Afisa Habari wa Kituo cha Habari
cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akifafanua jinsi
waandaaji wa vipindi wanavyoweza kutafuta habari nzuri zenye kuelimisha
kwa ajili ya redio za jamii na pia mbinu wanazoweza kutumia ili
kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii.
Akizungumza katika warsha ya
siku nne inayoshirikisha waandishi na maripota wa redio za jamii
inayofanyika Wilayani Sengerema mkoani Mwanza, Bi. Ledama ameongeza kuwa
upo umuhimu wa kuwajengea uweze watendaji katika redio hizo ikiwemo
kuwafundisha namna ya kutumia mtandao wa Intaneti kwa ajili ya kuboresha
uandishi na utangazaji , haswa katika maeneo muhimu yanayoigusa jamii
ikiwemo Elimu, Afya na Kilimo na pia jinsi redio hizo zinavyoweza
kuandaa vipindi vitakavyoigusa jamii moja kwa moja.
Kwa jumla warsha hiyo ya siku
nne kwa waandishi wa habari wa redio za jamii imeangalia kwa mapana
mambo muhimu ya kijamii, na kuchambua mambo hayo ni yapi ambapo imegusia
masuala ya Afya na Kilimo pamoja na mambo mengine na kuangali fursa
zinazopatikana, pia changamoto zinazokabili masuala hayo na kutathmini
nini kifanyike ili kuboresha utendaji na utoaji huduma katika sekta
hizo.
Mtaalam wa Kilimo kutoka Idara
ya Kilimo wilayani Sengerema Bw. Joseph Manota akizungumza katika warsha
ya waandishi wa habari wa redio za jamii inayofanyika mkoani Mwanza
ambapo fursa zinazopatikana katika sekta ya Kilimo na jinsi ya kuzitumia
ili kufanikisha sera ya Serikali ya Kilimo Kwanza na pia amezungumzia
changamoto zilizopo katika kutimiza sera hiyo na namna gani maafisa wa
Kilimo pamoja na Serikali kwa ujumla wanaweza wakafanya kukabiliana nazo
ili kutimiza malengo ya kukuza Kilimo.
Mshauri wa redio za jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Pichani juu na chini ni
waandishi na maripota wa redio za jamii wanaohurudhuria mafunzo hayo
yanayofanyika kwenyen kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre
Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Mwezeshaji kutoka Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mtaifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akionyesha
baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa ambayo yatawasaidia katika
kuandika habari zao kiufasaha.
Mmoja wa watangazaji wa Redio
Kahama FM William Bundala (Kijukuu cha Bibi K) akitoa mrejesho wa
mafunzo yaliyopita ambayo yameleta mabadiliko makubwa kwa kituo chao kwa
Mshauri wa Redio za Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu
Afisa Elimu, Takwimu na Vifaa
wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Pius Lwamimi akizungumza na waandishi
wa habari na maripota wa redio za jamii nchini ambapo aligusia
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta Elimu wilayani humo na kuwaasa
kutumia redio zao katika kutoa taarifa muhimu kwa jamii zitakazopelekea
kukua kwa Sekta ya Elimu nchini. Pia amewataka wazazi kuwa mstari wa
mbele na kujitokeza kuhudhuria vikao katika shule na kutoa maoni yao
kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo mitaala ya elimu na pia kushirikiana na
redio za jamii kwa kutoa taarifa muhimu na pia kuwahamasisha watoto wao
na jamii nzima kujenga utamaduni wa kusikiliza vipindi vya redio hizo
kwa manufaa yao.
Sehemu ya washiriki wanaohudhuria mafunzo hayo.
--
Zainul A. Mzige,
Operation Manager,
MO BLOG,
www.mohammeddewji.com/blog
+255714940992.
No comments:
Post a Comment