wa Pentagon Bw. George Little.
Marekani
imeonekana kutilia maanani tishio la hivi karibuni la Korea Kaskazini,
ambapo hivi karibuni ilipitisha bajeti ya zaidi ya trilioni 1.5
kuboresha mitambo yake ya kutungua makombora makubwa yakiwemo ya Nyuklia
huko iliyopo katika ardhi yake kama kinga dhidi ya shambulizi lolote,
hali ambayo ni changamoto kwa Korea Kusini na Japan ambao pia ni maadui
wa Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment