Friday, June 17, 2016

TANZANIA NA SWEDEN ZATILIANA SAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO

swe2
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), akizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya Tanzania na Sweden, kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo wa miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo Juni 16, 2016
swe3
Katibu Mkuu Wizara ra Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile (kushoto), na mgeni wake, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (kulia), wakipeana mikono na kubadilishana hati za mkataba baada ya  kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa maendeleo wa miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe4
Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Tasaf Ladislaus Mwamanga (kushoto) wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe5
Ujumbe wa Sweden ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa wa Sweden Mhe. Ulrika Modeer (Katikati), wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka mine kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016
swe6
Baadhi ya Maofisa wa serikali ya Tanzania wakifuatilia kwa makini tukio la kutiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden, utakao chukua miaka minne kuanzia 2016 hadi 2019, tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina Mjini Dodoma leo, Juni 16, 2016 (P.T)

TEA KUJENGA NYUMBA 40 ZA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Joel Laurent (katikati), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa na Watumishi Housing Company katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo. Kushoto ni Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa TEA, Julius Rugemalila. (Picha na Francis Dande)
Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati) akizungumza wakati wa kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (katikati), wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia), akibadilishana hati na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari zitakazojengwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara, ambapo familia 240 za walimu zitanufaika na ujenzi wa nyumba hizo.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (kulia) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa wakipongezana.
Picha ya pamoja.
 Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa akisaini kitabu cha wageni.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Joel Laurent (katikati) na Mkurugeni Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC), Dk. Fred Msemwa (kulia), wakizungumza mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa nyumba 40 za walimu wa Shule za Sekondari.

RC WA MWANZA MHE JOHN MONGELLA APOKEA GARI LA WAGONJWA

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza na watumishi kabla yakupokea msaada wa gari la wagonjwa.
 Mkuu wa mkoa akikata Utepe kuashiria uzinduzi wa mapokezi ya Gari la Wagonjwa kutoka Rafiki Surgical Mission.
 Balozi  Issaya Chialo alipokuwa akitoa maelezo mafupi juu ya msaada wa gari la wagonjwa walilo likabidhi kwa hospitali ya Mkoa wa Mwanza.
 Watumishi katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza, wakimasikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Mwanza hayupo pichani, wakati wa hafla fupi yakukabidhi gari hilo.
 Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Subi, akitoa maelezo ya awali kuhusu huduma za afya katika mkoa wa Mwanza wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
 Wananchi wanao hudumiwa katika hospitali hiyo ya mkoa nao hawakuwa nyuma katika hilo, hapo wakisiliza kwa makini maelezo ya mkuu wa mkoa.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, Bi Maricella, akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Mwanza.
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akikabidhi cheti cha Shukrani kwa Balozi Issaya Chialo, kama sehemu ya shukrani kwa kutambua mchango wa Rafiki Surgical Mission, walio utoa kwa Mkoa huo wa Gari la Wagonjwa.
Hilo ndilo gari lililotolewa na Rafiki Surgical Mission.
(Habari na picha zote na Afisa habari wa mkoa wa Mwanza)

Monday, June 13, 2016

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

Wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa sala ya kuliombea Bunge leo asubuhi mjini Dodoma na wakiendelea na msimamo wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mbunge wa Ukonga (CHADEMA) Mhe. Waitara Mwikwabe akiwa pamoja na Mbunge wa Same Mashariki (CHADEMA) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mary wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge hilo leo mjini Dodoma kuendeleas na msimamo wao wa wao wa kutomtambua Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto) na Lucy Magereli (katikati) mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge hilo leo asubuhi mjini Dodoma.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dkt. Dalali Kafumu akibadilishana mawazo na Wabunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Mhe. Mariam Msabaha (kushoto), Lucy Magereli na Mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Ester Matiku mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hiloi leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, ushirikiano wa afrika mashariki na Kikanda, Mhe. Susan Kolimba, akisalimiana na Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe. Anna Tibaijuka mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Wabunge wa CCM kutoka kushoto Sadifa Juma (Donge), Augustine Vuma (Kasulu Kusini) na Innocent Bilakwate (Kyerwa) wakibadilishana mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha asubuhi cha Bunge hilo leo. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI IKULU JIJINI DAR LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akimuapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kuwaapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR ATEMBELEA VITUO VYA AFYA MKOA WA KASKAZINI

Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na viongozi wa Chama na Serikali alipowasili Chaani Masingini kukagua kituo cha Afya cha kijiji hicho kufuatia mwaliko wa Mwakilishi wa Jimbo hilo Nadir Abdul- latif.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya Kaskazi ‘A’ Hassan Ali Kombo na Daktari dhamana wa Wilaya hiyo Rahma Abdalla Maisra wakati akikitembelea kituo cha Afya cha Chaani Masingini.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatana na viongozi wa Jimbo la Chaani wakiangalia tanuri la kuchomea taka za kituo cha Afya cha Chaani Masingini alipotembelea kituo hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif akimkaribisha Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kuzungumza na wananchi waliofika kituo cha Afya cha Chaani Masingi ambacho kinahitaji matengenezo makubwa.
Waziri Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha afya cha Donge na Kamati Kiongozi ya Jimbo hilo katika Kituo cha Afya cha Donge Wilaya Kaskazini B.
Mkuu wa kituo cha Afya Donge vijibweni Miza Ali Ussi akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho kujua changamoto zinazowakabili.
Mwakilishi wa Jimbo la Donge Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza katika mkutano huo (kulia kwake) ni Mkuu wa kituo cha Afya Donge Miza Ali Ussi. Picha zote na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR

Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amezitaka Kamati Kiongozi za Majibo kusimamia kikamilifu vituo vyao vya  Afya na kuhakikisha majukumu waliyopangiwa wanayatekeleza kikamilifu  ili kuimarisha huduma katika vituo hivyo.

Alisema Serikali imebadili mfumo katika kusimamia vituo vya afya kwa kuvipeleka moja kwa moja kwa jamii kusaidia huduma ndogo ndogo huku Serikali kuu  ikibakia na jukumu lake la msingi la  kuvipatia vifaa vya matibabu, dawa na mishahara ya wafanyakazi. 

Waziri Mahmoud Thabit Kombo alieleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya Afya vya Mkoa wa Kaskazini Unguja kujua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa vituo hivyo katika kutoa huduma bora.

Alisema huduma ya matengenezo madogo madogo, kulipia umeme na maji, kuviwekea uzio na ulinzi  sasa vipo chini ya  Kamati Kiongozi za Majimbo ambazo zinaundwa na Wabunge, Wawakilishi, Madiwani, Masheha na Mkuu wa kituo cha Afya husika.

Aliongeza kuwa hivi sasa Serikali haitoa kipaumbele kujenga vituo vipya vya Afya bali inaelekeza nguvu zake kuviimarisha vituo viliopo kwa kushirikiana na mradi wa ORIO na Milele pamoja na Kamati Kiongozi za Majimbo.

Aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Chaani kwamba kituo chao cha Afya cha Chaani Masingini, ambacho kimesitisha kutoa huduma kwa miaka mitano kutokana na kuwa kibovu, kitaanza kufanyiwa matengenezo makubwa hivi karibuni kupitia Mradi wa ORIO.

Waziri wa Afya aliwataka viongozi na wafanyakazi wa sekta ya Afya kuwapa ushirikiano wa karibu wakunga wa jadi ambao wanatoa mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga wakati wa kujifungua.

Alisema wakunga wa jadi bado wanaendelea kuaminiwa na wanachi wengi, hasa sehemu za vijijini, kutokana na huduma nzuri wanazotoa kwa wateja wao na ameshauri wapatiwe vitambulisho maalum  ili waweze kutambulika.

Aidha alisema Zanzibar imepata sifa kubwa mbele ya Jamii ya Kimataifa katika kupambana na Malaria na maradhi mengine yaliyokuwa yakiwasumbua wananchi, lakini hali sio nzuri katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga hivyo ametaka juhudi zaidi ifanywe kukabiliana na tatizo hilo.

Akinamama wa Jimbo la Chaani walimueleza Waziri wa Afya kuwa wanapendelea zaidi kujifungua kwa wakunga wa jadi kutokana na kauli zisizoridhisha kutoka kwa wakunga wa vituo vya Afya wanapokwenda kujifungua.

Walishauri kutolewa elimu ya ukarimu na upole kwa wakunga wa vituo vya afya ili kuwajengea imani wajawazito kwenda kujifungulia kwa wingi katika vituo hivyo.

Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Nadir Abdul-latif alimuhakikishia Waziri wa Afya kwamba yupo tayari kutoa kila msaada unaotakiwa ili kuona huduma za Afya katika Jimbo hilo zinaimarika.

Waziri wa Afya alitembelea vituo vya Afya vya Chaani Masingini, Chaani Kikobweni na Kituo cha Afya   Donge.

Sunday, June 12, 2016

WAFANYAKAZI TBL WAHUDHURIA SEMINA YA MALEZI YA FAMILIA

m1
Watoa mada Grace Makani Tarimo na Dk.Ellivid Waminian wakiongea na washiriki wa semina ya masuala ya kujenga familia bora iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam
m2
Wafanyakazi wakisikiliza mada
m3
Wafanyakazi wakisikiliza mada
m4
Wafanyakazi wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika semina.
Katika kuhakikisha wafanyakazi wake wanapata elimu ya masuala mbalimbali ya kijamii nje ya mazingira ya kazi,kampuni ya TBL Group imewezesha baadhi ya wafanyakazi wake kuhudhuria semina ya malezi  ya familia iliyofanyika jijini Dar es Salaam .
Katika semina hiyo wataalamu mbalimbali  wa masuala ya elimu jamii kutoka kampuni ya Grace Inc walitoa mada kuhusiana na masuala ya malezi bora ya familia na changamoto zilizopo katika kujenga familia bora ambapo washiriki walipata fursa ya kuuliza maswali yanaohusiana na malezi ya familia.
Wafanyakazi hao walishukuru kampuni kwa kuwapatia fursa ya kuhudhuria semina hiyo na walisema kuwa imewawezesha kupata maarifa mbalimbali yatakayowasaidia kujenga familia zao.(P.T)

NSSF YAWAFIKIA MADEREVA WA BODABODA MKOANI DODOMA

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limefanya semina na kuzindua mpango wa kuwaandikisha maadereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma, Mpango huo ulifanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Mji wa Dodoma, VETA , Trafiki Mkoa na NSSF umezinduliwa na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama.


Pamoja na Uzinduzi wa Uandikishaji Waziri Jenista Mhagama aliwapatia Vifaa vya Usalama Madereva hao wa BodaBoda Mkoani Dodoma vifaa hivyo ni Kofia ya Usalama na Kikoti Maalumu cha Usalama ambavyo vimeandikwa Namba kulingana na Kituo cha Bodaboda Wanachofanyia Kazi. Pia Waziri amezindua mfumo wa kuvipa namba na kuviweka alama Vibao vituo vyote vya Bodaboda mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akiongea na Madereva wa Bodaboda (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa rasmi wa Kampeni ya Kuandikisha Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akitoa elimu kwa Madereva wa Bodaboda wa Mkoa wa Dodoma waliouzulia zoezi la uzinduzi wa kampeni rasmi ya kuwatambua na kuwaandikisha NSSF madereva wa Bodaboda.
Waziri akikabidhi moja ya pikipiki ambazo wamekopeshwa madereva wa Bodaboda Dodoma na Manispaa ya Dodoma. Wakishuhudia ni Mwakilishi wa Kamanda wa Trafiiki Mkoa, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvalisha mmoja wa Madereva wa Bodaboda Kofia Ngumu ya Usalama iliyotolewa na NSSF. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof, Godius Kahyarara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvesha Jaketi maalumu la Usalama Dereva wa Bodaboda Mkoa Dodoma akimsaidia Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Francis Mwonga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa Kituo Cha Bodaboda kwa Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoani Dodoma Bang'ara Lucas Kang'alo akishuhudia katikati Mkurugenzi wa NSSF Prof Godius Kahyarara.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya wa Bahi Francis Mwonga( Wa Kwanza kulia kwa Waziri), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara (Kushoto kwa Waziri) na Mkuu wa Chuo cha Veta Dodoma Bw. Mattaka baada ya kupokea mfano wa kadi ya Mwanachama ya NSSF akiwa mmoja ya wanachama wapya waliojiunga NSSF.