Saturday, November 29, 2014

MHE.WASIRA AFUNGUKA NA KUSEMA TANZANIA HAKUNA NCHI

WASIRA AFUNGUKA YAKE ASEMA HADI WATU KUBEBA FEDHA KWENYE LUMBESA HAKUNA NCHI HAPA!



CAG sio mara ya kwanza kuchunguza na kuleta taarifa bungeni, na PAC nao hii ni kazi yao kuchunguza na kuleta Bungeni. Jambo la pili ni wajibu sasa wa Bunge hili kutazama ripoti hizi na kuzifanyia kazi. Kama kuna mtu anataka kuwa Rais na mbinu zake ni kuondoa wengine huyo hafai kabisa kuwa Rais wa Tanzania

Sisi bunge hili lazima tunangalie maslahi ya Watanzania, hatuwezi kutumiwa na mtu. Afadhali kuwa maskini mwenye heshima kuliko tajiri anayetukanwa. Tutakuwa Bunge la ajabu kama maneno haya yameandikwa na vyombo hivi vya Bunge halafu sisi tukalifumbia macho.



Nchi ambayo unaenda na sandarusi, mabox kubeba hela, hapa hatuna nchi, inabidi TAKUKURU watutajie ni kina nani hawa TAKUKURU iwachambue watu wote bila kujali vyama au nini ili tuwapeleke kwenye sheria.

Mwandosya naye amesema Suala hili linatuondolea sifa kama nchi, linatuondolea heshima kama taifa, kimataifa na mbele za wananchi.

Bonyeza hapa kusikiliza escrow-yazua-sura-mpya-bungeni

Friday, November 21, 2014

MGOMO WA WANAJESHI WA IVORY COAST WAPATIWA DAWA

Waziri wa mambo ya ndani wa Ivory Coast, Hamad Bakayoko ameahidi kuwa Serikali itashughulikia madai ya maelfu ya Wanajeshi walioandamana. Ametoa ahadi hiyo kwa njia ya Televisheni usiku wa jumanne baada ya Wanajeshi kufunga Barabara katika miji muhimu miwili.


Bayoko amesema Wanajeshi hawatawekewa vikwazo vyovyote kutokana na kuandamana kwao. Madai ni ya wanajeshi takriban 9,000 waliokuwa wapiganaji waasi ambao baadae walijiunga na Jeshi.
Wapiganaji hao walikua sehemu ya kikosi kinachomtii Rais Alassane Ouattara aliyechukua madaraka mwaka 2011, na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mapema siku ya jumanne,Waziri wa ulinzi Paul Koffi aliwataka Wanajeshi kurejea kambini baada ya kufunga barabara za mji wa Abidjan na Bouake.
Taarifa za jumatano zinasema Wanajeshi tayari wameondoka mjini Bouake. Haya ni maandamano makubwa kuhusisha jeshi tangu Rais Alassane Ouattara kuchukua madaraka Mji wa Bouake ni ngome ya Rais wa nchi hiyo.
Kutoka Mutalemwa Blog.

Tuesday, November 18, 2014

UTAFITI WA WABUNGE WATAKAO RUDI MAJIMBONI NA ASILIMIA ZAO.

Huu ni utaft uliofanywa na shirika linaonyesha alama za wabunge kama wanaoweza kurd bungeni 2015, porojo hazruhusiwi njoo na utafti wako na ushaidi wa utafi uliofanya
1. Ngereja (60%) - sengerema
2.Dr Tizeba (80%) - Buchosa
3.Ndasa (95%) -Sunve
4.Dr Kitwanga(50%)- Misingwi 
5.Wenje (70%)- Nyamagana
6.Kiwia (50%) - Ilemela 
7.Machemli (50%)- Ukerewe 
8.Max (15%)- Geita 
9.Bukwimba(50%) - Busanda 
10.Lembeli (99.5%)-kahama
11.Dr Maige (75)- Msalala 
12.Kigwangalla (40%)- Nzega 
13.Masele (45%)- Shinyanga mjini
14.Nchambi (90%) - kishapu
15.Dr kafumu (60%)-Igunga
16.Nchemba (90%)-Iramba Magharibi 
17.Opulukwa (80%)- Meatu 
18.Mpina (65%)- Kisesa 
19.Chenge(80%)- Bariadi magharib
20.Cheyo (50%)- Bariadi masharki
21.Dr kamani (85%)- Busega
22.Lugola (90%)- Mwibara
23 Nyambari (50)- Tarime
24.Wasira (60%)- Bunda 
24.Nyerere (100%)-Musoma mjini
25.Mkono (100%)- Musoma vijijin
26.Shibuda (75%)- Maswa magharibi
27.Kasulumbayi (80%)-Maswa mashariki
28.Lisu (80%)-Singida mashariki
29.Nyalandu (98%)-Singida kaskazin
30.Dewji (100%)-singida mjini
31.Ndugai(100%)-kongwa
32.Nkamia(90%)-kondoa kusin
33.Dr Malole (50%)- Dodoma mjin
34.Lusinde(80%)- Mtera 
35.Lukuvi (92%)- Isman
36.G. Mgimwa (75%)- kalenga
37.Msigwa (65%) - Iringa Mjini 
38.prof Msola (89%)- Kilolo 
39.Dr Mahenge (100%)-Makete
40.Mbilinyi (82%)- Mbeya Mjini 
41.Silinde (75%)-Mbozi magharibi
42.Kibona( 56%)- Ileje 
43.Zambi (75%)- Mbozi mashariki
44.Dr Makyembe (100%)- kyela 
45.Mwanjale (50%)- Mbeya vijijin
46.Dr Nchimbi (50%)- Songea Mjin 
47.Kawawa V(100%)- Namtumbo
48.Kilufi (96%)- Mbalali 
49.prof Mwakyusa (100%)- Rungwe Mashariki 
50.Prof Mwandosya (100%)- Rungwe magharbi
51.Prof kahigi(80)- Ushirombo 
52. Dr Magufuli (100%)- Chato 
53.Dr Mbasa (75%)- Biharamulo Magharibi 
54.Rage(100%)- Tabora Mjini 
55.Nkumba (90%)- Sikonge 
56.kafulila (100%)- Kigoma kusini
57.Mkosamali (91%)- Muhambwe
58.Machali (85%) - Kasulu Mjini 
59.Kabwe(60%)- Kigoma kaskazin
60.Lema (100%)- Arusha Mjin 
61.Natse (99%)- karatu
62.Nasari (67%)- Arumaru masharki
63.Selasini (56%)- Rombo 
64.Akunayi (60%)- Mburu 
65.Sendeka (80%)- Simanjiro 
66.Pro Maghembe (89%)- Mwanga 
67.Mbowe (100%) - Hai
68.Ndesamburo (100%) - Moshi Mjini 
69.Mrema (40%)- Vunjo 
70.Dr Chami (50%) - Moshi vijijin
71.Mwanry (100%) - Siha 
72.Kilango (65%)- Same masharki
73.Dr Mathayo (100%)-same mashariki
74.JItu (100%)- Babati mjini
75.Dr Nagu(100%)- Hanang'i
76. Lowasa (Ubunge/Urais) -Monduli 
77. Terere (100%)- Ngorongoro 
78.Prof Tibaijuka (100%)- Muleba kusini
79.Ntukamazina(50%)- Ngara 
80.Obama(50%)- Manyovu 
81.Serukamba (60%)- kigoma Mjini 
82.Aishi (40%)-Sumbawanga mjini
83.Afri (50%)- Mpanga mjini
84. Kessy (100%)- Nkasi kaskazin
85.Prof Kapuya (42%)- Urambo magharibi
86.Sita (50%)- Urambo mashariki
87.Kombani (67%)- Ulanga Mashariki 
88.Dr Mponda (50%)- Ulanga magharibi
89.Mkuro(100%)- Kilosa 
90.Aboud (100%)- Morogoro Mjini 
91.Makala (50%)- Mnvomero
92.Shabib (100%)- Gairo 
93.Mnyika (89%)- Ubungo 
94.Mdee (89%)- kawe
95.Dr Mahanga (43%)- Segerea 
96.Mwaiposa (42%)-
97.Dr Ndugulile (90%)- kigamboni
98.Zungu (100%)- kinondoni
99.Zungu (100%)- Ilala 
100.Mtenvu (60%)- Temeke 
101.Kawambwa (100%)-Bagamoyo 
102.Rithiwan (100%)- Chalinze
103.Dr Rashidi (100%)- Rufiji
104. Koka (50%) -kibaha
105. January (100%)-Bumbuli
106.Nundu (100%)- Tanga Mjini 
107.Airo (40%)- Rolya
108.Chiligati (100%)
109.Membe(Ubunge/Urais)-Mtama
110.Pinda (Ubunge/Urais)- Katavi
111. Komba (50%)- Mbinga magharibi
112.Mhagama(78%)- Peramiho 
113.Mahamud (100%)- Mufind kaskazin
114.Kigola (100%)-Mufind kusin
115.Mtanda(100%)- Mchinga.
Ukiona mbunge wako hayupo unaweza kuongeza na ukampa asilimia yako huu ni utafit wa shirika lisilo la kiserkali la HATUWEZI

Thursday, November 13, 2014

Mh Mbowe na mwenyekiti wa chadema Taifa amemuelezea Mh Zitto Zuberi Kabwe hadi kukua kwake na usaliti wake katika chama

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe,
amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuijua
historia ya mageuzi ya Mkoa huo ili kuepuka
kuwalaumu viongozi wanaosimamia vyama hivyo
pindi wanapochukua maamuzi magumu.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishabikia
na kuwahukumu viongozi hao bila kuangalia
chimbuko la vyama hivyo, vilikotoka na hatimaye
kufikia hatua vilipo sasa hususan katika mkoa huo
ambao umekuwa chimbuko la mabadiliko.
Akijibu swali lililoulizwa na mtu ambaye
alijitambulisha kwa jina la Cheche wa Cheche,
katika mkutano wa hadhara wa ‘Oparesheni Delete
CCM’, uliofanyika kwenye kijiji cha Mnanila
Manyovu mkoani hapa jana, Mbowe alisema Mkoa
wa Kigoma ulizalisha viongozi wengi maarufu
katika mageuzi.
Alisema utumishi ndani ya chama hicho haupimwi
kutokana na mtu kutoka mkoa gani, bali hupimwa
kutokana na ujasiri, uwezo wa mtu na kamwe
kiongozi makini hawezi kumpiga vita mtu kwa
sababu ya kabila au dini yake.
Akitoa mfano wa viongozi waliotegemewa na
wanachi wa mkoa huo katika kuendeleza mageuzi,
Mbowe, alisema Daniel Nsanzugwanko, Aman
Kabourou na Zitto Kabwe walionyesha umahiri wao
katika kuongoza vyama vya siasa enzi zao kabla
ya kurubuniwa na kuvisaliti.
Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa
zikielekezwa kwake na chama anachokiongoza,
hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe
alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia kwa kuwa
ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa
akiwa kijana mdogo.
Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe
ukweli wake. Mimi ndiye nilimwingiza Zitto katika
siasa akiwa kijana madogo, nilimwita akitokea
masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri
akagombee ubunge katika jimbo la Kigoma
Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka
sasa hajalirudisha,” alifafanua.
Alisema Zitto ndiye aliyetia mchanga kitumbua
chake kwa kusaliti chama kutokana na kukubali
kurubuniwa na viongozi wa CCM, jambo ambalo
lisingelivumiliwa ndani na nje ya chama.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliofurika
katika Uwanja wa Community Centre mjni Kigoma,
Mbowe alisema kuwa, atahakikisha anakilinda
chama hicho kwa gharama yoyote bila kumwonea
mtu ili kukijengea imani kwa watanzania.
Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge
wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Dk. Aman
Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana
mwanzilishi wa chama hicho, alishiriki kikamilifu
kumpigania Dk. Kabourou kumleta nchini na
hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika
uchaguzi mdogo.
“Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki
chama kilianza vipi katika mkoa huu. Mimi
nilishiriki kikamilifi kumwezesha Dk. Kabourou
kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli
ya kumleta kutoka Uingereza alikokuwa akiishi,
yeye na mkewe na pia nikampa pesa kumwezesha
kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe,”
aliongeza.
Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanafikiri
kuwa anampiga vita Zitto, jambo ambalo si kweli
kwa kuwa amemlea, amekula na kulala nyumbani
kwake kabla hajakua kiuchumi.
Jana, Mbowe alifanya ziara yake katika jimbo la
Manyovu, Kigoma mjini katika uwanja wa
Community Centre Mwanga, Munawila na
Mahembe ambako aliendelea kuwasisitiza
wananchi kuwapa dola upinzani kwa kuanzia
uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wednesday, November 12, 2014

UTAFITI: Lowassa na Dk Slaa waongoza kura za maoni za kuwa rais 2015, Nape Nnauye ashikwa na kigugumizi.

