MAANDAMANO
ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na
maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada
ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi
mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi
wa chama hicho.
Maandamano
hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya
jiji la Mwanza yalikuw ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa
Ilemela pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha
yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua
zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha
madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na
kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.
Polisi
wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo
la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa
Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK
068EXV aina ya Toyota Land Cruiser
Maandamano
hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama
yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku
yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya
Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni
pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao
walikuwa katikati ya maandamano hayo.
Baada
ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa
amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka
kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya
awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kw amara kesi
dhidi ya Matata na jingine lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji
barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.
Hata
hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani
yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na
kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea
maandamano hayo.
Kufuatia
kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja
na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya
kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje
alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa
wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi
walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.
Hata
hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza
waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo
kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na
hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.
Jeshi
la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi
za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao
walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi
kuwatawanya wafuasi hao.
Vurugu
hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa
baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe
na kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika
kufungwa kwa muda kupisha vurugu hizo.
Baadhi
ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana
wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu
ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na
waandamanji hao kwa jeshi la polisi.
MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa
chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi
yake imekalia barua a kurejeshwa kwa madiwani Abubakar
Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha
Chenyenge(Ilemela).
RC
Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi
na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote
toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao
baada ya kukata rufaa.
“Hata
Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua
hizo name nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia
kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi
wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa
wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.
“Lakini
cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua
za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali
walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba
kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI
kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze
wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.
Kuhusu
suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema
kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kw akuheshimu mamlaka ya mahakama
na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi
yake.
KAULI YA MBUNGE KIWIA.
Akizungumza
katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua
kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa
tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.
“Mheshimiwa
Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishw ani wawakilishi wa
wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa
halali ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha
madiwani hawa wanarejeshwa.
RPC MANGU.
Akizungumza
kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigw akwa mabomu
ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa
polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni
wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.
WANANCHI WAWALAUMU VIONGOZI NA WANASIASA NA KUWAPONGEZA POLISI.
Baadhi
ya wananchi waliozungumza na Mtanzania juu ya vurugu zilizotokea
waliwaonyoshea kidole wanasiasa pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza
kutokana na kushindwa kusema ukweli juu ya tukio hilo.
Baadhi
walisikika wakisema kuwa kama barua zipo kweli madiwani hao wanapaswa
kupewa na kama azipo basi walioeneza maneno hayo wachukuliwe hatua kali
kutokana na uchochezi.
Wananchi
hao pia walilipongeza jeshi la polisi kutokana na kutumia busara badala
ya nguvu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani.
No comments:
Post a Comment