Wengi wanasema ugumu wa maisha umemfanya jamaa kutafuta mbinu mbadala ya kujipatia kipato. Kuna wengine wanamshangaa kwa kujiamini kiasi hiko mpaka kuwa askari bandia.
Ni hali ya kushangaza kwa kweli na kila mtu ana haki ya kushikwa na butwaa. Badala ya kuishia tu kushangaa na kuachia hapo kuna somo kubwa sana la kujifunza kutoka kwa huyu mtu.
Huyu bwana ana nguo zote za traffic na mpaka kifaili cha kuwaandikia watu makosa, sawa huenda kavipata kwa njia za rushwa ama wizi ama kinginecho.
Huyu bwana aliweza kufanya kila kinachofanywa na traffic wa kawaida bila kuhisiwa na mtu yeyote yule. Kilichomfanya akamatwe ni kutopiga salute kwa askari wa cheo cha juu ambae huenda hakumfahamu kwa sura(kama angemfahamu bila shaka angempa heshima yake)
Huyu bwana hakutaka kukaa kariakoo wala ubungo wala tazara ama buguruni. Kajitafutia kaeneo kake ka ndani ndani, tabata kinyerezi na kuanza kula vichwa.
Ukiangalia mambo yote yaliyofanywa na huyu traffic feki yametumia ubunifu mkubwa sana, amejifunza kwa makini matrafiki wanavyofanya na amechagua eneo ambalo sio rahisi kwake kujulikana.
Niliwahi kuandika kila mtu ni mbunifu(soma; kila mtu ni mbunifu). Na somo kubwa tunaloweza kujifunza kwa huyu bwana ni kwamba ukiwa mbunifu unaweza kufanya chochote. Japo yeye kavuka mstari na kuvunja sheria.
Sikuambii ujifunze kufanya uhalifu ili kujikimu na maisha yako. Usijaribu kufanya hivyo hata kidogo. Tumia ubunifu ulionao ambao hujaweza kuutumia bado kupata njia za kufikia malengo yako.
Hakuna ambae sio mbunifu, tatizo ni wachache sana wanaotumia ubunifu wao. Anza na wewe kutumia ubunifu wako.
No comments:
Post a Comment