Thursday, August 8, 2013

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA::NDUGU WAGOMA KUZIKA MAREHEMU WAKIAMINI MGANGA ATAMFUFUA NDUGU YAO



 Dereva wa boda boda Cheni Abed akiwa chini baada ya pikipiki yake kugonga na baiskeli kwenye makutano ya barabara za Mafisa,Kichangani
Dereva wa boda boda  Aliyejulikana kwa jina Bw Cheni Abed kufariki dunia baada ya kugongana na baiskeli huku dereva wa baiskeli hiyo ambaye pia alimpakia mwanaye wakiwa salama salmini.
Cheni ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mchuma kata ya Kichangani mkoani hapa  alipoteza maisha baada ya kugongana na baiskeli hiyo na kuangukia kichwa kwenye makutano ya barabara za Msamvu,Mafisa,Mwembesongo huku dereva wa baiskel hiyo ambaye alimpakia mwanye wakisalimika kwenye tukio hilo.
                Umati wa watu ukishuhudi tukio hilo la aina yake
Kufuatia mazingira ya tukio hilo familia ya dereva boda boda huyo iliamua kusafiri hadi wilaya ya mvomero kwenda kwa mganga wa kienyeji kuchunguza mazingira ya kifo hicho ambapo Sangoma  Hamis Masai mkazi wa kijiji cha Changarawe kata ya Mzumbe Wilaya ya Mvomero mkoani hapa alimueleza baba wa mzazi wa marehemu huyo Bw Abed Shabani kwamba mama yake mzazi ndiye alimuua mjukuu wake huyo kwa kumchukua msukule na kwamba Sangoma huyo alimhakikishia Mzee Shabani kwamba alikuwa na uwezo wa kumrejesha dunia mwanye huyo aliekuwa nguvu muhimu kwenye familia hiyo.

Kufutia kauli hiyo Mzee Shabani aliludi Morogoro mjini na kusitisha mazishi ya kijana wake kwa siku nne akisubiri mganga huyo amfufue, kufuatia taarifa hizo majirani ambao yatari walishaanza kutoa msaada wa kuchimba kaburi na kuchanga michango ya mtaa walizuiwa kufanya shughuri hizo kwa maelezo kwamba Cheni angefufuliwa.
Habari za kufufuka kwa boda boda  huyo zilizagaa kwa kasi kubwa kama kile kimbunga cha sunami na kwamba siku ya nne aliyohadi mganga huyo kumfufua boda boda huyo ilipofika umati wa watu kutoka kona zote za mji wa morogoro walifuka nyumbani kwa mzee Shabani akiwemo wmandishi wa habari hizi kwa lengo akushuhida maajabu hayo. Na Dustan Shekidele..
Familia hiyo na wananchi hao walisubiri toka saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku bila kushuhudi boda boda huyo akifufu liwa na kwamba Sangoma huyo alipoulizwa na familia hiyo alidai kwamba kuna mashariti yalivunjwa na familia hiyo hivyo asingewe tena kumfufua marehemu wao na kwamba baada ya kauli hiyo watu walitawanyika na kurudi siku iliyofuta kumzika boda boda huyo.
Katika mazishi hayio kuliibuka mambo kadhaa ambapo miongoni mwa mwambo hayo ni mashekhe wote wa kata ya kichanga kugoma kwenda kumsalimi marehmu huyo wakiitaka familia hiyo kwenda kumwita mganga huyo wa kiennyeji wanayemuami aje kumsalia marehemu wao.

Familia hiyo baada ya kuona viongozi hao wa dini wamevuta 'Hend Breck' wameamu kukodi boda boda na kwenda kumfuta shekh Mageta ambaye ana undugu na familia hiyo na kwamba kwenye mawaidha yake Shekh Mageta akiipiga madogo familia hiyo kwa kuabudu mamboya kishirikina.

"Nimepata ahabari mashekh wenzangu wa eneo hili wamesusia kuja kwenye msiba huuu kwa mambo yetu ya kijinga ya kuabudu ushirikina kijana wetu amekufa kwa ajari na amenguaki kiichwa damu mwingi zimetoka leo mnaenda kuangua kwa mganga kuchunguza kifo chake na mnadanganywa eti mganga huyo naweza kumfufua mtu mbona ameshinwa kumfufua naomba sikunyingine msiludia jambo hili" alisema Shekhe mageta kwwnye mawaidha yake
Mwenyekitim wa taa huo wa chuma Bw Nathanael Chacha ambaye alikiri kupokea taarifa za familia hiyo kumfufua kijana wao alimu kuwaambia wajumbe wake waliokuwa kwenye zoezi la kuchanga pesa za pole kuacha zoezi hilo 
Jambo la tatu lililojiri kwenye msiba huo ni kwamba kwenye acouti ya simu ya marehmu kulikutwa pesa taslimu shilingi laki sita na kwamba dada za marehmu walihangaika kuzitoa pesa hizo bila mafanikia baada ya kushindw akuitambua namba ya siri ya marehmu huyo licha ya kujari kuweka namba ya siri ya mwaka wa kuzaliwa wa maremu huyo.
Baba mzaza wa marembu Mzee Abed Shabani alipohojiwa na mtandao huu alikiri simu ya mwanayen huyo kuwa na kiasi hicho cha fedha na kuda kwamba wanashindw akuzitoa baada ya kutoitambua namba ya siri,habari ambazo mtandao huu umezinasa zilidai kwamba mchumba wa boda boda huyo ambaye ameza naye mtoto mmoja ndiye pekee nayejua namba za siri za simu ya mpenzi wake na kwamba kuna habari zinadai kwamba wifi zake kwa sasa wamemficha jambo hilo naye amedai kwamba kamwe hawezi kuwataji namba hizo za siri mapka atakapohakikishiwa mgeno wa fedha hizo yeye na mtoto wake.
mwendezo wa tukio hili kwa maaba ya picha za mazishi utawajia kesho hivyo usikose kutemebea mtandao huu kujua mengi kujuu ya tukio hili ikiwemo ya bibi huyo wa marehmu aliyetumia uchawi naye kufariki duni kwa Sangoma huyo
 Pikipiki yake ikiwa safi haijaaribika a popote kama inavyyonekana 
 Polisi wakimpaki kwenye gari boda boda huyo kwa lengo la kuhospital ambayo kabla ya kufika hospital boda boda huyo alifika njiani

 Mungu ni mkubwa dereva wa baiskeli hiyo  alimpakia mwanae huyu ambaye hakuumia popote kwenye ajari hiyo
 Gari ya polisi akielekea hospita ya rufaa ya mkoa wa Morogor

No comments:

Post a Comment