KIKOSI cha
Taifa Stars kitashuka dimbani keshokutwa Jumapili kuivaa Ivory Coast
katika mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014, lakini habari ni
kuwa kiungo mshambuliaji wa Stars, Mrisho Ngassa hataruhusiwa kucheza
kwa kuwa ana kadi mbili za njano.
Taarifa ambazo Championi Ijumaa imezipata kutoka ndani ya Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), zimesema kuwa wamepokea ujumbe kutoka Shirikisho
la Soka Afrika (Caf) kuwa Ngassa ana kadi mbili za njano.
Taarifa hiyo imesema kuwa, kiungo huyo alipata kadi mbili za njano
katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini wakati Stars ikiumana na
Morocco, ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa Machi, Stars ilishinda mabao
3-1 kabla ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 ugenini.
“Tumepokea ujumbe kutoka Caf juu ya Ngassa, ni taarifa mbaya hasa
katika siku hizi mbili kwa sababu tunajua kocha alikuwa anajua atakuwa
naye katika mchezo wa keshokutwa,” alisema kiongozi huyo wa TFF.
Aidha, straika wa Stars, Mbwana Samatta: “Ile ni timu tu (Ivory
Coast) kama timu nyingine, sijaona sababu za kuiogopa au kuihofia, tuna
asilimia kibao za kushinda ukizingatia tunacheza nyumbani, ” alisema
Samatta.
No comments:
Post a Comment