 
KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad
Slaa na Waziri mkuu aliyejiuzuru na Mbunge
wa Monduli Edward lowassa wameibuka
kuwa wanasiasa wanapendwa zaidi nchini.
Na pia wanasiasa hao wametajwa
kupewa nafasi kubwa ya kumruthi Rais
anayemaliza mdawake, Jakaya Kikwete
kwenye uchaguzi Mkuu mwakani 2015.
Hayo yamegundulika leo Jijini Dar Es
Salaam, wakati wa uzinduzi wa Utafiti
uliofanywa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali
la TWAWEZA ambapo utafiti huo ulifanyika
kwa lengo la kuwapa sauti watanzania
kuelekea uchaguzi mkuu na kuwahoji
watanzania kuhusu hali ya kisiasa nchini
pamoja na mambo mbalimbali
yanawazunguka,uzinduzi huo ulishuhudiwa
na watu mbalimbali wakimemo wanasiasa
na waandishi wa habari,
Ambapo Akisoma Utafiti huo, Ervis
Mushi,ambaye ndio amesimamia suala hilo
amesema utafiti huo ulianza mwaka 2012
na kumalizika mwezi Agosti mwaka huu na
kusema kuwa katika utafiti huo wamewahoji
watu Elfu 1500,na wametumia njia
mbalimbali kukusanya maoni ya utafiti huo
ikiwemo nia ya simu na kuwafuata
wananchi walipo.
Bwana Mushi alisema kwaanzia mwaka
2012 waliwahoji watanzania katika utafiti
huo kama endapo uchaguzi mkuu
ungefanyika mwaka huo nani angefaa
kumrithi Rais anayemaliza mda wake
Jakaya Kikwete ambapo utafiti ulikuwa hivi
Dk Wilbroad Slaa alipata asilimia 19%
Mizengo panda alipata asilimia 16%
Edward Lowassa alipata  asilimia 6%
Profesa Ibrahimu lipumba alipata 3%
Nawasiojua nani watamchagua walikuwa
asilimia 22%
Bwana Mushi alisema mwaka 2013
walifanya utafiti bado Katibu huyo wa
Chadema alizindi kuongoza akiwaacha
wanasiasa kutoka vyama vingine nchini
ambapo mambo yalikuwa hivi
Dk Wilbroad Slaa alipata asilimia 19%
Edward Lowassa alipata  asilimia 13%
Mizengo pinda alipata asilimia 12%
Profesa Ibrahimu lipumba alipata 6%
Nawasiojua nani watamchagua walikuwa
21%
Mwaka 2014
Edward Lowassa alipata asilimia 13%
Dk Wilbroad Slaa alipata 13%
Mizengo pinda alipata 12%
Profesa ibrahimu lipumba alipata 6%
Freeman Mbowe alipata 3%
Nawasiojua nani watamchagua nan
walikuwa asilimia 33%
Kwa upande wa Mgombea ambaye
anakubalika ndani ya chama cha mapinduzi
CCM ambaye amepata alama nyingi ili
kuweze kumrithi Rais anayemaliza mda
wake Profesa Jakaya Kikwete,imeonekana
Edward Lowassa akichuana vikali na Waziri
mkuu Mizengo Pinda
Edward lowassa amepata 17%
Mizengo pinda amepata 14%
John Magufuli amepata 5%
Samwel Sitta amepata 5%
Wasiokuwa na upande ni 18%
Nao umoja wa Vyama vikuu vya upinzania
vinavyounda umoja wa UKAWA ambavyo
vimeungana,kuhusu wakati wa
kumsiamisha mgombea mmoja
kugombania Urais imeoneka bado Dk
Wilbroad Slaa ni kinara
Dokta Wilbroad Slaa amepata 44%
Profesa Ibrahim lipumba amepata 14%
Freemana Mbowe amepata 11%
Zitto Kabwe amepata 6%
Kuhusu chama cha siasa kinachopendwa
zaidi nchini hiko hivi
Mwaka 2012
Chama cha Mpinduzi CCM-65%
Chadema alipata 26%
CUF ilipata 3%
NCCR Mageuzi 0%
Mwaka 2013
Chama cha Mpinduzi CCM-54%
Chadema alipata 32%
CUF ilipata 4%
NCCR Mageuzi 1%
Wasiokuwa na chama 8%
Mwaka 2014
Chama cha Mpinduzi CCM-54%
Chadema alipata27 %
CUF ilipata 4%
NCCR Mageuzi 1%
Wasiokuwa na chama 10%
Akizungumzia Utafiti huo Profesa Benson
Bana kutoka chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
aliwapongeza Twaweza kwa utafiti huo na
kusema ni wakati wa wanasiasa kutafakali
kwa umakini kuhusu utafiti huo na
kuchukau maauzi ya mazuri katika kuvijenga
vyama vyao.
Na kuongeza kuwa utafiti bado unaonyesha
sana haiba ya mgombea binafsi
Katika hali ya kushangaza Katibu wa Itikadi
na Uenezi kutoka chama cha Mapinduzi
CCM,Nape Nnauye alionekana kama
kutokubaliana na utafiti wenyewe na
kujiondoa kumzungumzia Edward Lowassa
aliyetajwa sana na kujitita kusema wananchi
wa sasa wanaitaji matatizo yao ya msingi
yatatuliwe na sio wagombea na katiba mpya...

