Gulio
la simu Expo litakalofanyika katika viwanja vya posta Kijitonyama
jijini Dar es Salaam kesho Jumamosi na Jumapili wiki hii litawawezesha
wateja wa Vodacom Tanzania na wananchi kwa ujumla kujipatia simu za
uhakika zenye gharama nafuu ikiwemo simu za bure kwa wateja watakaonunua
vifurushi vya aina mbalimbali vya muda wa maongezi na intanenti.
Akiongea
juu ya gulio hilo,Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Rosalynn Mworia alisema kuwa lengo la gulio hili ni
kuwawezesha wateja wa kampuni kuweza kupata maelezo kuhusu huduma za
kampuni ikiwemo kuweza kununua simu halisi zenye viwango vinavyotakiwa
kwa gharama nafuu kuanzia simu za shilingi elfu 18/- na kuna ofa ya
wateja kujipatia simu za bure kabisa.
“Gulio
hili la Vodacom Simu Expo limekuja katika wakati mwaafaka ambapo tarehe
ya mwisho ya kuzima simu zisizo na viwango inakaribia hivyo
tunawakaribisha wateja wetu wote watembelee gulio hilo na kuweza
kujipatia simu zenye viwango vinavyostahili kwa gharama nafuu ambapo pia
watapata fursa ya kupata maelezo ya huduma zetu mbalimbali” Alisema.
Alisema
katika gulio hilo pia kutakuwepo na watoa huduma mbalimbali ambao
watashughulikia matatizo ya simu za mkononi pamoja na huduma zinginezo
kwa wateja watakafika kwenye gulio hilo.
Mworia
alisema katika Simu Expo pia yanakaribishwa makampuni yanayouza simu
nchini kushiriki na kuhakikisha yanatoa punguzo maalum kwa wateja kwa
ajili ya kuwanufaisha wateja hususani katika kipindi hiki cha mwisho
ambacho Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) inakaribia kuzima simu zisizokidhi
viwango,hatua ambayo itawaathiri baadhi ya watumiaji wa simu kwa kuachwa
nje ya mtandao.
Kuhusiana
na ofa ya kujipatia simu ya bure alisema kuwa mteja atakayenunua
kifurushi cha muda wa maongezi wa dakika 330 za kupiga mitandao yote
chenye jumbe fupi za maneno 2000 na MB 500 za intanent ambacho kinadumu
kwa mwezi mmoja atajipatia simu yenye thamani ya shilingi
18,000/-,wakati atakayenunua kifurushi cha dakika 550 cha kutumia
mitandao yote chenye jumbe fupi za maneno na MB 500 atajipatia simu
yenye thamani ya shilingi 25,000/-.
Pia
alisema kuwa wateja watakaonunua kifurushi cha dakika 1000 cha kupiga
mitandao yote chenye jumbe fupi za maneno 10,000 na MB 500 za internet
kinachodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja atajipatia simu ya bure yenye
thamani ya shilingi 50,000/-
Alisema
ofa ya simu za bure inawahusu wateja wanaotumia simu za Smart phone
wanaoishi jijini Dar e Salaam ambao tayari wamefahamishwa kuhusu ofa hii
kupitia jumbe fupi za maneno na pindi watakaponunua vifurushi kwa
mujibu wa maelekezo waliyopewa wataweza kujipatia simu bure za aina ya
Smart Phone ITEL 1406.
“…Tunawaomba
wateja wetu na wananchi wote wafike katika viwanja vya Kijitonyama ili
waweze kujipatia simu nzuri na za kisasa wazipendazo kwa punguzo la bei
hadi asilimia 50 kwa baadhi ya simu na kupata ofa ya simu za bure kwa
kununua vifurushi,” alisema
No comments:
Post a Comment