Tuesday, March 10, 2015

Mkanganyiko Uliojitokeza Kuhusu Mchinjaji Watu wa IS Jihad John Kutaka Kuingia Tanzania na Kuzuiwa!


Jihad John
Juzi nilikuja na uzi hapa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe aliliambia gazeti la The Times la Uingereza kuwa Mohammed Emwazi aka Jihadi John na marafiki zake wawili walizuiwa kuingia nchini mwaka 2009 kwa sababu y ulevi na kuwatukana maafisa wa uhamiaji. Kwa mujibu wa gazeti hilo pia Waziri Chikawe alikanusha madai kuwa Uingereza ndiyo iliyoitaarifu Tanzania kutowaruhusu Jihadi John na wenzake kuingia nchini.

BBC News imeripoti leo kuwa Waziri Chikawe amesema kuwa Johad John alitaka kufanya vitendo vya ugaidi nchini Tanzania. Akiongea na correspondent wa BBC Afrika Mashariki Ed Thomas, Waziri Chikawe amesema kuwa hakukuwa na tip-off yoyote kutoka kokote kumzua Jihad John kuingia nchini, lakini alitaka kutudhuru. Kwa maneno ya Kiingereza Waziri amesema:
Jihad John
"Because for us at that time he [Jihad John] was just like any other visitor trying to enter Tanzania, he wasn't special. They must have wanted to do some terrorist acts. I think maybe they wanted to harm us, definitely. We have been hit terrorists. The American embassy was blown up. We feel we are targets, and we don't want to be victims. We shall always defend ourselves."
Report ya Polis wa Airport Baada ya kumkamata Jihad John
Aidha Waziri Chikawe amesema ameziagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wakati Jihad John alipotaka kuingia nchini. Amesema amewaagiza waangalie footage ya CCTV kama ipo ili kuona nini hasa kilichotekea usiku ule wa usiku wa Mei 22, 2009.

My Take:

Maelezo ya Waziri yanaleta maswali mengi. Mojawapo ni kama Jihad John angekuwa hajalewa, kama alikuwa hajawatukana maasifa wa uhamiaji pale uwanjani kana inavyodaiwa, bado angeruhusiwa kuingia nchini pamoja na kuwa Waziri anaamini Emwazi alitaka kutudhuru aka "wanted to harm us"?

Pili, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Ernest Mangu, ashaliambia gazeti la The Citizen kuwa jina la Mohammed Emwazi halikuwepo kwenye database ya watuhumiwa wa kigeni waliokamatwa na kuondolewa nchini mwaka 2009 (IGP: Jina la Mohammed Emwazi halikuwepo kwenye database ya polisi). Kanusho hilo liliripotowa pia na BBC News. Ina maana IGP alidanganya au alikuwa hajuia alichokuwa anakisema? Kwa nini serikali inajichanganya sana kwenye hili suala la Jihad John? Au ni vyombo vya habari vinawanukuhu vibaya

No comments:

Post a Comment