AMPIGIA SIMU RAIS KUMUOMBA MCHANGO WA KUTOA MAITI MOCHWARI

 Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo marais, viongozi wa kidini na wengineo wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma za mitandao ya kijamii na simu za mkononi kuwasiliana na watu.
rais wa kenya, uhuru kenyatta ni moja ya marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia sana mitandao ya kijamii ikiwemo twitter.

Anita (mwenye t-shirt nyeusi) akiwa na familia yake.
huenda usiamini alichokifanya rais uhuru kenyatta, stori ni kwamba baada ya kutumiwa message na anita lipesa ambaye alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za kenya kwa ajili ya kutoa mwili wa dada yake aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia maiti.


anita amesema baada ya jitihada za kuchangisha michango kushindikana aliamua kumtumia ujumbe kwa rais kenyatta ingawa hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30 baada ya kutuma message hiyo kenyatta alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini kama rais angeweza kufanya hivyo
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa mwili wa dada yake huyo na kwenda kufanya mazishi.

MBOWE AUNGANA NA LOWASSA

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amesema serikali haipo makini kutafuta ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana na kutaka suala hilo liwe hoja maalum bungeni, serikali kuu, halmashauri na katika baraza la mawaziri, kwani ni janga la taifa.

Akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha bungeni juzi kuhusu mapendekezo ya Serikali ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2014/15, Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema), alisema ajira ni mkakati na siyo suala la kufumania ambalo linatokea tu na akashauri Rais wa awamu ya tano azingatie suala la ajira kwa vijana.

Akitoa mfano wa vijana 11,000 waliokwenda kufanya udahili wa kupata nafasi 70 za ajira Idara ya Uhamiaji iliyofanyika hivi karibuni Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, alisema tatizo la ajira ni kubwa na hana imani kama serikali ipo makini katika jambo hilo.

“Vijana 11,000 wanawania nafasi 70 za ajira Idara ya Uhamiaji, wabunge hapa tunaliona suala hilo kama mzaha tu, serikali iweke mikakati ya kupata ufumbuzi wa ajira,” alisema.

Alisema suala la ajira limezungumzwa na watu wengi akiwamo kiongozi mmoja mwandamizi sana katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), lakini akaelezwa kwamba anafanya jambo la kuzua.

Ndani ya CCM kiongozi ambaye amekuwa akilizungumzia suala la ajira ni Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Mbowe, alitaka serikali kufanya maamuzi magumu na kutambua kuwa utitiri wa vijana ambao hawana ajira mitaani ni bomu linalosubiri kulipuka. 

Mbowe alisema mfumo uliopo sasa wa kila kitu kurundikwa serikali kuu, kama ndiyo inayofikiri kwa niaba ya Watanzania wote katika kutengeneza ajira hautatatua tatizo hilo, alitaka halmashauri zote 133 ziwe na mkakati wa kutengeneza ajira katika maeneo yao.

