MAJINA YA WANAFUNZI WA CBE NA UDSM WALIONASWA WAKIJIUZA ( MAKAHABA)
Wanafunzi
wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya
biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi stadi [VETA],Dar
es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya
biashara ya kuuza mili yao.
Washitakiwa
hao waliokamatwa katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani
kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara
hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.
Kesi
hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha
mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika
mazingira tofautitofauti.
Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.
“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.
Kwa
mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa hao wamekosa dhamana baada ya
kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au
kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.
Wakati
huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716
waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38
na wanawake 678.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi
Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako
uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.
Maeneo
hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe
wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa
wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.
“Msako
huo ulifanyika Maisha Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia ,
Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango
pamoja na Mwinanyamala” Alisema
Kamanda
Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka
nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka
huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.
Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.
No comments:
Post a Comment