Kushoto ni Afisa
Mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Donald Mng'ong'o Katikati ni
Mwenyekiti wa Mtaa Kambarage Bwana Pancras Matinya na Kulia ni Afisa
Mtendaji wa Mtaa Huo Bi.Telesina Manga wakitolea Maelezo hayo mara baada
ya Maaafisa wa
Polisi Kufika katika Eneo Hilo leo Kushuhudia Tukio Hilo.
Wapenzi
waliosababisha Hofu kubwa kwa Wakazi wa Kambarage Mjini Njombe baada ya
Kupaki Gari lao Kwenye Nyumba ya Mtu walipo Lewa Pombe na Kisha Kulala
kwenye Binti Huyo hali iliyopelekea Serikali ya Mtaa Kulazimika Kufungua
Tairi za Nyuma Ili kumpata Mhusika ambaye amejitokeza Asubuhi ya Leo.
Binti aliyevalia Kofia ya CHADEMA Ndiye aliye Lala na Jamaa Huyo Chumbani Kwake hadi hali hiyo Kujitokeza.
Benedict akitoa
Namba yake kwa Askari Polisi kwa Mawasiliano baada ya Kukamilisha
Taratibu za Ofisi ya Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe.
Chumba cha Kwanza
ndiko Jamaa Huyo alipo Lala na Mpenzi wake baada ya Kufanya Maegesho
kya Gari Lake Kwenye Nyumba ya Jirani yake Usiku Mzima na Kisha Wananchi
Kutoa Matairi.
Binti wa
Mtuhumiwa aliyepaki gari kwenye Nyumba ya Bwana Lupenza Kambarage
Bi.Lamar ambaye ni Mpenzi Wake akielekea Nyumbani Waliko Lala wakati
Wananchi wakihangaika Usiku Mzima na Serikali Kumtafuta Mwenye Gari
Hilo.
Katika Hali Isiyo ya Kawaida Wananchi
wa Mtaa wa Kambarage wamejikuta Wakiingiwa na Hofu Kubwa kutokana na
Mtu Mmoja anaye Fahamika kwa Jina la Ben Matimbwi Mkazi wa Njombe
kuegesha Gari Lake Kwenye Nyumba ya Bwana Lupenza Usiku wa Kuamkia Leo
Bila Taarifa na Kisha kwenda Kulala kwa Mpenzi wake.
Kutokana na Matukio ya Mara kwa Mara
yanayojitokeza katika Mtaa Huo Wananchi Hao Pamoja na Uongozi wa
Serikali Ya Mtaa Huo walilazimika Kufungua Matairi ya NYUMA ya Gari Hilo
baada ya Mwenye Gari kutopatikana Wakidhani Huenda Gari Hilo hutumika
kwenye Matukio.
Pancras Matinya ni Mwenyekiti wa Mtaa
wa Kambarage ambaye amesema Licha ya wao Kuripoti Polisi kutokana na
Tukio Hilo lakini Mmiliki wa Gari Hilo anatakiwa Kulipa Faini ya
USUMBUFU Kwa Wakazi wa eneo Hilo na Uongozi Serikali kwani Usiku huo
wamepata Shida ya Kumtafuta Bwana Matimbwi Bila Mafanikio akiwa Amelala
na Mpenzi Wake.
Mtandao huu wa
www.gabrielkilamlya.blogspot.com ulizungumza na Binti Huyo anayefahamika
kwa Jina la Lamar Nuru ambaye amesema kuwa Tatizo Lililopelekea
kujitokeza kwa Tatizo hilo ni Kutokana na Mpenzi wake bwana Matimbwi
kunywa Pombe na Kulewa kisha Kuegesha Gari lake kwenye Nyumba ya Mtu
Jirani na walipo lala.
Kwa Upande wake Bwana Benedict
Matimbwi ambaye ni Mmiliki wa Gari Hilo amekiri kuwa Alikwenda Kunywa
Pombe katika Mtaa Huo mara Baada ya Kulewa sana Alishindwa Kurudi
Nyumbani Kwake na Kisha Kulazimika Kulala na Mpenzi Wake Huyo.
Bwana Matimbwi Ameongeza Kuwa Asubuhi
wakati Akiamka kwa Mpenzi wake ndipo alipo kuta Gari lake limetolewa
Tairi zote za nyuma ndipo alipo lazimika kuanza Kuulizia na kupata
taarifa hizo na kisha kuwasiliana na Ofisi ya Serikali ambao akaambiwa
asubiri Jeshi la Polisi lifike kwani wameshatoa taarifa Huko.
No comments:
Post a Comment