Ngasa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano
na kutakiwa kuilipa Simba kiasi cha Sh45 milioni kufuatia kubainika
kusajili mikataba ya klabu mbili kwa wakati mmoja.
Klabu yake ya Yanga imekata rufaa kupinga uamuzi
huo, ambapo pamoja na mambo mengine inaona mchezaji wake hakupewa haki
ya kujieleza kufuatia tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.
Lakini jana wakati Mwenyekiti, Mgongolwa
akizungumza na gazeti hili alisema kamati yake inafanya kazi na
vielelezo vya maandishi, hivyo hawakuona sababu ya kumwita Ngasa.
“Kimsingi, watu wanatakiwa kufahamu, sisi kama
kamati tunatumia maelezo ya maandishi ambayo ndio vithibitishoi vyetu,
na kama ushahidi wa vielelezo utakuwa na upungufu ndipo tunapomwita
mchezaji,” alisema Mgongolwa. Akifafanua alisema: “Kuna wachezaji wengi
usajili wao umeonekana kuwa na matatizo, lakini hatukuwai kuwahoji.”
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment