Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya,
Diamond, akiwaimbisha washiriki wa
semina
ya Fursa waliojitokeza kwa wingi mapema leo
kwenye ukumbi wa
Student's Center uliopo katikati
ya mji wa mkoa wa Tabora, kushoto kwake
ni Bwa.
Marco Vingila kutoka shirika la TPSF.
Mghani
mahiri wa mashairi hapa
nchini Mrisho Mpoto akizungumza kwa
msisitizo,
masuala ya fursa mbalimbali
zinazopatikana katika suala zima la
Fursa iliyofanyika katika
ukumbi wa Student's Center,
uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,
imefadhiriwa na shirika
la NSSF; Zantel,
MaxMalipo, Lake Oil.
Baadhi ya
Wasanii wa muziki wa
kizazi kipya wakishiriki semina ya
Fursa kwa
vijana ililiyofanyika leo kwenye
ukumbi wa Student's Center katikati ya
mji wa
mkoa wa Tabora mapema leo, kutoka kulia ni
Mkuu wa
Masoko na Mauzo wa
kampuni ya mafuta-Lake Oil, Bw Ben Temu
akizungumza
kwenye semina ya Fursa,
ambapo yeye alielezea mambo mbalimbali
ikiwemo
suala la vijana kuwa wenye moyo wa
kujituma na kutokata tamaa, alieleza
kwa kuwataka
vijana wawe wavumilivu na kutoka tamaa
kwa kila fursa
wanayokumbana nayo,badala yake
waitumie vizuri katika suala zima la
kujikwamua
na kujiendeleza kimaisha. Semina hiyo
iliyoandaliwa na Clouds
Media Group, imefadhiriwa na
shirika la NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake
Oil.
Semina ya
Fursa ikiendelea mapema leo
ndani ya ukumbi wa Student's Center
katikati
ya mkoa wa Tabora mapema leo. Semina hiyo
iliyoandaliwa na
Clouds Media Group,
imefadhiriwa na shirika la NSSF;
Zantel, MaxMalipo,
Lake Oil.
Msanii wa
Muziki wa Kizazi Kipya,
Mwasiti Almas akizungumzia baadhi ya
fursa
alizozipata mara baada ya kujiunga na
shirika la NSSF, mbele ya
Washiriki wa
Semina ya Fursa (hawapo pichani), kulia kwake ni
Mwakilishi
wa NSSF-Makao Makuu Bw. Salim
Khalfan akimsikiliza kwa makini. Semina
hiyo
iliyoandaliwa na Clouds Media Group, imefadhiri
wa na shirika la
NSSF; Zantel, MaxMalipo, Lake Oil.
Mwakilishi
wa Shiriki la NSSF kutoka
Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Salim
Khalfan
akielezea fursa mbalimbali zinazopatika
mara mtu yeyote anayejiunga ama
amejiunga na
NSSF,alifafanua zaidi kuwa mtu yeyeote
atakayejiunga na
shirika hilo atanufaika na
mambo mengi,ikiwemo suala la matibabu,
mikopo
na mengineyo lukuki yanayopatikana
ndani ya shirika hilo.Semina hiyo
iliyoandaliwa na Clouds Media Group
,imefadhiriwa na shirika la
NSSF;
Zantel,MaxMalipo, Lake Oil.
Baadhi ya
Wakazi wa Tabora wakifuatilia
kwa makini semina ya ujasiliamali
iliyokuwa i
kiendelea ndani ya ukumbi wa Student's Center
katikati ya
mkoa wa Tabora mapema leo.
Picha ya pamoja, kiukumbusho zaidi, Msanii
Mrisho Mpoto akiwa amepozi na Diamond.
Mmoja wa
akina Mama wajasiliamali
kutoka mkoa wa Tabora,Flora Zakaria
akiwa na
bidhaa zake alizozitengeneza
yeye mwenyewe kama mjasiliamali,akiuza
ndani
ya semina ya Fursa.semina hiyo ambayo
imewahusisha wadau
mbalimbali wakiwemo
wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakazi
mbalimbali
wa mji wa Tabora, Wanafunzi
kutoka vyuo mbalimbali.
Pichani
kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji kutoka Clouds Media
Group,Ruge
Mutahaba,Mkuu wa Wilaya ya Igunga
( Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tabora),
Mh. Elibariki Kingu
wakitazama paketi ya sabuti iliyotengenezwa
na mjasiliamali aliyehudhuria semina ya Fursa,
iliyofanyika kwenye ukumbi
Student's Center
uliopo katikati ya mji wa mkoa wa Tabora.
Wadau wajasiliamali wakifuatilia kwa
makini mada mbalimbali zilizokuwa
zikijadiliwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji
kutoka Clozds Media Group,Ruge
Mutahaba,
akizungumza mbele ya washriki wa Semina ya
Fursa ndani ya
ukumbi kwenye ukumbi Student
's Center uliopo katikati ya mji wa mkoa wa
Tabora.
Sehemu ya
Meza kuu.Kutoka kushoto
ni Wawakilishi kutoka shirika la NSSF,Salim
Khalfan (makao makuu),Alloys Banigwa
(Meneja wa NSSF-Tabora),Mkuu wa
Wilaya ya Iramba kutoka Mkoani
Singida,Mkuu wa Wilaya ya
Igunga,Mh.Elibarik
Kingu,Ruge Mutahaba-Clouds Media Group,
pamoja na Ben
Temu kutoka kampuni ya Lake Oil.
Baadhi ya Wasanii mbalimbali
wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri
kwenye semina ya Fursa,mapema leo mkoani Tabora.
Baadhi ya
wakazi wa Tabora wakiwa
kwenye semina ya Fursa ndani ya ukumbi
Student's Center mkoani Tabora mapema leo,
ambapo mada mbalimbali
zimezungumzwa,
ikiwemo mambo ya ujasiliamali kwa vijana,
mikopo,akiba
sambamba na namna
ya kujiongezea thamani ya fursa unayoipata.
No comments:
Post a Comment