Vurugu zimeendelea mjini Arusha
ambapo jana polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kudhibiti
mikutano ya hadhara kufuatia polisi kutangaza kutokuwepo kwa mikusanyiko
ili kuimarisha usalama kufuatia mlipuko wa pili uliotokea mjini Arusha,
baada ya mtu asiyejulikana kurusha bomu katika mkutano wa kisiasa
Wabunge wanne wa CHADEMA jana wametiwa mbaroni
kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko bila kibali ambapo viongozi hao wa
chama cha upinzani cha CHADEMA walikusanyika katika eneo lililotyokea
mlipuko wa bomu la viwanja vya Soweto kwa malengo ya kutaka kufanya
mkutanoHata hivyo kuna madai kuwa baadhi ya viongozi wengine wa chama cha Chadema wanasakwa na POLISI, wabunge hao wanatuhumiwa kuwahamasisha wafuasi wao kuwashambulia polisi kwa mawe wakati walipotakiwa kuondoka katika viwanja hivyo kwa hiari.
aidha polisi pia imekitaka chama cha CHADEMA kuwasilisha kile ilichodai kuwa ni ushahidi wa mtu aliyehusika na urushaji wa bomu hilo
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, inadaiwa kuwa bomu lililorushwa katika mkusanyiko huo lilitengenezwa nchini China. Kiongozi wa harakati dhidi ya tukio hilo Paul Chagonja amesema polisi wako tayari kupokea ushahidi kutoka kwa viongozi hao wa kisiasa wanaodai wana taarifa za mtu huyo aliye husika
Jana pia kumetokea vurugu kwa kile kilichodaiwa ni baada ya polisi kuzuia mkutano mwingine wa hadhara uliokuwa ukilenga kutaka kufanya ibada ya mazishi.
UPDATES
Wabunge wa chadema ndio wanapelekwa mahakamani muda huu.
Ni Tundu lissu, mustafa Akonay, na mbunge na makamu mwenyekiti bara mzee Said Arfi pamoja na Joyce Mukya,
• Mashtaka ni mkusanyiko usio kuwa halali
• Zaidi ya watu 70 pia wamepelekwa mahakamani kwa makosa ya kukusanyika bila kibali.
Ni Tundu lissu, mustafa Akonay, na mbunge na makamu mwenyekiti bara mzee Said Arfi pamoja na Joyce Mukya,
• Mashtaka ni mkusanyiko usio kuwa halali
• Zaidi ya watu 70 pia wamepelekwa mahakamani kwa makosa ya kukusanyika bila kibali.
No comments:
Post a Comment