Thursday, August 8, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 08. 08. 2013.

 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MNAMO TAREHE  07.08.2013 MAJIRA YA SAA  17:00 HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDAGA  WILAYA YA  RUNGWE  MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI T.101 CDR AINA YA  T-BETTER IKIENDESHWA NA RASHID S/O ISSA, MIAKA 32, MKINGA, MKULIMA  MKAZI WA KIJIJI CHA NTOKELA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO WILLY S/O EDWARD,MIAKA 5,MSAFWA MKAZI WA KIJIJI CHA NDAGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA  WILAYA YA  RUNGWE. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA  KYELA - AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA        
                                            KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.08.2013 MAJIRA YA  SAA 08:30 HRS HUKO KATIKA ENEO LA KALUMBULU  WILAYA YA  KYELA  MKOA WA MBEYA. GARI  T.932 BUF AINA YA  T/IPSUM IKIENDESHWA NA KAIMU S/O HENDE, MIAKA 33, MBONDEI, MKULIMA  MKAZI WA KYELA-KATI  ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO HAWA D/O GIBSON,MIAKA 6,MSAFWA,MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA S/MSINGI MBUGANI  MKAZI KALUMBULU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment