POLISI WANATUHUMIWA KUMPIGA RISASI MWALIMU HUYU
Mwalimu
mmoja wa Shule ya Sekondari Kitulo wilayani Makete aliyefahamika kwa
jina la Casto Sote Kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa Jeshi
la Polisi, Makete
Mkuu wa polisi wa wilaya ya Makete, SP Peter Kaiza akizungumza na FrancisGodwin blog kuhusu tukio hilo lililotokea katika eneo la benki ya NMB tawi la Makete juzi majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki, na kuamriwa na askari mmoja aitwaye Jose Msukuma, kuvaa kofia.
Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai ya kutokuvaa kofia na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindoni.
Hata hivyo mmoja kati ya askari ambaye jina lake halikufahamika mara moja alisikika akidai kuwa chanzo cha mtu huyo kupigwa risasi ilikuwa akihisiwa kuwa ni jambazi baada ya kufika kwa usafiri wa pikipiki (bodaboda) na kuhisiwa kuwa amefika kwa ajili ya kuora katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya kujihami alimpiga risasi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete, Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao Mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea.
Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.

kwa habari zaidi na picha ingia FrancisGodwin blog
No comments:
Post a Comment