By TwendeSasa
Habari
zilizoifikia Maisha Times muda huu zinaripoti kwamba hali sio nzuri huko
Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi
yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna
usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na
Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali
kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali
kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera
inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango
wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es
salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na
mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es
salaam Wananchi wa Mtwara wacharuka!
Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.
Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia yachomwa moto.
Lodge/Hotel
(Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la
Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea
imechomwa moto.
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika.
Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani. (habari haijathibitishwa rasmi)
Ni
magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu
kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.
Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi)
Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa wamepita jirani na gari yao.
Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka Masasi na Lindi.
Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia.
Vituo
vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari bali vinapiga
Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili
Wananchi wayapate.
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa.
Wakati
waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na
kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar Kauli mbiu ya
Wananchi wa Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
Wananchi
walalamikia kituo cha Television na Radio TBC kuzuia na kukata mawimbi
yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa muda. Hatimaye
hivi Punde matangazo yarejea.
Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni.
Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutukia Mtwara.
No comments:
Post a Comment