Umoja wa
Mataifa umekubaliana kuongeza jitihada za kumaliza janga la UKIMWI,
ifikapo mwaka 2030, ingawa Urusi imetaka kutowalenga zaidi watumiaji wa
dawa za kulevya na wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Makubaliano
hayo ya kisiasa yamefikiwa na wanachama 193 katika mkutano mkuu,
ulioweka msisitizo juu ya mahitaji ya kuwasaidia wanaotumia dawa za
kulevya kwa kujidunga sindano, wanaojihusisha na biashara ya ngono,
wanaobadilisha jinsia na wafungwa amabo wapo katika hatari kubwa ya
kupata maambukizi ya virus UKIMWI.
Maambukizo
ya Virusi vya UKIMWI yamekuwa yakipungua katika muongo mmoja uliopita,
lakini bado kuna kiasi ya watu Milioni 36.7 duniani kote wanaoishi na
Virusi vya UKIMWI ama UKIMWI, na wengi wao wakiwa katika eneo la Kusini
mwa Jangwa la Sahara, ambako Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia UKIMWI, UNAIDS, Michel Sidibe amesema ndiko kuna idadi
kubwa ya watu wanaotumia dawa.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amewaambia wajumbe wa mkutano huo
kwamba UKIMWI bado ni tishio, kwa hiyo mataifa bado yana nafasi ya
kuhakikisha yanabadilisha hali ya janga hilo katika kipindi cha miaka
mitano ijayo.
Ban
ametaka kutolewa kwa huduma na dawa kwa watu wote wanaoishi na Virusi
vya UKIMWI bila ya ubaguzi. Aliwalenga zaidi vijana wadogo, wahamiaji,
wanawake na wasichana, wanaofanya biashara ya ngono, wanaume
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, wanaojidunga dawa za kulevya,
wanaobadilisha maumbile na wafungwa.
Makubaliano
haya yanatokana na mipango ya awali ya Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI
yaliyopitishwa miaka mitano iliyopita, kwa kuweka msisitizo zaidi kwa
kwale walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi. Makubaliano hayo
yamelenga maeneo matatu yanayootakiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2020,
ambayo ni kupunguza maambukizi mapya ya Virus vya UKIMWI, kupunguza
idadi ya vifo na kuondoa unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na Virusi
vya UKIMWI.
Urusi
ilitaka mabadiliko ya mkakati huo mpya kuangazia sheria za kitaifa na
namna zinavyoyataja makundi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya
jinsia moja, watumiaji wa dawa za kulevya na wafungwa. Walisema
wanadiplomasia na makundi ya kiraia, Jumanne hii.
Mabadiliko
hayo yalipingwa vikali kutokana na hofu kwamba yataruhusu Urusi, Iran
na nchi nyingine zinazochukulia mapenzi ya jinsia moja kama uhalifu
kuzuia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na huduma nyingine kwa wanaume
hao.
Mkutano
huo wa siku tatu, ulianza kwa ombi la mjukuu wa aliyekuwa Rais wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela, Indaba ambaye baba yake alikufa kwa UKIMWI
mwaka 2005, akiwataka viongozi wa nchi 35 zinazozuia watu walioathirika
kuingia nchini mwao, ikiwa ni pamoja na Urusi na Singapore kuondoa
marufuku hiyo.DW
No comments:
Post a Comment