Monday, November 10, 2014

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume.

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania,
 Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa

 afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Upasuaji huo ulikuchukua kiasi cha saa moja unusu ambapo inaelezwa kuwa umefanyika
 salama na kwa mafanikio makubwa.

Taarifa hiyo inasema hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini
 akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Chanzo Sammisago.com 

No comments:

Post a Comment