Imeelezwa
ili kuwawezesha watoto yatima ambao walizaliwa wakiwa na Virusi vya
UKIMWI ambao wanapatikana katika Kituo cha Matumaini kilichopo Manispaa
ya Dodoma, Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuwasaidia
watoto hao ambao wanaishi katika kituo hicho ili kuwawezesha kuishi
mazingira bora pamoja na kupata huduma za bora za afya.
Hayo
yalisemwa na Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria
Gargiulo, alisema kituo hicho chenye watoto 151 wakati kimeanzishwa
kilikuwa kikipokea msaada kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na TACAIDS lakini kwa sasa msaada umesimama na
hivyo kuwafanya kwa sasa kuishi katika mazingira magumu.
Sister
Maria alisema kuwa hali ya maisha kwa watoto hao ni ngumu na hivyo
kuwataka Watanzania kuwakumbuka watoto hao ambao walizaliwa wakiwa na
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili waweze kupata huduma bora ambazo
zitawawezesha kuishi katika mazingira bora, kupata elimu na kupata dawa
ambazo zitaimarisha afya zao.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) na mfanyakazi
mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiongozwa na Msimamizi wa Kijiji cha
Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo mara baada ya kuwasili katika kituo
hicho kilichopo katika manispaa ya Dodoma karibu na Hoteli ya Mtakatifu
Gasper.(na Zainul Mzige)
“Hapa
wanakuja tu watu wa hapa Dodoma mara nyingi siku za Jumamosi na
Jumapili ila tofauti na hivyo hatuna msaada mwingine, watoto hawa
wanahitaji faraja kutoka kwa watu wengine inapendeza kuona watu wanakuja
kuwaona na kuwasaidia nao wanafurahi,
“Ukiangalia
hali ya kimaisha inazidi kupanda tunafanya jitihada kujisimamia sisi
wenyewe lakini tunashindwa bado tunahitaji msaada sisi tumejitoa
kuwasaidia hawa watoto hata hatulipwi lakini tunahitaji sana msaada wa
Watanzania,” alisema Sister Maria.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimsikiliza kwa makini mmoja
wa watoto wanaoishi kituoni hapo aliyewahi kumuona mara ya kwanza
alipofika kituoni hapo.
Nae
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999 na Mtalaam wa Mawasiliano wa
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu ambaye alifika kituoni hapo
kwa ajili ya kutoa msaada ambapo alituma ujumbe kwa Watanzania wengine
ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kutoa misaada kwa wahitaji na
kuwataka kubadilika.
Bi.
Temu alisema kuwa mazingira ambayo wanaishi watoto hao ni magumu na
hawana wazazi kutokana na wazazi wao kuwa wamefariki hivyo kuwataka
Watanzania kujitoa kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao kwa chochote
ambacho kinaweza kuwasaidia kuimarisha maisha yao ili waishi mazingira
bora.
“Jamani
kama watu wanasema tunapoishi kuna shida basi hakuna, shida zipo huku,
ukiangalia kuna watoto wengine wana wiki moja na hawana wazazi wametupwa
wanahitaji kupata misaada ya Watanzania,
“Nitoe
rai kwa Watanzania wenzangu kama una pesa au nguo au chochote ambacho
kinaweza kuwasaidia tutoe kwa watoto hawa mazingira yao ni magumu sana,
hawana makosa hawa hata mbele za Mungu naomba tuwasaidie,” alisema Bi.
Temu.
Kwa
yoyote atakayeguswa na angependa kufika kituoni hapo kusaidia anaweza
kupiga simu kwa Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria
Gargiulo +255754272707
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kulia) na mfanyakazi
mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiwa wamewabeba watoto yatima wanaoishi
kituoni hapo.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahia jambo mara tu
baada ya kuwasili katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma
kinacholea watoto yatima ambao 98% wanaishi na Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwa kwenye wodi ya watoto
wachanga ambao ni yatima wanaoishi waliozaliwa na maambuki ya Virusi vya
Ukimwi.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na mfanyakazi mwenzake
Beatrice Mkiramweni pamoja na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista
Rosaria Gargiulo (kulia) walipotembelea wodi ya watoto wachanga
waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahi na watoto wachanga
ambao ni yatima waliozaliwa na maaumbikizi ya Virusi vya Ukimwi
waliolazwa katika wodi ya watoto kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani
Dodoma.
Wewe
acheka afurahi kumuona Aunty....Jiji jiji jiji.....jamani acheka....Ni
maneno ya Mlimbwende Hoyce Temu akicheza na mmoja wa watoto hao katika
wodi hiyo.
Meneja
Mwendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige
akimbeleza mmoja wa watoto waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi wanaolelewa katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Eweee
Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, tunakuomba wajaalie Malaika wako hawa
afya njema, maisha marefu, wape uponyaji viumbe hawa wasiokuwa na
hatia, Amen!
Msimamizi
wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo akimsimulia Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu historia ya mtoto Richard
aliyeshikwa mikono na mlimbwende huyo.
Mmoja wa Masista wanaohudumia watoto hao Sista Mary Shayo akifurahi jambo wodini mbele ya kamera ya Modewjiblog.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akicheza kwaya ya wimbo
maalum aliokuwa akiimbiwa na bendi ya kijiji cha Matumaini kabla ya
kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali.
Hoyce Temu akigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa kwenye kijiji cha Matumaini mkoani Dodoma.
Mlimbwende
wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi 'Pampers' kwa
mmoja wafanyakazi wanaohudumia (jina lake halikuweza kupatikana) watoto
kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi mfuko wa sukari.
No comments:
Post a Comment