MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe,
amewataka wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuijua
historia ya mageuzi ya Mkoa huo ili kuepuka
kuwalaumu viongozi wanaosimamia vyama hivyo
pindi wanapochukua maamuzi magumu.
Alisema wananchi wengi wamekuwa wakishabikia
na kuwahukumu viongozi hao bila kuangalia
chimbuko la vyama hivyo, vilikotoka na hatimaye
kufikia hatua vilipo sasa hususan katika mkoa huo
ambao umekuwa chimbuko la mabadiliko.
Akijibu swali lililoulizwa na mtu ambaye
alijitambulisha kwa jina la Cheche wa Cheche,
katika mkutano wa hadhara wa ‘Oparesheni Delete
CCM’, uliofanyika kwenye kijiji cha Mnanila
Manyovu mkoani hapa jana, Mbowe alisema Mkoa
wa Kigoma ulizalisha viongozi wengi maarufu
katika mageuzi.
Alisema utumishi ndani ya chama hicho haupimwi
kutokana na mtu kutoka mkoa gani, bali hupimwa
kutokana na ujasiri, uwezo wa mtu na kamwe
kiongozi makini hawezi kumpiga vita mtu kwa
sababu ya kabila au dini yake.
Akitoa mfano wa viongozi waliotegemewa na
wanachi wa mkoa huo katika kuendeleza mageuzi,
Mbowe, alisema Daniel Nsanzugwanko, Aman
Kabourou na Zitto Kabwe walionyesha umahiri wao
katika kuongoza vyama vya siasa enzi zao kabla
ya kurubuniwa na kuvisaliti.
Akifafanua zaidi kuhusu lawama ambazo zimekuwa
zikielekezwa kwake na chama anachokiongoza,
hususan kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu
Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, Mbowe
alisema kuwa kamwe hawezi kumzibia kwa kuwa
ndiye aliyemtafuta na kumuingiza katika siasa
akiwa kijana mdogo.
Labda nilazimike kutoa ufafanuzi huu ili muelewe
ukweli wake. Mimi ndiye nilimwingiza Zitto katika
siasa akiwa kijana madogo, nilimwita akitokea
masomoni Ujerumani, kisha nikamshauri
akagombee ubunge katika jimbo la Kigoma
Kaskazini, nikampa pesa na gari ambalo mpaka
sasa hajalirudisha,” alifafanua.
Alisema Zitto ndiye aliyetia mchanga kitumbua
chake kwa kusaliti chama kutokana na kukubali
kurubuniwa na viongozi wa CCM, jambo ambalo
lisingelivumiliwa ndani na nje ya chama.
Huku akishangiliwa na umati mkubwa uliofurika
katika Uwanja wa Community Centre mjni Kigoma,
Mbowe alisema kuwa, atahakikisha anakilinda
chama hicho kwa gharama yoyote bila kumwonea
mtu ili kukijengea imani kwa watanzania.
Akizungumzia usaliti wa aliyewahi kuwa Mbunge
wa Kigoma Mjini kupitia chama hicho, Dk. Aman
Kabourou, alisema kwamba akiwa kijana
mwanzilishi wa chama hicho, alishiriki kikamilifu
kumpigania Dk. Kabourou kumleta nchini na
hatimaye kugombea ubunge mwaka 1993 katika
uchaguzi mdogo.
“Nyinyi vijana wengi inawezekana hamjui hiki
chama kilianza vipi katika mkoa huu. Mimi
nilishiriki kikamilifi kumwezesha Dk. Kabourou
kuwania ubunge wa Kigoma Mjini kwa kutoa nauli
ya kumleta kutoka Uingereza alikokuwa akiishi,
yeye na mkewe na pia nikampa pesa kumwezesha
kufanya kampeni, leo hii mnanihukumu Mbowe,”
aliongeza.
Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanafikiri
kuwa anampiga vita Zitto, jambo ambalo si kweli
kwa kuwa amemlea, amekula na kulala nyumbani
kwake kabla hajakua kiuchumi.
Jana, Mbowe alifanya ziara yake katika jimbo la
Manyovu, Kigoma mjini katika uwanja wa
Community Centre Mwanga, Munawila na
Mahembe ambako aliendelea kuwasisitiza
wananchi kuwapa dola upinzani kwa kuanzia
uchaguzi wa serikali za mitaa.

No comments:
Post a Comment