MWANDISHI CHARLES MULINDA AJITOA JUKWAA LA WAHARIRI
Charles Mullinda
Mhariri Mtanzania Jumatano
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la WahaririYAH: KUJITOA KWENYE
JUKWAANapenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa la
Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.Nimeamua
kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru
wa habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini
hayapaswi kufumbiwa macho.
Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi
ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa walikuwa na mawasiliano
yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph Ludovick.Aidha,
siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na wahariri
wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa upande
mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya
wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.
Kikao cha kwanza na TEF na kilichofanyika
leo kimedhihirisha pasipo mashaka kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda
maalumu ya kumshughulikia Mullinda kwa kuwa tu nilionyesha mawasiliano
ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo dhidi ya Ludovick kama ambavyo
gazeti la Tanzania Daima lilivyoonyesha mawasiliano ya Dennis Msaki na
Ludovick.
Ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza
ukweli wa habari iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Jumatano ina
upungufu mkubwa wa kimantiki ambao hata kwenye kikao niliuonyesha lakini
haukusikilizwa.Ushahidi wa Ngurumo kumtuma pesa Ludovick upo wazi,
lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa sababu tu timu ile iliundwa
kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika vigogo wa TEF ambao wako
karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.
Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana utazingatiwa.Charles Mullinda.
No comments:
Post a Comment