Daladala
ambayo ilikuwa inatoka Mbalizi kwenda Songwe yenye namba za usajili T
635 ALS ikiwa imeharibika vibaya Baada ya Ajali kutokea Eneo la Ifisi
Mbalizi Mbeya
Hapa ndipo eneo ambalo Daladala iliingia wakati ilijaribu kulipita Gari lengine akiwa mwendo kasi na kuukutana na Tela la Mafuta
Lori aina ya Scania yenye namba ZA usajili T378 AGD likiwa limepaki Baada ya ajali hiyo kutokea
Mabaki ya daladala
Wananchi mbalimbali wakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliyo tokea Ifisi Mbalizi Mbeya
Hivi ndivyo Daladala inavyo onekana upande wa Mbele baada ya Ajali kutokea
Dereva wa daladala ambaye ndiye aliye sababisha ajali hiyo Nikutusya Mwanja akiwa anapelekwa chumba cha matibabu ya Haraka.
Baadhi ya Majeruhi waliokuwemo katika ajali hiyo
Wakazi mbalimbali wakiwa katika Hospitali ya Ifisi Mbalizi Mbeya kutazama ndugu zao waliopata ajali.
Askari wa usalama barabarani wakiandikishana Dhamana na ndugu wa Dereva wa Daladala ili apate dhamana ya kutibiwa
*****************
WATU 17
wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuharibika
vibaya kufuatia ajali iliyohusisha Gari la abiria aina ya Toyota Hiace
na Scania.
Ajali
hiyo imetokea leo majira ya Saa Saba Mchana katika eneo la Ifisi nje
ya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Ifisi(ICC) Mbeya Vijijini.
Mashuhuda wa
ajali hiyo wamesema gari la abiria Toyota Hiace lenye namba za usajili T
635 ALS likiendeshwa na Nikutusya Mwanja likitokea Mbalizi kuelekea
Songwe iliingia kwenye Trela la Scania lililokuwa likitokea Tunduma
kuelekea Dar Es Salaam.
Wamesema
chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari ndogo ambapo Dereva alikuwa
akijaribu kulipita gari lingine lakini mbele akakutana na Lori ambalo
alipojaribu kulikwepa akaingia kwenye Trela lake na kupinduka vibaya.
Trela
hilo lenye namba za usajili T 675 ACT likiwa linavutwa na Kichwa chenye
namba za usajili T 378 AGD halikuweza kuumia sana kutokana na kwenda
kwa mwendo mdogo ambapo majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitale
teule ya Ifisi kwa matibabu zaidi.
Muuguzi
Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimath Sanga amethibitisha
kupokelewa kwa majeruhi 17 na kwamba kati ya majeruhi hao 3 hali zao
siyo nzuri sana ingawa majina yao hayakuweza kupatikana.
Ameongeza
kuwa majeruhi wengi wameumia sehemu za kichwani na miguuni na kwamba
baada ya kumaliza kupatiwa huduma ya kwanza wataangalia ni wangapi
wanaweza kuruhusiwa na wengine kulazwa.
Hata
hivyo habari kutoka eneo la tukio zimesema kuwa Kondakta wa gari dogo
aliyefahamika kwa jina moja la Ayubu alitoweka mara baada ya kutokea kwa
ajali ingawa haifahamiki kama ni kurukwa kwa akili au ni kukimbia kesi.
No comments:
Post a Comment