Mlango wa Katibu wa CCM wa tawi la Sinza E ukiwa umepigiliwa mbao kwa misumari kuzuia uongozi kuingia ndani.
...Kila mlango wa ofisi katika tawi hilo ulikuwa hivi.
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi
la Sinza E jijini Dar es Salaam wamefungiwa milango na vijana wa chama
hicho kwa madai kuwa kuna ubadhirifu wa fedha katika ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa Vijana wa Tawi hilo, Ally Ngoti ameuambia mtandao huu kuwa tangu viongozi wao waingie madarakani wamekuwa hawaelezi mapato ya ofisi hiyo yanakwenda wapi.
“Hapa tuna miradi mingi kama vile egesho la magari ambalo linaingiza mamilioni ya fedha lakini hatuoni zinakwenda wapi. Kuna fremu za maduka na watu wamepanga lakini fedha hatuzioni, tumeamua kufunga milango ya ofisi ili wasiiingine mpaka kieleweke,” alisema Ngoti na kudai kuwa viongozi hao hawawapendi vijana kwa kuwa wanawakosoa.
Hakuna kiongozi hata mmoja aliyepatikana kujibu tuhuma hizo au kusema watafanya nini ili kufungua ofisi yao.

(PICHA / HABARI: HARUNI SANCHAWA / GPL)
No comments:
Post a Comment