WILAYA YA ILEJE - AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA KUSABABISHA
KIFO NA MAJERUHI.
MNAMO
TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI
CHA NDOLA WILAYA YA ILEJE MKOA WA MBEYA. GARI STK 5485 AINA YA TOYOTA
HILUX MALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEJE IDARA YA
UJENZI LIKITOKEA KIJIJI CHA ITALE KUELEKEA ITUMBA LIKIENDESHWA NA
DEREVA VICENT S/O SCOT, MIAKA 35, MUHA, MKAZI WA ITUMBA LILIMGONGA
MPANDA PIKIPIKI YENYE NAMBA T. 367 BTB AINA YA T-BETTER
AITWAE CHONDE S/O MWASIMIAKA 32, MNDALI, MKAZI WA ITUMBA NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE WAKATI ANAPELEKWA HOSPITALI KWA MATIBABU PIA MAJERUHI KWA
ABIRIA WAKE WAWILI MAJINA YAO BADO KUFAHAMIKA AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI
YA RUFAA MBEYA. CHANZO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU
ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBOZI - AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI
CHA SELEWA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA MBOZI MKOA WA
MBEYA. GARI T. 598 BTK AINA YA FUSO TIPPER LIKIENDESHWA NA
DEREVA JAPHET S/O MWASHIUYA, MIAKA 21, MNYIHA, MKAZI WA ILEMBA - VWAWA
LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA BAADA YA GURUDUMU LA MBELE UPANDE WA KUSHOTO
KUPASUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MATOKEO S/O STEVEN MWASHIUYA MIAKA
27, MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA ISANGU PIA KUSABABISHA MAJERUHI KWA ABIRIA
WAKE WATANO AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI WILAYA YA MBOZI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. DEREVA ALIKIMBIA MARA
BAADA YA TUKIO, GARI LIPO ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIOA SHERIA
ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.AIDHA
ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA
GARI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO
TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA ENEO LA MAKUNGURU
JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA GREGORY
S/O JOHN, MIAKA 20, KYUSA, MKAZI WA MAKUNGURU AKIWA NA BHANGI UZITO WA
KILO 2. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE KIBANDA CHAKE CHA
BIASHARA. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA
ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA
KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
TAREHE 19.09.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MTANILA
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA STAFORD S/O SOMBAMIAKA 26, MNDALI, MKULIMA, MKAZI
WA MTANILA AKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 1. MBINU NI KUFICHA BHANGI
HIYO NDANI YA NYUMBA YAKE. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI.
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
No comments:
Post a Comment