Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy
Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa
ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu
baada ya kumaliza tour nyingine baran ulaya.
"yaah nimesaini mkataba na nitaondoka
kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo
kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni
niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania
ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz
nilipomuuliza kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema
"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa? .
No comments:
Post a Comment