“Ajira iwe hoja maalum katika bunge hili, serikalini, baraza la mawaziri … tuweke mkakati wa kitaifa wa kutengeneza ajira.

“Hakuna sababu ya kuwa na wakurugenzi na wataalam wa uchumi katika halmashauri kama hawawezi kutengeneza ajira,” alisema.

“Nitawaelekeza hapa namna ya kupata Sh. bilioni 500 mpaka 800 za mikakati ya kupata ajira. Iwapo miradi ya ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (PPP), kila wilaya ina utaratibu na mazingira yake, lakini moja inaweza kutengeneza ajira 500,000 kwa mwaka,” alisema.

Alishauri serikali kuanzia Mamlaka ya Majengo (Real Estate Authority - REA) ambayo itahusika kusimamia majengo mijini na kukusanya fedha kwa ajili kusaidia kujenga ajira.

Alisema miradi ya PPP katika halmashauri inaweza kupata kiasi hicho cha fedha na kuwapatia vijana ajira na kuwafanya wasikimbilie mijini baada ya kuona vijijini nako kuna maendeleo.

Alisema bila kufanya hivyo, vijana watalazimika kukimbilia mijini kwa sababu vijijini hakuna maendeleo na hakuna mwelekeo.
Alisema ni aibu kwa Halmashauri za Kinondoni na Ilala kutegemea ruzuku toka serikali kuu wakati inavyanzo vingi vya mapato ambavyo vinaweza kusaidia kutengeneza fedha na ajira kwa vijana.

“Mruhusu halmashauri zitengeneze fedha, zikusanye kodi…huu ni ushauri wa bure tu,” alisema.
Baada ya mchango huo, Naibu Spika Job Ndugai, alisema anakubaliana na Mbowe kwamba tatizo la ajira ni kubwa kuanzia kwa wahitimu wa darasa la saba, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.

“Mwaka 2015 ajenda ni ajira. Kama kuna mtu anayetaka kura ajue kuwa ajira ni ajenda.  Kila mtu aliye makini na anayetaka chama chake kiongoze ni lazima azungumzia suala la ajira,” alisema.

Akizungumzia suala la ajira nje ya bunge jana, Lowassa, alisema ajira ni bomu ambalo linaanza kupasuka.

Alisema serikali yoyote iliyopo madarakani inapaswa kuzingatia au kutengeneza ajira kwa vijana.

Alisema idadi ya Watanzania ni milioni 48 na kila mwaka wahitimu wa vyuo vikuu wanafikia zaidi ya 40,000, lakini hakuna ajira.

“Lazima serikali ifanye mikakati ya kutengeneza ajira…suala la ajira ni bomu litakalopasuka wakati wowote,” alisema.

Alisema kwa mfano, ujenzi wa kiwanda chochote kile kama kiwanda cha pamba ni lazima uangalie ni kiasi gani cha ajira kiwanda hicho kitazalisha.

Akitoa mfano wa Rais Barak Obama wa Marekani, alisema aliweza kuchaguliwa kuingia Ikulu kwa awamu ya pili kutokana na kutengeneza ajira.


Alisisitiza kwamba ni lazima serikali itengeneze ajira kwa vijana wake.
Mbunge wa Viti Maalum, Sarah Msafiri, aliwataka wabunge na serikali kujiuliza kuhusu tatizo la ajira.
“Lazima tuwe na mkakati wa kitaifa wa kuwasaidia vijana. Zaidi ya vijana 40,000 wanahitimu vyuo vikuu kila mwaka, hivyo, ni lazima wasaidiwe,” alisema.

PAYE KILIO
Baadhi ya wabunge wamelalamikia wafanyakazi kukatwa kodi kubwa kwenye mishahara (PAYE) na kupunguziwa kwa asilimia moja katika bajeti ya mwaka 2014/15 na kwamba kufanya hivyo ni kuwaongezea ushawishi wa kufikiria njia nyingine za kupata fedha.

HAJI
Mbunge wa Konde, Khatib Saidi Haji (CUF), alisema punguzo la asilimia moja kutoka kwenye mshahara wa wafanyakazi ni sawa na kutomfanyia lolote. Alisema kada ya wafanyakazi ndiyo pekee inayolipa kodi kwa asilimia 100 kwa sababu hawana pa kujificha. 

