Leo tarehe 08.11.2014
Wahitim 1,808 wa chuo cha uhasibu Tanzania tawi la Mwanza na Singida wagomea mahafali kwa muda baada ya kuambiwa hawatapiga picha na kushikana mkono na Mwigulu Nchemba.
Katika hali isiyo ya kawaida Mwigulu Nchemba alilazimika kupiga picha na wahitimu 1,808 wa uhasibu tawi la Mwanza na tawi la Singida baada ya wahitimu hao kuwagomea utawala waliosema kwa ajili ya wingi wa wahitimu hao na muda watasimama kwa makundi na kutunukiwa stashahada zao na ndg Mwigulu aliyekuwa mgeni rasmi.
Kwa mshangao wa utawala wa chuo hicho wahitimu hao walisema wako radhi kushinda juani na wako radhi kukesha ili wapate fursa ya kila mmoja kumshika mkono ndg Mwigulu Nchemba huku wakiimba kwa umoja wao "Tunaimani na Mwigulu, tunaimani na Mwigulu".
Wahitimu hao walifika mbali na kusema " tumepata bahati, amekuja mtetezi wetu, mtetezi wa watoto wa masikini, mtetezi wa wanyonge wa Tanzania. Bila Mwigulu watoto wa masikini nani angewakumbuka ili wapate mikopo ya elimu ya juu, nani angewakemea matajiri walipe kodi, nani angetukumbuka sisi watoto wa masikini kuwa bila mikopo ndoto ya shule ndio basi.
Wahitimu hao walitoa mpya waliopotamka kwa kurudiarudia " tuacheni tupige picha na Rais wetu wa Tanzania 2015, huku umati ukishangilia Rais,Rais,Rais, Rais.
Katika hatua nyingine mjumbe wa Bodi ya ushauri wa chuo hicho Prof Kamuzora aliungana na wahitimu hao kwa kusema, Mwigulu ni jembe, ni role model wa vijana wote wa Tanzania, tunajivunia uwepo wako. Nawaunga mkono vijana, Taifa linakutegemea, kipaji chako kimeibuka muda mfupi lakini Mungu anataka akutumie katika nafasi ya juu katika Taifa hili, hapo ulipo bado hujafikia kusudi la Mungu. Vijana jitahidini msiipoteze lulu hii nanyi fuateni nyayo za role model wenu. Tunakutakia Kila la kheri Ndg Mwigulu Nchemba kwa ustawi wa nchi yetu ya Tanzania."
Mbali na hatua hiyo ya kuungwa mkono na watumishi wa Chuo,Mh.Mwigulu Nchemba pia alipata nafasi ya kufungua jengo la kisasa la mihadhara lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja chuoni hapo Singida.
Wakati wa Ufunguzi wa jengo hilo Mwigulu Nchemba alisisitiza Usimamizi Mzuri wa mali ya Umma huku akitoa angalizo kuwa itakuwa ni fedheha endapo jengo hilo likadumu kwa mwaka mmoja tu na kuanza kuonesha hitirafu.
Mwisho,Wanafunzi waliokuwa wanahitimu kutoka tawi la Mwanza na Singida walikumbushwa kuwa waadilifu wakati w usimamizi wa fedha za umma na taasisi binafsi.

CHANZO JULIETH MTAYOBA.
No comments:
Post a Comment