Wednesday, August 28, 2013

SI MAAJABU::Daktari wa Kenya autibu Ukimwi kwa dawa za Kansa


HIV-virus
HIV Virus
Waathirika watano wa virusi vya HIV nchini Kenya wanaonekana kukishinda kirusi hicho kinachosababisha ugonjwa wa Ukimwi na kuongeza matumaini ya kupata tiba ya uginjwa huo hatari zaidi duniani.


Watano hao ni pamoja na wanaume wawili na wanawake watatu ambao sasa hawana tena virusi hivyo baada ya kutibiwa na dawa zinazotumika kutibu kansa. Watu hao walitibiwa na dawa iitwayo methotraxate.
bioniche_Methotrexate
Mmoja wa watu walioponeshwa na dawa hizo ni mama mwenye miaka 40 aitwaye Dorcas, mama wa mtoto mmoja. Dorcas, aliyekutwa na virusi hivyo mwaka 2006, alianza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi na kujaribu kuishi maisha ya afya kama alivyoelekezwa na daktari wake.
Ingawa ARVs ziliipa nafuu afya yake, anasema mwili wake hakuonesha mabadiliko makubwa. Baada ya miaka mitano, dalili za kuathirika na virusi hivyo zikaanza kuonekana wazi kwenye mwili wake.
“Nilianza kujisikia dhaifu, sikuwa na hamu ya kula na nywele zikaanza kuwa laini,” anasema. Na baadaye nikaanza kupata maumivu kwenye joint na misuli kuvimba hali iliyofanya nikaribie kuwa kilema.”
Akiwa na hamu ya kuendelea kuishi, Dorcas alijaribu kutafuta njia mbadala ya kupunguza kasi ya virusi mwilini mwake na nia yake ilimkutanisha Dr Barasa, famasia na mhadhiri kwenye chuo kikuu cha ufundi cha Nairobi aliyekuwa akifanya utafiti kuhusu virusi vya HIV kwa miaka mitano sasa.
DNDrBaraza
Dr Barasa

“Alisisitiza kuwa alitakiwa kuthibitisha kuwa nina virusi vya HIV, anasema Dorcas. Dorcas anasema aliwaomba AMREF waliokuwa wakifuatilia maendeleo yake kumtumia Dr Barasa historia yake ya matibabu.
“Baada ya hapa alianza kunipa matibabu, baada ya miezi sita nilibaini mabadiliko kiasi. Mwaka mmoja baadaye najisikia vizuri na vipimo vinaonesha sina tena virusi vya HIV.”
Taasisi ya Kenya ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Kemri) imethibitisha kuwa ni kweli Dorcas hana virusi (HIV negative). “Inavutia sana,” ilisema Kemri kwenye maelezo yake kuhusu kupoma kabisa kwa Dorcas. “Hatuna uhakika ni vipi imetokea lakini kweli mwanamke huyu anaonekana kupona HIV. Aliletwa hapa ka rufaa na Crescent Medical Aid Kenya, na imetuchukua zaidi ya wiki moja kufuatilia vipimo na kuthibitisha kuwa ni kweli kabisa hana tena virusi vya HIV.”
Mgonjwa mwingine aliyeonesha dalili za kupona Nancy, mfanyabiashara wa Nairobi aliyepata maambukizi ya virusi hivyo katikati ya January mwaka huu. Ilimchukua wiki chache kubaini kuwa kuna kitu hakikuwa sawa kwake na hivyo alimbana mpenzi wake ambaye alikiri kuwa ni muathirika na ARVs.
Hali hiyo ilimfanya aende kupima kwenye hospitali ya wanawake ya Nairobi ambako alikutwa hana maambukizi. Hata hivyo daktari alimwambia arudi tena baada ya siku 90 kwakuwa huchukua miezi mitatu ili kirusi kiweze kuonekana.
Hata hivyo Nancy hakuvulimia kusubiri kwa siku 90 hivyo alienda kupima kwenye hospitali nne tofauti nako akaonekana hajaambukizwa. Nancy aliamua kwenda Kemri, ambako wana maabara za kiwango cha juu zaidi ambako huko vipimo vilionesha kumbe ameathirika.
Akiwa amechanganyikiwa na mwenye hasira, alienda kwa Dr Barasa ambaye alianza kumpa pia tiba. Baada ya miezi mitatu ya matibabu Dr Barasa alimpeleka kwenye maabara ya Lancet kwa vipimo zaidi na kubainika kuwa ana virusi vichache mwilini. Baada ya miezi sita Nancy alienda kupima tena Crescent Medical Aid Kenya na majibu kutoka negative. Dr Barasa alimuomba aende tena Kemri kufanyiwa vipimo huko.
Majibu hayo si kuwa yalimshtua yeye bali pia wafanyakazi wa Kemri. Nancy alikuwa hana virusi vya HIV tena!!
 
Source: Daily Nation Kenya, soma zaidi habari hiyo hapa.

No comments:

Post a Comment