Wednesday, November 12, 2014

AMPIGIA SIMU RAIS KUMUOMBA MCHANGO WA KUTOA MAITI MOCHWARI

 Baadhi ya viongozi wakubwa duniani ikiwemo marais, viongozi wa kidini na wengineo wamekuwa na utaratibu wa kutumia huduma za mitandao ya kijamii na simu za mkononi kuwasiliana na watu.
rais wa kenya, uhuru kenyatta ni moja ya marais ambao wamekuwa wakitajwa kutumia sana mitandao ya kijamii ikiwemo twitter.

Anita (mwenye t-shirt nyeusi) akiwa na familia yake.
huenda usiamini alichokifanya rais uhuru kenyatta, stori ni kwamba baada ya kutumiwa message na anita lipesa ambaye alikwama shilingi milioni tatu na laki tano za kenya kwa ajili ya kutoa mwili wa dada yake aliyefariki kutoka chumba cha kuhifadhia maiti.


anita amesema baada ya jitihada za kuchangisha michango kushindikana aliamua kumtumia ujumbe kwa rais kenyatta ingawa hakuwa na tumaini lolote kujibiwa, dakika 30 baada ya kutuma message hiyo kenyatta alimpigia simu dada huyo ambaye hakuamini kama rais angeweza kufanya hivyo
Dada huyo anasema baada ya kumwelezea Rais kilichotokea alipata msaada wa kuutoa mwili wa dada yake huyo na kwenda kufanya mazishi.

No comments:

Post a Comment