Rais Dkt. Jakaya Kikwete.akiongea katika hafla hiyo leo kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akitoa taarifa yake wakati wa sherehe ya kutunuku hati idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki jijini leo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani)
Baadhi ya wadau wa elimu walioshiriki katika hafla ya kutunuku hati idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki wakiwa katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibadilishana na mawazo na Waziri wa Elimu na Ufundi Dkt, Shukuru Kawambwa wakati wa hafla ya kutunuku hati idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki leo jijini Dar es Salam
Picha ya pamoja ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na watunukiwa wa hati idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki

Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO..
Na Immaculate Makilika- Maelezo.
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku hati
Idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vishiriki 8 baada ya vyuo hivyo kutimiza
taratibu zote za uanzishwaji wake hapa nchini.
Vyuo
vilivyotunukiwa hati baada ya kutimiza taratibu zote ni Chuo Kikuu cha
Tumaini(TUMA),Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT),Chuo Kikuu
Kishiriki cha Ruaha(RUCo),Chuo Kikuu cha Mount Meru(MMU),pamoja na
Chuo Kikuu cha Arusha(UoA).
Vyuo
vingine vilivyotunukiwa hati hiyo ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini
Dar es salaam(TUDARCo) ,Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya
Sayansi na Teknolojia Arusha (NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya(MUST).
Rais Kikwete alivitunuku vyuo
hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam ,
ambapo alisema vimepiga hatua kubwa ya kuongeza idadi ya wanafunzi
wanaojiandikisha hadi kufikia laki moja sitini na sita elfu mwaka 2013
,ukilinganisha na idadi ya wanafunzi elfu arobaini ya mwaka 2005.
“Idadi
kubwa ya wanafunzi pekee haitoshi,ubora wa elimu uzingatiwe . Ikiwemo
kupata wakufunzi wengi na wenye sifa ni lazima sisi wenyewe tuwekeze
ndani ili kupata wakufunzi wakutosha katika vyuo vyetu ,” alisema Rais
Kikwete.
Aidha
Rais Kikwete alivitaka vyuo hivyo kutekeleza mkakati wa elimu
wa Matokeo Makubwa Sasa (Big results now) ipasavyo ili kuboresha
elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu ya vyuo vikuu nchini.CHANZO FULL SHANGWE BLOG
Aliongeza
kuwa lazima viwe na mahitaji yote muhimu kwa kutoa elimu bora ikiwemo
vifaa vya kutosha,maabara,vyuo vya zamani viwekwe kwenye viwango ili
kukidhi utoaji wa elimu bora, na kusisitiza vyuo vikuu vyetu
vishirikiane na vyuo vikuu vya nje na kuvishauri vitafute vyanzo
vingine vya mapato ili kukidhi uendeshaji badala ya kutegemea ada.
Utoaji
wa hati Idhini kwa vyuo vikuu ni zoezi endelevu
linalolenga kuboresha kiwango cha utoaji elimu ya juu nchini ili
kuwezesha wahitimu kukabiliana na changamoto za maendeleo ya taifa
letu kwa ujumla. Kwa mara ya mwisho zoezi hili lilifanyika tarehe 18
Agosti,2010 ambapo jumla ya vyuo vikuu na vyuo vishiriki 13
vilitunukiwa hati Idhini.
No comments:
Post a Comment