Vurugu kubwa zilizotokea Bungeni
muda huu ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya
upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa
kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
****
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni
hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa
kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani
hawakukubaliana na amri hiyo.
Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo
ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo
kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge
lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge
56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee
kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.
Mara baada ya zoezi la
upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge
ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe
naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari
wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada
ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi.
BONYEZA HAPA KWA VIDEO
No comments:
Post a Comment