Obama ataanza kufanya kampeni na Clinton
Rais wa
Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa
mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
baadaye mwaka huu nchini Marekani.
Amechukua
hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie
Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang’anyiro
cha kumchagua mgombea wa chama hicho.
Akizungumza
kwenye video ambayo imepakiwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama
amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa
Marekani.
Clinton: Siwezi kushindwa na Bernie Sanders
“Niko pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni na Hillary,” amesema Obama.
Obama alikutana na Sanders ikulu ya White House
Wawili hao sasa wanatarajiwa kuanza kufanya kampeni pamoja.
Bw
Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi
Clinton, kumshinda mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika
uchaguzi mkuu.
Hata
hivyo hakujiondoa kinyang’anyironi. Alisema ataendelea kufanya kampeni
yake na kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.BBC
No comments:
Post a Comment