Alisema pamoja na wafanyakazi kupeleka malalamiko yao kwa Muungano wa Vyama Huru vya Wafanyakazi (Tucta) angalau kodi  ishuke hadi asilimia 11, lakini busara imeonyesha ipungue kwa asilimia moja tu.

“Serikali iangalie wafanyakazi wapo katika hali ngumu sana na vishawisi vinaongezeka siku hadi siku. Mambo haya ya kodi kubwa yanawafanya wafikirie njia nyingine za kupata pesa,” alisema.


MATIKO
Esther Matiko (Viti Maalum, Chadema), alisema kodi ya wafanyakazi ndiyo sekta yenye uhakika ya kulipa kodi. Alipendekeza kuwa  angalau wafanyakazi wenye mishahara inayowawezesha kupata Sh. milioni nne kwa mwaka waanze kukatwa asilimia tisa ya kodi.

Aidha, wanaopekea Sh. 330,000 mpaka Sh. 700,000 kwa mwezi waanze kukatwa kodi kwa asilimia tisa ili kutoa unafuu katika kodi zao.

CHILOLO
Kwa upande wake Diana Chilolo (Viti Maalum, CCM), alisema  mfanyakazi kupunguziwa asilimia moja kwenye mshahara wake, haimsaidii kwani  akienda benki kukopa anakatwa, atakimbilia wapi matokeo yake ni kumuumiza.

“Mshahara unakatwa kodi, atabaki na nini, angalieni suala hili upya waondoleeni wafanyakazi kodi,” alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

MTOTO WA RAIS KIKWETE AKANUSHA KUMILIKI KAMUNI YA SIMBA TRUST

Mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Miraji Kikwete usiku wa Nov 11 2014 ameeleza kuhusu ishu inayosambazwa kwamba anamiliki kampuni ya Simba Trust iliyopo Australia akishirikiana na dada yake.Kufuatia tuhuma hizo Miraji alipost maandishi akikanusha hiyo ishu akisisitiza kwa eleweke hivi ningekuwa napokea milioni 100 kwa siku wallahi ningeshukuru kwa mola ila siwezi kuchukua fedha kinyume na haki ninayo stahili’
‘Katika jambo lililonishangaza ni hizi tuhuma za kuwa ninamiliki kampuni ya Simba trust ya Australia mimi na dada yangu Salama, naona sasas mmeishiwa hoja na kuanza kuzusha mambo, sijawahi kufika Australia na sina kampuni ninayomiliki na dada yangu, lakushangaza kwanini PAP wanilipe pesa bila sababu maalum’
‘Sina pesa nyingi kiasi hicho, kidogo ninachokipata ni kwa jasho langu, sijawahi na sitodiriki kupokea pesa ambazo si haki yangu kupata, acheni kupandikiza chuki zisizo na ukweli wowote, atakaethibitisha basi na aonyeshe hilo kwa vielelezo na ushahidi, chuki hazijengi, kweli umeishiwa hoja na mambo ya msingi ya kujadili’

Tuesday, November 11, 2014

HII NDIO ILIKUWA SAFARI YA MWISHO YA AMIGOLAS 'TANGULIA KAKA TUPO NYUMA YAKO'

Mwili wa marehemu, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ ukiwasili nyumbani kwao Mburahati leo jijini Dar es Salam.
Mjane wa marehemu, Bi Modesta Emmanuel akiwa amezimia msibani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere 'Steve Nyerere' akiwasili msibani.
Mkurugegenzi wa ASET, Asha Baraka akiwa msibani.
Wanenguaji wa Twanga Pepeta wakilia msibani.
Mwili wa marehemu, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ ukibebwa na waombolezaji kuelekea katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Filamu nchini, Jacob Steven 'JB' (wa pili kutoka kulia) akielekea makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Waombolezaji wengine wakijiandaa kuelekea katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa dini ya Kiisilam wakiomba dua mara baada ya kuzika marehemu Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ kwenye makaburi ya Kisutu Jijini Dar jioni hii.
Hili ndilo kaburi alimozikwa Marehemu Khamis Kayumbu ‘Amigolas’.
MAZIKO ya mwanamuziki wa zamani wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ aliyefariki juzi  amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na mamia ya watu.