Tuesday, March 10, 2015

AIBU!! MHUKUMU WATU VIFUNGO JELA APANDISHWA KIZIMBANI KWA UTEKAJI,WIZI NA PICHA ZA UCHI


Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Somanda Wilayani 
Bariadi Janeth Mazigi(28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa makosa manne(4)  aliyoyatenda dhidi ya mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi akimtuhumu kutembea na mme wake.


Hakimu huyo inadaiwa  kuwa alitumia wadhifa   alionao  kumteka mtumishi huyo  (jina linahifadhiwa) na  kumnyanyasa  kijinsia kinyume na sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.

Akisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoani Simiyu Yamiko Mlekano mbele ya hakimu Mfawithi mahakama ya wilaya  Bariadi Aidan Mwilapwa wakili huyo alisema kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kwa kosa la wizi, utekeji, unyanyasaji, pamoja na kukutwa na picha utupu.

Mlekano aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 3/03/2015  mshtakiwa pamoja na askati polisi wa kike walimteka Mtumishi huyo ofisini kwake kinyume na matakwa yake na kumpeleka nyumbani kwa mshitakiwa Kidinda Bariadi Mjini kinyume na kifungu namba 133 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.

Kosa la pili la unyanyasaji wa kijinsia , ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa  Mshtakiwa ,  alimpiga  picha za utupu  mtumishi huyo kwa kutumia simu yake  kwa lengo la kumdhalilisha na kumtolea maneno ya kashfa.

Kosa la tatu ni ,kukutwa na picha za uzalilishaji mshitakiwa ilidaiwa terehe hiyo hiyo majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa mshitakiwa alikutwa na picha za utupu zilizokuwa katika simu yake alizokuwa amempiga mtumishi huyo akiwa uchi  kwa  lengo za kuzituma katika mitandao ya kijamii ili kumdhalilisha kinyume na sheria na kanuni ya adhabu.

Kosa la nne ambalo ni wizi ilidaiwa mshitakiwa alimnyang'anya Mtumishi huyo kiasi cha pesa taslimu Tsh 50,000, power bank, chaji, airphone, simu mbili za aina ya Son na Tecno vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh Mil 1,405,000.

Hata hivyo mshitakiwa alikana makosa hayo, ambapo aliachiwa huru kwa baada ya kupata dhamana, huku hakimu wa mahakama hiyo akiahirisha kesi hadi mnamo tarehe 2/04/2015.

Hata hivyo mshitakiwa huyo wakati anatenda makosa hayo alishirikiana na askari polisi kituo cha polisi Bariadi, ambaye hakuweza kupatikana jina lake, huku taarifa zikisema kuwa askari huyo bado anashughulikiwa na mamlaka zilizoko chini yake kijeshi.

Mshtakiwa  anadaiwa kutenda   makosa hayo nyumbani kwake huko Kidinda na kwamba chanzo kinasadikiwa ni  wivu wa mapenzi ambao ulipelekea kumtuhumu   Mtumishi huyo kuwa anatembea na mume wake.
Via>>http://simiyunews.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment