Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta anaongoza mkutano wa Wabunge wa serikali kuteua
majina ya wajumbe watakaoketi katika Kamati maalum ya kutatua mzozo wa
Tume ya uchaguizi IEBC.
Hatua hii inakuja baada ya Rais Uhuru Kenyatta, kutangaza mpango mahsusi utakaosaidia kupatikana kwa suluhu.
Akizungumza
kwenye ikulu ya Nairobi, rais Kenyatta amesema ataunda kamati maalumu
itakayohusisha Bunge la kitaifa na lile la Seneti, na kwamba kamati hiyo
itakuwa na jukumu la kukusanya maoni na kupendekeza njia za kufuata
kuhusu shida ya IEBC na si vinginevyo.
Tangazo
la rais Kenyatta linaongeza shinikizo zaidi kwa kinara wa muungano wa
Cord, Raila Odinga, kukubali kurejea kwenye meza ya mazungumzo baada ya
juma hili kutangaza kuendelea na maandamano yao licha ya kupigwa
marufuku na polisi.
Rais
Kenyatta amewataka viongozi wa Cord kuheshimu hatua anazochukua kumaliza
tofauti zao, na kwamba hii ndio njia pekee kulinusuru taifa lao
kutumbukia kwenye machafuko.
Viongozi
wa Cord wakiongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, watakutana
na viongozi wa dini kuzungumzia kile walichoafikiana na rais Kenyatta na
namna Cord inavyoweza kushiriki vyema kwenye mchakato huu.

namna Cord inavyoweza kushiriki vyema kwenye mchakato huu.RFI(P.T)
No comments:
Post a Comment