Safari yangu kuelekea mkoani tabora ilikuwa na changamoto
nyingi, Ila kubwa namshukuru Mungu nilifika salama na kurudi salama. Najua kuna
FANS wangu wengi wananipa support haswa katika maombi ya familia yangu. So
najua itakuwa vizuri kama nitashare na nyie jinsi safari yangu nzima
ilivyokuwa.
Nimetumia siku tano so nitakuwa naielezea kwa day after day
ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka naenda mpaka narudi.
Ila wakati naipanga hii safari ili kwenda kumuona mume
wangu, iliniweka katika wakati na maamuzi magumu sana kama fans zangu
mnavyofahamu nina watoto wadogo akiwepo mdogo wa miezi mine 4, Tabora ni mbali sana ni mwendo wa karibia
masaa 14 kutokea Dar Es Salaam watoto ni wadogo nikisafiri nao nikaona nitakuwa
nawatesa, Nikafanya maamuzi magumu mno
ya kuwaacha wanangu kwa wadada wasaidizi wangu wa nyumbani. Hizi ni changamoto
za maisha inapofika wakati mgumu kama huu ulionifikia mimi inabidi ufanye
maamuzi mazito, so nikawaacha wanagu Lincon na Linstone.
Lincon na Mdogo Wake Linston.
DAY1. IJUMAA 28/06/2013
Siku ya Ijumaa tarehe 28/June Tulikutana Ubungo, Tukitumia
usafiri binafsi na tulikuwa watu 5. Tukaanza safari yetu na tunamshukuru Mungu
tulifika salama Mkoani Morogoro, Tukaendelea na safari Ila tukiwa kati ya Morogoro na Dodoma gari
yetu kidogo ikaleta tabu,
hapa ni kati ya Moro na Dom
Baridi ya hapa ilikuwa ni balaa.
hapa baba mkwe akicheki tatizo la gari.
Baada ya dk kadhaa gari ikawa iko poa.
Baada ya gari kuwa poa tukaendelea kwa safari
tukaingia Dodoma, Tukapata chai kidogo
Tukisubiria Chai hapa ni Dodoma.
Baada ya chai tukirudi garini kuendelea na safari.
na gari nayo ikapata lishe/mafuta.
then tukaendelea na safari.
Tulipofika
Ikungi Kabla hatujafika Singida mjini
gari ikaharibika tena , dereva akasema ni tatizo dogo linarekebishika fasta
then tutaendelea na safari.
Tukapata Fundi pale pale Ikungi, hapa akitazama tatizo.
dah ikawa vise versa tatizo likawa kubwa, it was
around saa tisa hivi alasiri tupo Ikungi, mpaka saa 6 usiku gari haikufaa
ikabidi tutafute hotel kulala hapo.
Mida ya saa sita hivi gari ikawa bado haijatengamaa.
DAY2.JUMAMOSI 29/06/2013
Siku ya pili tukaamka na kujiandaa, ila mpaka tunamalizia
kujiandaa gari ilikuwa bado haijatengamaa, ili wote tusiwe tumestuck sehemu
moja tukaamua kugawana wengine wabaki na gari na wengine tutangulie. Kutokea
hapo Ikungi tukapata usafiri wa NOAH mpaka Singida Mjini si Mbali sana ilikuwa
mwendo kama wa dk 20 ama 30 hivi, Tulipofika Singida Mjini tukapata HIACE
ambayo tulianza safari kuelekea Igunga.
hapa ilibidi tufanye safari za kuunga
unga mana usafiri pia ulikuwa wa tabu,
mwendo wa masaa kama mawili na nusu ama
matatu tukawa tumefika Igunga, tukakata tiketi za kuelekea Tabora mjini..
Hapa ni stendi Igunga tukisubiria basi,huyu ni dereva wa Hiace Tuliyokuwa tumepanda.
Usafiri ni wa Tabu mno tukapata basi ila tulikosa siti takasimama ,
it was a
very rough road kutokea hapo Igunga mpaka Tabora mjini na ni mwendo karibu wa
masaa 3 na nusu hivi, Ila Mungu alisadia tukafika salama Tabora mjini mida ya
saa 11 kama na dk 20
Mwenyeji wetu akitusaidia kutuonyesha hoteli.
Kutoka stendi ya mabasi mpaka ilipo hoteli ni mwendo wa dk 2 tu kwa miguu.
na kuanza tafuta hotel. By the way nilitamani sana
nikiingia Tabora nielekee Gerezani Ila nilikuwa nilishachelewa kwa kuuuliza uliza
niliambiwa Kutembelea gerezani mwisho ni saa 9 alasiri.
Uchovu wa safari.
Katika kuulizia ulizia hoteli tukapelekwa Hotel inaitwa
Mwafrika Hotel, Pale Tulikosa nafasi ila meneja wa pale akachukua jukumu la
kututafutia sehemu nyingine , tukapata sehemu nyingine lakini tukapanga next
day wakitoka watu tutarudi pale.
Aliyevaa Jezi ni Meneja Wa Mwafrika Hoteli, Anayenielekeza ni Mmiliki wa Mwafrika Hotel.
Huyu ni shemeji yangu kabisa kabisa, ni
mume wa dada yangu"post ya changamoto na Opportunity" mtamfahamu vyema.
Hapa ndo alituchukua na kutupeleka hotel nyingine kwa usiku huu.
DAY3. JUMAPILI
Tuliamka asubuhi tukajiandaa kuelekea gereza Kuu Uyui, ila
tulipitia Mwafrika hotel kuacha mizigo yetu mana kwa siku hiyo tutakuwa pale.
Then safari ya kuelekea Gereza Kuu la Uyui,
Si mabali
kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5 hivi kwa Gari, tukawa tumefika
gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata kujiandikisha na kila kitu
halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana pia tulikuta watu wengine ambao
nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na
sie tukaitwa katika listi tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria
zao za kuzima simu na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko
kijichumba kidogo tu.
Kiukweli it was a very SAD moment, nilipomuona mume
wangu, akiwa kwa upande wa pili na sikuwa namuona vizuri mana hiyo nyavu
iliyotenganisha hapo ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa Kujizui MACHOZI yalianza
kunitoka, Ila mume wangu alikuwa MORE THAN STRONG akinisihi nisilie ye yuko
poa, Kiukweli Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na mie Napata nguvu. Swali
la Kwanza aliniuliza Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako
salama , Kutokana na umbali wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia Naendelea
Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko Upande Wetu, Misukosuko niliyoipata njiani nawaza
ningekuwa na watoto ingekuwaje”?? .Tukaongea mawili matatu kama dakika tano
hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka. Kuna nguo nilibeba tukaambiwa
zikakaguliwe kwanza then ndo atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka
then tukaondoka.
Kiukweli after
kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia kuwa yuko
mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache sana na nilikuwa
na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale wakatuambia kwa waliotoka mbali
huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at least hata dk kumi, so nikipanga
kurudi tena siku ya Jumatatu.
Jioni Baada ya Kutoka Gerezani,
Nilikutana na Sister Wangu ambaye hatujaonana zaidi ya miaka 20. Kwenye
post ya changamoto na opportunity nae mtamfahamu.
DAY4.JUMATATU
Niliamka asubuhi na kujiandaa, Baada ya kumaliza nikatoka
kwenda kutafuta baadhi ya vitu alivyoniagiza, So nilipokamilisha vyote nikaanza
safari ya kwenda Gereza Kuu Uyui kwa siku nyingine tena, Leo nikiwa
nimeongozana na mwanasheria ambaye yeye
anafanya shughuli zake kule kule kwa ajili ya mambo mawili matatu.
Tukafuata
taratibu zao kama kawaida kuandikisha, na baada ya muda tukapata nafasi
ya kwenda kumuona, Leo Kidogo ikawa nafuu kwa vile tunatoka mbali” ipo
sheria
kabisa kwa mtu mfano anayetoka mbali na Tabora kuwepa nafasi kidogo
zaidi mana
ametokea mbali “. Kama Kawaida ya pale tukatakiwa kuacha kila kitu na
siimu
kuzizima, tulichoruhusiwa kupita nacho leo hii ilikuwa ni pesa tu,
Nikiwa na mwanasheria.
Tukapelekwa
katika chumba cha wazi ni pa kuonea wafunga tulikuwa chini ya ulinzi mkali wa uangalizi wa askari
si chini ya 7, akiwepo askari mmoja wa kike , na masharti makubwa mawili hakuna
kulia na hakuna kuongea kwa kunong’ona “WHISPER”. Dah kweli ilikuwa ni wakati
mgumu hali ambayo nilikuwa naisikia uchungu then napewa masharti hakuna kulia,
Ila narudia kusema Mungu hawezi Kuniacha , Nilipata Ujasiri wa ajabu na kuacha
kulia na kuanza kuongea mawili matatu kuhusu familia na kuhusu maswala ya kazi,
Ila pia napo kama after dakika kumi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka
. Tukatoka na kurudi zetu hotelini. Usafiri wa Tabora kwa sasa ni tabu tukakosa
usafiri wa kurudi Dar kwa siku ya Jumanne.
Hapa Nikiagana na Mwanasheria.
DAY5.JUMANNE
Baada ya kukosa usafiri wa kurudi Dar Siku ya Jumanne,
nikitazama Tabora ni mbali nikasema ngoja niende Gerezani kuomba hata dakika
moja ya kumuaga mume wangu, nikaelekea gerezani Uyui, Ila dah nikaomba sana
wanilikatalia, nikaamua kurudi zangu kiunyonge hotelini, kuja kusubiria
Jumatano kusafiri kurudi zangu Dar.
DAY6.JUMATANO
Nikaanza safari ya kurudi dar, Tuliondoka Tabora saa 12
asubuhi, After Masaa Mengi njiani by saa 2 na nusu hivi nikafika salama Dar,
nilikuwa So excited kuwaona wanangu, Thanx God Nilifika salama na niliwakuta
wanangu wako salama.
NYONGEZA
Jumatatu tarehe 8/Julai/2013, mume wangu anapandishwa tena
mahakamani huko Tabora, Bado nahitaji msaada wenu katika kunisaidia maombi.
No comments:
Post a Comment